UFAFANUZI WA AWALI KUHUSU KIKAO CHA KAMATI KUU YA CHADEMA
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
UFAFANUZI
WA AWALI KUHUSU KIKAO CHA KAMATI KUU YA CHADEMA
KAMATI
Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyoketi kikao chake cha
kawaida kwa siku mbili, Desemba 15-16, 2012, katika Hotel ya Blue Pearl, jijini
Dar es Salaam, imemaliza kikao chake Desemba 16, usiku.
Pamoja
na kwamba maazimio yote ya kikao hicho yatatolewa kwa umma kupitia vyombo vya
habari, Desemba 18, 2012, huu ni ufafanuzi wa awali kutokana na kuwepo kwa
taarifa zinazowakanganya wanachama na Watanzania kwa ujumla, zilizoandikwa tangu
jana Jumapili na Jumatatu, katika baadhi ya vyombo vya habari.
Mbali
ya kujadili masuala mbalimbali, ikiwemo kupokea taarifa ya hatua kadhaa za
utekelezaji wa maazimio yatokanayo na vikao viwili vilivyotangulia, Kamati Kuu
pia ilijadili hali ya siasa nchini, mchakato wa Katiba Mpya na Vuguvugu la
Mabadiliko (M4C).
Kamati
Kuu pia ilipokea taarifa ya mwenendo wa chama kutoka maeneo mbalimbali nchini,
ambapo ilijadili pia kasoro za utendaji wa viongozi wa chama katika Wilaya ya
Karatu.
Kamati
Kuu ilichukua uamuzi wa kusimamisha uongozi mzima wa Wilaya ya Karatu na kuweka
shughuli za utendaji wa chama chini ya uangalizi wa Kamati Kuu mpaka hapo
itakapotolewa maagizo mengine baadae.
Aidha,
Kamati Kuu pia ilipokea na kujadili mwenendo wa utendaji kazi wa baadhi ya
viongozi wa taasisi za kiserikali wanaotokana na CHADEMA, hasa katika masuala ya
ardhi na maji Wilayani Karatu.
Kikao
pia kilibaini kuwa taarifa zinazohusu masuala hayo ya maji na ardhi ni tofauti
na namna zilivyoripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari. Aidha kutokana na
mjadala, iliazimiwa hatua kadhaa zichukuliwe, ambazo umma utaarifiwa katika
tamko la Kamati Kuu litakalotolewa kupitia waandishi wa habari.
Imetolewa
leo, Desemba 17, 2012, Dar es Salaam na;
Tumaini
Makene
Ofisa
Mwandamizi wa Habari
CHADEMA
No comments:
Post a Comment