POLISI WASTUKIA DILI LA KUMUUA JUSTIN BIEBER
|
Justin Bieber |
|
Watuhumiwa wanaoshikiliwa na polisi kwa kupanga kumuua Justin Bieber, Tanner Ruane (kushoto) na Mark Staake |
|
Justin
Bieber akiwa na mama yake Pattie Malette wakati wa tamasha la 40th la
kila mwaka tuzo za American Music Awards kwenye Ukumbi wa Nokia Theatre
mjini Los Angeles, California Novemba 18, 2012.
WAPELELEZI wamestukia mpango wa mfungwa
wa mauaji wa kutaka kumuua na kukata maungo nyeti ya muimbaji kijana
Justin Bieber, mtandao wa habari wa KRQE news umeripoti.
Kwa
mujibu wa tovuti hiyo, Dana Martin -- ambaye hivi sasa anatumikia
vifungo viwili vya maisha mjini New Mexico kwa kumbaka na kumuua binti
wa umri wa miaka 15 huko Vermont miaka 12 iliyopita -- alimkodi mfungwa
mwenzake katika gereza la Las Cruces amsaidie kufanya mfululizo wa
mauaji, mojawapo yakiwa mauaji ya muimbaji wa "Beauty and the Beat".
Maafisa
wa polisi wamesema mfungwa aliyoachiwa kutoka gerezani hivi karibuni
Mark Staake na mpwa wake Tanner Ruane walikuwa wamuue nyota huyo wa pop
wakati wa onyesho lake ambalo limeuza tiketi zote kwenye ukumbi wa
Madison Square Garden mjini New York City mwezi Novemba. Mpango ulikuwa
kumnyonga nyota huyo mtoto pamoja na mabodigadi wake kwa kutumia tai, na
kisha kuwakata maungo yao ya uzazi.
Kabla ya tukio hilo la
kinyama kufanywa, Staake alikamatwa mjini Vermont. Hata hivyo, Martin --
ambaye mtandao wa KRQE umesema ni mtu "anayempenda kupindukia" Bieber
na amejichora tattoo ya muimbaji huyo kwenye mguu wake -- aliharibu
mpango mwenyewe na kuwasimulia polisi kila walichopanga. Wapelelezi
baadaye walirekodi simu baina ya Martin na Ruane ambazo wawili hao
walikuwa wakijadilia mauaji hayo.
Ruane anashikiliwa na polisi wa New York, ambao walikuta zana zote zilizopangwa kutumika katika mauaji hayo wakati akikamatwa.
Meneja
wa Bieber, Scooter Braun, alizungumza na gazeti la Us Weekly kuhusu
mpango huo wa shambulizi, akisisitiza kwamba usalama wa muimbaji huyo ni
jambo linalopewa umuhimu wa kwanza na timu yake.
"Tunachukua kila tahadhari kumlinda na kuhakikisha usalama wa Justin na mashabiki wake," Braun aliliambia gazeti la Us. |
|
|
No comments:
Post a Comment