MWENYEKITI WA CHADEMA UK CHRIS LUKOSI AMEVULIWA MADARAKA NA KUSITISHWA UANACHAMA
Ikiwa ni takribani miezi minne tangu tawi la CHADEMA UK
lifunguliwe rasmi na Mr Godbless Lema, kumekuwepo na maendeleo makubwa ya
ujenzi wa tawi hili lakini vile vile kumekuwepo na changa moto mbali mbali
kutokana na uelewa wa watu ktk dhana nzima ya M4C. M4C ikiwa na maana ya
Movement for Change, ni sharti mtu yeyote anayeingia ktk movement hii kwenye
ngazi ya uongozi aelewe haya machache ya msingi:
1) Kwanza aone matatizo
yanayomgusa yeye na jamii yake
2) Ajue na kutambua fika
chimbuko la matatizo haya
3) Awe tayari kuwa kiini
cha mabadiliko ya kweli anayoyataka kwa jamii
4) Aweze kutoa ufumbuzi
kwa kukemea maovu, kuelimisha na hata yeye binafsi kuelimika
5) Ili afanikiwe ktk
kipengele cha (4) ni sharti ajitambue yeye binafsi ya kwamba ni:
i) Lazima awe safi na
mwenye sifa za kukemea waovu
ii) Aweke maslahi ya jamii
mbele na si yake binafsi
iii) Awe na sifa za uongozi
zinazotakiwa, nidhamu ikiwa nambari moja ktk orodha.
iv) Awe na msimamo wa
kiitikadi
Kwa hiyo, uongozi wa CHADEMA UK kwa baraka za watetezi wa haki
ya kweli (CHADEMA TZ) unawatangazia umma watanzania kokote mlipo kwamba kuanzia
leo
tarehe 12/12/12, Mr Christopher Lukosi amevuliwa rasmi uongozi na
amesitishwa uanachama kutokana na kutokidhi mengi ya yaliyotajwa hapo juu.
Uongozi wa CHADEMA UK unamshukuru sana kwa mchango na
ushirikiano wake mkubwa kwa kipindi ambacho matundu ya chujio yalikuwa makubwa.
Tutaendelea kumkumbuka na hata kutumia misemo yake yenye maana nzito kwa jamii
ya kitanzania, kama vile: -
i) Sisi sote ni ndugu,
tatizo ni CCM
ii) Kila kwenye msafara
wa mamba na kenge wamo
Uongozi unamwakikishia Mr Christopher Lukosi kwamba mamba wote
wa CHADEMA UK kwa kushirikiana na wote wenye kuelewa mageuzi ya kweli
,
tutaliondoa tatizo ifikapo 2015. Tunamtakia kila la kheli katika maisha na ni
imani yetu tutaendelea kuwa ndugu yake baada ya tatizo kutatuliwa !!!!.
“We fail in most of our endeavours because we too often
underestimate People’s Power” [M4C UK, 2012]
No comments:
Post a Comment