WAKILI: KORTI ILIKOSEA KUMVUA LEMA UBUNGE
Na :James Magai
WAKILI wa Serikali Mkuu Timon amedai kuwa Mahakama Kuu Kanda ya 
Arusha ilikosea kutengua ubunge wa aliyekuwa Mbunge wa Arusha mjini, 
Godbless Lema, kwa madai ya kutumia lugha za matusi kwa kuwa Bunge 
limeruhusu wanasiasa kutukanana kwenye kampeni.
                
              
Wakili Vitalis alitoa madai hayo jana, wakati wa 
usikilizwaji wa rufaa ya Lema, aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),katika Mahakama ya Rufani 
jijini  Dar es Salaam.
                
              
Wakati wakili huyo wa serikali akitoa madai hayo, 
Wakili wa wajibu rufaa, ambao walishinda katika kesi ya msingi, Alute 
Mughway, naye alidai kuwa Mahakama Kuu, Arusha ilikosea katika uamuzi 
wake, pamoja na mambo mengine, kwa kukataa baadhi ya madai yao.
                
              
Lema alivuliwa ubunge April 5, 2012, katika hukumu
 iliyotolewa na Jaji Gabriel Rwakibalia, kufuatia kesi iliuyofunguliwa 
makada watatu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mkanga, Happy Kivuyo 
na Agnes Mollel, wakipinga ushindi wake katika uchaguzi mkuu wa mwaka 
2010.
                
              
Lema kupitia kwa Wakili wake Method Kimomogoro 
alikata rufaa Mahakama ya Rufani, lakini Novemba 8, 2012 mahakama 
ilitupilia mbali rufaa hiyo baada ya kubaini kuwepo kwa dosari za 
kisheria, kutokana na pingamizi lililowekwa na upande  wa wajibu rufaa.
                
              
Hata hivyo mahakama hiyo ilimpa nafasi nyingine 
ya  kukata rufaa tena baada ya kumpa siku 14 kufanya marekebisho ya 
dosari hizo za kisheria na kuiwasilisha mahakamani ndani ya muda huo, 
amri ambayo aliitekeleaza.
                
              
Wakati Lema akikata rufaa kupinga hukumu ya 
Mahakama Kuu kumvua ubunge, wajibu rufaa nao walikata rufaa (Cross 
Appeal) kupinga uamuzi wa mahakama hiyo, huku wakibainisha hoja nne.
                
              
Katika hoja ya kwanza hadi ya tatu walidai kuwa 
Jaji alikosea katika hukumu yake kwa kuchanganya vituo vilivyotolewa 
ushahidi na mashahidi wanne na hatimaye akakataa ushahidi wapo, pamoja 
na tarehe za ratiba ya kampeni ya CCM nay a Chadema.
                
              
Hoja ya nne walidai kuwa Jaji alikosea kwa kuamua 
kuwa hata kama Lema kwenye kampeni zake alidai kuwa Dk. Buriani ni mkazi
 wa Zanzibar hatafaa, wakidai kuwa ukazi si sifa ya kuchaguliwa kuwa 
mbunge.
                
              
Hatimaye rufaa hizo zilisikilizwa jana na jopo 
la   Majaji watatu wa Mahakama ya Rufani, lililoundwa na Jaji Salum 
Massati, Jaji Bernard Luanda, chini ya uongozi wa  Jaji Nathalia Kimaro.
                
              
Wakati wa usikilizwaji wa rufaa hiyo, mawakili 
wawili ambao ni ndugu, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lisu na kaka 
yake Mghway, walipambana vikali kwa hoja za kisheria.
                
              
Lisu, Kada wa Chadema ambaye pia ni Mnadhimu wa 
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alikuwa akimtetea Lema mrufani (Lema), 
akisaidiana na Wakili  Method Kimomogolo, huku Mughway akiwatetea wajibu
 rufani ambao ni makada wa CCM.
Chanzo ni mjengwa blog 

No comments:
Post a Comment