TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA HAKI ZA BINADAMU KWA KAULI MBIU YA "SAUTI YANGU INACHANGIA"
Mgeni rasmi Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda
akisoma hotuba yake ambapo amesema Pamoja na kuadhimisha kumbukumbu ya Siku ya
Haki za Binadamu, pia tunaadhimisha kumbukumbu ya Siku ya Kimataifa ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa kwa pamoja. Kaulimbiu ya mwaka huu katika Kupambana na
Rushwa ni “Unaweza kuzuia rushwa, chukua hatua sasa”. Kauli hii inaonesha
umuhimu wa Wananchi wa rika zote kupiga vita rushwa.
Mh. Pinda amesema hatua ya kuunganisha
maadhimisho haya na kufanyika sehemu moja kunapunguza gharama kwa upande wa
Serikali, na pia kunatoa nafasi kwa Wananchi kufahamu umuhimu wa siku zote mbili
bila kulazimika kuondoka eneo moja la tukio kwenda eneo jingine. Napenda
kuzipongeza Taasisi zote husika kwa kuunganisha matukio haya mawili na
kuadhimisha sehemu moja na kwa wakati mmoja.
Ameongeza kuwa Huu ni mwaka wa tano tangu
Taifa letu lilipoanza kuadhimisha siku hii Kitaifa. Kaulimbiu ya Kimataifa kwa
mwaka huu ni: “Sauti yangu inachangia” (My voice counts). Ujumbe huu unatukumbusha kushiriki katika kutoa maoni katika shughuli mbalimbali za Kijamii
au Kitaifa.
Aidha Afisa Mipango kutoka Ofisi ya Umoja wa
Mataifa ya Haki za Binadamu Kanda ya Afrika Mashariki Bw. Abdu Mohammed akisoma
hotuba kwa niaba ya Kamishna wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa
ambapo amesisitiza kila raia anapaswa kuwa na haki na fursa ya kushiriki katika
masuala ya umma, moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi huru wa kuchaguliwa,
pia kila binadamu ana haki ya kupiga kura na kuchaguli na na kuweza kufikia
huduma za kijamii sambamba uhuru wa kujieleza, kukusanyika na
kuungana.
Amongeza kuwa haki hizi zinatakiwa kumhusu
kila mtu na hakuna hata mmoja atakaye baguliwa kwa moja kati ya hizo kwa sababu
ni mwanamke, au anatoka katika kundi dogo, au anaabudu katika dini Fulani, au
kwa sababu ni shoga, au ana ulemavu, anaamini siasa Fulani, au mkimbizi au ana
rangi fulani, anatoka katika kabila Fulani.
Pia Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo
la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot akizungumza kwa niaba ya
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa ambapo amesema chini ya mpango wa pamoja,
Umoja wa Mataifa nchini Tanzania unasaidia vitengo muhimu vya serikali na wadau
wengine wa mzunguko wa Haki za Binadamu, kwa mfano ofisi ya Mwanasheria Mkuu,
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na idadi kubwa ya Asasi zisizo za
kiserikali zinazohusika na masuala ya Haki za Binadamu.
Vilevile amesema Umoja wa Mataifa
unaendelea kuinga mkono serikali kufuatilia ahadi zilizotolewa kwa Baraza la
Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na mapendekezo yakiwemo kutoka katika Bodi
za Mikataba ya haki za Binadamu.
No comments:
Post a Comment