KAMBI YA MISS UTALII KUANZA
Jumla ya warembo Sitini
(60) kutoka nchi nzima na vyuo vikuu watakao shiriki fainali za Miss Utalii
Tanzania 2012/2013 wanatarajia kuanza kambi Rasmi Tarehe 19.12.2012 katika
hoteli ya kitalii ya Ikondolelo Lodge iliyopo kibamba Dar es salaam.
Wakiwa katika kambi kwa siku ishirini na moja , warembo hao watashindana kuwania taji la taifa
la Miss Utalii Tanzania , na tuzo mbalimbali za kijamii kitalii kitamaduni na
kiuchumi. Zikiwemo tuzo za Mazingira, utalii wa ndani, wanyama pori,hifadhi za
Bahari, Mitindo, urembo, maziwa makuu, SADEC, Afrika Mashariki, umoja wa Afrika Afya ya jamii, Jinsia wanawake na watoto,
Rushwa, uwekezaji, Madawa ya kulevya, mazao ya biashara, madini , uchukuzi na
Miundombinu mbalimbali ya utalii.
Washiriki pia
watajifunza stadi mbalimbali za maisha , Mbinu za utangazaji utalii na bidhaa
mbalimbali za Tanzania, Pia mbinu za kuhamasisha kampeni dhidi ya uharibufu wa
mazingira, tamaduni kongwe na potefu, kupenda kutumia huduma za Tanzania (
Madre in Tanzania), uvuvi haramu, amna uwindaji haramu.
Washindi wa fainali
hizo za taifa watawakirisha fainali mbalimbali za kitaifa na kimataifa yakiwemo
ya, Miss Tourism world, Miss Tourism HeritageWorld Miss Tourism University
World, Miss Tourism Uniterd Nation,International Miss tourism World, Miss
Global International.
No comments:
Post a Comment