Na Heka Wanna na Shakila Galus,MAELEZO
20/12/2012
MATUKIO ya uhalifu nchini imepungua kutokana na ushirikiano mzuri baina ya wananchi kwa kutoa taarifa za uhalifu kwa jeshi la polisi.
Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Isaya Mnguru
alisema kuwa kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Novemba, 2012
ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2011 takwimu zinaonesha hali
ya uhalifu imepungua.
Aidha kumejitokeza na matukio kadhaa ya
makosa dhidi ya kuania mali,makosa dhidi ya binadamu, makosa dhidi ya
maadili na makosa dhidi ya usalama barabarani.
DCP
Mnguru alisema kuwa hali ya mwenendo wa uhalifu kwa mwaka 2012 makosa
makubwa ya jinai yaliyotolewa taarifa katika vituo vya polisi ni 66,255
ikilinganishwa na makosa 69,678 yaliyo ripotiwa kwa kipindi cha mwaka
2011 ni upungufu wa makosa 3,423 ambao ni sawa na 4.9%.
Aliendelea
kuwa takwimu zinaonesha matukio makubwa ya usalama barabarani
yaliyoripotiwa ni 21,531 ikilinganishwa na matukio 22,208 yaliyoripotiwa
mwaka jana ambapo ni upungufu wa matukio 677 ambao ni sawa na 3%.
Mnguru alisema kuwa matishio ya usalama nayo yamepungua kwani mpaka sasa hivi hakuna tishio la dhahiri hapa nchini kuhusiana na tishio la ugaidi.
Alisema hali hiyo imetokana
na hatua zilizochukuliwa katika kuimarisha ulinzi kwenye mipaka na
maeneo nyeti sambamba na kuwatahadharisha wananchi kuwa waangalifu na
kutoa taarifa za nyendo za watu au vikundi wanavyovitilia mashaka.
Aliongeza kuwa jeshi
la polisi linaendelea kubuni na kutekeleza kikamilifu mikakati ya
kukabiliana na uhalifu ikiwemo kushirikiana na wadau wote wa ulinzi na
usalama katika kubadilishana taarifa za kiintelijensia pamoja na uzoefu
wa kuzuia uhalifu kwa kuibua mifumo mipya na kuboresha ya zamani.
Alisema namba za simu za makamanda wa polisi zimesambazwa
nchini kote wananchi wasisite kuzitumia wapoona viashiria vya uhalifu.
aliwaonya wale wote wasiopenda kutii sheria kwa hiari yao kuacha tabia
hiyo wakiemo madereva wa mabasi ya abiria kutotii sheria za barabarani
pamoja na waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda kutovaa kofia ngumu
na kupakia abiria zaidi ya mmoja.
No comments:
Post a Comment