HOTEL YA DOUBLE TREE YA JIJINI DAR ES SALAAM YAFUNGIWA
Na: Lulu Mussa na Ali Meja
Waziri wa Nchi wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Dk. Terezya Huvisa hii leo ameifungia hotel ya Double Tree ya Jijini Dar es Salaam kutokana na kutiririsha maji taka baharini.
Waziri Huvisa ametoa agizo hilo 
mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza akiwa na Naibu Waziri Ofisi ya
 Makamu wa Rais Mheshimiwa Charles Kitwanga.
Ziara hiyo ililenga kuona 
utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa awali na Naibu Waziri Mh. Charles 
Kitwanga mapema mwezi huu, alipofanya ziara kutembelea viwanda na hoteli
 zilizo pembezoni mwa bahari kuona mfumo wa maji taka.
Katika ziara hiyo, Hotel ya Double Tree
 iliagizwa kuwa na mpango wa muda mfupi na wa haraka wa kusitisha 
utiririshaji wa maji taka baharini ambao mpaka leo hotel hiyo ilikuwa 
bado haijatekeleza.
Sambamba na hilo na hilo Waziri 
Huvisa amefuta hati ya ukaguzi wa Mazingira (Environemental Audit) na 
kuitaka hoteli hiyo kurekebisha mara moja mfumo huo ikiwa ni sambamba na
 kulipa faini kwa baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira  
(NEMC)
No comments:
Post a Comment