TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Sunday, June 30, 2013

WAGHANA WAMLAANI NANDO WA TANZANIA KWA KUZINI NA DEMU WAO ( SELLY) NDANI YA BBA......MAMA MZAZI WA BINTI AMTETEA

 
Wiki iliyopita wapenzi Nando wa Tanzania na Selly wa Ghana  waliucheza ule mchezo wa kikubwa   katika Big Brother ‘The Chase’ inayoendelea, na inasemekana baada ya Ghana na Afrika kwa ujumla kushuhudia mechi hiyo ya kirafiki watu wa karibu na mpenzi wa Selly wamemshauri ampige kibuti.

Wote tunafahamu kwamba washiriki wote wa BBA wana maisha yao nje ya Big Brother na inawezekana kila mmoja anamahusiano huko alikotoka, lakini mission iliyowapeleka BBA ‘The Chase’ ni kushinda $300,000 inayomsubiri kinara mmoja, na ili kupenya njia nyembamba za kuufikia ushindi kila mmoja anajitahidi kufumba macho na kujisahaulisha kama camera ziko on ili aweze ku accomplish mission hiyo bila kujali njia anazotumia.

Baada ya video clip ya wapenzi wa BBA The chase Nando na Selly wakifanya mapenzi kusambaa ,baadhi ya watu wa karibu na boyfriend wa Selly wa Ghana wametoa maoni yao juu ya kitendo hicho cha ‘aibu’.

Steven Fiawoo maarufu nchini Ghana kama Praye Tiatia ndiye boyfriend wa Selly, na ni msanii maarufu nchini humo.
Praye na Selly
Kwa mujibu wa mtandao wa News One wa Ghana, CEO wa Record lebel ya nchini humo iitwayo Bull Haus Entertainment, Bull Dog ni kati ya watu ambao wametoa maoni yao juu ya kitendo alichokifanya shemeji yao ‘Selly’, na kusema kwamba kama yeye angekuwa Praye (something that will never be) angevunja mahusiano na Selly bila kujali sababu za kufanya hivyo.
“One thing I will note is that the BBA is just a game and there is no way I’m going to agree that my girlfriend or wife will go there and have sex in order to bring home that money. If I do that, then it means I’m lazy as a man and I’m unable to take care of my girlfriend or wife. Let us not forget the Praye Tiatia is a celebrity,” Alisema Bull Dog.

Katika Interview aliyofanyiwa na mtandao huo, Bull Dog alimshauri Praye aachane na Selly kwasababu yeye ni mtu maarufu na amemtia aibu kwa kiasi kikubwa kwa kufanya mapenzi na Nando huku karibia Afrika nzima ikishuhudia kupitia TV zao.
“Maybe if it was just a kiss I would have let it go but going to the extent of having sex? Not me, I won’t allow that because the whole world saw you giving it out willingly.” Aliongeza Bull Dog.
Kwa mujibu wa Ghana Web Mama mzazi wa Selly aitwaye Benedicta Galley amemtetea binti yake kuhusiana na maneno yanayozungumzwa na watu kwa kitendo alichokifanya.

 Akizungumza exclusive na kituo cha Peace FM, Mrs Galley alisema yeye haamini kama mwanae na Nando wali fanya  mapenzi, sababu alichokiona katika video ni wawili hao wamejifunika blanketi hivyo hata ‘biggie’ hana ushahidi wa kilichokuwa kinaendelea chini ya blanketi hivyo watu wasimhukumu binti yake.

“In the Big Brother house things are not that open especially about the romantic scenes for everybody to see that people are having sexy openly because everything is done under the blanket. We always see male and females together so for me I don’t think they had sex as it is being speculated all over”. Alisema.
Benedecta aliongeza kuwa amefurahishwa na kitendo cha boyfriend wa Selly, Praye Tiatia kukataa kutoa maoni yake kuhusu swala hilo na kuwa anamsubiri Selly atakaporudi 
Ghana ampe nafasi kuelezea ukweli wa kilichotokea.
 
Couple nyingine ambayo video clip ilivuja ikionesha wakikata kiu ya viungo viwili muhimu vya mwili ni Betty ambaye tayari ameshauaga mchezo pamoja na Bolt.

Friday, June 28, 2013

NAY WA MITEGO NA DIAMOND KUJA NA NGOMA MPYA..."SALAMU ZAO"

Baada ya kutamba na Muziki Gani, Diamond na Nay Wa Mitego wako mbioni kuachia ngoma nyingine hivi karibuni baada ya kupembua ipi ianze kati ya ‘Salamu Zao na Kwa Masela’.
Nay ameiambia mpekuzi kuwa kuna nyimbo tatu ambazo zipo tayari, Salamu Zao, Kwa Masela na Utakula Jeuri Yako, hawajajua ipi itaanza kutoka kwasababu kila mmoja yupo katika tour zinazoendelea. 
Wamesema wakikaa wakashauriana na wadau mbalimbali ndipo watakapoamua mzigo upi uingie mtaani kwanza.
“Kuna kazi ambazo zinakuja hivi karibuni ambazo nimefanya na Diamond lakini mpaka sasa hivi sijajua ni ipi ambayo itaanza kutoka lakini tutawaita wadau wachague ipi ianze kati ya ‘Salamu Zao na Kwa Masela’ ambazo zipo tayari na ‘Utakula Jeuri Yako’ nimefanya mwenyewe...
"Ilibidi tutoe nyimbo ambayo tumefanya na Diamond lakini mpaka sasa hivi hakuna maamuzi ya moja kwa moja tuitoe au kila mtu atoe ya kwake au tutaendelea na project yetu iliyoendelea, kwahiyo wadau wakae mkao wa kula,” amesema Nay.
RAIS OBAMA ANAELEKEA AFRIKA KUSINI
senegal 94b3a
RAIS wa Marekani Barack Obama leo Ijumaa anaelekea Afrika Kusini ambapo miongoni mwa shughuli zake atazuru kisiwa cha Robben Island  alikozuiliwa jela rais wa zamani Nelson Mandela kwa miaka 27.
Rais Obama anakwenda nchini humo wakati Mandela akiwa katika hali mbaya ya afya. Rais huyo wa zamani anatibiwa katika hospitali moja ya Pretoria.  
Alihamis rais Obama alisema ziara yake katika eneo ambalo watumwa wa Afrika waliondoka barani humo kwenda Amerika kaskazini imempa hamasa mpya ya kulinda haki za binadamu.
Obama alitembelea kisiwa cha Goree kwenye ufukwe wa Senegal Alhamis.   Wanahistoria wanasema maelfu ya Waafrika wanaume kwa wanawake wakiwa wamefungwa minyororo walishikiliwa huko na kupitia kile kilichoitwa mlango wa kutorudi tena kupanda meli ya watumwa wakielekea bahari ya Atlantic.  
Rais Obama alisema ziara yake katika kisiwa hicho ilimpa hisia kali na nafasi ya kutathmini upya biashara ya utumwa katika karne ya 16 na 19. Chanzo: Voaswahili
OBAMA AISIFU SENEGAL KWA DEMOKRASIA
obama 02bf1
RAIS wa Marekani Barack Obama ambaye yuko katika ziara yake ya Afrika, amesifu nchi ya Senegal kwa kuwa moja ya nchi zenye demokrasia thabiti barani Afrika.
Akiwahutubia waandishi wa habari nchini Senegal kwa mkondo wake wa kwanza wa ziara yake Afrika,baada ya mazungumzo na rais Macky Sall, Bwana Obama alisema kuwa Senegal iliandaa uchaguzi huru na wa haki pamoja na kuwa na kipindi salama cha mpito.
Pia aliisifu kwa kuwa na mtindo wa kusuluhisha migogoro kwa...
mazungumzo na mashauriano, wala sio kwa njia ya ghasia.
Alisema kuwa Afrika kama bara limepiga hatua kubwa upande wa demokrasia katika miaka ya hivi karibuni.
Obama atazuru Afrika Kusini ambako rais mstaafu Nelson Mandela anaugua sana na amelazwa hospitalini.
Aliwaambia waandishi wa habari kuwa wanamuombea Mandela pamoja na familia yake. Chanzo: bbcswahili
MEMBE:MSIJE DAR WAKATI WA ZIARA YA OBAMA
03 f39ab
Rais wa Marekani, Barack Obama
Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe amewashauri watu walioko mikoani kusitisha safari za kuja Dar es Salaam wakati wa ziara ya Rais wa Marekani, Barrack Obama kutokana na wingi wa wageni katika jiji hilo. Ugeni huo pamoja na ule wa viongozi kumi na moja kutoka nchi mbalimbali duniani watakaohudhuria mkutano wa kimataifa wa Smart Partnership utakaofunguliwa kesho na Rais Jakaya Kikwete kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, umesababisha kuimarishwa kwa ulinzi katika maeneo mbalimbali hasa katika hoteli za kitalii ambazo zimeanza....
utaratibu wa upekuzi kwa wageni wake.
Akizungumza na katika mahojiano na Redio ya Clouds jana, Membe alisema jiji limefurika kwa wingi wa wageni.
“Hoteli na nyumba za wageni zimefurika wageni na magari mengi yamekodiwa. Kwa ujumla, huduma za kijamii zitakuwa shida,” alisema.
Rais Obama na mkewe Michelle watawasili nchini Jumatatu na tayari wapambe na maofisa usalama kutokana Marekani wameanza kuwasili. Mbali ya ujio huo, wake wa marais kutoka nchi 14 za Afrika watakaokutana na Laura Bush, mke wa Rais wa zamani wa Marekani, George Bush. Pia Michelle atahudhuria mkutano huo utakaofanyika Jumanne na Jumatano ijayo.
“Jiji la Dar es Salaam litakuwa na mambo mengi kwa hiyo wale wenye kuja kutaka kustarehe wafute safari zao,” alisema na kuongeza: “Kama kuna watu ambao hawapo Dar es Salaam na hawana sababu za kuja mjini waache tu mpaka wageni watakapoondoka kwa sababu jiji la litakuwa limejaa na baadhi ya barabara zitachukuliwa zitumike na wageni hao.”
Alisema katika kipindi cha siku tano zijazo, baadhi ya barabara za Jiji la Dar es Salaam zitakuwa na shughuli nyingi na nyingine zitalazimika kufungwa. Barabara itakayofungwa ni pamoja na ile ya Mwai Kibaki na ile ya Bagamoyo itakuwa na shughuli nyingi pia wakati Michelle atakapokwenda Jumba la Makumbusho, Jumanne ijayo.
Wasafiri wa mikoani
Wasafiri wa mikoani wataathirika zaidi Jumanne ijayo wakati Rais Obama atakapokwenda kutembelea mitambo ya kufua umeme ya Kampuni ya Symbion Ubungo.
Kituo hicho kipo Barabara ya Morogoro, ambayo ndiyo inayotumiwa na magari yanayoingia na kutoka mikoani.
Rais Obama atakwenda katika kituo hicho yapata saa 4.00 asubuhi na kwa kiasi kikubwa itaathiri magari ya usafirishaji wa mizigo na abiria yatakayokuwa yanatoka na kuingia Dar es Salaam kabla na wakati huo.
Wengine watakaoathirika ni wakazi wa Kimara, Mbezi, Kibamba hadi Kiluvya. Athari nyingine ya usafiri itakuwa katikati ya jiji ambako Obama na msafara watakuwa na shughuli nyingi na hasa ile ya ufunguzi wa barabara karibu na Ikulu na kukutana na wafanyabiashara kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, Jumatatu ijayo.
Watumiaji wengine wa barabara watakaopata shida ni wale wa Barabara ya Bagamoyo hasa pale Rais Obama na mkewe watakapokwenda kuweka mashada ya maua kwenye ubalozi wa zamani wa Marekani uliopuliwa na mabomu mwaka 1998.

Ulinzi hoteli za kitalii
Mashushushu wa ndani na nje ya nchi wamezingira kwenye hoteli kubwa za Dar es Salaam na walionekana katika baadhi ya hoteli hizo, wakiwatumia mbwa maalumu kufanya ukaguzi wa chumba hadi chumba.
Tofauti na utaratibu uliozoeleka, baadhi ya hoteli zenye hadhi ya nyota tano zimeanza kutumia mitambo maalumu ya kompyuta kuwafanyia ukaguzi wageni wote wanaoingia.
Wamchongea JK
Mtandao wa Kutetea Waandishi wa Habari Duniani (CPJ), umemwandikia barua Rais Obama ukimtaka kujadiliana kwa kina na mwenyeji wake Rais Kikwete wakati wa ziara yake nchini kuhusiana na vitendo vya kuuawa na kuteswa kwa waandishi wa habari wa Tanzania.
Katika barua hiyo iliyosainiwa na Mtendaji Mkuu wa CPJ, Joel Simon na nakala yake kusambazwa kwa viongozi mbalimbali akiwemo Rais Kikwete mwenyewe, mtandao huo ulitolea mfano wa kuuawa kwa Mwandishi wa Channel 10, Daudi Mwangozi na Issa Ngumba wa Redio Kwizera. Pia kupigwa na kuteswa kwa Mhariri Mtendaji wa Habari Corporation, Absalom Kibanda.
Marais waja Smart Partnership
Akizungumzia mkutano wa Smart Partnership utakaoanza kesho, Membe alisema utajadili jinsi ya kutumia sayansi na teknolojia kukuza uchumi.
Viongozi watakaohudhuria mkutano huo ni Waziri Mkuu wa Malayasia, Najib Razak, Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Uhuru Kenyetta (Kenya), Boni Yayi (Benin), Ali Omar Bongo (Gabon), Ikililou Dhoinine (Comoro), Faure Gnassingbe (Togo), Ernest Koroma (Sierra Leone), Blaise Compaore (Burkina Fasso), Mahinda Rajapaska (Sri Lanka) na Mfalme wa Swaziland, Mswati II, ambaye aliwasili jana. Chanzo: mwananchi

Thursday, June 27, 2013

MISS REDD'S KANDA YA NYANDA ZA JUU KUPATIKANA LEO



Kinyang’anyiro cha kumpata Miss Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kinatarajiwa kufanyika kesho katika ukumbi wa Mikutano wa Mtenda SunSet uliopo Soweto Jijini Mbeya.   Mratibu wa Shindano hilo Fredy Herbet, amesema baada ya warimbwende kutoka Mikoa yote inayounda Kanda kukaa kambini tangu Juni 25, Mwaka huu na kupata mafunzo mbali mbali wanatarajia kuivunja Juni 29, Mwaka huu baada ya Msindi kupatikana.   Ameongeza kuwa Shindano hilo limeandaliwa na Lake Victoria Arts & Culture Promotion chini ya Udhamini wa TBL kupitia kinywaji chake cha
REDDS, SBC kupitia  Mountain Dew, Man Company, My Choice Botique, Ebony Fm na Bomba Fm radio.   Amesema kinyang’anyiro hicho kitasindikizwa na burudani kutoka kwa bendi ya FM Academia ya Jijini Dar Es Salaam na kuongeza kuwa kiingilio kitakuwa  shilingi 10,000/= kwa watu wa kawaida na 25,000/= kwa VIP.   Amewataja washiriki wanaong’ang’ania kuibuka kidedea kwa kuiwakilisha Kanda katika shindano la kumpata Miss Tanzania Mikoa wanakotoka kwenye mabano na namba aliyoshinda Mkoani kwake  kuwa ni pamoja na Lina J. Allan (Rukwa 1), Aneth B Mapugilo(Mbeya 2), Jesca Mikambi(Katavi 2), Nuru Baraka ( Katavi 1) na Neema Mality (Iringa 1).   Wengine ni Lucy George (Iringa 3), Nuriath Suleiman (Njombe 1), Evamary Gamba( Rukwa 2) Lilian Samson (Iringa 2), Naba Magambo (Mbeya 4), Jacklin J Luvanda (Mbeya 1) na Winfrida Felix Miss Njombe namba 2.   Kwa Upande wake Mwalimu wa Walimbwende hao Naomi Jones  ambaye ndiye anayeshikilia taji hilo amesema kambi iko vizuri na washiriki wote wanafuata maelekezo vizuri hivyo Majaji wawe makini kumtafuta Msindi kutokana na wote kuwa na sifa zinazofanana.
Picha na Mbeya yetu Blog
BFT:UCHAGUZI UTAFANYIKA JULAI 7
 MG 2400 28013
 Yah:- Uchaguzi wa viongozi wa BFT.
Uchaguzi wa viongozi wa BFT uliopangwa Kufanyika tarehe 7/7/2013 jijini Mwanza, utafanyika kwa tarehe hiyo kama ulivyopangwa.
Kikao cha kamati ya utendaji ya BFT kilichofanyika juzi katika  ofisi za BFT kikiongozwa na Rais wa shirikisho Joan Minja kimesisitiza kuwa uchaguzi utafanyika kama ulivyopangwa na haujaairishwa kama baadhi ya kikundi cha watu wachache wanaojiita wadau wanavyoweka pingamizi na  kupotosha  kwa kuwashawishi wajumbe wa mkutanao mkuu hasa kutoka mikoani kutohudhuria mkutano huo wa uchaguzi,kwa manufaa yao binafsi na kinyume na katiba yetu.
Upotoshaji huo unafanywa na  Akaroly Godfrey aliyekuwa  kiongozi katika uongozi uliojiudhuru kutokana na kashfa za kusafirisha madawa ya kulevya na kusababisha Tanzania kufutwa uanachama na chama cha ngumi cha dunia (AIBA) na kusababisha  kutoshiriki mashindano,mikutano na shughuri zote za kimataifa za chama cha ngumi cha Dunia AIBA. Naomba wadau na serikali kuwa makini na watu wanaoshawishi kwa lengo la masilahi yao binafsi na kusababisha michezo kudolola badala ya kusonga mbele.
Fomu za uchaguzi zilishaanza kutolewa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) toka tarehe 4//2013 na zitaendelea kutolewa hadi tarehe 4/7/2013 jijini Mwanza na tarehe hiyo  ndio itakuwa siku ya mwisho ya kuchukua na kurudisha fomu, tarehe 5/7/2013 itatakuwa siku ya usaili na utafanyika jijini mwanza, tarehe 6/7/2013 kupitia pingamizi na kuzitolea maamuzi na tarehe 7/7/2013 ndio siku ya uchaguzi.
Kimsingi taratibu zote za kuitisha uchaguzi kwa mujibu wa katiba yetu zimezingatiwa na zimekamilika.
Aidha BFT inatoa tamko kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu kufika katika uchaguzi uchaguzi, ili kupata viongozi halali kwa mujibu wa katiba, waendelee na shughuri za kuendeleza mchezo wa ndondi na kuaandaa timu ya taifa kushiriki katika mashindano ya Afrika nchini Mauritius Sept. 2013
BFT inatoa wito kwa watu wote wenye sifa, nia, moyo na uwezo wa kuongoza wajitokeze kuchukua fomu za kugombea uongozi kwani wakati ndio huu. 
Makore Mashaga
Katibu Mkuu.

Wednesday, June 26, 2013

OMMY DIMPOZ APATA SHAVU LA KUFANYA TOUR MAREKANI NA CANADA

Omary Fereji Nyembo a.k.a Ommy Dimpoz, amesaini mkataba na kampuni ya DMK Global Promotion leo hii kwa ajili ya tour atakayoifanya Canada na Marekani mwezi wa tisa mwaka huu baada ya kumaliza tour nyingine barani ulaya.

"Yaah nimesaini mkataba na nitaondoka kwenda kwenye tour hiyo mwanzoni mwa mwezi wa tisa, imekuwa hivyo kwasababu tunasubiri mwezi mtukufu upite si unajua tena, kampuni niliyosaini nayo inaitwa DMK global promotion ambayo ni ya mtanzania ambae anaishi marekani." amesema Dimpoz 

Alipoulizwa  kuhusu mkwanja alioingiza kwa mkataba huo, Dimpoz aligoma kutaja kiasi na kusema 

"aaaah unajua tena kwa matatizo yaliyotokea nikitaja tena na mkwanja nilioingiza si ndio itakuwa matatizo kabisa? .
TEVEZ KAMA MFALME ITALIA APATA MAPOKEZI MAKUBWA
tevez2 403cf
 Carlos Tevez kushoto akiwasili jijini Turin
 tevez4 7dfa1

tevez 2fa1b

tevvez3 90137

 MSHAMBULIAJI Carlos Tevez amewasili Italia na kupata mapokezi makubwa kuelekea uhamisho wake wa Pauni Milioni 10 Juventus kutoka Manchester City.

Mpachika mabao huyo wa Kiargentina alitua katika Uwanja wa Ndege wa Malpensa mjini Milan na kupokewa na umati wa mashabiki ambao mara zote hupenda kuwalaki nyota wao wapya.
Tevez, mwenye umri wa miaka 29, anataraji kusaini mkataba wa miaka mitatu jijini Turin baada ya vipimo vya leo huku makubaliano yakiwa yamefikiwa. Chanzo: Sportmail
SAFARI YA RONALDO KUREJEA MAN U YAIVA
ronaldo2 b06e8
CRISTIANO Ronaldo anaweza kurejea Manchester United baada ya kugundulika atakuwa na mkutano na viongozi wa klabu hiyo ya Old Trafford ndani ya siku tatu zijazo. 
Nyota huyo wa Real Madrid amekuwa akihusishwa na kurejea England baada ya kupitia msimu wa bila furaha Bernabeu, lakini ilitarajiwa kuwasili kwa kocha mpya, Carlo Ancelotti kungemfanya abaki Hispania. 
Na gazeti la Hispania, El Pais limeripoti kwamba nahodha huyo wa Ureno atakutana na viongozi wa Man u kabla hajaenda kuanza msimu mpya Madrid.

Kwa kuwa FIFA inazuia klabu kufanya mazungumzo na wachezaji walio ndani ya Mikataba na klabu zao, pande zote zimejipanga kukana kufanya mazungumzo, ambayo itamsaidia sana kocha mpya, David Moyes kuelekea msimu ujao.

Lakini Ancelotti amesema wakati akitambulishwa kuwa kocha mpya wa Madrid leo kwamba: "Cristiano ni mchezaji mkubwa na ninajivunia kufanya naye kazi. 

"Nimewakochi Zidane, Ronaldo na Ronaldinho, na ninajivunia kumuongeza na yeye.' 

Alipoulizwa kuhusu Radamel Falcao, mchezaji aliyekuwa anawaniwa na Madrid ambaye amesaini Monaco, Ancelotti alisema: "Ni mchezaji mzuri, lakini kuna Ronaldo, Higuain na Benzema,"alisema. Chanzo: binzubeiry

UCHAGUZI WA ARUSHA WAAHIRISHWA TENA ILI KUIMARISHA HALI YA AMANI NA UTULIVU


TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeahirisha tena uchaguzi wa madiwani kata nne za Arusha hadi Julai 14 kuruhusu kurejea utulivu baada ya mlipuko wa bomu kwenye mkutano wa kampeni wa Chadema ulioathiri uchaguzi huo wiki iliyopita.
Bomu hilo lilirushwa Juni 15 na mtu asiyejulikana katikati ya mkutano wa Chadema katika viwanja vya Soweto, mjini Arusha na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine kujeruhiwa na uchaguzi huo wa Juni 16 kulazimika kuahirishwa.
Baada ya tukio hilo, Msimamizi wa Uchaguzi wa Arusha aliuahirisha hadi Juni 30, lakini jana Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva alisema utafanyika Julai.
Kata zinazohusika ni Elerai, Kimandolu, Thani na Kaloleni. Akizungumza na waandishi wa habari, Jaji Lubuva alisema walipotangaza kuwa uchaguzi ungefanyika Juni 30 waliamini kuwa hali ya utulivu na amani ingekuwa imetengemaa.
“Lakini kwa bahati mbaya tumejiridhisha kuwa hali bado inahitaji kuangaliwa kuhakikisha imerejea katika utulivu wake kikamilifu. “Hiyo haimaanishi kuwa ni mbaya, isipokuwa tumeona bado tunahitaji muda wa kama wiki mbili hivi kuona vumbi lililokuwa likitimka limetulia,” Jaji Lubuva alisema.
Kwa mujibu wa Jaji Lubuva, wapiga kura hawapaswi kutekeleza haki yao ya kupiga kura katika wasiwasi hivyo ni wajibu wa Tume kuhakikisha unaondoka na wapiga kura wanatekeleza haki yao kwa amani.
“Tunataka watu wajihisi huru wakati wa kupiga kura, ndiyo maana tumeahirisha uchaguzi wa kata hizo kwa mara nyingine. Wanapokuwa na amani na uhuru wapiga kura wanaweza kuchagua wanayemtaka kwa utaratibu mzuri, vinginevyo, shughuli yote ya kupiga kura inaweza kuharibika,” alisema Lubuva.
Aidha, alitaka wagombea na vyama kutoendeleza kampeni kwa sababu kuahirishwa kwa uchaguzi hakumaanishi kuwaongeza muda wa kujinadi au kutafuta wapiga kura wa kuwaunga mkono.
“Muda wa kupiga kura haujabadilika. Vituo vya kupigia kura havijabadilika na vitafunguliwa saa moja asubuhi na kufungwa saa 10 jioni. 
Waliokuwa katika mstari ndio watakaopiga kura na watakaofika vituoni baada ya muda huo kwisha hawataruhusiwa kupiga kura ili kutoa nafasi ya kura kuhesabiwa,” alisema.
Jaji Lubuva alisema matokeo ya uchaguzi huo mdogo yatatangazwa mapema na taratibu za uchaguzi zitazingatiwa ili kutoa haki kwa wapiga kura na wanaopigiwa kura.
Inadaiwa bomu hilo lililokuwa kwenye mfuko wa plastiki, lilirushwa na mtu asiyejulikana. Waliopoteza maisha katika tukio hilo ni Amir Ally (7), Judith Moshi na Amir Ally.
Habari Leo:

ULINZI WA RAIS OBAMA JIJINI DAR NI BALAA....MITAMBO MBALIMBALI YA MAWASILIANO IMEFUNGWA UWANJA WA NDEGE WA KIA


Maandalizi ya ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama nchini yanazidi kupamba moto huku maofisa wa usalama wa Marekani wakipiga kambi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Aidha, kutokana na ujio huo, Serikali imeagiza mashirika yote ya ndege kubadili ratiba zao za safari Julai Mosi, siku ambayo Rais huo atatua nchini.

Jana, waandishi wetu walishuhudia pilikapilika za kuimarisha ulinzi katika uwanja huo jambo ambalo uongozi wa uwanja huo jambo wamelieleza kwamba halijawahi kutokea.

Ulinzi haujawahi kutokea
Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Moses Malaki alisema jana kwamba ratiba za uwanjani hapo zitabadilika kutokana na uzito wa ugeni huo.


Alisema kwa kawaida anapokuja kiongozi mkubwa wa kitaifa katika uwanja huo hakuna ndege inayoruhusiwa kutua kwa kipindi cha nusu saa.

“Ni kweli hali hiyo pia itakuwapo atakapokuja Rais Obama na safari za ndege zitabadilika kulingana na ratiba ya kutua na kuondoka kwa Rais huyo,” alisema Malaki.

Pia alisema ulinzi katika uwanja huo umeimarishwa kwa mwezi mmoja sasa na tangu wakati huo, maofisa wa usalama wa Marekani wamekuwa wakifika kwa nyakati mbalimbali.

“Sijawahi kuona ulinzi mkali kama huu, wamekuja marais wengi hapa nchini lakini ulinzi huu ni wa kutisha, sijui kwa sababu gani?” alisema Malaki.


Alisema awali, wakati maofisa hao walipoanza kuwasili nchini hawakutambua ni mgeni gani anayetarajia kufika lakini baadaye walipelekewa taarifa kuwa ni Rais Obama na baadaye walitaarifiwa kuwa angetua saa 8.40 mchana, Julai Mosi.


Mkurugenzi huyo alisema Rais Obama atakuja na ndege nne, moja itakayombeba, ya pili kwa ajili ya mizigo, ya tatu itakuwa ya waandishi wa habari na maofisa wa usalama na ya mwisho ni kwa ajili ya dharura ambayo itaegeshwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).


Malaki alisema maofisa wa Marekani wanaowasili nchini wamekuwa wakifanya shughuli mbalimbali za kuhakikisha kuwa hali ya usalama inaimarishwa na kuwaacha wazawa wakifanya shughuli za kawaida.


“Ulinzi ni mkali mno, yapo masharti kadhaa wanayoyataja kuwa yatatumika kwa watu watakaoingia eneo la uwanja au kuisogelea ndege ya Rais Obama. Jamaa wameweka masharti magumu,” alisema.


Mkurugenzi huyo alisema maofisa hao wanakuja kwa makundi na hivi karibuni lilifika kundi la kusimamia mawasiliano ambayo yatatumiwa wakati watakapokuwa nchini.

“Pia wamechukua kwa muda karakana ya Shirika la Ndege la Precision Air iliyoko kwenye eneo la Uwanja wa Ndege. Maofisa wa Usalama wa Marekani wanataka kufanya shughuli ndani mle,” alisema Malaki.

Pia, ndege mbovu zilizokuwa kwenye maeneo ya uwanja huo zimeondolewa. Viongozi wa Precision Air hawakupatikana kuzungumzia suala hilo.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Fadhili Manongi alisema ni utaratibu wa kawaida kwa karakana kuazimwa wakati wanapokuja wageni mashuhuri.

“Nafasi ile mara nyingi hutumiwa na maofisa wa usalama pale wanapokuja wageni mashuhuri kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere,” alisema.


Alidokeza pia pamoja na ugeni wa Rais Obama, pia kumekuwa kuna presha ya ugeni wa marais wa nchi mbalimbali duniani wanaokuja kuhudhuria mkutano wa Smart Partnership unaonza keshokutwa.

Pia wana kazi ya kuwapokea wake za marais wa Afrika watakaokutana na mke wa Rais Obama, Michelle na mke wa Rais wa zamani wa nchi hiyo, George Bush, Laura.
Kazi inayofanyika

Ofisa mmoja wa Uwanja Ndege ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema maofisa hao walifanya ukaguzi wa hali ya juu kwenye sehemu mbalimbali za uwanja huo wakitumia mitambo maalumu ya kung’amua mabomu.

“Hawa jamaa wako juu sana katika mambo ya usalama maana wana kifaa cha kuchunguza mabomu hata yaliyo chini ya ardhi,” alisema na kuongeza kuwa licha ya kukagua uwanja huo, pia walikwenda mbali zaidi na kukagua maeneo ya jirani.

Mitambo mbalimbali ya shughuli za usalama imefungwa kwenye eneo hilo la uwanja na maofisa wa Marekani walionekana wakiwa juu ya paa la moja ya majengo ya uwanja huo wakifunga mitambo katika minara mirefu kwa ajili ya kuimarisha mawasiliano.


Yavuruga ratiba za ndege
Manongi alisema kampuni za ndege zimeagizwa kufanya mabadiliko ya ratiba za safari siku atakapowasili Rais Obama ili kutoa nafasi kwa anga hilo kutumika kwa shughuli za mapokezi yake.

Alisema kampuni zote za ndege zimeshapewa taarifa kuhusu hatua hiyo.

“Kubadilishwa kwa ratiba kunatokea mara kwa mara na huwa tunawapa taarifa kampuni za ndege mapema ili wajue namna ya kujipanga,” alisema Manongi.

Kutua Senegal leo
Rais Obama anatarajiwa kuanza ziara yake ya barani Afrika leo na alitarajiwa kutua Dakar, Senegal saa 9.30 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki.

Akiwa nchini humo, ratiba inaonyesha kuwa atakuwa na mazungumzo na Rais wa Senegal, Macky Sall kwenye Ikulu ya nchi hiyo. Pia ratiba hiyo inaonyesha kuwa atakutana na majaji kutoka mikoa yote ya nchi hiyo.

Pia atakwenda katika Kisiwa cha Goree ambacho kiko kwenye Bahari ya Atlantic na atatembelea Jumba la Makumbusho katika kisiwa hicho ambacho kilikuwa kituo cha kuhifadhi watumwa waliokuwa wanasafirishwa kutoka Afrika kwenda Marekani.

“Baada ya shughuli hiyo, Rais Obama atahudhuria dhifa ya taifa kabla ya kupumzika kwa muda mfupi na kuanza safari ya kwenda Afrika Kusini,” ilisema taarifa hiyo ya Ikulu ya Marekani.

Mwananchi:

SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU KAULI YA WAZIRI MKUU...YADAI POLISI WANARUHUSIWA KUPIGA NA KUUA KISHERA


Serikali imetoa tamko bungeni kuhusu mauaji ya raia mikononi mwa polisi ikieleza kuwa sheria ya kanuni ya adhabu inaruhusu kutumia nguvu za kadiri hata kiasi cha kusababisha madhara au kifo.


Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kunukuliwa bungeni akiwataka polisi kuwashughulikia kwa kuwapiga watu wote wanaokaidi kutii sheria.

“…Nasema wapigwe tu, maana tumechoka sasa,” alisema Pinda alipojibu maswali ya papo hapo Alhamisi iliyopita.


Akisoma tamko hilo bungeni jana, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Ame Silima alisema kuwa kifungu cha 18(B) na 18(C) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu kinatoa uwezo kisheria wa kutumia nguvu za kadiri hata ikibidi kiasi cha kusababisha madhara au kifo katika mazingira ya kisheria.


Aliyataja mazingira hayo kuwa ni pamoja na kuokoa uhai wa mtu mwingine, kuzuia madhara makubwa ya mwili yasitokee kwake au kwa mtu mwingine na kumzuia mtu anayetenda tendo ovu la kubaka au kunajisi mtoto au kufanya vitendo kinyume na maumbile.

Pia kumzuia mtu anayevunja nyumba usiku au unyang’anyi wa kutumia silaha au kuchoma nyumba moto au kufanya kitendo chochote kinachohatarisha uhai wa mtu au mali.


Alieleza kuwa Kifungu cha 18 na 18(A) cha Sheria ya Adhabu Sura namba16 iliyofanyiwa mapitio mwaka 2002, kinampa haki mtu yeyote akiwemo askari kujilinda, kumlinda mtu mwingine, kulinda mali yake au mali ya mtu mwingine ikiwemo ya Serikali na taasisi zake, ambayo iko chini ya uangalizi wake kisheria.


Kauli hiyo ya Serikali kuhusu mauaji ya raia mikononi mwa polisi, ilitolewa ikiwa ni ufafanuzi wa jibu la swali la nyongeza lililoulizwa bungeni Mei 28,2013 na Rashir Ally Abdalah (Tumbe-CUF), ambapo Silima alisema mauaji yanayofanywa na askari polisi ni mauaji ya kisheria. 


Kutokana na kauli hiyo, Mbunge wa Wawi, Hamad Rashi Mohammed aliomba mwongozo wa spika kupata ufafanuzi wa kauli hiyo, na jana Silima kutoa kauli ya Serikali kujibu mwongozo huo.

“Ikumbukwe pia kuwa, kifungu cha 29 cha Sheria ya Jeshi la Polisi na Polisi wasaidizi Sura322, pamoja na Kanuni za Kudumu za Utendaji za Jeshi la Polisi Na274, vinampa haki ya kisheria askari polisi kubeba na kutumia silaha za moto ikiwamo bunduki na mabomu katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku..,”alisema Silima.


Alifafanua kwamba katika kutafsiri sheria, kanuni na taratibu mbalimbali ikiwamo alizozitaja, mahakama katika nyakati tofauti imetoa msimamo wa kisheria juu ya suala hilo.


Akitoa mfano alisema: “Mathalan katika kesi ya Seif Mohamed Senzagala dhidi ya Jamhuri ya mwaka 1994 kama ilivyonukuliwa na Tanzania Law Report ukurasa wa 122, ambapo mshitakiwa (mwomba rufaa) alimjeruhi kwa panga mlalamikaji ambaye alimfuata nyumbani kwake na kuanza kumshambulia.”


Alisema katika kesi hiyo,mahakama ya rufaa pamoja na kuridhia uamuzi wa mahakama ya awali wa kumtia hatiani kwa kutumia nguvu kupita kiasi, ilibainisha kuwa mshtakiwa hakustahili adhabu kwani alitenda kosa lile wakati akijihami dhidi ya mashambulizi toka kwa mlalamikaji.

“Kwa msingi huo, tarehe 28 Mei, 2013 wakati nikijibu swali Na 290, nilitumia maneno ‘mauaji yanayofanywa kisheria’ nikimaanisha mauaji yanayotokea katika mazingira niliyoeleza..,”alisema Silima.

Hata hivyo alisema siyo nia ya Serikali kuhalalisha vitendo vya matumizi mabaya ya silaha ambavyo vinaweza kufanywa na askari wasio waadilifu.

Alibainisha kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, kuheshimu haki za raia na kutumia busara kutatua migogoro.

Hata hivyo, Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni imelaani kauli ya Serikali kuhusu mauaji ya raia mikononi mwa polisi iliyoitoa jana na kueleza kuwa haikubaliani nayo kwa kuwa inatoa baraka kwa polisi kuendeleza mauaji ya raia.

Akizungumza na mwandishi wetu baada ya kikao cha bunge kuahirishwa, Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani wa kambi hiyo rasmi, Vicent Nyerere alisema kauli hiyo ingekuwa na uthabiti kama askari polisi wangekuwa waadilifu.


“Kauli ingekuwa thabiti kama polisi wangekuwa waadilifu. kabla ya kutoa kauli hiyo, Serikali ilitakiwa kuchuja miongoni mwa askari wa jeshi la polisi, wa ngazi zote na kuwaondoa wasio waaadilifu ndipo wakatoa kauli hiyo wananchi wataielewa Serikali,”alisema Nyerere ambaye pia ni Mbunge wa Musoma Mjini(Chadema).


Kwa upande wake, Mbunge wa Ole, (CUF) Rajab Mbarouk Mohammed akizungumzia kauli hiyo ya Serikali alisema kuwa majibu ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Ame Silima ni ya kisiasa.


Alisema kwamba kauli hiyo ni mwendelezo wa kauli iliyotolewa Alhamisi iliyopita na Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akiwataka pilisi kuwashughulikia kwa kuwapiga watu wote watakaokaidi kutii sheria.


“Hakuna mwenye haki ya kuua, kuua ni kuua tu. Mahakama pekee ndiyo ina haki ya kuhukumu kifo baada ya kumtia hatiani mshtakiwa husika. Lakini kuwa polisi wanafundishwa utii, siyo kuua,”alisema Rajab.

Alifafanua kuwa kazi ya polisi ni kulinda raia na mali zao na kwamba kuruhusiwa kujihami haimaanishi kuua raia.
Nao Wabunge Aeshi Hilaly na Aly Keissy walisema ni vizuri raia wakatii mamlaka iliyopo na kutekeleza utii wa sheria bila shuruti.

Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu alisema: “Maoni yangu haki za watuhumiwa lazima ziheshimiwe.”

Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, (TLS), Francis Stola alisema hakuna sheria inayompa mamlaka askari polisi kutumia nguvu za ziada ikiwemo kupiga raia pindi anapotekeleza majukumu yake,isipokuwa tu anaweza kutumia nguvu kiasi iwapo raia anayekabiliana naye anaonyesha vitendo vya kukaidi amri ama kuhatarisha usalama.


Stola ambaye alikuwa akitoa ufafanuzi wa kisheria kuhusiana na kauli bungeni alisema kuwa kwa kufuata sheria polisi haruhusiwi kupiga raia. “ Ukisoma sheria hakuna mahala utakuta kuna neno limeandika piga…. Askari polisi anachoweza kufanya ni arrest(kamata) na siyo vinginevyo, hana mamlaka kabisa ya kupiga raia”

Alisema sheria imetamka wazi kuwa kunapojitokeza hali yoyote inayopaswa kdhibitiwa na vikosi vya ulinzi, nguvu inayopaswa kutumika ni ile ya kawaida na kwamba kitendo cha kutumia risasi za moto ama kupiga raia ni ukiukwaji wa sheria za nchi.

Alisema polisi anapaswa kutoa mwongozo kwa raia kumwelekeza jambo la kufanya iwapo kunajitokeza hali ya sintofahamu,lakini hapaswi kutumia nguvu kupita kiasi ikiwemo kuwapiga raia

“ Sheria inasema wazi kwamba panapojitokeza hali yoyote korofi, polisi wanatakiwa kutumia nguvu ya kawaida tu kukabiliana na hali hiyo na wala siyo kutumia silaha za moto… silaha za moto zinaweza kutumika tu iwapo kunajitokeza tukio ambalo linaweza kuhatarisha usalama wa maisha ama mali isipotee” alisema

Kuhusu wananchi kufanya maandamano, rais huyo alisema maandamano ni haki ya msingi ya kila raia,lakini yanafanyika katika utaratibu maalumu. “ maandamano ni haki ya kila raia lakini panapaswa kuwa na utaratibu maalumu…. Kama kunajitokeza maandamano ambayo hayana utaratibu polisi wanapaswa kutumia reasonable force (nguvu ya kawaida) kudhibiti maandamano hayo na wala siyo kutumia nguvu za ziada.
 Mwananchi:

Tuesday, June 25, 2013

"TUTAIFUTA CHADEMA ENDAPO ITABAINIKA KUWA WALIRUSHA BOMU LA ARUSHA WENYEWE"....TENDWA

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini John Tendwa,  amedai kuwa ikibainika kuwa CHADEMA ndio waliohusika katika kulipua bomu katika mkutano wao wa 15/06/2013 atakifuta.
Tendwa  ameyasema   hayo alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Hot Mix cha East Africa Television akijibu swali la mtangazaji wa kipindi Adrian Stepp  kuhusu  hatua  zitakazochukuliwa...
Alipoulizwa kama itathibitika kuwa CCM ndio walihusika kulipua bomu hilo amedai kuwa hawezi kukifuta kwakuwa kwa kufanya hivyo itakuwa ni kufanya mapinduzi ya kalamu.
Source :Jamiiforum
CHELSEA YAFIKA BEI KWA CAVANNI,YALIPA PAUNI 49 KWA NAPOLI
20 6ff29
Mshambuliaji wa Uruguay na Napoli, Edinson Cavanni
10 7b966
KITUO cha Redio cha Napoli, Marte kimetangaza kwamba dau la Pauni Milioni 49.3 limetolewa na Chelsea kwa ajili ya mshambuliaji  Edinson Cavani ambaye muda wote anampasua kichwa mmiliki wa klabu ya Chelsea Bilionea Roman Abramovich mwenye lengo la kuimarisha kikosi chake chini ya kocha Jose Mourinho.
Katika taarifa ya jana usiku, Radio Marte ilitangaza: “Tumepokea taarifa kutoka ofisini kwa vyanzo vya kuaminika kwamba, Napoli imekubaliana dili la kuiuzia Chelsea Cavani.
“Rafa Benitez pia amebariki, lakini kabla ya kutangaza rasmi, Napoli inataka kupata mshambuliaji atakayeziba pengo la Il Matador.
“Aurelio De Laurentiis”, klabu itasomba kiasi cha Euro Milioni 58, sawa na dili la Ezequiel Lavezzi kwenda PSG mwaka jana.
“Mchezaji huyo atajiingizia mshahara wa Euro Milioni 8.5 kwa msimu pamoja na haki za picha,”. Habari zimevuja kama kwamba Cavani ametangaza anataka kukutana uso kwa uso na Rais, Aurelio de Laurentiis na kuna taarifa kwamba Manchester United nayo imo kwenye mbio hizo. 
Mshambuliaji huyo wa Uruguayna baba yake awali walionyesha nia ya kutaka kwenda Real Madrid. Klabu hiyo ya Hispani iliwasiliana na Napoli, lakini sasa itabidi waipiku ofa iliyotolewa na Chelsea. Chanzo: Baraka Mpenja
FELLAINI ATAKA PAUNI 100,000 KWA WIKI
article-2347673-18C30F23000005DC-982 634x4931 fa7ea
Marouane Fellaini anataka kujiunga na  Arsenal
KIUNGO Marouane Fellaini anataka kujiunga katika orodha ya wachezaji wanaolipwa Pauni 100,000 kwa wiki Arsenal, lakini The Gunners tayari imetenga dau kubwa kwa usajili mwingine.
Huku mshambuliaji wa Real Madrid, Gonzalo Higuain akiwa njiani kutua kwa dau la Pauni Milioni 22, The Gunners wataelekeza nguvu zao katika kuboresha safu ya kiungo.
 Fellaini ametokea kuwa mshindani mkuu wa nafasi mbele ya zoezi la Arsene Wenger kusaka kiungo, lakini dau kubwa linalotakiwa linaleta kama uhamisho huo utafanikiwa.
  Kutoka kikosi cha sasa cha Arsenal, ni Theo Walcott na Lukas Podolski peke yao wapo katika kiwango cha mshahara cha Pauni 100,000 kwa wiki.
 Mbali na kudai mshahara mkubwa, Arsenal pia watalazimika kufika bei anayouzwa Fellaini, Pauni Milioni 22- ambayo itafanya dili zima la usajili wake liendee kwenye Pauni Milioni 50. Chanzo: sportmail
MAREKANI YATOA ONYO KALI KWA MSAFARA WA RAISI OBAMA
obama1 51ff9
Rais wa Marekani, Barack Obama
LICHA ya ujumbe wa Rais wa Marekani, Barrack Obama kutarajiwa kufikia katika hoteli kubwa zenye hadhi wakati kiongozi huyo atakapowasili nchini Julai Mosi mwaka huu, Ikulu ya Marekani imetoa tahadhari ya vyakula ambavyo hawatakiwi kuvigusa wakiwa nchini ikiwa ni pamoja na kutumia maji ya bomba.
Mbali na tahadhari hiyo, ziara hiyo ya Obama itakuwa na ulinzi mkubwa ambao pengine haujawahi kutokea katika historia ya viongozi wa nje wanaotembelea Tanzania kwani utahusisha idadi kubwa ya magari, ndege za kijeshi na meli kubwa ya kivita ambazo zitakuwa zikifanya doria karibu na pwani ya Tanzania.
Tahadhari za matumizi ya chakula, maji na nyinginezo zimetolewa katika nchi zote tatu za Afrika ambazo Obama atatembelea, kila moja kwa jinsi Wamarekani hao wanavyoitathmini.
Rais Obama atatembelea nchi za Tanzania, Senegal na Afrika Kusini.
Ulinzi

Vyombo vya usalama vya Marekani vimejipanga kuhakikisha ziara ya kiongozi huyo haivurugwi kwa namna yoyote ile. Tayari ndege za jeshi zilizobeba magari ya akiba 56, yakiwemo 14 aina ya ‘Cadillac One’ maalumu kwa ajili ya kiongozi huyo, yamewasili katika nchi hizo tatu za Afrika atakazotembelea.

Kwa mujibu wa gazeti la Washington Post la Marekani, ndege hizo pia zimebeba malori matatu ambayo yamesheheni karatasi maalumu za kuzuia risasi kupenya kwenye vioo, zitakazobandikwa kwenye madirisha ya hoteli ambazo Rais Obama na ujumbe wake watafikia.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, mamia ya mashushushu wa Marekani tayari wako katika nchi hizo. Meli maalumu za kubeba ndege za kivita, maarufu kwa jina la ‘amphibious ship,’ ikiwa na hospitali maalumu na yenye vifaa vyote itaweka nanga baharini, jirani na nchi atakayokuwa Rais Obama, tayari kukabiliana na dharura yoyote itakayotokea. Gazeti hilo liliandika kuwa ndege za kivita za Marekani zitakuwa zikipeana zamu kufanya doria kwa saa 24, katika anga la nchi ambayo Rais Obama atakuwepo, iwapo ndege za ‘adui’ zitakaribia eneo linaloitwa ‘anga ya rais.’ Kwa mujibu wa gazeti hilo, ziara ya Rais Obama aliyoifanya hivi karibuni katika nchi za Ujerumani na Ireland Kaskazini, japo kulikuwa nagharama kwa walinzi, lakini safari za nchi za Afrika zimeelezwa kuwa na gharama kubwa zaidi.
Tahadhari

Kwa mujibu wa taarifa ya maelekezo ya Ikulu ya Marekani, ambayo Mwananchi imepata nakala yake, watu watakaokuwa kwenye msafara wa Obama wametakiwa kutotumia kachumbari. Pia imewataka kutumia maji ya chupa zaidi.

“Kutokana na mfumo wa maji uliopo, tunashauri watu wetu kutumia maji ya chupa zaidi kwa kunywa na hata kwa kupiga mswaki,” ilisema taarifa hiyo.

Kwa kuelewa fika tatizo la ugonjwa wa malaria nchini, ujumbe wa Obama umeshauriwa kutumia dawa ya mbu ya kupaka na kupuliza inayoitwa Deet.

Deet ni dawa maarufu huko Marekani na ikiwa katika aina tofauti ikiwamo ya kupaka na kupuliza na imekuwa ikitumiwa na jeshi la Marekani kwenye vita mbalimbali tangu miaka ya 1940 kabla ya kuanza kutumiwa na raia mwaka 1957.
ATM nazo noma
Pia watu watakaokuwa kwenye msafara wa Rais Obama wametakiwa kuhakikisha wanatumia mashine za kutolea fedha (ATM) zilizoko karibu na hoteli watakazofikia.
“Kuna tatizo la uhalifu kwa hiyo siyo vizuri kutumia ATM ambazo ziko katika sehemu zisizo salama. Pia katika kipindi watakachokuwa Tanzania watu wanapaswa kutumia teksi ambazo zimeidhinishwa na hoteli.
“Pia siyo vizuri kuacha kompyuta ya fedha kwenye vyumba mtakavyolala. Pia kina mama wanapaswa kuchukua tahadhari ya mabegi yao watakapokuwa wanapita mitaani,” ilitahadharisha taarifa hiyo. Chanzo: mwananchi.co.tz
AZIMIO LA KUPAMBANA NA MANYANYASO YA NGONO
un a49d6

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha kwa kauli moja azmio la kuimarisha njia za kupambana na manyanyaso ya ngono yanayotumiwa kama silaha ya kivita.
Taasisi za Umoja wa Mataifa  zinakisia kuwa zaidi ya wanawake  elfu 40 walibakwa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Liberia kati ya mwaka wa 1989-2003 na katika iliyokuwa Yugoslavia zamani, wanawake elfu 60 walibakwa mapema  miaka ya 1990 na wengine laki mbili katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo tangu mwaka wa 1998.  
Syria sasa imeongezewa kwenye orodha hiyo, huku kukiw ana ripoti za wanawake na wasichana  na hata wavulana waliobakwa kutokana na mzozo wa kivita unaoendelea.    
Umoja wa Mataifa unasema hiyo ni mifano michache tu na kwamba hata baada ya kumalizika kwa mitafaruku manyanyaso ya ngono huendelea ambapo wasichana na wanawake wanatunga mimba au kuambukizwa magonjwa ya zinaa , kutengwa na jamii na hata kubaguliwa.  
Azmio la Jumatatu la baraza la Usalama  la Umoja wa Mataifa linalenga kuimarisha njia  zote katika mfumo wa Umoja wa Mataifa kupambana na ubakaji wakati wa vita ikiwa ni pamoja na kuwapeleka washauri wa kijinsia,walinda amani na tume za kisiasa  katika maeneo yaliyoathiriwa na hata kuweka vikwazo kwa wanaofanya manyanyaso ya kingono.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague alisema manyanyaso ya ngono  kama silaha ya kivita ni sawa na bunduki na vifaru, ambavyo vinalenga kutenganisha na kuvuruga jamii ili kufikia malengo ya kijeshi na lazima hilo lifike kikomo.


Mcheza filamu mashuhuri wa Marekani Angelina Jolie ambaye pia ni balozi maalum wa Umoja wa Mataifa kwa maswala ya wakimbizi alihutubia kikao hicho cha Jumatatu. Chanzo: voaswahili

KAMPUNI ZA FEDHA TAABANI SOMALIA 

KAMPUNI zinayofanya biashara ya utumaji wa fedhwa nchini Somalia kwa kushirikiana na Benki ya Barclays zimeiomba benki hiyo kutofunga akaunti zao kwani hatua hiyo itafanya maisha kuwa magumu kwa wanaotegemea huduma hiyo.
Wasomali wengi wamekuwa wakitegemea njia hiyo kupokea fedha kutoka kwa ndugu na jamaa wanaoishi nje kupitia...
huduma hiyo kutokana kukosekana kwa mfumo kamili wa kibenki nchini humo.
Benki ya Barclays inatarajia kufunga akaunti za kampuni hiyo mwezi ujao,imesema ina wasi wasi juu ya utumaji fedha haramu.
Mamilioni ya watu wanategemea pesa zinazotumwa kwa njia hiyo, ambazo utafiti wa hivi karibuni umesema kuwa pesa hizo zinafika dola bilioni laki tau na nusu kila mwaka. Chanzo: bbcswahili
MWANAWE MUSEVENI ASEMA HANA UCHU WA MARADAKA
MWANAWE Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, amekanusha madai kuwa kuna mipango ya kutaka kumrithi babake huku akileta mwanga kwa madai ya upinzani kuwa anaandaliwa kuchukua madaraka baada ya babake kuondoka mamlakani mwishoni mwa utawala wake.
"Uganda sio ufalme ambapo uongozi unarithiwa kutoka baba hadi kwa..
mwanawe, alisema Muhoozi Kainerugaba, mwenye umri wa miaka 39, ambaye ni kamanda wa kikosi maalum cha jeshi nchini humo.
Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwenye mtandao Jumapili usiku kulingana na gazeti la Daily Monitor la nchini Uganda.
Mwezi jana polisi walifunga magazeti mawili ya binafsi nchini Uganda na vituo viwili vya redio kwa siku kumi baada ya kuchapisha barua kuhusu mgawanyiko jeshini kuhusiana na mpango wa rais Museveni kutaka kumkabidhi mwanawe mamlaka.
"uamuzi wa kuamua ambavyo Uganda itaongozwa ni jukumu la wananchi wenyewe wala sio mtu mmoja kama wanavyosema baadhi ya watu,'' inukuu taarifa ya Kainerugaba na ambayo ilitolewa na msemaji wa kikosi maalum cha jeshi la nchi hiyo, Edson Kwesiga.
Magazeti ya Daily Monitor na Red Paper yalichapisha barua iliyofichuliwa na ambayo ilikuwa na maudhui ya mpango wa kumrithisha mamlaka mwanawe Museveni. Barua hiyo iliandikwa na generali mkuu katika jeshi, David Sejusa, akidai kuwa Museveni ambaye amekuwa mamlakani tangu mwaka 1986 anamuandaa mwanawe kumrithi.
Sejusa, kwa jina lengine Tinyefuza, amekimbilia nchini Uingereza baada ya kudai kuwepo mpango wa kuwaua wanajeshi wanaopinga mpango huo, ingawa madai hayo yalikosolewa na majenerali wengine jeshini.
Kainerugaba, ambaye ni Brigedia, na ambaye anaongoza kikosi maalum cha jeshi, amekuwa akipandishwa cheo jeshini, ingawa rais Museveni hajatamka lolote kuhusu mpango wa kumkabidhi mamlaka mwanawe.
Kwesiga alisema kuwa mwanawe Museveni alitoa taarifa hiyo ili kueleza msimamo wake kuhusiana na madai hayo, kuwa wanamuandaa kuwa rais
Uganda inapaswa kuandaa uchaguzi mwaka 2016 lakini haijulikani ikiwa Museveni ambaye mwenyewe ni generali wa jeshi anapanga kuwania kwa mara nyingine. Chanzo: bbcswahili
MMILIKI WA AC MILAN ATUPWA JELA MIAKA SABA KWA KUFANYA NGONO NA BINTI WA MOROCCO
italy4 440aa
Berlusconi ni mmiliki wa AC Milan, hapa akiwa katika picha ya pamoja na kocha wa zamani wa klabu hiyo, Carlo Ancelotti mwaka 2007
italy2 bfcf7
Binti wa Morocco, Karima El Mahroug
italy3 a5283
Rais wa Mahakama, Giulia Turri (katikati) akisoma hukumu
italy bac8b
Mwanasheria wa Silvio Berlusconi, Niccolo Ghedini akizungumza na Waandishi wa Habari nje ya Mahakama.
MMILIKI wa AC Milan, Silvio Berlusconi amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela na kufungiwa maisha kufanya kazi katika ofisi za umma baada ya kukutwa na hatia ya kumlipa binti mdogo afanye naye ngono katika moja ya pati zake za 'bunga bunga'.
Waziri huyo Mkuu wa zamani wa Italia, Berlusconi, mwenye umri wa miaka 76, alimlipa binti mdogo wa Morocco, Karima El Mahroug, anayekwenda kwa jina la utani, Ruby, kwa ajili ya ngono na baadaye akajaribu kumbambikizia kesi ya wizi kwa kuwapigia simu Polisi na binti huyo akakamatwa. Berlusconi na mwanamke huyo wamekanusha kufanya ngono.
  
Mwendesha mashitaka alipendekeza afungwe miaka sita kwa kuzini ni binti mdogo na matumizi ya nguvu, lakini majaji watatu wa kike katika Mahakama ya Jijini Milan jana walitaka afungwe muda mrefu zaidi, miaka saba. 
Berlusconi pia amefungiwa maisha kufanya kazi katika ofisi za umma baada ya Waziri huyo Mkuu wa zamani kukutwa na hatia leo. 
Lakini mfungwa huyo anaweza kukata rufaa mara mbili kabla hajamaliza kifungo chake, ambayo inaweza kuchukua miezi au miaka.
  
Maana yake hatatumikia kifungo chake hadi ashindwe rufaa zake. 
Klabu yake ya AC Milan - ambayo amekuwa Rais wake kwa vipindi vitatu tofauti tangu mwaka 1987 - inayoundwa na nyota kadhaa akiwemo Mario Balotelli - ilimaliza katika nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu ya Italia, Serie A msimu uliopita ikizidiwa pointi 15 nyuma ya wapinzani, Juventus.
Baada ya hukumu, Mwanasheria wa Berlusconi, Niccolo Ghedini, mara moja alitangaza kukata rufaa akisema hukumu hiyo ni kama ilivyotarajiwa, haikutenda haki.
"Hii ni kinyume cha uhalisia," Ghedini aliwaambia Waandishi wa Habari nje ya Mahakama. "Nimetulia kwa sababu nimekuwa nikisema kwa miaka mitatu kwamba kesi haiwezi kuendeshwa hapa," alisema Ghedini. 

Kimwana: Karima el-Mahroug anafahamika kama 'Ruby the Heartbreaker'
Alisema pati hiyo ya chakula cha usiku ilikuwa kwa ajili ya watu maaum; Mwendesha mashitaka amesema walifanya ngono na mwanamke huyo aliyelipwa kuhudhuria.

Hata kama Berlusconi alikuwa anamjua mwanamke huyo katikati ya kesi hiyo, Karima el-Mahroug, anafahamika vyema kwa jina lake la utani, Ruby the Heart Breaker, ametoa ushahidi.

Alikuwa ana umri wa miaka 17 wakati huo anadaiwa kufanya kitendo hicho, lakini sasa amefikisha miaka 24. wakati umri wa kufanya ngono Italia ni miaka 14, na ni kinyume cha sheria kumlipa binti aliye chini ya umri wa miaka 18 kwa ajili ya ngono.

El-Mahroug aliitwa kwa utetezi, lakini akashindwa kutokea kwa sababu kadhaa,kuchelewesha hukumu. Timu ya Berlusconi mara moja ikamengua katika orodha ya mashahidi. Chanzo: AFP
WASHINDI WA 2013 NBA CHAMPIONSHIP NDIO HAWA
The Miami Heat have done it again.Yes ni game 7 Chini ya King Lebron James, Miami Heat imeondoka na Points 95 Kwa 88 za San Antonio Spurs. Lebron ametoka na Point 37. Wade nae ametoka na point 23, rebounds 10 , Shane Battier ana points 18. Mpaka sasa Lebron ni Mshindi wa NBA Mara mbili na MVP Mara Mbili.

The Spurs wameongozwa na Tim Duncan akiwa na points 24, rebounds 12 na Kawhi Leonard ametoka na point 19 na rebounds 16 , Manu Ginobili ametoka na points 18.

Monday, June 24, 2013

SUGU AGOMA KUOMBA RADHI BAADA YA KUDAI KUWA WAZIRI MKUU NI MPUMBAVU

Juzi, mbunge  wa  mbeya  mjini  alitoa  tusi  zito  kwa  waziri  mkuu  wa  Tanzania  na  kudai  kuwa  Tanzania  haijawahi  kuwa  na  waziri  mkuu  mpumbuvu  kama  yeye...

Kupitia  account  yake  ya facebook, Sugu, ambaye  ni  mbunge  wa  mbeya  amezidi  kusisitiza  kuwa  hawezi  kuomba  msamaha wala  kuifuta  kauli  yake....

Hii   ni  post  yake  facebook:
"...naskia kuwa watu wanasema kwamba eti nimefuta kauli yangu kuhusu waziri mkuu na amri yake kwa polisi kupiga wananchi?!...

Sina sababu ya kufuta wala kuomba radhi, na nasimamia kauli yangu to the end...kwanza 'upumbavu' sio tusi,upumbavu kwa kiingereza ni stupidity-which is lack of knowledge and understanding...
So hata uwe na cheo gani kama ukishindwa kuwa na 'understanding' juu ya madhara ya kauli zako kwa taifa then u r 'stupid'...ambapo kwa kiswahili ndio 'mpumbavu'..."
OMMY DIMPOZI AAMUA KUOMBA RADHI TENA KWA YALE MATAMSHI YAKE , BAADA YA KUPIGWA MAWE JUKWAANI DODOMA.

Ommy Dimpoz  kwa  mara  nyingine  ameamua  kupaaza  sauti  yake  na  kuwaomba  watanzania  wamsamehe  kwa  kauli  zake  mbaya  kuhusu  marehemu  Ngwea....
Sambamba  na  msamaha  huo,Ommy  anadai  kuwa  amejifunza  kutokana  na  kosa  lake  na  kwamba  hatarudia  tena...
Uamuzi  wa kuomba  msamaha  kwa  mara  ya  pili  umekuja  baada  ya  msanii  huyu  kupigwa  mawe  mjini  Dodoma  hivi   juzi
Hii  ni  kauli  yake  kupitia  ukurasa  wake  wa  facebook: