MKUU WA MKOA WA ARUSHA AMZAWADIA TUZO MWANDISHI WA NEW HABARI
ARUSHA
MKUU
 wa Mkoa wa Arusha amemzawadia   tuzo ya uandishi bora  wa habari za 
jamii na maendeleo Meru , mwandishi wa habari  Mary Mwita   wa magazeti 
ya Mtanzania na Rai ya  Kampuni ya New habari (2006) LTD.
 Mkuu wa Mkoa huyo ametoa  tuzo 
hiyo ,ikiwa ni ahadi yake ,na agizo alilotoa kwa uongozi wa Halmashauri 
hiyo kupeleka jina la Mwandishi wa habari aliyeandika habari bila 
kupotosha jamii katika Halmashauri hiyo ,na kuweza kumpata Mwandishi 
huyo .
 Mkuu alitoa Tshs 500,000 ikiwa ni
 tuzo  na kiasi cha fedha zilizokabidhiwa kwa wadau wengine mwaka huu 
waliobainika kuchangia maendeleo ya Meru.
 Mkuu huyo alisema kuwa  huwezi 
kutaja maendeleo bila kuhusisha vyombo vya habari na waandishi wa habari
 ,na kuwa kila Halmashauri inatakiwa kutambua  mchango wa maendeleo ya 
wadau  ikiwa ni pamoja na waandishi wa habari .
 Akimpongeza Mwandishi  Mary Mwita
 ,alisema wakati umefika wa waandishi wa habari kuandika habari za 
kweli  bila kupotosha umma ,ikiwa ni kuwawezesha wananchi kujifunza na 
kupata ujuzi kupitia habari hiyo ,badala ya kuandika habari za uongo .
 Mlongo alisema kuwa ni wazi kuwa 
kila mtu katika jamii akisimama katika nafsi yake kulingana na karama 
aliyopewa Maendeleo ya haraka yatafikiwa na kuwawezesha wananchi 
kupunguza kasi ya umaskini katika jamii .
 Katika hatua nyingine alipongeza 
uongozi wa Halmashauri ya Meru kwa kutambua mchango wa maendeleo ya 
wadau  na kutaka Halmashauri nyingine kuiga mfano huo wa kutunikia 
zawadi wadau waliosaidia maendeleo ya Halmashauri.
 Kwa upande wake  Mkurugenzi 
Mtendaji wa Halmashauri ya Meru Trisas Kagenzi alisema kuwa  zoezi la 
kuwazawadia wadau ni endelevu ,na kuwa wataendelea kutambua mchango wao 
kwa kuwa bila ushirikiano na wadau  wa maendeleo ,maendeleo yanaweza 
kuchelewa .
 Kagenzi alisema kuwa Mwandishi 
Mary Mwita ,amekuwa akiandika habari bila kupotosha umma  kwa kujituma 
na kutaka waandishi wengine kuiga mfano wake.
No comments:
Post a Comment