TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Thursday, August 29, 2013

RAY C AOKOKA RASIMI...HIZI NI PICHA ZAKE AKIBATIZWA 

  
Yule dada yetu msanii maarufu wa nyimbo za bongo fleva  leo hii amewaka bayana ya kuwa yeye na shetani sasa ni paka na panya. Ray C am

ethibitisha hayo katika post zake za instagram. 


WENGER AMSAJILI FLAMINI KWA MKATABA WA MIAKA MITATU

flamini 36655
Arsene Wenger amefanya usajili wa pili katika dirisha hili la usajili linaloelekea mwishoni kwa kumsajili kiungo wa zamani wa timu Mathieu Flamini kwa uhamisho wa bure kutoka AC Milan. (HM)
Kiungo huyo ambaye aliondoka Gunners mwaka 2008 kujiunga na AC Milan, amesaini mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya £40,000 kwa wiki.
Flamini, 29, ni mchezaji wa pili kusajiliwa baada ya mshambuliaji kinda wa kifaransa Yaya Sanogo, ambaye amejiunga na Arenal akitokea Auxerre bure.

Flamini amekuwa akifanya mazoezi na Arsenal wakati wote wa pre season baada ya kuachwa na AC Milan mwishoni mwa msimu uliopita. Chanzo: Sportmail

KAGAME ATUA RASMI KENYA 

marais1 27613
MKAKATI wa kiuchumi na kimiundombinu unaozihusisha nchi za Kenya, Uganda na Rwanda ambao pamoja na mambo mengine unaitenga Tanzania, ulizinduliwa rasmi mjini Mombasa juzi na marais watatu wa mataifa hayo ya Afrika Mashariki. (HM)
Katikati ya mkakati huo wa mataifa hayo matatu yuko Rais wa Rwanda, Paul Kagame ambaye jana aliwasili Mombasa na kushiriki katika mkakati wa kuzinduliwa kwa gati namba 19 katika bandari ya Mombasa ambayo inakusudiwa kutumiwa na nchi hizo kupakulia na kusafirishia mizigo yake.
Mbali ya Rais Kagame, uzinduzi wa gati hilo uliwakutanisha pia Rais wa Uganda,Yoweri Museveni , Salva Kiir wa Sudani Kusini na mwenyeji wao Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.
Tukio la Kagame kuwapo katika tukio hilo la kihistoria kiuchumi katika ukanda huu linakuja siku chache, baada ya kuwapo kwa taarifa kwamba wafanyabiashara wa Rwanda walikuwa wameamua kuacha kuitumia bandari ya Dar es Salaam katika kupakua na kusafirishia mizigo yao.
Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Kenyatta alisema uamuzi wa Kenya kuipanua bandari hiyo ni jambo lisiloweza kuepukwa iwapo mataifa hayo ya mashariki mwa Afrika yana kusudi la kweli la kujiendeleza kiuchumi.
"Tunalenga ufanisi na kupunguza vikwazo vya biashara na kuboresha fursa za nchi zetu. Bandari hii, ni muhimu kwa maendeleo ya eneo letu na uzinduzi wa gati namba 19, unawakilisha dhamira ya serikali ninayoiongoza.
"Dhamira ya serikali yangu ni kuona bandari ya Mombasa inakuwa kubwa zaidi, yenye shughuli nyingi na mazingira rafiki zaidi ya kibiashara katika pwani ya Afrika Mashariki," alisema Kenyatta.
Akizungumza baada ya tukio hilo, Rais Kagame alisema ni hatua muhimu ya maendeleo na katika kuimarisha uwekezaji.
"Kuzinduliwa kwa bandari hii, kutaongeza biashara na kuvutia wawekezaji katika ukanda wa Afrika Mashariki," alisema Rais Kagame.
Eneo hilo jipya la maegesho lenye urefu wa mita 240 linatarajia kuboresha shughuli za upakiaji na upakuaji makontena na uwezo wa bandari hiyo.
Rais Museveni ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, alisema bandari hiyo itakuwa kichocheo cha kutoa bidhaa na huduma ndani ya nchi hizo na katika masoko ya kimataifa.
Alisema nchi wanachama wa jumuiya hiyo, zinapaswa kuwa na umoja na kuanzisha masoko yenye bidhaa bora na huduma kwa watumiaji.
"Tunategemea bandari hii itakuwa mkombozi katika masoko yetu na kukabiliana na ushindi mkubwa wa biashara duniani," alisema Rais Museveni.
Kutokana na hali hiyo, Museveni alimwagia sifa Rais Kenyatta kwa uamuzi wa kuondoa vikwazo ambavyo vimekuwa chanzo kikubwa cha kuenea kwa rushwa.
"Hatua hii, ni nzuri beria nyingi zimegeuka kuwa za wala rushwa, naamini sasa bidhaa, huduma na wananchi wa Kenya na Uganda wataufurahia," alisema Museveni.
Ujenzi wa gati namba 19 lililozinduliwa jana na marais hao unakadiriwa kugharimu dola za Marekani milioni 66.7 na utaongeza uwezo wa huduma zake kwa asilimia 33 zaidi ya sasa.
MZOZO BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI
Wakati viongozi hao wakizindua gati hilo, jijini Arusha, kwa siku ya pili mfululizo kuliibuka mzozo miongoni mwa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki.
Mzozo huo ambao unaonekana kuchochewa zaidi na uhasama wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Rwanda, jana uliendelea baada ya wabunge wa Tanzania katika bunge hilo kutoka nje ya ukumbi wa bunge.
Wabunge wa Tanzania, walifikia uamuzi huo kwa kile walichodai kupinga kitendo cha wabunge wenzao wa Rwanda wanaoungwa mkono na wale wa kutoka Kenya na Uganda kutaka hoja yao ya vikao vya bunge vifanyike kwa mzunguko katika nchi zote wanachama, ijadiliwe bila kufuata kanuni za bunge.
Katika kikao cha juzi, Mbunge wa Rwanda, James Ndahiro, aliomba mwongozo kwa Spika akitaka hoja ya vikao vya Bunge hilo kufanyika kwa mzunguko ijadiliwe katika kikao hicho.
Mbunge Ndahiro, aliomba mwongozo huo baada ya Mbunge wa Kenya, Peter Mathuki kutoa hoja ya kutaka suala la vikao hivyo kufanyika kila nchi wanachama, lijadiliwe lakini Spika wa Bunge, Margaret Zziwa,
alitoa utaratibu kuwa limekuwa jambo la haraka na muda uliobaki ni mchache hivyo anaweza kulileta jambo hilo kama motion kwa muda mwingine.
Kauli hiyo ya Spika iliwaudhi wabunge wa Rwanda ambao walisimama na kutoka nje ya ukumbi wa Bunge huku wakieleza kuwa hawataki kuburuzwa na walifuatiwa na wa Kenya.
Katika kikao cha jana, wabunge wa Tanzania wakiongozwa na Abdula Mwinyi nao walisusia kikao kwa kutoka nje ya ukumbi wa Bunge.
Kabla ya kufikiwa kwa hatua hiyo, Mwinyi alisimama na kulieleza Bunge hilo kuwa kitendo kilichofanywa na wabunge wa Rwanda juzi hakikuwa cha kistaarabu na si utamaduni mzuri, bali ni dharau kubwa kwa kiti cha spika na Bunge zima la Afrika Mashariki kwa sababu hoja iliyowasilishwa haikufuata utaratibu wa kibunge.
"Mheshimiwa Spika, nimesikitishwa na kilichotokea jana (juzi) hapa, haikuwa utamaduni mzuri tuliouzoea ni udhalilishaji wa kiti na kimechafua hata sifa ya Bunge lako, tunatakiwa kuweka utaratibu sawa ili kiti kiheshimiwe," alisema Mwinyi.
Baada ya kumaliza kuzungumza, wabunge wa Tanzania walitoka nje ya ukumbi wa Bunge, ambapo kwa mujibu wa utaratibu vikao haviwezi kuendelea kama wabunge kutoka nchi mwanachama wakitoka nje kama ishara ya kutokukubaliana na hoja inayojadiliwa.
Wakizungumza nje ya ukumbi, baadhi ya wabunge hao walisema utaratibu wa kidemokrasia kote duniani ni kwamba anayeshambuliwa kidemokrasia anapaswa kujibu mapigo.
"Katika demokrasia mtu 'akikuhit', wewe unapaswa 'kumhit' zaidi ya kile alichokufanyia, sasa sisi tumeamua kujibu zaidi yao kama ishara ya kupinga kitendo chao cha jana," alisema Shy rose Bhanji.
Kwa upande wake, Mwinyi alikiita kitendo kilichofanywa na wenzao kuwa ni uhuni na ukosefu wa ustaarabu, kwani kabla ya kuwasilisha hoja hiyo hakukuwa na kusudio la kuwasilishwa kwa hoja hiyo mezani kwa spika.
"Tunataka kuweka rekodi sawa, huu sio utaratibu ni uhuni na hatutaki urudiwe popote katika jumuiya...kwanza hawakutoa 'notice' mezani kwa spika kama utaratibu unavyotaka wanaamua tu na kushinikiza mambo wanavyotaka haikubaliki.
"Kutoka kwetu nje ni kupinga uhuni huu, wao hawakuwa na sababu yoyote ya kutoka na kama walitaka kuwepo na mzunguko katika vikao vya bunge wangefuata utaratibu," alisema Mwinyi.
Wabunge wengine wa Tanzania waliokuwepo katika kikao hicho cha jana ni pamoja na Twaha Taslima, Makongoro Nyerere na Nderikio Kessy. Chanzo: mtanzania

COPA COCA-COLA KANDA KUANZA SEPTEMBA 2

 copa-cocacola1 e40d3

Michuano ya Copa Coca-Cola kwa vijana wenye umri chini ya miaka 15 inayoshirikisha mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani inaanza kutimua vumbi Septemba 2 mwaka huu katika vituo sita tofauti. (HM)

Kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa leo (Agosti 29 mwaka huu), kituo cha Mwanza mechi zake zitachezwa katika viwanja vya Alliance ambapo timu zitakazofungua dimba ni Kagera vs Kigoma, Mara vs Tabora, Simiyu vs Geita na Mwanza vs Shinyanga.

Kituo cha Mbeya ambapo mechi zitachezwa viwanja vya Iyunga ni Katavi vs Njombe, na Ruvuma vs Mbeya. Kituo cha Pwani ni Ilala vs Kaskazini Unguja, na Lindi vs Pwani.

Ufunguzi katika kituo cha Arusha ambapo mechi zake zitachezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta AMri Abeid ni Manyara vs Kilimanjaro, na Arusha vs Singida.

Uwanja wa Jamhuri ambapo utatumika kwa mechi za kituo cha Morogoro, Tanga itacheza na Dodoma wakati Morogoro itaumana na Temeke. Mjini Zanibar kwenye Uwanja wa Chuo cha Amaan ni kati ya Kaskazini Pemba na Mjini Magharibi, na Kusini Pemba dhidi ya Kusini Unguja.

Katika hatua nyingine, Usaili kwa wanaoomba kuteuliwa kuwa wagombea uongozi katika uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na ule wa Bodi wa Ligi Kuu (TPL Board) unaanza kesho (Agosti 30 mwaka huu).

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Agosti 30 mwaka huu ni usaili kwa waombaji uongozi wote katika Bodi ya Ligi Kuu pamoja na waombaji uongozi wa TFF kwa kanda namba 11 (Morogoro na Pwani), kanda namba 12 (Kilimanjaro na Tanga) na kanda namba 13 (Dar es Salaam).

Agosti 31 mwaka huu ni kanda namba sita (Rukwa na Katavi), kanda namba saba (Mbeya na Iringa), kanda namba nane (Njombe na Ruvuma), kanda namba tisa (Lindi na Mtwara) na kanda namba kumi (Dodoma na Singida).

Usaili kwa kanda namba moja (Geita na Kagera), kanda namba mbili (Mara na Mwanza), kanda namba tatu (Simiyu na Shinyanga), kanda namba nne (Arusha na Manyara) kanda namba tano (Kigoma na Tabora), na nafasi za Rais na Makamu wa Rais wa TFF utafanyika Septemba Mosi mwaka huu.

Waombaji wote wamepangiwa muda wao wa usaili. Kwa mujibu wa ratiba usaili ufanyika kuanzia saa 3 kamili asubuhi hadi saa 2 usiku. Wasailiwa wote wanatakiwa kuzingatia muda waliopangiwa. Chanzo: Boniface Wambura

SAMUEL ETO'O ATAMBULISHWA RASMI CHELSEA

etoo1_5a024.jpg
Chelsea imemsajili mshambuliaji wa Cameroon, Samuel Eto'o kutoka klabu ya Anzi Makhachkala ya Urussi.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka thelathini na miwili amesaini mkataba wa mwaka mmoja na Chelsea.
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho, aliamua kumsajili Eto'o baada ya maombi yake ya kumsajili nyota wa Manchester United Wayne Rooney kukataliwa.(P.T)

etoo2_0fe65.jpg
Mapema wiki hii, ilibainika kuwa Rooney hakuwa tayari kulazimisha uhamisho wake kwa kuwasilisha ombi lake la kutaka kuondoka na hivyo kuzima matumaini ya Chelsea ya Kumsajili mchezaji huyo.
Mchezaji huyo ambaye ni mshindi mara nne wa mchezaji bora wa soka barani Afrika, alikuwa nyota wa AC Milan mwaka wa 2010 wakati Mourinho alipoiongoza kushinda kombe la klabu bingwa barani Ulaya.
Mwaka wa 2011, Eto'o alivunja rekodi ya kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi duniani.
Klabu hiyo ya Anzi pia imemuuza kiungo wake Willian, mwenye umri wa miaka 25 kwa klabu ya Chelsea, baada ya mmiliki wa klabu hiyo mfanya biashara tajii Suleyman Kerimov kupunguza bajeti ya klabu hiyo.
etoo3_69077.jpg
Eto'o alianza kucheza soka ya kulipwa na klabu ya Real Madrid, lakini alisajiliwa na vilabu vya Leganes na Real Mollorca kwa mkopo kabla ya kupata mkataba wa kudumu Mallorca mwaka wa tisini na tisa.
Mchezaji huyo ambaye alikuwa katika kikosi cha Cameroon kilichoshinda kombe la mataifa ya Afrika mwaka wa 2002, vile vile alishinda kombe la Copa del Rey, kabla ya kujiunga na klabu ya Barcelona mwaka wa 2004.
Akiwa katika uwanja wa Nou Camp, alishinda kombe la klabu bingwa barani ulaya mara mbili mwaka wa 2006 na 2009 na alifunga bao katika fainali hizo mbili pamoja na kushinda kombe la ligi kuu ya La Liga mara tatu.
Mwaka wa 20098, Barcelona iliilipa Inter Milan pauni milioni arubaini pamoja na mchezaji huyo ili kumsajili Zlatan Ibrahimovic na mshambuliaji huyo alifanikiwa kushinda kombe la klabu bingwa barani Ulaya kwa mara nyingine chini ya Uongozi wa Mourinho katika uwanja wa San Siro.
Alijiunga na klabu ya Anzi na ripoti zinasema kuwa alikuwa akilipwa £167,825 kwa wiki mwaka wa 2011.

SAA 4 ZAWATENGANISHA MAPACHA WALIOUNGANA

karima_98974.jpg
Jopo la Madaktari Bingwa Saba wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na Taasisi ya Mifupa ya hospitali hiyo (Moi), wamefanikiwa kuwatenganisha pacha waliokuwa wameungana kiwiliwili.Iliwalazimu mabingwa hao kutumia saa nne kufanikisha upasuaji huo. Mmoja wa watoto hao waliotenganishwa, amelazwa kwenye Wodi ya Uangalizi Maalumu (ICU) Taasisi ya Mifupa Moi wakati kiwiliwili kingine kilifariki.(P.T)
Jopo la madaktari waliofanikisha upasuaji huo ni; bingwa mstaafu wa watoto ambaye aliitwa maalumu kwa kazi hiyo, Petronila Ngiloi, Dk Robert Mhina (mifupa) na Profesa Karim Manji aliyekuwa akifuatilia kwa karibu mapigo ya moyo.
Wengine ni Dk Karima Khalid aliyekuwa akiratibu dawa ya usingizi, Dk Hamis Shaaban (ubongo na uti wa mgongo), Dk Zaitun Bokhary (bingwa upasuaji watoto) na Dk Nyangasa (moyo na mishipa ya fahamu).
Akizungumza baada ya upasuaji huo, Dk Shaaban alisema walimfanyia vipimo mtoto ambaye hakuwa amekamilika na kugundulika kuwa hakuwa amekamilika viungo vyote achilia mbali kutokuwa na kichwa na macho pia hakuwa na moyo, figo, tumbo, maini ila alikuwa na uti wa mgongo.
"Uti wa mgongo ulikuwepo na ndio uliokuwa umeshikana na mwenzake na kuna mshipa mmoja wa fahamu ulikuwa unafanya kazi ndio maana alikuwa ukimgusa anachezesha mguu."
Alisema kinachoratibiwa kwa sasa ni kuangalia dawa ya usingizi aliyopewa mtoto ambaye anaendelea kupumua na kwamba ndani ya saa 24, dawa ya usingizi waliyomuwekea mtoto huyo itakuwa imeisha na ataanza kunyonya kama kawaida.
Upasuaji
Kazi ya upasuaji huo ilianza saa mbili asubuhi kwa mtoto huyo wa jinsi ya kike aliyetimia kuchukuliwa vipimo mbalimbali ikiwemo CT Scan, MRI, Ultra sound na vingine vingi kabla ya upasuaji kamili kuanza saa tano asubuhi.
Dk Shaaban alisema ni mara ya kwanza kwa Moi kufanya upasuaji wa aina ile na kwamba mara nyingi wamekuwa wakifanya upasuaji wa watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa pamoja na mgongo wazi ambao tatizo hilo linasababishwa na upungufu wa madini ya folic acid.
Kabla ya upasuaji kuanza, mama wa mtoto huyo Pili Hija (24) alitumia muda wa nusu saa kufanya maombi maalumu ya kumwombea mtoto wake kisha kuwaruhusu madaktari kuendelea na upasuaji huo.
Akizungumza muda mfupi baada ya kuruhusiwa kumwona mtoto wake, Hija alisema: "Ninamshukuru Mungu kwa yote na nazidi kumwomba amjalie mwanangu apone kabisa, nawashukuru na nitazidi kuwaombea madaktari wanaomtibu mwanangu."Alijifungulia nyumbani Agosti 18 maeneo ya Jang'ombe, Zanzibar watoto pacha walioungana mmoja akiwa amekamilika viungo vyote na mwingine akiwa na kiwiliwili.

MWANAJESHI JWTZ AUAWA KONGO 

 mwamnyange_a6872.jpg

Mpiganaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, JWTZ Khatibu Mshindo aliuawa kwa kupigwa bomu juzi na waasi wa M23 kwenye Mji wa Goma ulioko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kuzuka mapigano makali.Wakati Mshindo ambaye alikuwa miongoni mwa askari wa Tanzania wanaounda Jeshi la Umoja wa Mataifa akifikwa na mauti, wapiganaji wengine 10 walijeruhiwa.(P.T)
Askari wa Tanzania na wale wa Afrika Kusini wako DRC kwa kazi ya kulinda amani. Malawi bado haijapeleka majeshi yake.
Meja Mshindo alikuwemo katika kikosi cha vifaru na alikuwa kwenye Kambi ya 83KJ iliyoko Kiluvya Dar es Salaam.
Kuuawa kwa askari huyo kumekuja ikiwa ni siku 47 tangu kuuawa kwa askari saba wa Tanzania waliokuwa wakilinda amani kwenye Mji wa Darfur Sudan na Kikundi cha Janjaweed.
Msemaji wa JWTZ, Meja Erick Komba alikiri kutokea kifo hicho na kusema: "Jana (juzi) Agosti 28, Wanajeshi wetu wakiwa katika eneo lao la ulinzi waliangukiwa na bomu katika eneo hilo na kusababisha majeruhi.
"Wakati wanapelekwa hospitali kwa matibabu, kwa bahati mbaya mwanajeshi wetu mmoja, Meja Khatibu Mshindo alifariki dunia. Majeruhi wengine wanaendelea na matibabu na hali zao zinaendelea vizuri."
Habari zaidi kutoka Congo zinaeleza kuwa mwili wa marehemu Meja Mshindo ulisafirishwa jana kupelekwa Entebbe, Uganda ambako ungefanyiwa matayarisho ya mwisho na tayari kwa kuletwa nyumbani.
Katika hatua nyingine, Askari wawili wa Umoja wa Mataifa, mmoja akiwa Mtanzania na mwingine raia wa Afrika Kusini walijeruhiwa kwa bomu eneo la Munigi huko Congo.
Bomu hilo lilirushwa na waasi wa M23 kuelekezwa kwa askari wa Umoja wa Mataifa waliokuwa wakikagua maeneo mbalimbali karibu na Mji wa Goma.
Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-moon amelaani mashambulizi na mauaji hayo ya askari huyo wa Tanzania na kusema: "Ninatoa pole kwa Watanzania na familia ya mpiganaji huyu na ninalaani kwa nguvu zote mauaji haya na majeruhi kwa walinzi wa amani."
Msemaji wa UN, alisema Majeshi ya UN kwa kushirikiana na yale ya Serikali, yalianzisha mapigano makali dhidi ya waasi wa M23 kwenye eneo la Kibati Kaskazini mwa Goma, kwenye Mji wa Kivu ya Kaskazini.
Majeshi ya UN na Fardc yalitumia helikopta, vifaru na askari wa miguu kutekeleza mashambulizi hayo yaliyojibiwa na waasi. Kwa mujibu wa msemaji huyo, mapigano bado yanaendelea.
Chanzo:mwananchi

UINGEREZA INAWEZA KUSHAMBULIA SYRIA BILA IDHINI YA UN

david_cameron_304x171_none_nocredit_06901.jpg
Uingereza huenda ikaanzisha mashambulio dhidi ya utawala wa Syria, bila kuungwa mkono na Umoja wa Mataifa.
Hayo ni kwa mujibu wa ushauri wa wataalamu wake wa masuala ya kisheria.
Ushauri huo unasema, mashambulio hayo yatahitajika ikiwa yatatekelezwa ili kuzuia raia kuuawa, hata ikiwa wanachama wa kudumu wa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Urussi na Uchina zikitumia kura zao za turufu kupinga mikakati za kijeshi dhidi ya utawala wa Syria.(P.T)
Maafisa wa ujasusi nchini Uingereza wamemueleza Waziri Mkuu, David Cameron kuwa, kuna uwezekano mkubwa kuwa serikali ya Syria ilihusika na shambulio la kemikali wiki iliyopita mjini Damascus.
Wabunge wa Uingereza wanatarajiwa kujadili suala hilo katika kikao chao cha leo jioni.
Serikali ya Syria imekana madai ya kutumia silaha za kemikali katika shambulio mjini Damascus tarehe 21 mwezi huu, ambapo mamia ya watu waliuawa.
Lakini Bwana Cameron anaamini kuwa kuna ushahidi wa kutosha kutoka wa maafisa wake wa ujasusi na pia kutoka kwa wanainchi kuhusu ukatili unaofanywa na utawala wa sasa wa Syria.
Ofisi ya Waziri mkuu wa Uingereza, imechapisha ripoti hiyo, kuambatana na ushauri wa mkuu wake wa sheria Dominic Grieve, inayotoa idhini ya mashambulio ya kijeshi ili kuzuia utumiaji wa silaha za kemikali siku zijazo, kuambatana na sheria za kimataifa.
Umoja wa Mataifa
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon amesema atapokea ripoti kutoka kwa wachunguzi wake wa silaha, wanaochunguza ikiwa silaha za kemikali zilitumika nchini Syria.
Mamia ya watu wanaripotiwa kuuawa kwenye shambulio hilo, lililofanyika karibu na mji mkuu wa Damascus wiki iliyopita.
Rais wa Marekani Barack Obama, amesema hajaamua kuhusu mpango wa kuishambulia Syria kijeshi.
Mataifa mengine pia yanajadili hatua watakayo chukua na Uingereza imekuwa ikishinikiza baraza la Usalama la Usalama la Umoja wa Mataifa kuidhinisha azimio litakalihakisha raia wamelindwa nchini Syria.
Rais wa Syria Bashar al-Assad amesema taifa lake litajilinda kutokana na shambulio lolote kutoka kwa mataifa ya kigeni.
Syria kujilinda asema Assad
Awali Kiongozi wa chama cha Upinzani cha Labour, nchini Uingereza, Ed Miliband, amesema bunge la nchi hiyo halipaswi kuamua ikiwa itaidhinisha mzozo wa Syria kutatuliwa Kijeshi.
Milliband ameyasema hayo muda mfupi kabla ya bunge la Uingereza kupiga kura ikiwa Uingereza itaishambulia Syria, kufuatia madai ya kutumia silaha za kemikali mjini Damascus.
Waandishi wa habari wanasems serikali ya Uingereza inahofia huenda ikapoteza kura hiyo na hivyo kukosa idhini ya kuingilia mzozo huo wa Syria.
Milliband amesema wamejifunza mengi kutokana na maamuzi yaliyochukuliwa miaka ya zamani kama ule wa kuivamia Iraq.
Amesema jamii ya kimataifa inapaswa kuipa jopo maalum na wachunguzi wa Umoja wa Mataifa nafasi ya kufanya kazi yao.
Serikali ya Uingereza imesema ina habari za kujasusi kuhusu Syria na itachapisha ripoti hiyo na ushauri wa kisheria kabla ya mjadala huo kuanza bungeni.

ZAIDI YA WATU 40 WAFARIKI KWENYE AJALI KENYA 

ajali_kenya_cbf50.jpg
Takriban watu 41 wanadaiwa kuuawa baada ya basi moja la abiria lililokuwa likitoka Nairobi kuelekea Homabay Magharibi mwa Kenya kuanguka na kubingirikia mara kadhaa katika eneo la Narok.(P.T)
Polisi wamethibitisha kuwa miongoni mwa waliouawa ni watoto wanne.
Mkuu wa polisi wilayani Narok Patterson Maelo amesema kuwa dereva wa basi hilo alishindwa kulithibiti katika eneo la kona na hivyo basi hilo kupoteza mwelekeo na kuanguka.
Maafisa wa shirika la msalaba mwekundi ambao tayari wamefika katika eneo la tukio hilo wamesema kuwa watu wengine 33 waliojeruhiwa wamesafirishwa hadi hospitali ya wilaya ya Narok kwa matibabu.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ni miongoni wa viongozi waliotuma risala zao za rambi rambi kwa jamaa na marafiki wa abiria waliouawa.
Katika ripoti iliyochapishwa katika mtandao wake wa twitter, rais Kenyatta ametoa amri kwa idara ya polisi kuchukua hatua dhidi ya wamiliki wa magari ya umma wanaokiuka sheria za barabarani.
ASKOFU MOSES KULOLA AFARIKI DUNIA
moses_b8f0d.jpg
Nimepokea taarifa kutoka kwa Rev. Daniel Kulola ambaye ni mtoto wa Bishop Moses Kulola kwamba, Askofu Kulola amefariki dunia muda mfupi uliopita. Nitaendelea kuwapa updates. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina la bwana lihimidiwe.(P.T)
Na:Katulanda Frederick

MWIGULU NCHEMBA ATAKA MBOWE NA DR. SLAA WAKAMATWE KWA MAUAJI YA RAIA

 MBUNGE wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba (CCM), amechafua hali ya hewa bungeni kwa kuitaka Serikali kuwachukuliwa hatua viongozi wa juu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Mbunge huyo alisema mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe pamoja na Katibu Mkuu wake, Dk. Wilbroad Slaa, wanapaswa kuchukuliwa hatua kwa madai ya kusababisha mauaji ya raia.

Mwigulu, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bara, alisema katika kipindi cha miaka miwili tangu nchi ilipotoka kwenye uchaguzi, viongozi hao wamekuwa wakihamasisha maandamano na kusababisha umwagaji wa damu za Watanzania.

“Mheshimiwa Naibu Spika, katika kipindi cha miaka miwili tangu nchi yetu ilipomaliza Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Mbowe na Dk. Slaa wamekuwa wakitoa kauli za wazi na hata kusababisha mauaji ya watu bila hatia.

“Kutokana na hali hii, sijui Serikali inafanya nini katika kuwachukulia hatua, kwani viongozi hawa wamekuwa wakitafuta umaarufu wa kisiasa kwa kuchochea chuki na mauaji dhidi ya raia.

“Kwa hali hiyo, tangu kipindi hicho hadi leo hii wanasubiri nini badala ya kwenda kuwaweka jela, kwani huko ndiko wanatakiwa kuwa,” alisema.

Mwigulu, alisema kukosekana kwa maadili kwa baadhi ya viongozi wa siasa, ambao wamekuwa wakitumia majukwaa na kuhubiri umwagaji damu ni hatari kwa taifa.

Alisema viongozi hao wamekuwa wakitumia majukwaa hayo na kusababisha vifo vya wananchi, huku akitaja vurugu zilizotokea katika mikoa ya Morogoro, Iringa, Arusha na Singida.

Akijibu swali hilo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika, alisema Serikali inafanya kazi kwa mujibu wa sheria, ikiwa ni pamoja na kukusanya ushahidi na kwamba mahakama ndicho chombo chenye uamuzi wa mwisho dhidi ya adhabu kwa raia au kiongozi yeyote wa kisiasa.

Kauli hiyo ya Mwigulu ilionekana kuchafua hali ya hewa ndani ya Bunge, ambapo Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje (Chadema), alisimama na kuomba mwongozo wa Spika, huku akimtaka Mwigulu kuthibitisha kauli yake, vinginevyo aombe radhi.

Wenje alisema hoja ya Mwigulu imekosa mashiko na ina lengo la kuwadhalilisha viongozi wa Chadema, huku akisahau kuwa baada ya uchaguzi wa Arumeru Mashariki, aliyekuwa Mwenyetiki wa Chadema tawi la Usa River, Omari Mbwambo, aliuawa na watu anaodaiwa kuwa ni wafuasi wa CCM.

Awali katika swali la msingi, Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango (CCM), alitaka kujua Serikali inachukua hatua gani kwa wanasiasa wanaokiuka maadili na kusababisha uvunjifu wa amani.

“Wanataaluma kama vile madaktari, wahandisi, wahasibu na hata wakandarasi pindi wanapokiuka maadili ya kazi zao huchukuliwa hatua kwa kufutiwa leseni zao.

“Vile vile viongozi wa kisiasa wanayo maadili yanayowaongoza, kwanini pale wanapokiuka maadili ya kazi zao hawachukuliwi hatua kama ilivyo katika makundi hayo? (taaluma),” alisema Kilango.

WABUNGE WA TANZANIA NAO WASUSIA KIKAO CHA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI


Kikao cha Bunge la Afrika Mashariki (EALA), jana kilivunjika kwa mara ya pili baada ya Wabunge wa Tanzania, kutoka ndani ya ukumbi wakipinga kanuni kuvunjwa juzi. 
 
Baada ya wabunge wa Tanzania kutoka nje, Spika wa Bunge hilo, Margareth Zziwa aliahirisha Bunge kwa dakika 15 ili kuweka mambo sawa, lakini jitihada za kuwashawishi ziligonga mwamba na kuamua kuahirisha Bunge hadi leo.

Hata hivyo, Mbunge wa Tanzania, Makongoro Nyerere hakuungana na wenzake kugoma kwani alibakia ukumbini na kuungana na wabunge 32 wa Burundi, Kenya, Uganda na Rwanda.
 
Awali, Mbunge Abdullah Ali Hassan Mwinyi alitoa msimamo wa wabunge wa Tanzania kuwa walitoka, kupinga kitendo cha wabunge wengine kudharau kiti cha Spika juzi na kutoka nje ili kushinikiza hoja yao.
 
Mwinyi alisema ili kushinikiza kuheshimiwa kiti cha Spika, wameamua kutoka nje ya ukumbi huo kwa kuonyesha hawaungi mkono, tabia ya baadhi ya wabunge kushinikiza hoja zao, kujadiliwa na Bunge hata kwa kukiuka kanuni na taratibu.
 
“Jana(juzi) ilikuwa ni mara ya pili wenzetu, kudharau kiti cha Spika na kutaka kutoa hoja na kujadiliwa bila kufuata kanuni, sasa tumeona ni vizuri na sisi kwa kupinga kuvunjwa kanuni, tutoke ili kuonyesha tunapinga mchezo huu,” alisema Mwinyi.
 
Mwinyi alisema kitendo cha wabunge wenzao kutoka nje ya ukumbi kwa kukataliwa kuvunja taratibu, kinadhalilisha kiti cha Spika na hata wabunge wenyewe.
 
Mbunge mwingine wa Tanzania, Twaha Taslima alisema kanuni zipo wazi kuwa kama mbunge ana hoja na kutaka Bunge lijadili mambo ambayo si ya dharura ni lazima aiwasilishe saa 24 kabla kwa Spika.
 
“Sasa jana(juzi), Mbunge wa Kenya, Peter Mathuki alitaka hoja yake ya kutaka utaratibu wa kufanyika bunge kwa mzunguko ijadiliwe kitu ambacho hakikuwa sahihi,” alisema Taslima. 

Muthuki, juzi aliungwa mkono na nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), isipokuwa Tanzania.

Jana aliwasilisha hoja hiyo kwa kufuata utaratibu lakini haikujadiliwa baada ya wabunge wa Tanzania kutoka nje.
 
Katika hoja hiyo, msimamo wa wabunge wa Tanzania na Kamati ya Uongozi ya Bunge ni kuwa vikao vyote vifanyike katika ukumbi wa Bunge, Arusha baada ya kukamilika.

Wabunge wa Tanzania ambao jana walitoka ni Shyrose Bhanji, Profesa Nderakindo Kessy na Taslima. Wabunge wanne hawakuwapo.
 
Kwa mujibu wa kanuni za Bunge hilo, kama wabunge watatu wa nchi moja, wakitoka nje kupinga jambo lolote basi kikao kinaahirishwa kwa dakika 15 na wasiporejea bunge linaahirishwa.
 
Akizungumzia mgogoro huo, Ofisa Habari wa EALA, Bobi Odiko alisema kilichotokea jana si ukiukwaji wa taratibu na kuongeza kuwa ana imani mambo yatakuwa sawa na vikao vitaendelea leo kwa amani.

BASI LA HOOD LAUA MTU MMOJA NA KUJERUHI 15


Mtu mmoja amefariki dunia na 15  wamejeruhiwa baada ya basi  la Kampuni ya Hood  likitokea kilombero kwenda jijini  Dar es salaam kumgonga  mtembea kwa miguu na kisha kuacha njia na kupinduka katika eneo la Kiembeni  Mikese Mkoani  Morogoro.
  
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Morogoro  Bonifasi Mbao  akizungumza kwenye  eneo la tukio amesema chanzo cha ajali  hiyo ni mwendo kasi ambapo dereva wa basi  gari  ilimshinda na kugonga mtembea kwa miguu na kisha kupinduka ambapo  dereva wa basi amekimbia mara baada ya tukio la ajali...
 
Taarifa za  madaktari  katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro  zimeeleza  majeruhi wanaendelea na matibabu na mwili wa marehemu umehifahiwa katika chumba cha maiti hospitali ya mkoa wa morogoro .

CAG ADAI KWAMBA MAGUFULI SIYO FISADI.....ATOA UFAFANUZI WA KINA KUHUSU ZILE BIL. 252

 
MKAGUZI na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh amesema taarifa ya Sh bilioni 252 zilizokuwa zimeoneshwa katika taarifa ya Wizara ya Ujenzi, zilihamishwa kwenda Wakala wa Barabara (Tanroads) kulipia madeni ya wakandarasi na kwamba hapakuwa na ufisadi.
 
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Utouh alisema vyombo vya habari viliripoti suala hilo tofauti, baada ya Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) kukutana na wizara na kuhoji juu ya matumizi ya fedha hizo.
 
Utouh alisema baada ya PAC na Kamati ya Kudumu ya Serikali za Mitaa (LAAC) kupitia ripoti ya Wizara ya Ujenzi, kumejitokeza upotoshaji wa taarifa kuhusu hesabu za wizara hiyo na taarifa zisizo sahihi, zikidai kulikuwa na ufisadi.
 
Alisema fedha hizo zimeoneshwa kwenye taarifa ya hesabu za Wizara hiyo, kama vile ni miradi mipya ya mwaka 2011/2012 tofauti na uhalisia wake.
 
Utouh alisema uhalisia wa fedha hizo ni kuwa mara baada ya kupokewa na Wizara ya Ujenzi kutoka Hazina, zilihamishwa kwenda Tanroads kulipia madeni ya wakandarasi wa miradi ya barabara, iliyotekelezwa na wahandisi washauri, ambao walikuwa hawajalipwa kwenye mwaka wa fedha 2010/2011.
 
“Fedha hizi zilijumuishwa kimakosa kwenye hesabu za Wizara kama matumizi ya akaunti ya maendeleo, hivyo kuongeza matumizi ya Wizara kimakosa kwa kiasi hicho. 

Kihasibu fedha hizo zilipaswa kuoneshwa kwenye hesabu za mtumiaji halisi wa fedha ambaye ni Tanroads na siyo Wizara hiyo,” alisema Utouh.
 
Alisema kutokana na hali hiyo, hesabu za wizara hazikuwa sahihi, kutokana na uwepo wa ongezeko hilo kubwa la fedha na hivyo kusababisha kupewa hati ya ukaguzi yenye mashaka.
 
“Hivyo katika kujadili hesabu za Wizara ya Ujenzi hakukuwepo na tuhuma zozote za ufisadi, ila Kamati ya PAC ilimtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuihakikishia matumizi ya fedha hizo, jambo ambalo tumejiridhisha nalo kwa ushahidi wa namna mlolongo wake ulivyo hadi zilipotumika” aliongeza Utouh.
 
Aidha, alisema mbali na dosari hiyo ya kihasibu, Wizara ya Ujenzi inafanya kazi nzuri ya kusimamia na kujenga barabara katika kona zote za nchi, hivyo viongozi wake wanapaswa kupongezwa kwa kazi hiyo wanayoifanya huku akiwataka kuwa na moyo wa kuchapa kazi zaidi kwa ajili ya maendeleo ya taifa.
 
Katika hatua nyingine, Utouh alimpongeza Spika wa Bunge Anne Makinda kwa uamuzi wake wa kupanga upya Kamati za Kudumu ya Hesabu za Serikali Kuu (PAC), kwa madai kuwa utasaidia kuleta ufanisi na tija katika utendaji kazi wa kamati hiyo.
 
Alisema uamuzi wa Spika kuipanga upya PAC na kuwa na vyombo viwili PAC 1, itakayokuwa ikishughulikia taarifa za Hesabu za Serikali Kuu, idara zinazojitegemea na taasisi zingine za Serikali chini ya Mwenyekiti wake Zitto Kabwe na PAC 11, itakayokuwa ikishughulikia hesabu za Mashirika ya Umma chini ya uenyekiti wa Deo Filikunjombe, kutasaidia kuleta ufanisi mkubwa katika ufuatiliaji.

Wednesday, August 28, 2013

ZIMBABWE KUJENGA BUSTANI YA KIFAHARI

victoriafalls_6fed8.jpg
Serikali ya Zimbabwe imetangaza mpango wa kujenga kivutio cha kitalii, "Disneyland in Africa" katika maporomoko ya maji ya Victoria ili kuimarisha secta ya utalii nchini humo.
Waziri wa utalii wa Zimbabwe Walter Mzembi ameiambia BBC kuwa serikali ya nchi hiyo itatumia dola milioni mia tatu kujenga bustani hiyo.(P.T)
Serikali ya nchi hiyo inajaribu kufufua secta ya utalii iliyosambaratika kufuatia mzozo wa kisiasa uliodumu kwa takriban miaka kumi iliyopita na kushuka kwa dhamani ya safaru ya nchi hiyo.
Rais Robert Mugabe alichaguliwa kuhudumu kuwa rais wa nchi hiyo kwa muhula wa saba katika uchaguzi mkuu uliokamilika mwezi uliopita.
Lakini waziri huyo amesema, serikali yake haitategemea maporomoko hayo ya maji ya Victoria pekee, lakini amesema bwawa hilo linauwezo wa kuinua uchumi wa taifa hilo kwa kiasi kikubwa.
''Tunafikiria kuijenga bustani hiyo ili iwe sawa na bustani ya Disneyland nchini Marekani, na itajumuisha hoteli za kifahari, medani ya burudani, hoteli na vifaa vya kuandaa mikutano. Hii ndio maoni yetu na tunahitaji watu ambao wataweza kuiendesha'' Alisema waziri huyo.
Awali Mzembi aliliambia shirika la habari la serikali la nchi hiyo kwua serikali ya rais Robert Mugabe inadhamiria kuanzisha mfumo ambao utaruhusu soko huria katika secta ya mabenki nchini humo, ambapo watu ambao sio raia wa nchi hiyo wanaweza kufungua akaunti nchini humo.
Waziri huyo aliyasema hayo wakati wa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu utalii unaoandaliwa kwa pamoja na Zimbabwe na Zambia.
Uamuzi huo wa kuipa Zimbabwe fursa ya kuandaa kongamano hilo la Umoja wa Mataifa, umeshutumiwa vikali na shirika la kutetea haki za kibinadam la Umoja huo, lililo na makao yake mjini Geneva, likadai serikali ya nchi hiyo inaendelea kukiuka haki za kibinadam na kuwa uchaguzi uliokamilika hivi majuzi haukuwa huru na wa haki.
Serikali ya Zimbabwe pia inapanga kupanua uwanja wa Ndege wa Victoria Fall, mradi ambao utagharimu dola milioni mia moja hamsini.
Katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza mwaka huu, secta ya utalii nchini humo ilikuwa kwa asilimia kumi na saba na ikiwa uthabiti wa taifa hilo utadumishwa secta ya utalii ina uwezo wa kuchangia pato la taifa hilo kwa asilimia kumi na tano.

Watu 20 wauawa nchini Nigeria; 

BokoHaram2_7d708.jpg
Watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Boko Haram wamewauwa takriban watu ishirini wanachama wa makundi kadhaa ya ulinzi waliokuwa wakipinga kundi hilo Kaskazini mwa jimbo la Borno.
Wakuu wa jeshi la nchi hiyo wanasema vifo hivyo vilitokea katika mashambulio mawili tofauti siku ya Jumapili na Jumatatu.(P.T)
Kundi hilo la Boko Haram limekuwa likifanya mashambulio nchini Nigeria tangu mwaka wa 2009.
Mwezi Mei mwaka huu, rais wa nchi hiyo Goodluck Jonathan, alitangaza hali ya hatari katika majimbo matatu ta Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo, akisema kundi hilo la Boko Haram linahatarisha usalama wa taifa hilo.
Jeshi la nchi hiyo lilianzisha operesheni kali ya kuwasaka wapiganaji wa kundi hilo, ambalo linataka kuundwa kwa taifa huru litakalozingatia sheria za Kiislamu maarufu kwama Sharia.
Jeshi la nchi hiyo lilihimiza wakaazi wa majimbo hayo kuunnda makundi ya raia ili kukabiliana na kundi hilo endapo watawavamia.
Lakini kwa sasa kundi hilo la Boko Haram, linaonekana linalipiza kisasi dhidi ya makundi hayo ya kiraia na hivyo kuongeza wasi wasi kuwa kuundwa kwa makundi hayo huenda kukachochea ghasia zaidi nchini humo.
Siku ya Jumapili, watu waliokuwa na sare rasmi za jeshi la nchi hiyo walivamia mkutano wa kundi moja la ulinzi wa kiraia na kuwafyatulia risasi na kuwauawa watu kumi na wanne.
Afisa mmoja wa serikali ya nchi hiyo ameliambia shirika la habari la AFP kuwa watu wengine wanne waliuawa kwenye shambulio lingine siku ya Jumatatu usiku katika kijiji cha Borno, wilayani Damasak.
Wapiganaji hao waliwashambulia wanachama wa kundi lingine linalojiita jeshi la wanainchi au Civilian Joint Task Force wakiwa usingizini katika hoteli moja.

ETO'O KUTUA CHELSEA NDANI YA SAA 48

etoo 57ec8
KLABU ya Chelsea iko katika hatua za mwishoni za kukamilisha usajili wa Samuel Eto'o kutoka Anzhi Makhachkala na dili hilo linaweza kukamilika ndani ya saa 48. (HM)
Tayari wamekwishamsajili Willian kutoka Anzhi ambaye anasubiri kibali cha kufanya kazi leo na usajili wa Eto'o utakuwa sehemu ya Pauni Milioni 32 zilizotengwa.
Mkataba wa mshambuliaji huyo wa Cameroon utakuwa mfupi tu wa mwaka mmoja.
Eto'o alianzia soka yake Ulaya katika klabu ya Real Madrid, lakini alicheza mechi tatu tu na akapelekwa kwa mkopo katika miaka yake minne na klabu hiyo ya Jiji la Hispania.
Alitengeneza jina alipokuwa akichezea Mallorca kabla ya kusajiliwa na Barcelona. Aliiwezesha kushinda Ligi ya Mabingwa, akifunga dhidi ya Arsenal katika Fainali mwaka 2006.
Baadaye akaenda kuungana na Jose Mourinho Inter Milan, na hiyo inaweza kuwa sababu moja ya kuchaua kutua Chelsea. Kocha huyo Mreno anaweza kuwa na imani naye zaidi kuliko washambuliaji wake wa sasa, Fernando Torres, Romelu Lukaku au Demba Ba. Chanzo: binzubeiry

MAJANGA ARSENAL, PODOLSKI NJE SIKU 21, RAMSEY NA WILSHERE NAO WAUMIA

10 74adc
Lukas Podolski ameongeza idadi ya majeruhi Arsenal na chini akitolewa uwanjani jana (HM)

20 d00eb
Jack Wilshere aliumia kifundo cha mguu, lakini akaendelea na mechi Arsenal ikiifunga Fenerbahce
30 8c787
Aaron Ramsey aliondoka uwanjani kabla ya mwisho wa mechi kutokana na maumivu ya nyonga
MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Lukas Podolski ataukosa mchezo wa Jumapili wa wapinzani wa London Kaskazini, dhidi ya Tottenham baada ya kuumia nyama katika mchezo wa Ligi ya Mabinwa jana dhidi ya Fenerbahce.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ujerymani anatarajiwa kuwa nje ya Uwanja kwa wiki tatu baada ya kuumia katika dakika za mwanzoni za kipindi cha pili kwenye ushindi wa 2-0 katika mchezo huo wa marudiani, hivyo timu yake kusonga mbele hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla wa 5-0 dhidi ya Waturuki.
Kocha Arsene Wenger amesema: "Tmetugharimu mno kwa majeruhi hayo, kwa sababu tunampoteza Podolski.
Aaron Ramsey alifunga mabao yote katika usiku huo Arsenal ikijikatia tiketi ya kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya 16 mfululizo.
Lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales naye pia alikuwa miongoni mwa wachezaji walioumia, akitoka nje kabla ya mwisho wa mchezo na kuiacha Gunners ikimalizia mechi na wachezaji 10.
Kiungo Jack Wilshere pia naye alipatwa na misukosuko, alipokabiliana na Raul Mereiles na Bruno Alves, na kumuachia maumivu.
Wenger alisema: "Sifahamu kiasi gani Ramsey ameumia. Sifahamu Wilshere anaendeleaje. Tutaangalia hiyo kesho (leo) asubuhi. Makwanja mawili kwa Wilshere yalisikitisha, lakini anaonekana yuko sawa.
"Jack atakuwa sawa Jumapili. Natumai hivyo kwa Aaron pia. Nilimuona akitoka nje zikiwa zimesalia dakika tatu au nne mechi kumalizika, lakini sijui anajisikia vibaya kiasi gani. Alitaka kubaki uwanjani,".
Wenger alitaka kumtoa nje Wilshere, kutokana na historia ya matatizo ya maumivu ya kifundo cha mguu kwa mchezaji huyo, lakini mchezaji huyo akaamua kuendelea kucheza.
"Nilitaka kumtoa nje, ndiyo," Wenger alisema. Chanzo: binzubeiry

UCHAGUZI WA TFF: WALLACE KARIA APINGWA URAIS, VEDASTUS KALWIZIRA UMAKAMU 

Wallace-Karia1 52e1e
Wanamichezo wawili walioomba kuwania uongozi kwenye uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) utakaofanyika Oktoba 27 mwaka huu wamewekewa pingamizi. (HM)
Waliopingwa ni Wallace John Karia anayeomba kupitishwa kuwania urais na Vedastus Kalwizira Lufano anayewania ujumbe wa Kamati ya Utendaji kupitia Kanda Namba Mbili ambayo ni mikoa ya Mara na Mwanza. Anyempinga Karia ni Shamsi Rashid Kazumari wa Dar es Salaam wakati Lufano anapingwa wa Samwel Nyalla wa Mwanza.
Pamoja na mambo mengine, Kazumari anampinga Karia kwa madai kuwa akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi, aliwashawishi wajumbe wenzake kuingia mkataba na Azam Tv wakati akijua kamati hiyo ni ya muda, hivyo haina nguvu za kisheria kusaini mkataba huo.
Naye Nyalla ambaye pia ni mmoja wa wanamichezo waliojitokeza kuwania ujumbe kupitia Kanda hiyo anampinga Lufano kwa madai hana uzoefu wa miaka mitano katika uongozi wa mpira wa miguu.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF chini ya Mwenyekiti wake Hamidu Mbezeleni itakutana kesho (Agosti 28 mwaka huu) saa 4 kamili asubuhi kusikiliza pingamizi hizo ambapo wawekaji pingamizi na waliopingwa wanatakiwa kufika wenyewe ndani ya muda kwa vile uwakilishi hautakiwi.
MAANDALIZI MKUTANO WA UCHAGUZI TFF
Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inaendelea na maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Uchaguzi utakaofanyika Oktoba 26 na 27 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Awali mkutano wa uchaguzi ulikuwa ufanyike Februari 23 na 24 mwaka huu lakini tukauahirisha kusubiri maelekezo ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), hivyo tayari wajumbe wana taarifa rasmi kuhusu mkutano huo.
Orodha ya wajumbe iliyotumwa awali kwa ajili ya Mkutano tunayo, isipokuwa kama kuna wanachama wetu wana mabadiliko ya majina ya wajumbe watakaohudhuria wanatakiwa kutuma majina hayo kabla ya Septemba 30 mwaka huu.
Wanachama wa TFF ni vyama vya mpira wa miguu vya mikoa, vyama shiriki na klabu 14 za Ligi Kuu ya Vodacom.
Chanzo: Shaffihdauda

MMAREKANI PHIL WILLIAMS kupambana na CHEKA IJUMAA 

box 897aa
Kocha wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akiwa na bondia Phil Williams wa marekani baada ya kutua nchini kwa ajili ya mpambano wake na Francis Cheka utakaofanyika August 30 siku ya ijumaa hii katika ukumbi wa Diamon Jubilee jijini Dar es salaam. (HM)

box2 12c0e
Bondia Phil Williams wa marekani akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa mchezo huo kushoto ni promota Jay Msangi kulia ni Kocha wa kimataifa wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila 'Super D wengine ni wadau waliokuja kulaki uwanja wa ndege.
box3 32db8
Bondia Phil Williams wa marekani akiwa na mkanda wake wa ubingwa wa WBUChanzo: www.superdboxingcoach.blogspot.com

Wananchi waishio Mbezi Beach ‘walia’ bomoabomoa ya Dawasa 

dawasa_7af8f.jpg
Wakazi wa Mbezi Beach, Tegeta na Wazo katika Manispaa ya Kinondoni wamelalamikia kazi ya ubomoaji wa nyumba zao ili kupisha utandazaji wa bomba la majisafi la Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa), kwamba inafanywa kwa ubaguzi.Hata hivyo, ilielezwa kuwa Dawasa ilitoa siku 14 kwa wakazi hao kubomoa nyumba zao zipatazo 400 kupisha mradi huo wa bomba utakaogharimu Sh120 bilioni.(P.T)
Dawasa imelaumiwa kutokana na baadhi ya nyumba za vigogo na watumishi wa Serikali kuachwa licha ya kuwekewa alama ya X kuashiria zinatakiwa kubomolewa.
Mwandishi wa Mwananchi aliyekuwa eneo la tukio, alishuhudia baadhi ya wananchi hao wakidai kuwa moja ya nyumba ambayo imeachwa ni ya ndugu wa mmoja wa vigogo wa Serikali.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana huku ubomoaji ukiendelea, mmoja wa waathirika wa bomoabomoa hiyo, alilalamikia ubomoaji kufanyika kibaguzi.
Juma Shaaban alisema: "Ninashangaa kuona tunabomolewa nyumba zetu huku nyumba zao zinaachwa,"Ninaweza kukuonyesha nyumba ya ndugu yake kigogo (anamtaja) imewekewa X, lakini chakushangaza haijabomolewa, hii tulalamike."alisema.
Mkazi mwingine wa Tegeta, Khamis Ramadhani alisema: "Tunashangazwa na bomoabomoa hii kufanyika bila hata kutupa muda wa kuhamisha mali zetu."
Katika hatua nyingine, bomoabomoa inayoendelea ilisababisha hitilafu ya umeme na kusababisha moto ulioteketeza Baa maarufuya Samaki Samaki.
Moto huo ulitokea Saa 4 asubuhi na kusababisha watu kujaa na kufungwa barabara kwa muda ili kuzima moto huo kabla ya magari ya kuzima moto kuwasili eneo la tukio.

Dk Ndalichako: Siasa zisipewe nafasi kwenye mitihani yetu;

ndalichako_35ec2.jpg
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk Joyce Ndalichako amesema siasa hazipaswi kupewa nafasi katika mchakato wa usimamizi wa mitihani na kwamba athari za mwenendo wa aina hiyo ni kubwa kwa taifa.Dk Ndalichako alisema akiwa kiongozi wa Necta hapendi ifike mahali ambako kila mtu atatakiwa afaulu hata kama hana sifa kwani madhara yake yatakuja kuonekana kwenye rasilimali watu siku zijazo.(P.T)
Akizungumza katika mahojiano maalumu Arusha hivi karibuni alisema: "Tukiruhusu mitihani iingiliwe na wanasiasa tutakuwa tunajimaliza wenyewe, kama ni wanasiasa wafanye kazi ya kushauri halafu waache wanataaluma husika wafanye kazi yao.
"Wanaohusika na kutunga sheria watekeleze jukumu lao siyo kuingilia moja kwa moja suala la mitihani. Sisemi kuwa tuachwe tu tufanye kazi kama tunavyotaka, ikibidi kuwe na chombo cha wanataaluma kutukagua, kwa sababu hii ni taaluma siyo kitu cha kila mtu kuingilia.
"Madhara ya kuingilia mitihani matokeo yake yataweza kuja kuonekana baada ya miaka hata 10 ijayo, ili kukwepa hali hiyo, kila mtu afanye kazi yake kama itaonekana watendaji hawana sifa waondolewe wawekwe wengine wenye sifa."
Dk Ndalichako ambaye hivi karibuni alichaguliwa kuongoza Mabaraza ya Mitihani Afrika (AEAA) alisema: "Mtu akipewa alama asizostahili na akawa mwalimu atawafundisha nini watoto? Hawa ndiyo utakuta wana sababu zisizokwisha, kila siku utamsikia akisema watoto wa siku hizi hawaelewi kabisa."
Dk Ndalichako pia alipinga mawazo kwamba Necta inapaswa kushirikiana na wadau wa elimu katika kila kitu. Alisema ni hatari... "Tusifike mahali tuambiwe tuwaulize watoto tuwaletee maswali gani kwenye mtihani."
Kauli ya Dk Ndalichako imekuja wakati taifa likiendelea kuugulia maumivu yaliyotokana na matokeo mabaya ya mitihani ya kidato cha nne ya 2012 ambayo karibu nusu ya wanafunzi walifeli. Matokeo hayo yaliifanya Serikali kuunda tume iliyoogozwa na Katibu Mkuu wa sasa wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome ambayo ilipendekeza matokeo hayo yafutwe na yapangwe upya, hatua ambayo wengi waliita ni ya kisiasa.
Mahojiano kati ya Dk Ndalichako
Swali: Hii ni mara ya tano kwa Necta kuwa mwenyeji wa mkutano wa AEAA, na pia mmekuwa mkihudhuria mikutano kama hii inapofanyika nje ya nchi, ni nini hasa mmeona kuwa ni changamoto kwa mitihani inayotungwa katika ngazi ya shule?
Jibu: Hii mitihani inayotungwa shuleni ni changamoto sana, lakini ukiangalia utagundua kuwa tatizo lipo kwenye mitalaa ambayo walimu wanafundishiwa. Huko suala la ufundishaji limetiliwa mkazo sana lakini lile la kuwapima watoto halijapewa kipaumbele kabisa.
Wanachofundishwa huko ni kama orientation (utangulizi) tu, walimu wanatakiwa wajue mbinu gani zitumike kutunga mitihani.
Sisi kwenye ngazi ya taifa tunapotunga maswali tunazingatia mengi, kuanzia idadi ya watahiniwa na mambo kama hayo. Mwalimu darasani angetakiwa kutunga mtihani kwa kuangalia watoto wake na ajue ni mbinu gani za kutumia.
Tumekuwa tukifanya mafunzo kwa baadhi ya walimu kuhusu namna bora ya kutunga mitihani, ili waweze kufanya tathmini ya kile walichowafundisha watoto. Hata hivyo kwa kuwa sisi tupo wachache na mitihani yetu ni mingi tunashindwa kuwafikia wote. Tuna mpango wa kutoa mafunzo hayo kwa wakufunzi 200 wa walimu.
Swali: Vipi kuhusu ubora wa mitihani inayotungwa na Necta, mnadhani inakidhi viwango?
Jibu: Ubora wa mitihani inayotungwa na Baraza upo juu sana, hata usahihishaji wake ni wa hali ya juu. Mfumo wa kuwa kila mwalimu anasahihisha swali lake ni wa kipekee na sisi tulikuwa kati ya nchi za kwanza kuutumia.
Kuna nchi mtu anapewa burungutu la mitihani ya watoto anakwenda nayo nyumbani kusahihisha akishamaliza analeta majibu kisha watoto wanatangaziwa. Sisi mfumo wetu ni bora sana na sijui kwa nini watu wanakuwa na mtazamo hasi na Necta. Sifa kubwa ya baraza lolote lile la mitihani ni kutoa majibu yanayofanana na hali halisi ya elimu ilivyo.
Tunachotaka siku zote kuona ni mtu anapewa kile anachostahili. Watu wengine wanasema mitihani inayotungwa na kupewa watoto wote siyo sawa kwa sababu kuna baadhi ya shule walikuwa hawana walimu au vitabu, sasa swali la kujiuliza nani alitakiwa kutoa hivyo vitabu?
Kwa vipi utunge mtihani mmoja useme ni kwa ajili ya shule ambayo haina vitabu na walimu! Ni watoto gani ambao tumewaandaa kwa sababu ya kwenda kwenye hizo shule?
Naona ni bora kabisa shule isiwepo kama hakuna walimu na vitabu kwa sababu hii ndiyo roho ya elimu. Kukiwa na walimu na vitabu watoto wanaweza kukaa hata chini ya mti na wakafundishwa na kupata maarifa.
Necta tunatunga maswali kwa kuzingatia vitu vingi na kutokana na suala la uwazi, kila swali linalotungwa kuna sehemu tunaonyesha mada ambayo swali hilo lilipotolewa kwa mujibu wa silabasi pia kuorodhesha baadhi ya vitabu vyenye mada hiyo, mpaka ukurasa tunaonyesha. Hata Tume ya Waziri Mkuu walipokuja tuliwaonyesha vitu vyote hivyo.
Swali: Katika mkutano huu, baadhi ya mambo yaliyozungumziwa ni pamoja na athari za siasa kuingizwa kwenye mitihani, kwa upande wa Tanzania unazungumziaje hali hiyo?
Jibu: Tukiruhusu mitihani iingiliwe na wanasiasa tutakuwa tunajimaliza wenyewe, kama ni wanasiasa wafanye kazi ya kushauri halafu wawaache wanataaluma husika wafanye kazi yao, wanaohusika na kutunga sheria watekeleze jukumu lao siyo kuingilia moja kwa moja suala la mitihani.
Sisemi kuwa tuachwe tu tufanye kazi kama tunavyotaka, ikibidi kuwe na chombo cha wanataaluma kiwe kinatukagua, kwa sababu hii ni taaluma siyo kitu cha kila mtu kuingilia.
Madhara ya kuingilia mitihani matokeo yake yataweza kuja kuonekana baada ya miaka hata 10 ijayo, ili kukwepa hali hiyo kila mtu afanye kazi yake kama itaonekana watendaji hawana sifa waondolewe wawekwe wengine wenye sifa.
Tukitaka kila mtu afaulu hata kama hana sifa madhara yake yatakuja kuonekana kwenye suala la rasilimali watu, mtu akipewa alama asizostahili na akawa mwalimu atawafundisha nini watoto? Hawa ndiyo utakuta wana sababu zisizokwisha, kila siku utamsikia akisema watoto wa siku hizi hawaelewi kabisa.
Pia hili suala la kusema kila kitu tushirikishe wadau ni la kuangalia. Tusifike mahali tuambiwe tuwaulize watoto tuwaletee maswali gani kwenye mtihani.

LUKUVI: WABUNGE WENGI WENGI WAMO ORODHA YA DAWA ZA KULEVYA 

lukuvi_213a3.jpg
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi amesema baadhi ya majina ya wabunge yametajwa miongoni mwa watu wanaoshukiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya lakini Serikali haiwezi kuwataja hadharani kwa haraka.Majibu hayo ya Waziri Lukuvi yamekuja baada ya wabunge kumbana na wengine wakizomea baada ya kueleza ugumu wa kutaja majina ya washukiwa pasi na ushahidi wa kutosha.(P.T)
"Serikali haiwezi kutaja majina haraka kiasi hicho kwani inaogopa kukurupuka na kushindwa mahakamani, hivyo lazima tuwe makini sana na jambo hilo. Hatuwezi kukurupuka tu eti ni fulani wakati hatuna vithibitisho.
"Kumbukeni wengine mpo humu ndani ya Bunge na tukianza wengi mtakwisha maana katika orodha hiyo kubwa na ninyi mmo na orodha ni kubwa kweli ambayo wakati mwingine inatakiwa umakini wa hali ya juu," alisema Lukuvi alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Karatu (Chadema), Mchungaji Israel Natse.
Katika swali lake ambalo lilisababisha kelele za kuzomea, Natse alitaka majina hayo yatajwe hadharani. Hata hivyo, hali ilitulia baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda kuingilia kati na kusema: "Hii tabia ya zomeazomea siitaki humu ndani, acheni tabia hiyo lazima mumsikilize mtu kwa kile anachokisema kwanza lakini mtindo huu si mzuri..."
Patashika hiyo ilitokana na swali la Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Catherine Magige aliyetaka kujua iwapo Serikali inaweza kuwaambia Watanzania ukubwa wa biashara hiyo nchini na kama haioni kama kuna tatizo katika ukaguzi wa abiria na mizigo katika viwanja vya ndege na juhudi za Serikali kumaliza tatizo hilo.
Akijibu swali hilo, Lukuvi alisema ukubwa wa biashara hiyo hapa nchini unadhihirishwa na idadi ya Watanzania 274 waliokamatwa kati ya mwaka 2008 hadi Julai mwaka huu kwa kosa la kujihusisha na dawa za kulevya katika nchi mbalimbali za nje.
Alisema Serikali inafahamu ukubwa wa tatizo la matumizi ya biashara hiyo haramu ya dawa za kulevya nchini na alitaja takwimu za ukamataji wa dawa hizo katika kipindi cha kuanzia mwaka 2000 hadi Machi, 2012.
Alisema pamoja na kukamatwa kwa Watanzania hao nje ya nchi, wageni 31 wanashikiliwa mahabusu katika Magereza ya Keko na Ukonga, Dar es Salaam ambao ni raia wa Iran, Pakistan, Senegal na Afrika Kusini.
Hata hivyo, katika swali lake la nyongeza, Magige alisema uteketezaji wa dawa zinazotajwa kukamatwa umekuwa wa siri kiasi cha kutiliwa shaka kuwa huenda zinachukuliwa na maofisa waliozikamata ndiyo maana hakuna uwazi.
Kuhusu hilo, Waziri Lukuvi alisema suala la uteketezaji wa dawa hizo hauko wazi kutokana na sheria zilizopo kutotoa nafasi ya kuteketezwa mapema kwa kuwa zinatumika kwa ajili ya ushahidi akisema wakati mwingine hukaa zaidi ya miaka 10.

MAREKANI YAPIMA MIKAKATI YA KIJESHI DHIDI YA SYRIA

marekani_syria_abc3f.jpg
Kufuatia shambulizi la silaha za sumu lililoua mamia nchini Syria, yaonekana muda wa kutafuta suluhu ya muafaka umekwisha. Marekani inaona msitari mwekundu umevukwa, na inapima uwezekano wa kuingilia kijeshi.(P.T)
Baada ya kutokea shambulizi linalodhaniwa kuwa la kemikali, ambalo liliwauwa mamia ya raia na kujeruhi zaidi ya 3000 nchini Syria kwa mujibu wa shirika la misaada la madaktari wasio na mipaka, mataifa mengi ya magharibi na hasa Marekani, yanaaamini kuwa rais Bashar al-Assad ndiye anawajibika kwa shambulizi hilo. Kwa sababu kwa miezi kadhaa rais wa Marekani, Barack Obama, alionya kuwa matumizi ya silaha za kemikali yatamaanisha kuwa msitari mwekundu umevukwa, katika mazingira haya, laazima utawala wa Assad uchukuliwe hatua nzito. Kwa mujibu wa vyanzo vya Usalama vya Marekani, Ikulu ya mjini Washington inajadili njia tatu za kuchukuwa.
Eneo lisiloruhusiwa ndege kuruka
Njia ya kwanza ni kuweka eneo lisiloruhusiwa ndege kuruka nchini Syria, hii ikimaanisha kuwa Wamarekani watazipiga marufuku ndege na helikopta za utawala katika baadhi ya maeneo. Hii itamaanisha kuwa vikosi vya Assad havitaweza tena kuwashambulia waasi kupitia angani. Hans-Joachim Schmidt, kutoka taasisi ya amani na utatuzi wa migogoro ya Hessian, anasema hatua hii ingekuwa ya msaada mkubwa kwa waasi kwa sababu "Assad hangeweza kuwashambulia waasi kwa kutumia helikopta na ndege zake za kivita. Hii ingewanufaisha moja kwa moja waasi."

Lakini Paul Rogers, mtaalamu wa masuala ya usalama kutoka shirika la ushauri la Oxford Reseach Group la Uingereza, anasema Marekani laazima izime mifumo ya ulinzi wa angani ya Syria, jambo ambalo anasema litakuwa ghali na la hatari sana kwa kuzingatia kuwa Urusi iliahidi kuipatia Syria mitambo ya kisasa. Juu ya wasiwasi huo, Hans-Joachim Schmidt anasema ikiwa kweli Urusi imekwisha iuzia Syria mitambo hiyo ya kisasa, basi Wamarekani watapata taabu sana. Lakini anasema haoni uwezekano mkubwa kwa Marekani kutumia mkakati huu, kwa sababu utawavuta zaidi katika mgogoro huu, kitu ambacho serikali ya Marekani haitaki. Wakati huo huo, kanda isiyoruhusiwa kuruka ndege laazima iidhinishwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, na huko Urusi na China bila shaka zitatumia kura ya turufu kuizuia.
Mashambulizi dhidi ya maeneo ya kimkakati
Njia nyingine ni kushambulia maeneo ya kimkakati kwa makombora na maroketi kama vile viwanja na njia za kurukia ndege, na hivyo kudhoofisha uwezo wa jeshi la angani la Syria. Marekani ina meli kadhaa za kivita na nyambizi katika bahari ya Mediterannean, ambazo zinaweza kutumiwa kutekeleza mashambulizi ya namna hii na kufanya vigumu kwa ndege kuruka na kutua.

Lakini uharibifu kwa njia za ndege unaweza kukarabatiwa haraka. Schmidt anaiona njia hii kuwa ndiyo yenye uwezekano mkubwa zaidi wa kutumiwa, licha ya ukweli kuwa nayo itahitaji kuidhinishwa na baraza la usalama. "Wamarekani hawataki kujiingiza moja kwa moja katika mgogoro huu, hivyo shambulio la kijeshi lingekuwa ishara yenye ufanisi, japokuwa yenye mipaka, ya kuzuia matumizi zaidi ya silaha za kemikali," anafafanua mtafiti wa amani na utatuzi wa migoro Hans-Joachim Schmidt.
Kuwapatia waasi silaha
Njia ya tatu inaweza kuwa kuwapatia silaha waasi. Hadi sasa Marekani haijawapatia msaada wa silaha waasi, ukiachilia mbali misaada ya kawaida kama vile vifaa vya tiba. Lakini Rogers anasema waasi wamekuwa wakipokea vifaa vya kijeshi kutoka Saudi Arabia na Umoja wa falme za Kiarabu kupitia Uturuki na Jordan. Lakini anasisitiza kuwa uwezekano wa waasi kupatiwa silaha moja kwa moja na Marekani ni mdogo sana, kwa sababu watahitaji kupewa mazoezi kwanza kabla hilo halijafanyika. Hofu nyingine kuhusiana na hili, ni silaha hizo kuangukia mikoni mwa kundi lenye itakadi kali la Al-Nusra Front.

Na diplomasia je?
Lakini Uingiliaji wa tahadhari bado unabaki kuwa uingiliaji, na kwa hivyo Marekani bado inasita kufanya hivyo, kwa kuzingatia madhara yake. Tayari rais Bashar al-Assad ameonya kuwa hatua yoyote ya kuingilia kati kijeshi itasababisha moto utakaoizingira kanda nzima ya mashariki ya kati. Iran nayo inaweza kuliimarisha kundi la Hezbollah dhidi ya Israel na kundi la Taliban linaweza kuzidisha mashambulizi dhidi ya maslahi ya Marekani.
Schmidt kwa hivyo anapendekeza njia ya nne ambayo haizungumzwi katika vyombo vya habari kwa sasa: Shinikizo la diplomasia. Hata hivyo, mtaalamu huyo anahisi kuwa uamuzi wa kuishambulia Syria kijeshi umekwisha chukuliwa na kinachosubiriwa ni lini na vipi. Kinachoonekana sasa ni kwamba Marekani inatafuta washirika katika operesheni hii.
Mwandishi: Jansen Klaus

WAZIRI MEMBE AZUNGUMZIA KUHUSU URAIA WA NCHI MBILI 

membe_uraia_e153f.jpg
Serikali ya Tanzania iko mbioni kuwaruhusu wananchi wake kuwa na uraia wa nchi mbili baada ya kubaini kuwa idadi kubwa ya raia walioko nchi za ng'ambo wanakosa fursa za kushiriki kwenye shughuli za kimaendeleo.
Serikali ya Tanzania iko mbioni kuwaruhusu wananchi wake kuwa na uraia wa nchi mbili baada ya kubaini kuwa idadi kubwa ya raia walioko nchi za ng'ambo wanakosa fursa za kushiriki kwenye shughuli za kimaendeleo.(P.T)
Katika kufanikisha shabaha yake hiyo, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe amepeleka pendekezo rasmi kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, akitaka akitaka suala la uraia wa nchi mbili kitambulike kwenye katiba ijayo. Mwenzetu George Njogopa alikutana na Waziri Membe jijini Dar es saalam na kumuuliza sababu za kupekeka mapendekezo hayo katika tume ya mabadiliko ya katiba.

Tuesday, August 27, 2013

MATUKIO YA PICHA KATIKA IBADA YA JUMAPILI KATIKA KANISA LA HABARI NJEMA LILILOPO MAJOHE

 TEAM YA PRAISE AND WORSHIP WA KIMWIMBIA BWANA