TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Thursday, December 6, 2012

JUA STORIA YA JACQLINE WOLPER VIZURI KATIKA SAFARI YAKE YA USTAA WA FILAM


ILI kufikia hatua ya maendeleo kwa kila mmoja inabidi juhudi zako mwenyewe zionekane , pamoja na watu wengine wanahitajika kukusapoti ili ndoto zako ziweze kutimia.Fuatana nami katika histori fupi ya Msanii mahiri nchini Jacquline Wolper .

Tofauti ilivyokuwa kwa wasanii wengi ambao wamefanikiwa kwa kutokea katika makundi, Jacquline Wolper hakuonja kabisa msoto  wamakundi. Alishauriwa, akathubutu na kuanza kufanya kweli kwenye soko la filamu nchini.
Ndoto yake ya kufanya masuala ya urembo aliyokuwa nayo tangu akiwa shule ya sekondari, ndiyo yaliyomfanya Wolper aangukie kwenye uigizaji baada ya kushawishiwa aingie kwenye gemu hilo.
 HISTORIA YAKE KIFUPI
Wolper alizaliwa Moshi December 6, 1988 na alijiunga na shule ya msingi Mawenzi mwaka 1994 - 2000 mkoani humo na kuhitimu elimu yake hiyo ya awali baada ya hapo Mwaka 2001 - 2004 alifanikiwa kumaliza elimu yake ya sekondari ijulikanoayo Masai Girls mkoani humo, akiwemo katika shule hiyo alifanikiwa kushiriki mashindano ya umisi,urembo na maonyesho ya mavazi, alipenda sana kuonekana mrembo. Baada ya hapo Wolper alijiunga na Chuo cha USA Contant mkoni humo na kusomea masomo ya biashara katika ngazi ya Diploma .
Kwa bahati mbaya hakuweza kumaliza masomo yake hayo ya chuo kutokana na sababubmbalimbali zilizokuwa nje ya uwezo wake na kulazimika kuhamia huku Dar.
Akiwa kwenye harakati za kutoka kimaisha, mwaka 2007 alikutana na msanii Lucy Komba aliyemshauri ajiunge na uigizaji, Wolper akakubali ndipo maisha ya sanaa yalipoanza rasmi.
“Hapo ndipo safari ya uigizaji ilipopamba moto. Nikapata nafasi ya kuigiza katika filamu ya Ama Zangu Ama Zao pamoja na kipande kimoja katika filamu ya Oprah,” anasema Wolper.
Kutoka hapo, sura ya Wolper ikapokelewa vyema na mashabiki, akapata mialiko katika filamu mbalimbali za wasanii wakubwa Bongo ikiwamo Red Valentine iliyoandaliwa na Kampuni ya Mtitu Game First Quality.
ASIMAMA MWENYEWE
Mwigizaji huyo ambaye tayari alijizolea umaarufu kupitia filamu mbalimbali za watu, hadi kufikia mwaka 2010 tayari aliweza kusimama na kuanzisha kampuni yake ya kuzalisha filamu iliyojulikana kama Line Wolper Production.
“Nakumbuka filamu yangu ya kwanza kuzalisha mimi kama mimi ilikuwa ni Candy kisha zikafuata nyingine ka
MAPENZI
Ukiachana na uhusiano ‘kishuleshule’, mapema mwaka huu Wolper alizama katika penzi zito la mfanyabiashara maarufu aitwaye Ramadhani Mtoro ‘Dalas’. Walidumu kwa miezi kadhaa, wakaachana hivi karibuni.
MAFANIKIO
Nje ya usafiri wa kutembelea, kuwasomesha wadogo zake na matumizi ya kila siku, kikubwa anachoshukuru ni kumiliki kampuni yake ya kuzalisha filamu.
ma My Princess, Mr No Body, Time After Time na nyingine nyingi,” anasema Wolper.

'Usikate tamaa katika maisha pambana utafanikiwa na pia muamini Mungu. '

No comments:

Post a Comment