BECKHAM AAGA MAREKANI KWA KUIPA KOMBE L.A. GALAXY
DAVID Beckham alihitimisha kipindi chake
cha miaka mitano na nusu cha kucheza soka Marekani kwa kuisaidia timu
yake ya LA Galaxy kutetea Kombe la 'Ligi' la MLS kwa ushindi wa 3-1
dhidi ya Houston Dynamo katika mechi yake ya mwisho kuichezea klabu
hiyo.Houston waliongoza wakati wa mapumziko kupitia shuti kali la Calen Carr, lakini goli la kichwa la Omar Gonzalez na penalti ya utulivu ya Landon Donovan vilibadilisha mwelekeo wa mechi.
Penalti ya pili, iliyofungwa na Robbie Keane katika dakika za majeruhi, ilikamilisha ushindi katika mechi hiyo ilichochezwa mjini Los Angeles.
Beckham (37) kisha akapumzishwa na kushangiliwa na mashabiki ambao waliinuka kumuaga.
"Nina machungu kwa sababu leo ndiyo mwisho," alisema Beckham.
"hapa ni mahala 'spesho' kwangu na pataendelea kuwa hivyo. Nina furaha sehemu ya klabu hii kwa miaka sita na nina furaha imekuwa timu ya mafanikio katika miaka minne iliyopita.
"Naweza nisicheze tena hapa lakini nitaendelea kujitoa katika kusaidia kukua kwa klabu hii, ligi hii na mchezo huu."
Beckham amehusishwa na mipango ya kujiunga na klabu ya Paris St Germain na Monaco, lakini amesisitiza kwamba "hajui" atacheza wapi msimu ujao.
Ni mara ya pili kwa Beckham kubeba Kombe la 'Ligi" la MLS, LA Galaxy ikiwafunga wapinzani wao hao hao 1-0 katika fainali ya mwaka jana.
No comments:
Post a Comment