TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Thursday, March 27, 2014

Seif: Hatuko tayari kujadili serikali mbili

maalim 229b9
Mapendekezo yaliyowasilishwa na Jaji Warioba hayakuwa maoni yake, yale ni maoni ya wananchi, Tanganyika imevaa koti la Muungano, ametoa ushahidi wake ili kujenga mwafaka katika kuendeleza Muungano wenye mfumo wa serikali tatu,"
 Zanzibar. Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema chama chake cha CUF hakiko tayari kujadili mfumo wa Muungano wa serikali mbili kama inavyotetewa na wabunge wa CCM na Rais Jakaya Kikwete.
Amesema tayari amewaandikia barua Rais Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein kuwaeleza juu ya msimamo huo.
Maalim Seif alitoa msimamo huo jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Kibandamaiti mjini Unguja.(Hudugu Ng'amilo)
Isitoshe, alisema CUF imebaini kuwa kuna njama za kufuta kipengele katika Katiba ya Zanzibar kinachosema; "Zanzibar ni nchi" na kwamba hiyo ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu kwa kuwa Wazanzibari kamwe hawatakubali kufanya hivyo.
Maalim Seif alisema haikuwa mwafaka kwa Rais Kikwete kukosoa mapendekezo ya Rasimu ya Katiba yanayotaka mfumo wa Muungano kuwa wa serikali tatu.
Alisema Jaji Warioba aliweka kando itikadi yake ya CCM katika utendaji wake kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kuja na uamuzi huo kwa vile ndiyo tiba ya kero za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
"Mapendekezo yaliyowasilishwa na Jaji Warioba hayakuwa maoni yake, yale ni maoni ya wananchi, Tanganyika imevaa koti la Muungano, ametoa ushahidi wake ili kujenga mwafaka katika kuendeleza Muungano wenye mfumo wa serikali tatu," alisema Maalim Seif.
Alisema Muungano wa serikali mbili hauvumiliki na kama kuna watu wanaendelea kuutetea mfumo huo, Zanzibar inaweza kutumia sheria yake ya kura ya maoni kuwauliza wananchi wanaotaka na wasiotaka jambo hilo.
"Nimemwandikia barua Rais Kikwete, nakala nimempelekea Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, Tanzania Bara wanataka Zanzibar iondoe kifungu cha Katiba kinachosema Zanzibar ni nchi, jambo hilo halitapita...tutafanya kampeni wananchi walikatae," alieleza Katibu Mkuu huyo wa CUF.
Alisema ni jambo la kusikitisha katika hotuba yake alijisahau kama ni mkuu wa nchi na analihutubia Bunge Maalumu badala yake akaegemea kuwa mwenyekiti wa CCM.
Alisema haikuwa sahihi kutoa vitisho na kutaja ikiwa Serikali ya Muungano chini ya Serikali tatu italegalega, jeshi litachukua madaraka ya nchi.
"Rafiki na ndugu yangu Kikwete, usifikiri huu ni wakati ule wa Julius Nyerere, akisema yeye hakuna wa kumpinga. Mambo yamebadilika, usijifanye ni Nyerere mpya, hakuna atakayekusikiliza na kubabaika," alisisitiza Maalim Seif.Alisema ikiwa viongozi wa Muungano wanajiandaa kutisha watu na kusababisha ghasia katika nchi, mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ipo na watakaosababisha fujo na umwagaji wa damu watafikishwa mbele ya mikono ya sheria bila ya kujali nyadhifa na madaraka yao.
CHANZO MWANANCHI

WALAGHAIWA KUSHIRIKI UKAHABA CHINA

 bernad_17899.jpg

Serikali ya Tanzania imesema kuwa imebaini kuwepo kwa biashara haramu ya kusafirisha watoto wa kike kwenda nchini China kwa lengo la kuwashirikisha katika ukahaba ambao unadaiwa kusababisha kunyanyaswa kwa wasichana hao na wengine kuuawa.
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimatifa nchini humo Bernard Membe amesema serikali itatuma wachunguzi nchini Uchina kuchunguza biashara hiyo.
Hatua hiyo imechukuliwa mwezi mmoja baada ya msichana mmoja Mtanzania kuuawa kikatili katika mji wa Guangzhou nchini Uchina.
Waziri Membe amesema huenda baadhi ya wahusika wa bishara hiyo ni Watanzania wanaosafirisha wasichana wa dogo kwa kisingizio cha kuwatafutia ajira. Baadhi ya wanaosafirishwa hujipata pabaya baada ya kuwasili Uchina ambapo hunyang'anywa hati zao za usafiri na kulazimishwa kushiriki ukahaba.(P.T)

LUGOLA:NITAKUWA WA MWISHO KUISALITI RASIMU YA WARIOBA

nyalandu_95dc3.jpg
Mjumbe wa Bunge la Katiba, Kangi Lugola ameapa kuwa atakufa na tai shingoni kwa kuitetea hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kwa kuwa ndiyo iliyobeba mawazo ya watu wengi.
Kutokana na hilo, Mbunge huyo wa Jimbo la Mwibara anaonekana kutofautiana waziwazi na Mwenyekiti wa chama chake cha CCM, Rais Jakaya Kikwete ambaye aliipinga baadhi ya vipengele vya rasimu hiyo.
Akizungumza baada ya kupangwa kwenye kamati, Lugola alisema kuwa haoni tatizo katika hotuba ya Warioba na kwamba atakuwa wa mwisho kuisaliti.
Alisema kuwa mawazo ya Tume ya Jaji Warioba ndiyo mawazo ya Watanzania walio wengi ambao walipendekeza kuhusu Katiba wanayoitaka.
"Sasa mkisema napingana na Mwenyekiti wangu, nadhani siyo dhambi kufanya hivyo kama tunapingana kwa misingi ya hoja, lakini msimamo wangu mimi ni Serikali tatu ambayo ndiyo hotuba ya Warioba aliyesimama pale kwa niaba ya watu wote," alisema Lugola.(P.T)
Alisema kuwa Katiba anayoitaka ni ile iliyotoka kwa wananchi na wala siyo Katiba inayotoka kwa viongozi na kuongeza hata Mwenyekiti wa CCM (Rais Kikwete) atakuwa analijua hilo.
Mbunge huyo machachari alisema kuwa mbali na kupangwa katika kamati ambayo imejaa vigogo wakubwa wa CCM hatajali na kuapa atapambana hadi mwisho.
Mwenyekiti wa Bunge Samuel Sitta alitangaza orodha ya majina kwa kila kamati jana na Lugola amepangwa kamati namba 6.
Hata hivyo, huenda akapata upinzani mkubwa kutokana kamati hiyo kuwa na vigogo wa CCM, Sophia Simba, Stephen Wasira, John Magufuli.
Vigogo wengine wa CCM walioko kwenye kamati hiyo ni pamoja na Margareth Sitta, Dk. Fenela Mukangara. Pia yumo Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema jambo linalodhihirisha atapata wakati mgumu.
Tangu kuanza kwa Bunge la Katiba, Lugola amekuwa na msimamo wa kuunga mkono Serikali tatu yeye pamoja na Mbunge wa Nkasi, Ali Keissy.
Chanzo:Mwananchi

MKUU WA JESHI KUGOMBEA URAIS MISRI

Mkuu wa majeshi na waziri wa ulinzi Misri, Abdul Fattah al-Sisi, ametangaza kujiuzulu jeshini ili kugombea katika uchaguzi wa urais mwezi ujao.
Wagombea wote wanapaswa kuwa raia.
Akizungumza Kwenye hotuba ya Televisheni huku akiwa amevalia sare ya kijeshi Abdel Fattah El Sissi amesema yeye sio mwanajeshi tena baada ya miaka 44 na kwamba amechukua hatua hiyo ili aweze kutimiza jukumu lingine muhimu.
Ni Bayana kwana Sisi hatakua na kibarua kigumu kujipatia ushindi katika uchaguzi wa Urais. Anaungwa mkono na idadi kubwa ya raia wa Misri na hadi sasa hana wapinzani wowote.
Baadhi ya waliotaka kugombea urais wamejiondoa wakidai kwamba hawataweza kuendesha kampeni zao kwa njia huru.
Wafuasi wake Sisi wanamuona kama kiongozi imara ambaye anaweza kurejesha amani na udhabiti nchini Misri baada ya miaka mingi ya machafuko.
Wakosoaji wake wanasema ana msimamo mkali na amechangia pakubwa katika kusambaratisha na kuhujumu upinzani nchini Misri.
Mkuu huyo wa jeshi atakabiliwa na majukumu mazito ya kufufua uchumi uliofifia , kupambana na uasi na kuileta pamoja nchi iliyogawanyika. Ameahidi kutekeleza mabadiliko makubwa lakini akaonya kuwa hawezi kufanya miujiza.
Chanzo:BBC

Wednesday, March 26, 2014

Kosa lililofanya mlinzi wa Rais Obama kuachishwa kazi saa kadhaa zilizopita

ob
Jarida la Washington Post nchini Marekani limeripoti kwamba askari watatu ambao ni walinzi wa president wameachishwa kazi kwa muda na kurudishwa nyumbani ili uchunguzi ufanyike.
Askari mmoja kati ya hao alikutwa amelewa pombe chakari kwenye hoteli moja huko Amsterdam ambapo Obama alienda kwa ajili ya mkutano wa mambo ya Nuclear.
Msemaji wa idara ya upelelezi Marekani alikataa kutoa taarifa zaidi kuhusu tukio hilo ingawa alisisitiza kuwa watatu hao wameachishwa kazi kwa muda huku uchunguzi ukiendelea.
Mwaka 2013 majasusi wawili waliondolewa katika kikosi cha ulinzi cha Rais Obama kufuatia tuhuma za kuhusika na kashfa ya ngono na utovu wa nidhamu.
Mwaka 2012 majasusi kadhaa waliachishwa kazi kufuatia madai kuwa walikodi makahaba walipokuwa mjini Cartagena Colombia.

Monday, March 24, 2014

Picha 9 za jinsi taarifa mpya za ndege ya Malaysia zilivyopokewa na ndugu na msg waliyotumiwa.

Screen Shot 2014-03-25 at 1.00.53 AM
Waziri wa Malaysia amebadilisha vichwa vya habari duniani kwa kusema ripoti ya shirika moja la Uingereza inadhihirisha kwamba ndege ya Malaysia iliyopotea zaidi ya siku 15 zilizopita, ilianguka kwenye bahari ya hindi na kuua watu wote waliokuwemo ndani.
Ni habari ambayo imepokewa kwa machungu sana hasa kwa ndugu waliopoteza wenzao waliokua wakisafiri na ndege hii…
Screen Shot 2014-03-25 at 1.00.46 AM
Ndege hii ya Malaysia ilikua na abiria 239 ndani yake.
Screen Shot 2014-03-25 at 1.12.01 AM
Screen Shot 2014-03-25 at 1.11.58 AM
Wengine ilibidi wapewe huduma baada ya mshtuko.
Wengine ilibidi wapewe huduma baada ya mshtuko.
Screen Shot 2014-03-25 at 1.11.48 AM
Screen Shot 2014-03-25 at 1.19.23 AM
Hii hapa juu ndio msg waliyotumiwa na shirika la ndege la Malaysia.
Screen Shot 2014-03-25 at 1.19.19 AM
Screen Shot 2014-03-25 at 1.19.14 AM
Screen Shot 2014-03-25 at 1.19.09 AM

Kuhusu kamati 12 zilizoundwa na Sitta na hotuba ya JK kujadiliwa

Screen Shot 2014-03-25 at 12.45.46 AM
Kufuatia kuwepo kwa hoja mbalimbali za wajumbe wa Bunge maalum la katiba kuhusu kukinzana kwa Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa wakati wa uzinduzi wa bunge hilo na rasimu ya katiba iliyowasilishwa na mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba jaji Joseph Warioba, mwenyekiti wa bunge maalum Samwel Sitta ameridhia kujadiliwa kwa hotuba hizo.
Amesema baada ya kutolewa kwa hotuba hizo amekuwa akipokea maombi ya Wajumbe mbalimbali wakishauri kutaka zijadiliwe na kupendekeza mjadala huo ufanyike siku ya Jumatano wiki hii.
Kauli ya Mwenyekiti huyo imetokana na muongozo ulioombwa na mmoja wa wajumbe wa Bunge hilo Julius Mtatiro aliyetaka mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Jaji Joseph Warioba aitwe bungeni kujibu baadhi ya hoja zilizotolewa na Rais kikwete ambazo zinapingana na rasimu iliyowasilishwa.
Namkariri Mtatiro akiuliza ‘kwa sababu Rais alikaribishwa tu kwa heshima kwenye bunge hili kuja kufungua na sasa akaanza kujibu ile hotuba, hatuoni kama kuna haja ya kujenga utaratibu wa kumleta tena mtoa hoja ili na yeye aje kujenga hoja juu ya maswali aliyoeleza Rais?’
Kwenye sentensi nyingine mwenyekiti wa Bunge hili maalum la katiba Samwel Sitta ameunda kamati 12 zitakazokuwa zikijadiliana kuhusu ibara za katiba zitakazopangwa kwa ajili ya kuwasilishwa bungeni kwa mijadala ya jumla.

100 wakamatwa mjini Mombasa, Kenya 

140212145434_mombasa_vijana_304x171_bbc_nocredit_92a51.jpg
Watu 100 wamekamatwa mjini Mombasa Pwani ya Kenya kufuatia mashambulizi yaliyofanywa ndani ya kanisa moja mjini humo siku ya Jumapili. Watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki na kufunika nyuso zao waliwapiga risasi waumini wa kanisa moja mtaani Likoni na kuwaua watu wanne Watu  walifariki papo hapo wengine wakifariki hospitalini wakati wakipokea matibabu. Wengine 17 walijeruhiwa vibaya.
Polisi wanasema kuwa watu watatu waliokuwa wamejihami walivamia kanisa la Joy Jesus na kuanza kuwafyatulia waumini risasi kiholelea. Kadhalika polisi walisema kuwa washukiwa wakuu wa shambulizi hilo wametoweka (J.G)
Hakuna mtu yeyote aliyekiri kufanya mashambulizi hayo , ila Kenya imekuwa ikishuhudia ongezeko la mashambulizi tangu kuanza kujihusisha na vita nchini Somalia mwaka 2011. Jeshi la Kenya linasaidiana na wanajeshi wa Muungano wa Afrika kupambana na kundi la wanamgambo la Al Shabaab.
Hali ya usalama imedhibitiwa mjini humo kufuatia shambulizi hilo ambalo limekuja siku chache tu baada ya polisi kunasa washukiwa watatu wa ugaidi wakiwa na mabomu mawili makubwa tayari kufanya shambulizi kubwa. Pia walinasa vilipuzi vingine ndani ya gari lililokuwa limeegeshwa karibu na kituo cha polisi. Mji wa Mombasa wenye sifa ya utalii, umekuwa ukikumbwa na suitofahamu ya kiusalama kutokana na vijana wengi kujiunga na itikadi kali za dini hiyo.

Washiriki shindano la Maisha Plus waingia kijijini rasmi 

2c_8880f.jpg
Uzinduzi wa Kijiji cha Maisha Plus; Jana washiriki wapatao 29 waliingia katika kijiji cha Maisha Plus kuanza kukabiliana na changamoto za maisha kuwania shilingi milioni 25 za Kitanzania. Pichani ni Mkuu wa Kijiji...Mwite babu wa kaya akiwepo kuhakikisha wanakijiji wanakaribishwa kwa shangwe kijijini hapo.
1_d2b0b.jpg
Ofisa Mtendaji wa Kampuni ya dMb ambao ni wamiliki wa Maisha Plus, Masoud Ally (Masoud kipanya kulia) akizungumza katika uzinduzi wa Kijiji cha Maisha Plus, ambapo jana washiriki wapatao 29 waliingia kijijini kuanza kukabiliana na changamoto za maisha kuwania shilingi milioni 25 za Kitanzania.
2_8d6ce.jpg
Mmoja ya wawakilishi toka Oxfam ambao ni wadhamnini wa Maisha Plus 2014 akizungumza machache. Pembeni yake ni Afisa mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Masoud kipanya).
6_3d207.jpg
Safari ya kuelekea kijiji cha Maisha Plus imeanza rasmi... washiriki wakiwa wamebeba mabegi yao ambapo kila mmoja alibeba mzigo wake mwenyewe kwa kutembea kwa miguu umbali wa kilometa 1.5. (J.G)
7_61dae.jpg
9_30fd5.jpg
3_c40bc.jpg
4a_f4851.jpg
Wadau kutoka Oxfam wakibadilisha mawazo mara baada ya kufika katika tukio la uzinduzi wa wawashiriki kuingia kijijini.
3a_fac35.jpg
Kazi ya kujenga nyumba za kuishi washirki wa maisha plus ikiendelea... ambapo washiriki hao walitakiwa kujenga nyumba zao za kuishi ndani ya masaa 48.
11_9006d.jpg
Wengine waliamua kulala ili waweze kunyoosha mgongo.

MAANDAMANO YASHTADI UKRAINE KUIPINGA SERIKALI HIYO

40432AB7-5CDC-4B69-B647-CB503D486891_mw1024_n_s_d2bcc.jpg
Miji ya kusini na mashariki nchini Ukraine imekuwa uwanja wa maandamano makubwa ya wananchi dhidi ya viongozi wa serikali ya nchi hiyo. Maelfu ya wananchi katika miji ya Donetsk, Kharkiv, Odessa na miji mingine ya kusini na mashariki mwa nchi hiyo, walimiminika mabarabarani hapo jana wakipinga mwenendo wa viongozi wa serikali ya Kiev. Kwa mujibu wa ripoti, waandamanaji wametaka nao kuitishwa kura ya maoni kwa ajili ya kujitenga na kujiunga na shirikisho la Russia kama lilivyofanya hivi karibuni jimbo la Crimea sanjari na kurejeshwa madarakani Viktor Yanukovych kama Rais wa halali aliyechaguliwa na wananchi wa nchi hiyo. Kwa upande mwingine, maelfu ya wananchi wamejitokeza mjini Kiev, mji mkuu wa Ukraine wakiunga mkono viongozi wa sasa na kutaka kudumishwa umoja wa kitaifa nchini humo. Hayo yanajiri katika hali ambayo suala la kujitenga eneo la Crimea kutoka Ukraine na kujiunga na Russia limeendelea kushadidisha uadui kati ya Moscow na nchi za Magharibi.
(J.G)

Alichosema Cristiano Ronaldo baada ya kufungwa na Barca hiki hapa

382168_heroaCristiano Ronaldo amezungumza baada ya kipigo cha jana kutoka FC Barcelona akisema walikuwa wakicheza Barca yenye wachezaji 12.
Mwanasoka huyo bora wa dunia amesema kwamba refa wa mchezo huo Undiano Mallenco alichangia timu yake kupoteza wa El Clasico hapo jana usiku katika dimba la Santiago Bernabeu.
Madrid walipewa penati ya utata muda mfupi baada ya kipindi cha pili kuanza, lakini Mallenco aliwapa Barca penati mbili muda mfupi baadae — pia alimtoa kwa kadi nyekundu Sergio Ramos – na Ronaldo anasema anahisi refa alikuwa akiwapendelea Barcelona kwa makusudi.
“Undiano Mallenco hafai kuchezesha michezo ya namna hii. Tulikuwa tunacheza dhidi ya wachezaji 11 na mwingine wa ziada. Mara zote imekuwa hivi. Ni kama vile hawataki tushinde ili Barca watetee taji la La Liga,” Ronaldo aliwaambia waandishi wa habari.
“Sitafuti visingizio, lakini sitaki kukaa kimya kuhusu hili. Refa huyu hakustahili kuchezesha mchezo wa namna hii.
“Nimekuwa hapa kwa muda mrefu – miaka mitano, nafahamu mambo yanavyoenda. Kama Barcelona wangepoteza mchezo hu, wasingekuwa na matumaini ya ubingwa tena. Sijawahi kuona Madrid wakipendelewa na refa.”
“Pamoja na yote yaliyotokea, Madrid bado tutachukua ubingwa wa La Liga.”

Picha za harusi ya Paul wa P Square na Anita Isama

1
Baada ya pacha wake kufunga ndoa, hivi sasa ni zamu ya Paul Okoye ambaye amefunga ndoa ya kimila na mchumba wake wa muda mrefu Anita Isama.
Paul na Anita wana mtoto wa kiume na harusi yao imehudhuriwa na watu kama Omotola,D Banj,Naeto C,Banky W,Ini Edo,Iyanya na wengine wengi.
Hizi ni baadhi ya picha kutoka kwenye harusi hiyo.
2
3
4

Saturday, March 22, 2014

HOTUBA YA JK,WAKATI WA KULIHUTUBIA BUNGE MAALUM LA KATIBA

 

Mheshimiwa Samuel Sitta, Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba;
Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi;
Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar;
Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Mheshimiwa Anne Semamba Makinda; Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano;
Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho, Spika wa Baraza la Wawakilishi na Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba ;
Mheshimiwa Rashid Othman Chande, Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa Othman Makungu, Jaji Mkuu wa Zanzibar;
Viongozi Wakuu Wastaafu;
Waheshimiwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba;
Waheshimiwa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba;
Wageni waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Pongezi
Nakushukuru sana Mheshimiwa Mwenyekiti kwa kunipa fursa ya kuja kuzungumza na Waheshimiwa Wajumbe wa Bunge letu Maalum la Katiba katika siku hii muhimu na ya kihistoria kwa nchi yetu. Nimekuja kuwatakia heri na naungana na Watanzania wenzetu wote kuwaombea baraka za Mwenyezi Mungu, ili muweze kuifanya kazi yenu kwa utulivu, hekima, umakini mkubwa na kuimaliza kwa salama na kwa mafanikio yanayoyatarajiwa na Watanzania.
Natoa pongezi nyingi kwako na kwa Makamu wako kwa kuchaguliwa kwenu kuongoza Bunge hili maalumu na la kihistoria. Ushindi mkubwa mliopata ni kielelezo tosha cha imani kubwa na matumaini waliyonayo Wajumbe wenzenu kwenu. Matumaini yao ndiyo matumaini ya Watanzania wote, kwamba mtaliongoza vizuri Bunge hili, ili liweze kutimiza kwa ufanisi mkubwa jukumu lake muhimu sana katika historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

BENKI YA DUNIA KUUDHAMINI MRADI WA INGA  Mitambo mikongwe kwenye bwawa la Inga ambalo Benki ya Dunia imekubali kulidhamini

Mitambo mikongwe kwenye bwawa la Inga ambalo Benki ya Dunia imekubali kulidhamini
Benki ya Dunia imeridhia kutoa dola milioni 73 kuisaidia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mpango wake wa ujenzi wa bwawa la Inga, ambalo ndilo kubwa kabisa duniani la kuzalisha umeme kutumia nguvu ya maji.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Benki ya Dunia, fedha hizo dola milioni 73 zikichanganywa na zengine dola milioni 33 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika, zitasaidia kufadhili utafiti wa kiufundi kuchunguza hali ya mazingira karibu na eneo la bwawa na kuhakikisha mradi huo ni endelevu.
Fedha hizo pia zitasaidia kuzindua usimamizi wa maendeleo ya Inga unaojitegemea ambao unatarajiwa kufuata mfumo mzuri wa Kimataifa katika kuuendesha mradi huo, na hata kuteua mashirika binafsi yatakayosaidia katika kuufadhili zaidi mradi wa bwawa la Inga.
Bwawa la kuzalisha umeme la Inga ndilo kubwa zaidi duniani

Hata hivyo, Benki ya Duinia imeiorodhesha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kama moja ya maeneo 10 yaliyo magumu kufanyia biashara. Kwa miongo kadhaa sasa miradi ya kulipanua bwawa hilo la Inga imeshidnwa kutokana na migogoro na vita vinavyotokea mara kwa mara nchini humo, huku wanamazingira wakionya kuwa mipango ya mabwawa makubwa inajulikana kwa kucheleweshwa kwa muda mrefu na kuwa na gharama kubwa.
Benki ya Dunia inakadiria kuwa Kongo itakuwa na uwezo wa kutoa takribani jigawati 100 ya nguvu za umeme, ikiwa ni ya tatu duniani baada ya China na Urusi. Lakini ni asilimia 9 pekee ya idadi ya raia wa Congo milioni 65 walio na uwezo wa kupata umeme huku katika sekta ya madini inayochangia kiwango kikubwa cha uchumi wa nchi hiyo uhaba wa umeme ukisalia kikwazo kikubwa.
Ramani hii inaonyesha njia ndefu ya kusafirisha umeme kutoka Inga hadi Afrika Kusini
Lakini kwa sasa mpango wa Afrika Kusini kununua umeme kutoka Inga, umefufua mazungumzo ya mradi huo mkubwa. Kwa sasa mashirika matatu makubwa ya kimataifa yanapigania kandarasi ya kujenga bwawa hilo linalojulikana kama Inga ya tatu, na kuuza nguvu ya umeme inayopatikana inayokadiriwa kuwa megawati 4,800.
Hii ni takriban mara tatu ya nguvu ya umeme iliyokuwa inatolewa kwa mabwawa mawili ya Inga, yalioko kwa muda mrefu sasa na yalioharibiwa kutokana na madeni ya serikali ya Congo na wafanyabiashara walioogopa kuwekeza katika miradi hiyo.
Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Congo, Augustin Matata Ponyo, ametoa taarifa akisema kuwa mradi wa Inga ni mradi unaoweza kuibadilisha Afrika katika karne hii ya 21.
Wakati huo huo kundi moja liitwalo International Rivers limeukosoa mpango huo kwa kutokuwa na manufaa zaidi kwa raia wa nchi hiyo na kutoa wito kwa Benki ya Dunia kufadhili mipango midogo ya kawi kama ya umeme wa kutumia jua ambayo limesema haitadhuru mazingira kwa kiwango kikubwa.
dw.de/swahili (R.M)

MAN U YAPANGWA NA BAYERN,CHELSEA NA PSG

 UEFA Champions League Quarter Final Draw: LIVE

Manchester United imepangwa kucheza na Bayern Munich katika michuano ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya huku Chelsea ikipangwa kukutana na Paris St-Germain.
Mabingwa wa ligi ya Uhispania, Barcelona watapambana na Atletico Madrid, huku Real Madrid ikipangwa kukutana na Borussia Dortmund.
Mechi zao za mzunguko wa kwanza zitaanza tarehe 1 mpaka 2 mwezi Aprili na marudiano yatakuwa tarehe 8-9 Aprili.
Fainali ya michuano hiyo itachezwa katika uwanja jijini Lisbon wa Estadio da Luz tarehe 24 mwezi Mei.
Manchester na Bayern wanakutana tena tangu mwaka 1999 kwenye fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa, ambapo Ole Gunnar Solkjaer na Teddy Sheringham waliiwezesha Manchester kutwaa kikombe chini ya Kocha wao Alex Ferguson.

Mara baada ya kupangwa kwa timu hizo nchini Switzerland, kiungo mshambuliaji wa Bayern, Philipp Lahm amesema kuwa hawawezi kutetereshwa na nafasi waliyonayo United kwa sasa katika ligi kuu na kusema kuwa watasafiri mpaka Manchester kwa kazi moja tu, nayo ni kufunga magoli.
Chelsea inayoongoza kwenye msimamo wa ligi itaifuata PSG nchini Ufaransa katika mzunguko wa kwanza.
bbcswahili (R.M)

Mazungumzo ya amani Sudan Kusini yacheleweshwa 

 Wawakilishi wa waasi wa Sudan Kusini wakizungumza na mwakilishi wa Marekani kwa Sudan Kusini, Donald E. Booth

Serikali ya Sudan Kusini imeweka wazi kuwa haitaki kushiriki katika utaratibu wa amani kama kundi la viongozi wa zamani wa kisiasa wenye vyeo vya juu ambao serikali iliwakamata baada ya mapigano kuzuka mwezi Disemba watajiunga na mazungumzo kama kundi la tatu.
Waziri wa zamani na mfungwa wa kisiasa, Deng Alor alisema bila ya kundi hili migawanyiko ya kisiasa katika serikali ya Juba ambayo ilisababisha mapigano kuendelea basi hakutakuwa na amani. " tatizo lilianza ndani ya mfumo wa kisiasa, lilianza na sisi kundi la tatu. Tunatofautiana juu ya masuala ya mageuzi na demokrasia katika chama. Tulisisitiza juu ya mageuzi. Kama unataka kutatua mzozo huu unatakiwa kusuluhisha tofauti ndani ya chama tawala".

Baada ya zaidi ya miezi mitatu ya mapigano mafanikio pekee ya utaratibu wa amani yaliyopatikana ni sitisho la mapigano ambalo limekuwa likikiukwa mara kwa mara tangu mwezi Januari.
Wanadiplomasia wa kimataifa wanaishiwa na ustahmilivu na wiki hii waliwaonya wadau wote huko kutakuwa na madhara kwa wale ambao wanavuruga maendeleo. Alisema mwakilishi maalumu wa Marekani kwa Sudan Kusini, Donald Booth. "Kama serikali au mtu mwingine yeyote anajaribu kudumaza utaratibu wa amani na kuwakejeli viongozi wa nchi wanachama wa IGAD, watakabiliwa na madhara. Watu wa Sudan Kusini wanatarajia kufanyika tena kwa mashauriano. Wanatarajia sauti zao zitasikika katika kusukuma mbele amani endelevu. Biashara kama kawaida siyo njia muafaka ya kusonga mbele".
Jenerali Taban Deng Gai anaongoza mashauriano kwa upande wa upinzani unaomtii Makamu Rais wa zamani, Riek Machar. Anasema kwamba kinyume na serikali ya Rais Salva Kiir wao wapo tayari kwa mazungumzo na wahusika wote.
Voaswahili (R.M)

Vitu vinavyoelea Bahari ya Hindi huenda vikawa mabaki ya ndege ya Malaysia

Indonesia Malaysia Plane
Waziri mkuu wa Australia Tony Abbott ameliambia bunge kwamba picha za setaliti zinaonesha vifaa vinavyo fanana na mabaki ya ndege ya Malyasia iliyopotea nje ya pwani ya kusini magharibi ya Australia katika eneo kusini ya Bahari ya HIndi.
Bw. Abbott anasema ndege ya kijeshi imepelekwa katika eneo hilo na inatazamiwa kuwasili Alhamisi mchana saa za Austrlia, na ndege nyingine tatu zitapelekwa kuanza uchunguzi wa kina kutafuta eneo hilo.
Hata hivyo Bw Abbot alionya kwamba kazi za kutafuta na kupata vyombo hivyo inaweza kua ngumu na huwenda visihusiane na ndege hiyo nambari MH370.
Voaswahili (R.M)

Libya yaomba msaada UN kupambana na ugaidi 

Waasi chini ya kiongozi wa waasi Ibrahim Jathran wakiwa kwenye eneo la mafuta la al-Ghani.
Libya inaiomba jumuiya ya kimataifa kuisaidia kupambana na kile inachosema ni vita dhidi ya ugaidi.
Katika taarifa iliyosambazwa Jumatano jioni serikali ya muda nchini humo ilisema inaomba hususan msaada wa Umoja wa Mataifa katika kutokomeza ugaidi kutoka miji ya Libya. Ilisema makundi ya ugaidi yanaendesha operesheni zake huko Benghazi, Sirte na maeneo mengine.
Benghazi ilikuwa eneo lililotegwa bomu ndani ya gari siku ya Jumatatu tukio ambalo liliuwa watu wasiopungua saba.

Serikali imekuwa ikipambana na vitisho vya usalama tangu kuondolewa kwa Moammar Gadhafi mwaka 2011. Makundi mbali mbali ya wanamgambo ambayo yalisaidia kuondolewa kwa kiongozi wa muda mrefu nchini humo yanaendelea kuendesha operesheni zao kwenye maeneo makubwa ya Libya ikiwemo huko mashariki mwa Libya ambako wamechukua udhibiti wa maeneo makubwa.
Viongozi wa muda wameyaagiza majeshi maalumu nchini Libya kukamata tena bandari katika wiki kadhaa zijazo.
Jumatatu kikosi maalumu cha Marekani cha NAVY SEAL kilichukua udhibiti wa lori moja la mafuta ambalo lilijaza mafuta ghafi kutoka bandari inayoshikiliwa na waasi ya As-Sidra kabla ya kuvamia majeshi ya Libya kwenye eneo la kuingia maji ya kimataifa karibu na Cyprus.
Libya inasema waasi hawawezi kuuza kihalali mafuta nchini humo lakini kupoteza udhibiti wa bandari huko mashariki kumezorotesha serikali kuwa na uwezo wake wenyewe wa kuuza mafuta na kusababisha usafirishaji wa nje kushuka kwa asilimia 80.
Umoja wa Mataifa ulijibu juu ya hali hiyo hapo Jumatano kwa azimio la Baraza la Usalama kupiga marufuku uuzaji usio halali wa mafuta ghafi kutoka Libya. 
Voaswahili (R.M)

DAKIKA 155:46 ZA HOTUBA YA RAIS JAKAYA KIKWETE KWA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA


 Rais Jakaya Kikwete, akiwahutubia Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba leo katika ukumbi wa Bunge mjini Dodom, ambapo katika hotuba yake ametumia dakika 155:46, kwa kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yahusuyo muundo wa Katiba mpya ikiwa ni pamoja na kufafanua kuhusu shinikizo la muundo wa Serikali tatu na mambo kadhaa ya Muungano.

 Wajumbe wakinyanyuka kwa pamoja na kupiga makofi kumshangilia Rais Jakaya, baada ya kukonga kwa Speech yake.

 Sehemu ya Wajumbe waliohudhuria .....

 Sehemu ya Mabalozi waliohudhuria ufunguzi huo wa Bunge la Katiba katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo jioni.

 Mama Maria Nyerere (katikati) Mama Siti Mwinyi (kushoto) na Mama Salma Kikwete, wakiwa ukumbi  humo wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete.

 Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal (kushoto) Mama Tunu Pinda na Mama Asha Seif Balozi, pia wakifuatilia hotuba hiyo kwa makini.

 Rais Jakaya Kikwete, akikagua gwaride maalum kabla ya ufunguzi rasmi wa Bunge hilo.

Badhi ya waandishi wa habari wapiga picha wakiwa bize.

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta na Makamu wake, Samiah Suluhu, wakijadiliana jambo wakati wakisubiri kuwapokea viongozi.

Waandishi na watu mbalimbali wakiwa nje ya ukumbi huo wakati wa maopokezi ya viongozi mbalimbali.

Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu, akiwasili kwenye viwanja vya bunge.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye viwanja vya Bunge.

Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta, akiwasili kwenye viwanja vya Bunge.

Baadhi ya waandishi.....

James Mbatia akiwasili na mjumbe mwenzake....Picha zote na Ofisi ya Makamu wa Rais.(P.T)