TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, April 30, 2013

UINGIAJI MAGARI WAONGEZEKA BANDARINI DAR

                                                                    Bandari ya EDar es Salaam

Dar es Salaam. 
Kumekuwa na ongezeko kubwa la takriban asilimia 50 la magari yanayoingia nchini kupitia bandari ya Dar es Salaam katika kinachoelezwa kuwa matokeo ya uboreshaji wa huduma na usalama katika bandarini hiyo.

Takwimu zilizotolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), zinaonyesha kuwa magari yanayopita Bandari ya Dar es Salaam, yameongezeka hadi kufikia 83,440 kwa kipindi cha miezi minane kilichoishia Februari mwaka huu.

Magari hayo yameongezeka kutoka magari 55,819 kwa kipindi kama hicho kilichoishia Feburuari 2012.

Takwimu hizo za TPA zinaonyesha kuwa kwa kipindi cha kati ya Julai mwaka 2012 na Feburuari mwaka 2013, Bandari ya Dar es Salaam ilihudumia magari 83,440 yaliokuwa yanaingia nchini na yale yaliyokuwa yanapelekwa nchi jiran.

Februari mwaka huu takriban magari 10,000 yalipokelewa.
Kaimu Meneja wa Mawasiliano wa TPA, Janeth Ruzangi, alisema ongezeko magari, limechangiwa na uwekezaji mkubwa katika vitendea kazi na mafunzo kwa wafanyakazi.

Bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni ilitangaza ongezeko kubwa la mizigo inayohudumiwa na kueleza kuwa ongezeko hilo la biashara ni matokeo ya ufanisi wa kazi uliotokana na uwekezaji.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari imewekeza kiasi cha Euro milioni 10.4 (zaidi ya bilioni 20 za Kitanzania) katika ununuzi wa mitambo ya kisasa ya kupakia na kupakua mizigo katika bandari zake za Dar es Salaam na Tanga. TPA pia imewekeza katika mafunzo kwa wafanyakazi, hatua ambayo imeripotiwa kuongeza morali ya kazi.

MITAMBO YA ANALOJIA KUZIMWA LEO MBEYA

Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungi 
Mbeya. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema mitambo ya Analojia mkoani Mbeya itazimwa rasmi leo saa 6:00 usiku.
Akizungumza na waandishi habari jana, Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungi, alisema Mkoa wa Mbeya umekuwa wa mwisho katika hatua za kuzima mitambo hiyo, katika awamu ya kwanza.
Mungi alisema uzimaji wa mitambo ya analojia na kuhamia katika mitambo ya Digitali katika awamu ya kwanza, ulihusisha Mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Tanga, Mwanza, Moshi na Arusha.
Alisema wakazi wa Mbeya walikwishafahamishwa kuhusu kuzimwa kwa mitambo hiyo kwa kufanya maandalizi yaliayohitajika ili kuepuka usumbufu ambao ungejitokeza.

Aliwataka Watanzania kuacha kunung’unika wanapokabiliwa na changamoto mbalimbali na hasa yanayohusu matatizo ya ving’amuzi na badala yake, wachukue za kutafuta ufumbuzi
Alisema baadhi ya Watanzania wamekuwa wakitumia muda mrefu kunung’unika na kushindwa kuchukua hatua za kukabiliana na changamoto zinazowakabili.

MWANAFUNZI WA DSJ AFA, 22 WAJERUHIWA CHALINZE

                                                Marehemu Diedon Eliason Kibona

Na Nyendo Mohamed.

WANAFUNZI wa Chuo cha Uandishi wa Habari (DSJ) wapata ajali katika eneo la Chalinze walipokuwa wakitokea Mbeya kuelekea Dar es Salaam ambapo wanafunzi ishirini na mbili wamejeruhiwa na mmoja kupoteza maisha pamoja na dereva aliyekuwa amewabeba wanafunzi hao.
Akizumgumza na wanahabari jana kiongozi wa msafara huo Victor Sinka alisema kuwa ajali hiyo ilitokea siku ya jumapili juzi majira ya saa tatu na nusu usiku katika eneo la Chalinze walipokuwa wakitokea Mbeya kuelekea Dar ea Salaam.
Alisema kuwa wanafunzi hao walikuwepo  Mkoani Mbeya kwa takribani siku nne ambapo walikuwa katika ziara ya kutembelea vivutio mbalimbali vilivyomo mkoani humo na kutembelea baadhi ya vituo vya habari ambapo ziara hiyo atahusisha matokeo ya mtiahani wa mwisho wa wanafunzi hao.
Ziara hiyo ambayo ilkuwa  idadi ya wanafunzi 180 wakiwemo wanafunzi wa ngazi ya Stashahada na cheti pamija na walimu 3 na msafara huo ulikuwa na jumla ya magari 6 aina ya costa.
Ambapo alisema chanzo cha ajili hiyo imesababishwa na lori lililokuwa limebeba mafuta baada ya dereva aliyekuwa akiendesha gari hilo kuacha njia na kusababisha lori hilo kugongana na costa hiyo iliyobeba wanafunzi uso kwa uso na kusababisha dereva aliyekuwa akiendesha costa hiyo na wmwanafunzi mmoja kupoteza maisha na dereva wa lori akiwa amejeruhiwa na babadhi ya wanafunzi kujeruhiwa.
Aliongeza kwa kusema kuwa baada ya ajali kutokea majaruhi wote walipelekwa katika hospitali ya Tumbi ambapo Dereva aliyekuwa amebeba wanafunzi aliyefahamika kwa jina la Ally Zungu na mwanafunzi aliyefahamika kwa jina la Diedon Eliason Kibona wote walipoteza maisha ambapo waanfunzi wawili akiwemo Zubeda kishangi na  Dorotea Sarara wakiwa wamejeruhiwa vibaya wote wakiwa katika ngazi ya shahada.
Afisa wa Habari wa serikali ya wanafunzi Alex Mallya amesema kuwa mawanafunzi huyo alikuwa akitumikia serikali ya wanafunzi wa  Dsj akiwa kama Waziri Mkuu na kusema kuwa wamepokea msiba huo wa mwanafunzi mwenzao mpaka utakaposafirishwa kuelekea Tabora  kwa wazazi wake kwa mazishi ambapo kwa sasa mwili wa marehemu huyo uliwa kwa mama mdogo wa marehemu Tabata Dar es Salaam.
Mallya alisema kuwa majeruhi wawili waliokuwa katika hali mbaya wameamishwa katika hospitali hiho ya Tumbi wameweza kutolewa kutokana na ndugu wa majeruhi hawa kuwaleta Dar es Salaam.
Aidha mmoja kati ya wwanafunzi aliyeshuhudia ajali hiyo  Groly Amphrey alisema kuwa alishuhudia ajali hiyo baada ya kuona lori hilo likiwa linayumbayumba na ghafla aliona likiacha njia na kuvaana na gali walikuwa wamepanda na wanafunzi waliokuwa upande wa dereva kujeruhiwa vibaya.
Pia alisema kuwa baada ya kupata ajali wamepoteza baadhi ya vitu mbalimbali ikiwemo kamera, simu pamoja na mabegi yao na vibaka waliokuwa eneo hilo babada kutopata msaada wa haraka kutoka kwa polisi.
Hata hivyo taarifa kutoka kwa Kamanda wa Pwani kuhusiana na ajali hiyo ameshindwa kupatikana kutokana na kupigiwa simu kwa muda mrefu na kutopatiakana.

LADY JAYDEE KUADHIMISHA MIAKA 13 YA KUWA KATIKA FANI YA KUZIKI


JIDE

TANGAZO RASMI
Katika mwaka huu 2013, Inatimia miaka 13 tangu nianze kazi ya muziki.
Nashukuru MUNGU tuko pamoja na pia, nashukuru umma wa Tanzania kwa kuendelea ku support muziki wa Tanzania na kunipa nguvu mimi kama msanii.
Nashukuru vyombo vyote vya habari vinavyoshiriki kikamilifu kukuza na kulinda sanaa ya Tanzania bila kujali maslahi binafsi.
Tumeandaa sherehe kubwa na nzuri ya miaka 13 ya LADY JAYDEE, katika muziki.
Na mdhamini mkuu kwa upande wa media ni East Africa TV.
Sherehe ya miaka 13 ya Lady JayDee katika muziki itaambatana na uzinduzi wa album yangu ya sita inayokwenda kwa jina la NOTHING BUT THE TRUTH ambayo ina jumla ya nyimbo 10.
Katika sherehe hizo pia kutakuwa na show ya nyimbo zote bora za JayDee nikishirikiana na baadhi ya wasanii wenzangu hapa nchini.
Sherehe zitafanyika Ijumaa tarehe 31 May 2013.
Nawakaribisha wote tufurahi pamoja
Na Mungu awabariki

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi siku ya wafanyakazi duniani Mei mosi

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbasi Kandoro akizungumzana waandishi
Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za siku ya wafanyakazi duniani Mei mosi itakayofanyika kitaifa Mkoani Mbeya.
Pamoja na kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo pia anatarajiwa kuzungumza na wakuu wa shule na Wamiliki wa Vyuo binafsi ( katika ukumbi wa mkapa Apri 30 mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbasi Kandoro akizungumzana waandishi wa habari ofisini kwake amesema Raisi Kikwete anatalajiwa kuwasiri mkoani hapa Apri 30 mwaka kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa songwe majira ya saa4 na Nusu asubuhi.
Amesema mara baada  ya kuwasili mkoani hapa atazungumza na wamiliki wa shule hizo ambao alitajiwa kuzungumza nao Aprii 29 mwaka lakini ikashindikana kutokana na kuwepo kwa mkutano wa viongozi nchi za Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha.
Amesema mara baada ya kuingiliana kwa ratiba hiyo baadhi ya ratiba ambazo zilitarajiwa kufuatwa zimevunjwa hasa zile za uzinduaji wa shughuli mbalimbali za kimaendeleo hasa katika Wilaya ya Rungwe,Mbarali,Mbozi ambapo Mweshimiwa Rais Kikwete anatalajiwa kufanya ziara nyingine kwa ajili ya shuhuli hizo hapo baadae.
Kutokana na hali hiyo Mkuu huyo wa Mkoa amesema mara baada ya kuzungumza na wakuu wa shule pamoja na viongozi wa chama cha wafanyakazi( Tucta)ambapo baada ya hapo atapokea taarifa ya mkoa pia  kuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha Mei mosi ambapo jioni atalejea jijini Dar es salaam kuendelea na vikao vingine. 
Pia katika taarifa yake kwa waandishi wa habari jijini hapa Kandoro amewaomba radhi wananchi wa mkoa wa mbeya ambao walijiaanda kwa lengo la kumpkea kiongozi wao kutokana na kusitishwa kwa tatiba hizo.

REDD'S MISS HIGHER LEARNING MOROGORO 2013.

Mshindi wa Shindano la Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro, Anitha Mwakitwange kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe akipunga mkono mara baada ya kuvikwa taji hilo
 
Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro, Anitha Mwakitwange(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Rosemary Aloyce (kulia) na Mshindi wa Tatu Tarchisic Mtui mara baada ya warembo hao kutawazwa kuwa ndio washindi wa Shindano hilo
MAZOEZI YA MISS KIBAHA YAPAMBA MOTO

Mkufunzi wa Warembo wa Miss Kibaha Rehema Uzuwiya akizungumza na warembo hawo wakati wa mazoezi yao yanayo endelea katika ukumbi wa Vijana Kinondoni picha na www.burudan.blogspot.com

Warembo wa miss kibaha wakiwa katika pozi wakati wa mazoezi yao
Warembo watakao wania taji la Miss Kibaha wakiwa katika pozi wakati wa mazoezi yao yanayoendelea katika ukumbi wa vijana Kinondoni Dar es salaam picha na www.burudan.blogspot.com

NOMINEES KILIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARDS 2013

 
 
Majina ya wasanii, waandaaji muziki na vikundi kwa ajili ya tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013


WIMBO BORA WA MWAKA

Dear God - Kala Jeremiah
Leka dutigite - Kigoma all star
Mapito - Mwasiti Feat Ally Nipishe
Me n U - Ommy Dimpoz Feat Vanessa Mdee
Pete- Ben pol

MSANII BORA WA KIUME
Ben Pol
Diamond
Linex
Mzee Yusuf
Ommy Dimpoz

MSANII BORA WA KIKE
Isha Mashauzi
Khadija Kopa
Lady Jaydee
Mwasiti
Recho

MSANII BORA WA KIKE - TAARAB
Isha Mashauzi
Khadija Kopa
Khadija Yusuph
Leila Rashid

MSANII BORA WA KIUME - TAARAB
Ahmed Mgeni
Hashim Said
Mzee Yusuf

MSANII BORA WA KIUME - BONGO FLAVA

Ally Kiba
Ben Pol
Diamond
Linex
Ommy Dimpoz

MSANII BORA WA KIKE - BONGO FLAVA
Linah
Mwasiti
Recho
Shaa

MSANII BORA WA HIP HOP

Fid Q
Joh Makini
Kala Jeremiah
Profesa J
Stamina
 

Msanii Bora wa Kiume - Bendi
Chalz Baba
Dogo Rama
Greyson Semsekwa
Jose Mara
Khaleed Chokoraa

Msanii Bora wa Kike - Bendi

Anneth Kushaba
Luiza Mbutu
Mary Lucos
Vumilia

Msanii Bora anayechipukia

Ali Nipishe
Angel
Bonge la Nyau
Mirror
Vanessa Mdee


Video Bora ya Wimbo ya Mwaka

Baadae - Ommy Dimpoz
Kamili gado - Professor J Feat Marco Chali
Marry Me - Rich Mavoko
Nichum - Bob Junior
Party Zone - AY Feat Marco Chali

Mtunzi Bora wa Mashahiri - Taarab

Ahmed Mgeni
Hemed Omary
Khadija Kopa
Mzee Yusuf
Thabit Abdul

Mtunzi Bora wa Mashahiri - Bongo Flava

Ally Kiba
Barnaba
Ben Pol
Linex
Ommy Dimpoz

Mtunzi Bora wa Mashahiri - Hip Hop

Fid Q
Joh Makini
Kala Jeremiah
Mwana Fa
Stamina

Mtunzi Bora wa Mashahiri - Bendi

Chalz Baba
Grayson Semsekwa
Jonico Flower
Jose Mara
Khaleed Chokoraa

Mtayarishaji Bora wa Mwaka - Muziki wa Kizazi Kipya

Bob Junior
Ima the boy
Man Water
Maneke
Marco chali
Mensen Selecta

Mtayarishaji wa Wimbo wa Mwaka - Taarab

Bakunde
Enrico

Mtayarishaji wa Wimbo wa Mwaka - Bendi

Allan Mapigo
Amoroso

Mtayarishaji Chipukizi wa Mwaka

Imma the Boy
Mensen Selecta
Mr T Touch
Sheddy Clever

Rappa Bora wa Bendi

Fagasoni
Greyson Semsekwa
J4
Jonico Flower
Sauti ya Radi

Wimbo wenye vionjo vya asili

Aambiwe - offside trick
Atatamani - AT
Boma la utete - Young D
Chocheeni kuni - Mrisho Mpoto Feat Ditto
Mdundiko - Momba Feat Juma Nature

Wimbo Bora wa Bendi

Chanzo ni sisi - Mapacha watatu
Jinamizi la Talaka - Mlimani Park Orchestra
Risasi kidole - Mashujaa band
Shamba la twanga - African Stars band

Wimbo Bora wa Reggae

Hii si ya waoga - Yuzzo
Kilimanjaro - Warriors from The East
NATAFUTA PARADISE - Mac Malick Simba
Salvation - Delayla Princess
Tunda - Hardmad

Wimbo Bora wa Africa Mashariki

Fresh All Day - Camp Mulla
Make you dance - Keko Feat Madtrax
Maswali ya polisi - DNA
Still a Liar - Wahu
Valu Valu - Jose Chameleone

Wimbo Bora wa - Bongo Pop

Aifola - Linex Feat fundi Samweli
Baadae - Ommy Dimpoz Feat Angel
Chuki Bure - Sharo Milionea Feat Dully Sykes
Marry Me - Rich Mavoko
Me and you - Ommy Dimpoz Feat Vanessa Mdee

Wimbo Bora wa Kushirikiana/kushirikishwa

Chuki Bure - Sharo Millionea Feat Dully Sykes
Mapito - Mwasiti Feat Ally Nipishe
Me and U - Ommy Dimpoz Feat Vanessa Mdee
Sihitaji marafiki - Fid Q Feat Yvonne
Single Boy - Alikiba Feat Lady Jaydee


Wimbo Bora wa Hip Hop

Alisema - Stamina Feat Jux
Bum kubam - Nikki wa Pili Feat G Nako
Dear God - Kala Jeremiah
Nasema Nao - Nay wa Mitego
Sihitaji Marafiki - FID Q Feat Yvonne

Wimbo Bora wa RnB

Amerudi - Belle 9
Kuwa na Subira - Rama Dee Feat Mapacha
Maneno maneno - Ben Pol
Pete - Ben Pol

Wimbo Bora wa Ragga/ Dancehall

Je ni nani - Ras Six
Muda upite - Susu Man
Predator - Dabo
Push Dem - Dr Jahson
Take it down - Chibwa and Tanah

Wimbo Bora wa Taarab

Mjini chuo kikuu - Khadija Kopa
Mpenzi chocolate - Jahazi [Mzee Yusuph]
Si bure una mapungufu - Isha Mashauzi [Mashauzi Classic]
Sina muda huo - Jahazi [Leila Rashid]
Siwasujudii Viwavi jeshi -Isha Mashauzi [Mashauzi Classic]

Wimbo Bora wa Zouk/Rhumba

Gubegube -Barnaba
Mapito - Mwasiti Feat Ally Nipishe
Nashukuru umerudi - Recho
Ni wewe - Amini
Sorry - Barnaba

Bendi Bora ya Mwaka CD1 African Stars Band

Mapacha wa tatu
Mashujaa Band
Mlimani Park Orchestra [Sikinde]
Msondo Ngoma Music band

Kikundi Bora cha Taarab

Dar modern Taarab
Five stars modern Taarab
Jahazi Modern Taarab
Kings modern Taarab
Mashauzi Classic


Kikundi Bora cha Muziki wa Kizazi Kipya

Jambo squad
Makomando
Tip Top Connection
Tmk wanaume family
Weusi

Saturday, April 27, 2013

ARSENAL YASAKA VIFAA
asernal 06070
Arsenal iko tayari kumwaga mpunga kwa ajili ya Stevan Jovetic
 
asernal2 ee0dc
Arsenal pia inamtaka kipa wa Hamburg, Rene Adler

KLABU ya Arsenal imepiga hatua katika mbio zake za kuwania saini ya Stevan Jovetic baada ya kuanza mazungumzo na klabu yake, Fiorentina.
 
Habari zinasema kwamba, kocha Arsene Wenger anaihofia Chelsea kwa namna ilivyopanga kujisuka upya. 

The Gunners wamekuwa wakimfuatilia Jovetic, mwenye umri wa miaka 23, tangu mwaka 2011 na wakati klabu hiyo ya Serie A inamthaminisha kwa kiasi cha Pauni Milioni 25, Arsenal — ambayo ina bajeti ya Pauni Milioni 70 za usajili, inataka ipunguziwe bei ya kumnunua mchezaji huyo.

Hatua ya klabu hiyo kufanya jitihada za mapema kumnasa Jovetic ni dalili nzuri, haswa ikizingatiwa Manchester City na Juventus zote zinamtaka mshambuliaji huyo. Dili lolote litategemea na Arsenal kama itafuzu kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Wenger, pia anatazamia kumsajili kipa mpya wa kwanza, na amekuwa akimmulika mlinda mlango wa Hamburg, Rene Adler tangu Machi. 

Arsenal inaona kulikoni kutoa Pauni Milioni 15 kuwanunua ama kipa wa Stoke, Asmir Begovic au wa Sunderland, Simon Mignolet, bora kutoa Pauni Milioni 8 kumnasa kipa huyo Mjerumani. 

Wenger anataka kuboresha kikosi chake kujiandaa kupambana na Chelsea ambayo iko mbioni kuwasajili kiungo mshambuliaji wa Bayer Leverkusen, Andre Schurrle na mshambuliaji wa Atletico Madr
AFRIKA IKATAE KUGAWANYWA , KUNYONYWA
Baraza Kuu la  Umoja wa Mataifa,  mwishoni mwa wiki limepitisha kwa kauli moja  Tamko la Kisiasa kuhusu Utatuzi wa  Migogoro  Barani Afrika kwa njia ya  Amani.

Tamko hilo  ambalo ndani yake  linaainsha  na kutambua mchango mkubwa wa   Muungano wa Nchi Huru za Afrika  (OAU) na sasa Muungano wa Afrika ( AU)  katika kuchagiza  na kusimamia  pamoja na mambo mengine, maendeleo ya nchi za Afrika na watu wake,  kupiga vita  umaskini, ujenzi wa utawala bora, demokrasia , haki za  binadamu na utatuzi wa migororo kwa njia za amani.
 
Kabla ya kupitishwa kwa Tamko hilo,  Baraza Kuu la Umoja wa  Mataifa,  kwa siku nzima ya Alhamisi na ijumaa asubuhi lilijikita katika  majadiliano  ya mada iliyohusu ‘utatuzi wa migogoro kwa njia ya amani barani afrika’, ikiwa pia ni sehemu na  Baraza hilo kuadhimisha miaka  50   tangu kuanzishwa kwa OAU na baadaye AU.
Miongozi wa viongozi wakuu walioshirikia majadilaino hayo, na ambayo yaliandaliwa na Bw. Vuk Jeremic,   Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon,   Rais wa  Equatoria Guinea Theodore Obiang Nguema Mbasogo, Rais Mstaafu wa Burundi Jean Pierre Buyoya  ambaye pia     Mwakilishi  maalum wa Muungano wa Afrika  huko Mali na Sahel,  wakiwamo pia mawaziri  kadhaa wa  Mambo ya Nchi za Nje.

Akiungana na wazungumzaji wengine katika mkutano huo, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Tuvako Manongi, pamoja na kuainisha sababu na vyanzo vya migogoro Barani Afrika, alisema, Afrika lazima ifikie mahali ikatae kugawanywa.

“Bara la Afrika lina fursa  nyingi,  Afrika inapanda chati. Afrika lazima ikatae kugawanywa, ikatae kudharauliwa na ikatae  kunyonywa” akasema Mwakilishi wa Kudumu, Tuvako Manongi.

Na kubainisha kwamba,  Afrika lazima pia ikatae kutambuliwa kama bara ambalo limejaa migogoro  . “  Huu ni wakati wa  kufufua  upya pan africanism,  hiki ni kipindi cha mwamko mpya wa Afrika. Lazima tufanye kazi kwa pamoja  ili kuwapa matumaini watu wetu” akasisitiza Manongi.

Wakati tukisherehekea maadhimisho ya miaka 50 wa OAU,  ni  vema kila mmoja wetu akaahidi  upya  kuimarisha ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na
Muungano wa Afrika  kama ilivyoainishwa  katika  Sura ya Saba ya Katima ya Umoja  wa Mataifa.

Akatoa mfano kwa kusema  uhusiano huo unapashwa kuendelezwa katika nyanja zote za  usalama na  maendeleo.  Kama ambavyo imeshashuhudiwa  katika   uundwaji wa Jeshi la  Mseto  kati ya Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika   katika Jimbo la Darfur ( UNAMID),  Misheni ya  Muungano wa Afrika huko Somalia, (AMISOM0  na tukio la hivi karibuni la kurejewa na  kuongozewa uwezo mpya Misheni ya Kutuliza Amani katika DRC ( MONUSCO) kulikoendana na kuridhiwa  upelekaji wa Brigedi Maalum inayoundwa na wanajeshi kutoka Tanzania, Afrika ya Kusini na Malawi.

Aidha akasema majadiliano hayo  ya Baraza  Kuu la Umoja wa Mataifa, yamefanyika ikiwa  ni siku chache tu,   tangu kufanyika kwa Mkutano wa Baraza la Usalama la Afrika katika ngazi ya Mawaziri nchini Tanzania,  mkutano ambao pia ulijadili kwa kina pamoja na mambo mengine  hali ya usalama  barani afrika , vyanzo vya migogoro na ufumbuzi wake.

Karibu wazungumzaji wote  wakiwamo wawakilishi wa Marekani na Jumuiya ya Ulaya waliochangia majadialiano hayo ya utanzuaji wa migogoro kwa njia ya amani, licha ya  kutambua, kusifu na kupongeza kazi kubwa ambayo imefanywa na inaendelea kufanywa na   Muungano wa  Afrika na Taasisi za Kikanda katika kipindi cha miaka 50 iliyopita, walisisitiza haja na  umuhimu wa Jumuiya ya Kimataifa kuendeleza ushirikiano wake na Muungano wa Afrika.
Aidha wazungumzaji huo walitambua na kukiri kwamba  Bara la Afrika licha ya  changamoto mbalimbali zikiwamo za migogoro inayoibuka hapa na pale,  imepiga hatua kuubwa za kimaendeleo, kiuchumi na kijamii na kwamba   Bara hilo linastahili kupongezwa na kuendelea kusaidiwa.

Friday, April 26, 2013

UGONJWA HATARI WA MAHINDI WAINGIA NCHINI
1 d4899
Ugonjwa hatari unaoshambulia mahindi na kusababisha saratani kwa binadamu umeingia nchini na wakulima sasa wametahadharishwa kutokula mahindi hayo wala unga ambao haujakobolewa.
Mahindi yaliyoathiriwa na ugonjwa huo huota 'fungus' ambao ina sumu inayoitwa 'Aflatoxin' ambayo inaweza kusababisha madhara kwa wanyama na binadamu hususan ugonjwa wa saratani.
Mbali na kutikisa mikoa kadhaa na kusababisha hasara kubwa kwa wakulima, ugonjwa huo ambao umeanzia nchini Kenya unaendelea kusambaa kwa kasi na sasa umeingia pia nchini Uganda.
Awali ugonjwa huo uliripotiwa kuzikumba wilaya za Babati mkoani Manyara na Meatu mkoani Shinyanga tu, lakini sasa umesambaa hadi katika mikoa jirani ikiwamo Kilimanjaro
.
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Leonidas Gama jana alilithibitishia gazeti hili kuwa mkoa wake umekumbwa na ugonjwa huo na tayari umesambaa katika wilaya tatu; Moshi Vijijini, Siha na Hai. "Ni kweli baadhi ya wilaya zimekumbwa na ugonjwa huo, bahati mbaya sana hauna tiba na unasambaa kwa kasi... Wataalamu wanaendelea kuwaelimisha wakulima kutambua dalili zake," alisema Gama.
Gama alisema endapo mkulima atabaini shamba lake kushambuliwa na ugonjwa huo katika hatua za awali, anachotakiwa kufanya ni kung'oa mimea yote ya mahindi na kuichoma moto.
Mkuu wa Wilaya ya Hai, Novatus Makunga alisema takriban hekari 14 zimeshambuliwa na ugonjwa huo katika shamba la Watawa wa Kanisa Katoliki Mailisita na shamba la mkulima wa Lambo.
Alisema tayari wataalamu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo ya Selian (SARI) ya Jijini Arusha wamefika wilayani humo na kutoa tahadhari kwa wakulima juu ya athari za ugonjwa huo. Mfanyabiashara mashuhuri wa mjini Moshi, John Bennett anayemiliki mgahawa wa Golden Shower aliitaka Serikali kutoa elimu kwa wananchi na wafanyabiashara na kuchukua tahadhari.
"Utajuaje unga wa dona haukutokana na hayo mahindi au pumba ya chakula cha mifugo hayakutokana na hayo? Hili jambo ni zito sana si la kufanyia utani hata kidogo"alisema Bennett.
Mkulima wa Kijiji cha Kikavu Chini wilayani Hai, Justine Mvungi alisema wataalamu kutoka SARI wamewataka kuchoma moto miche ya mahindi ambayo watagundua imeshambuliwa.
"Wametuambia takriban shamba likishambuliwa, tung'oe mahindi hayo na kuyachoma moto, wametuambia kama tulishavuna basi tukoboe mahindi hayo maana kiini chake kina madhara,"alisema.
"Aliongeza kusema" hata tukikoboa mahindi tumeambiwa zile pumba zake tusiipe mifugo kwa sababu itaathirika... Ugonjwa huu wa mmea wa mahindi umeleta taharuki kubwa kwa wakulima na wananchi."CHANZO MWANANCHI
LEMA ATIWA MBARONI
lema ee56f
Godbless Lema

Jeshi la polisi mkoani hapa limemtia mbaroni mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godless lema kwa tuhuma za uchochezi kwa wanafunzi  kwenye chuo cha uhasibu mwanzoni mwa wiki katika vurugu zilizotokea chuoni hapo baada ya mwenzao kuuwawa juzi usiku huko maeneo ya njiro jijini hapa.
Akizungumza na vyombo vya habari leo ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani hapa kamishna msaidizi wa polisi Liberatus Sabas alisema kuwa mh.lema alikamatwa huko nyumbani kwake Njiro majira ya saa 9 usiku.
Sabas alisema jeshi hilo linaendelea na mahojiano na mtuhumiwa na kuwa katika tukio hilo zaidi ya watuhumiwa 14 walifikishwa mahakamani jana na kuwa hao hawezi kuwaongelea kwani kesi yao ipo kwenye chombo hicho cha sheria.

Pia kamanda sabas alisema kuwa mh.lema anashikiliwa kutokana na vurugu zilizotokea juzi kwenye chuo cha uhasibu na kuwa atafikishwa mahakamani siku ya jumatatu.
Kwa upande mwengine akijibu baadhi ya maswali ya wanahabari kamanda alisema kuwazaidi ya hao 14 na  Lema hakuna mtuhumiwa mwingine aliyakamatwa kwani ilisemakana wakili wake Albert Msando nae amekamatwa.
Mnamo siku ya jumatatu mwanafunzi mmoja aliuwawa kwenye mitaa ya njiro hali iliyoleta tafrani hadi wanafunzi hao walipoleta vurugu chuo hapa na polisi kutumia mabomo ya machozi kuwatawanya sekeseke hilo lilimalizwa na jeshi la polisi baada ya wanafunzi kutotii amri ya mkuu wa mkoa huo  Magessa Mulongo na kuanza kuingia barabarani kuandamana. Chanzo: www.fullshangweblog.com
MAONYESHO YA NDEGE ZA KIVITA KWENYE SHEREHE ZA MUUNGANO
un16 b0a8e
 
un17 bc80f
Ndege za kivita.
ndege2 26788
 

ndege3 93d4d

 ndege dda40

Chanzo: Muhidin Michuzi
YANGA YATWAA UBINGWA BAADA YA AZAM KUTOKA SARE 1-1 NA COASTAL UNION
Yanga f391d
Kikosi cha Yanga

Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salam
Klabu ya Yanga ya Dar es salaam leo imejitangaziwa ubingwa wake wa 24 wa ligi kuu soka Tanzania bara baada ya wapinzani wake wakubwa kwa muda mrefu klabu YA Azam fc kutoa sare ya kufunga bao 1-1 na Wagosi wa kaya Coastal unioni katika dimba la CCM Mkwakwani jijini Tanga.

Matokeo hayo yana maanisha, Azam FC waliokuwa washindani wakuu wa Yanga SC waliojikusanyia pointi 56 kibindoni, hawawezi tena kufikisha pointi hizo ambazo wanazo mabingwa hao wapya, kwani hata wakishinda mechi zao nyingine  mbili zilizobaki, watamaliza na pointi 54. 

 Shukurani kubwa kwa  nyota wa Coastal union Danny Lyanga, ambaye aliifungia Coastal bao la kusawazisha dakika ya 72 akipokea pande maridhawa kutoka kwa nyota wa zamani wa Yanga Pius Kisambale. 
Azam ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao katika mchezo wa leo, lililofungwa na beki Aggrey Morris kwa penalti dakika ya 60, baada ya mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC, Gaudence Mwaikimba kuchezewa rafu kwenye eneo la hatari  na beki Yussuf Chuma- na refa Andrew Shamba wa Pwani akaamuru pigo hilo.

Matokeo haya yanakuwa sawa na Coastal kulipa fadhila kwa Yanga, kwani hata wao, ubingwa wao pekee wa Ligi Kuu waliochukua mwaka 1988 ulitokana na ‘msaada’ wa wana Jangwani hao.
Kilichobaki kwa Yanga sasa ni kulinda heshima kutokana na kubakiwa na mechi mbili ambapo watashuka dimbani kuvaana na Coastal union waliowapa ubingwa msimu huu pamoja na mechi ya kufunga dimba dhidi ya Mnyama Simba uwanja wa Taifa Dar es salaam
Lakini licha ya Coastal union kuwapa ubingwa wanajangwani hao, Kocha mkuu wa wagosi Wakaya Hemed Morroco  amesema mchezo wa leo walistahili kushinda na kilichokwamisha ushindi leo ni waamuzi kuchezesha hovyo.

“Unajua Azam walikuwa na Presha kubwa ya kutaka ushindi, lakini tuliwabana na waamuzi wameshindwa kuchezesha vizuri na ndio maana wameambulia sare vinginevyo walikuwa wanafungwa leo”. Alisema Morroco.
Kikosi cha Coastal Union leo kilikuwa; Shaaban Kado, Hamad Khamis, Othman Tamim, Philip Mugenzi, Yussuf Chuma, Abdi Banda, Joseph Mahundi, Razack Khalfan, Pius Kisambale/Mohamed Soud dk85, Suleiman Kassim ‘Selembe’/Danny Lyanga dk71 na Twaha Shekuwe. 
Azam FC; Mwadini Ally, Himid Mao, Erasto Nyoni, David Mwantika, Aggrey Morris, Jabir Aziz/Salum Abubakar ‘Sure Boy Jr.’ dk75, Brian Umony/Seif Abdallah Karihe dk68, Ibrahim Mwaipopo, Gaudence Mwaikimba/Abdi Kassim ‘Babbi’ dk82, Humphrey Mieno na John Bocco ‘Adebayor’.


TASWIRA ZA MBALIMBALI ZA SHEREHE ZA MIAKA 49 ZA MUUNGANO 
00 6acbb
Rais Jakaya Kikwete akiingia uwanjani huku akiwasalimia wananchi


11 eeed4
Rais Akikagua gwalide


22 4d38c

33 8d047
USD 117 M ZIMETENGWA KWA AJILI YA BAJETI YA JUMUIYA YA AFIRKA MASHARIKI
Logo-ya-Jumuiya-ya-Afrika-Mashariki
Mahmoud Ahmad Arusha
Jumla ya kiasi cha dola za marekani million 177,238,966 zimetengwa kwenye bajeti ya jumuiya ya Afrika ya mashariki kwa mwaka wa fedha 2013-14 na kuidhinishwa na baraza la mawaziri wa jumuiya hiyo kwenye kikao chao cha 26 dharura kilichoisha leo(jana) jijini hapa. Mbali ya bajeti hiyo;
mkutano huo ulioanza mnamo tarehe 22-23 kwa ngazi ya wataalamu na kufuatiwa na mkutano wa makatibu wakuu wa nchi wanachama na kupokea hatua zilizofikiwa katika majadiliano ya itifaki ya umoja wa fedha wa jumuiya ya Afrika ya mashariki ambao unatarajiwa kutiwa saini na wakuu wa jumuiya hiyo katika mkutano wao wa 15 mwezi wa november mwaka huu.
 Aidha mkutano huo utajadili pia pendekezo la kuongeza wigo wa mamlaka ya mahakama ya Afrika ya mashariki kwa kupitia mapendekezo yaliojadiliwa kwenye vikao vya wataalamu na makatibu wakuu wa jumuiya hiyo.
 Katika hatua nyingine mkutano huu wa dharura wa 26 wa jumuiya ya Afrika ya mashariki ambao unaisha leo na kuwakutanisha wataalamu na makatibu wakuu kutoka nchi wanachama wa jumuiya ya Afrka ya mashariki umejadili mambo matatu makuu yatakayopelekwa kwenye mkutano wa viongozi wakuu wa jumuiya hiyo kwa ajili ya kutia saini.
 Kwa upande mwingine mkutano huu umejadili pia hatua iliyofikiwa katika uandaaji wa itfaki ya hadhi na kinga kwa watumishi wa jumuiya na taasisi zake zote.
KENYATTA ATANGAZA MAJINA 12 YA MAWAZIRI
3 ff781
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta (kushoto) akiwa na Makamu wa Rais William Ruto wakati wa kutangaza majina ya Mawziri wapya.
Orodha ya leo imefanya idadi ya Mawaziri hao walioteuliwa kufikia Mawaziri 16 huku wananchi wakiendelea kusubiri nafasi mbili kwani awali Rais Kenyatta aliutangazi umma kuwa baraza lake la mawaziri litakuwa na watu 18 tu:CHANZO MWANANCHI.

Wednesday, April 24, 2013

DORTMUND 4-1 MADRID: LEWANDOSKI AWA MCHEZAJI WA KWANZA KUIFUNGA MADRID MABAO MANNE KWENYE HISTORIA YA CHAMPIONS LEAGUE - CRISTIANO RONALDO AWEKA REKODI 2 BINAFSI

Dortmund* Mshambuliaji wa Dortmund Robert Lewandowski ndio mchezaji wa kwanza kufunga mabao manne dhidi ya Real Madrid katika historia ya ligi ya mabingwa wa ulaya.

* Ilikuwa ni mara ya 10 kwa mchezaji mmoja kufunga mabao zaidi ya manne katika mechi moja ya Champions League. Lionel Messi pekee ndio mchezaji aliyefunga mabao manne mara mbili katika mechi 2 za ligi ya mabingwa wa ulaya.


* Huu ndio msimu wa kwanza ambapo timu zimeruhusu nyavu zao kuguswa mara 4 katika mechi za hatua ya kutoana kwenye ligi ya mabingwa wa ulaya. Bayern 4-0 Barcelona, Dortmund 4-1 Real Madrid.


* Cristiano Ronaldo nae ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa 3 kufunga kwenye mechi sita mfululizo za ligi ya mabingwa ulaya, wengine waliofanya hivyo ni Chamakh na Burak Yilmaz.


* Ronaldo amekuwa mchezaji wa tano kuweka rekodi ya kufikisha mabao 50 ya Champions League. Akiwafuatia Raul 71, Lionel Messi 59, Ruud van Nistelrooy 56 and Thierry Henry 50.


* Timu pekee iliyowahi kugeuza matokeo baada ya kufungwa 4-1 katika mchezo wa kutoana wa Champions League ni Deportivo La Coruna ambao walifungwa 4-1 na AC Milan katika mechi ya kwanza jijini Milan lakini wakaenda kushinda 4-0 kwao Hispania.


* Katika historia michuano ya ulaya ya klabu kumekuwepo na fainali moja tu iliyowakutanisha timu kutoka Ujerumani. 1979-80 UEFA Cup, Frankfurt wakiwafunga Borussia Moenchengladbach.
WACHEZAJI SIMBA WAWEKWA KITI MOTO KUHAKIKISHA TIMU INAMALIZA NAFASI YA 3


Benchi la ufundi la Simba jana liliwekwa kitimoto na uongozi wa klabu hiyo kutakiwa kuakikisha  inamaliza ligi katika nafasi ya tatu.

Ofisa habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alithibitisha kuwepo kwa kikao hicho jana ambapo alisema kilikuwa cha kupanga mikakati ya mechi zilizobaki.  "Ni kweli tulikuwa na kikao jana kati ya benchi la ufundi na uongozi.
"Tageti ni kupanga mikakati jinsi gani tufanye kuakikisha timu yetu inamaliza ligi katika nafasi yatatu. Pia, wao walitoa maoni yao. Kwa hiyo kilichobaki ni utekelezaji kutimiza malengo ambayo tumejiwekea." alisema Kamwaga.
"Azam ambayo inashika nafasi ya pili, wametupita na pointi 11. Kwa hiyo nafasi ya pili itakuwa ngumu kwetu." 

Aliongeza kuwa labda itokee Azam wapoteze michezo yao yote iliyobaki na kisha wao washinde kitu ambacho ni kigumu kwa upande wao.
Simba imebakiza mechi tatu dhidi ya Ruvu Shooting, Polisi Moro, Mgambo JKT na Yanga ambayo akishinda yote atakuwa na pointi 48.
Kwa sasa, Simba inagombea nafasi ya tatu na Kagera Sugar ambayo ina pointi 40 na kubakiwa na mechi mbili. Alisema wamekubali kuwa msimu huu wamepoteza lakini wazishuke zaidi ya nafasi ya tatu hivyo iliwaweze kujipanga kwa ajili ya mwakani
LUIS SUARES AFUNGIWA MECHI KUMI KWA KUMNG'ATA IVANOVIC

LUIS SUAREZ amefungiwa mechi 10 kwa kitendo chake cha kumng'ata Branislav Ivanovic.

Mshambuliaji huyo wa Liverpool ambaye haiishi vituko uwanjani jana alikiri kwamba alifanya kweli shambulio hilo. Na leo hii FA wamemaliza msimu wake kwa kumpa adhabu ya mechi 10. 
Kwa kawaida adhabu ya kitendo cha vurugu huwa ni mechi zisizodi 3 lakini wamesema kwamba adhabu hiyo haitoshi kwa Suarez ambaye amekuwa mtukutu kwa matukio ya ajabu ajabu kila mara. 

Suarez jana usiku alikataa kukubaliana na adhabu ya zaidi ya mechi 3. Lakini leo FA wameamua vinginevyo kwa bad boy Suarez na hivyo atakumbana na adhabu ya kutocheza mechi 10 za mashindano yaliyo chini ya FA. l

Mkurugenzi wa Liverpool  Ian Ayre alisema: "Sote klabu na mchezaji husika tumeshtushwa na kutopendezewa na maamuzi haya - tunasubiri sababu za kimaandishi kabla hatujatoa uamuzi wowote hapo kesho."

Suarez ana muda mpaka Ijumaa kupinga adhabu hiyo kwa kukata rufaa.
UJUMBE WA TANZANIA KATIKA CHAKULA CHA PAMOJA WASHINGTON DC
IMG 3865 ed0d4
Kutoka kushoto ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Natu Mwamba, Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Harry Kitilya pamoja na Katibu wa Waziri wa Fedha Bw. Omary Khama wakati wa chakula cha pamoja.

  IMG 3914 42890
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma, Mdau wa Ubalozini Bw. Baraka Daudi na Afisa Mawasilianowa Wizara ya Fedha Bi. Eva Valerian wakitabasamu mara baada ya chakula cha pamoja katika ofisi za ubalozi wa Tanzania Washington DC.

IMG 3879 78219
Ujumbe wa Tanzania katika chakula cha pamoja. Kutoka kushoto ni Afisa Mawasiliano Ubalozi wa Tanzania-Washington DC Bi Mindi Kasiga, Afisa Itifaki Wizara ya Fedha Bw. Cyprian Kuyava, Naibu Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Prof. Longinus Rutasitara, watatu wanaofuata ni wachumi wa Wizara ya Fedha Bw. Erasto, Patric Pima, Veronica Maina na mchumi wa Benki Kuu ya Tanzania Dkt. Dickson Lema.

IMG 3920 6bc1e
Baadhi ya viongozi wa Tanzania waliohudhuria mikutano ya majira ya kipupwe katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa ubalozi wa Tanzania Washington DC. Waliokaa, kutoka kushoto ni Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Harry Kitilya, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu, Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa Kaimu Balozi wa Tanzania Washington DC Bibi. Lily Munanka na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bi. Natu Mwamba.

IMG 3924 0a017
Ujumbe wa Tanzania katika picha ya pamoja na Kaimu Balozi wa Tanzania Washington DC aliyevaa blauzi nyekundu Bibi. Lily Munanka baada ya chakula cha pamoja. Chanzo: Eva Valearian na Ingiahedi Mduma, Wizara ya Fedha.
VURUGU ZAZUKA CHUONI ARUSHA BAADA YA MWANAFUNZI KUCHOMWA KISU NA KUFARIKI
5 3d33a
6 0f854
7 d7068
*CAUTION/ILANI: Taarifa hii ni ya awali kutoka kwa watu mbalimbali. Unafahamishwa tu kuwa na ufahamu wa kinachoendelea. Taarifa kamili na iliyo rasmi itatolewa na vyombo husika.
---
Taarifa katika mitandao jamii zinaeleza kwamba usiku wa kuamkia leo, kijana mmoja wa kiume ambaye ni mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (Arusha Institute of Accountancy) aliyekuwa anasomea shahada ya kwanza Uchumi na Fedha (Bachelors Degree in Economic and Finance) mwaka wa pili (BEF2), amefariki dunia baada ya kuchomwa kisu.

Taarifa za awali kutoka chuoni hapo ambazo bado hazijathibitishwa na Jeshi la Polisi zinaeleza kwamba kijana huyo anahisiwa kuchomwa kisu na vibaka wakati akirejea kwenye maeneo yao ya malazi (hosteli) eneo la ESAMI.
Inaelezwa kuwa, kabla ya kufika hostel, alipigiwa simu na mwenziye kuwa amsubiri ili waongozane pamoja kuelekea hostel. Wakati akisubiri rafiki yake amfikie, ndipo watu wasiofahamika waliokuwa wanadai wapatiwe fedha, walimvamia na kumchoma kisu tumboni na shingoni.
Rafiki wa marehemu naye pia alichomwa kisu tumboni.
Mbunge wa Arusha Mjini, Mhe. Godbless Lema alifika chuoni hapo na kuzungumza na wanafunzi hao ili kuwatuliza baada ya kutaarifiwa kuwa kuna vurugu zilizotokana na hasira ya Wanachuo kumshutumu Mkuu wa Chuo kutokuwapa msaada wa haraka hasa baada ya wao kulalamika kwa muda mrefu sasa kuhusu hali duni ya usalama katika chuo hicho. Mwaka jana mwanafunzi mmoja aliuawa na katika nyakati tofauti, wanafunzi wamekuwa wakivamiwa na kuibiwa vifaa vyao.
Taarifa pia zilimfikia Mkuu wa Mkoa, Magessa Mulongo ambaye aliwasili chuoni hapo na kuzungumza na wanachuo lakini ilizuka tafrani ndipo Wanachuo walianza kurusha mawe.
Kikosi maalumu cha Askari Polisi wa kutuliza ghasia, FFU, kipo katika eneo hilo kwa ajili ya kufanya kazi yake.
CHANZO:WAVUTI

POMBE YAMTOA MADEE...ANADAI IMEMPA HESHIMA KUBWA MTAANI


Msanii wa Kundi la Tip Top Connection, Madee au Rais wa Manzese ameeleza kuwa wimbo wake wa Nani Kamwaga Pombe Yangu umempa heshima kubwa.
  

Akiongea  na  mwandishi  wetu, Madee, ambaye jina lake halisi ni Hamad Ally Seneda alisema licha ya kupata shoo nyingi, lakini pia ni wimbo ambao unapigwa sana kwenye klabu mbalimbali na kila unapopigwa hakuna anayekaa kitini.
Alisema kuwa kufuatia kutoa wimbo huo ameshakusanya Shilingi 16 milioni.
Alisema pamoja na kupata fedha nyingi kupitia wimbo huo bado hajaamua azifanyie nini ila ameamua atulie kwanza akitafakari nini kinafuata.
“Wimbo bado upo juu na unafanya vizuri, hivyo ninachofanya kwa sasa ni kuendelea kukusanya fedha kutokana na shoo ambazo nitapata kutoka kwenye wimbo huo baada ya hapo ndio nitajua nifanyie nini,” alieleza.
Aidha, Madee alisema kuwa anafurahi kuona amefanya kitu ambacho kila mpenda burudani kinamfurahisha kwani sio wasanii wengi ambao wanaweza kufanya kitu kama hicho hasa kwa wale waliopo kwenye usanii kwa muda mrefu. Kalunde Jamal

Tuesday, April 23, 2013

"HATUOGOPI VITISHO VYA WAASI WA M23....NI LAZIMA TUPELEKE JESHI DRC"....WAZIRI MEMBE

Dar es Salaam haitarudi nyuma katika kupeleka majeshi huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kama sehemu ya kikosi cha kuingilia kati cha Umoja wa Mataifa, licha ya maonyo mawili ya maandishi kutoka kikundi cha waasi cha March 23rd Movement (M23), maafisa wa Tanzania wasema.

Waasi wa M23 wakiondoka toka milimani tarehe 30 Novemba, 2012, baada ya kuondoka kijiji cha Karuba cha mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. [Na Phil Moore/AFP]

Salva Rweyemamu, mkurugenzi wa mawasiliano wa raisi wa Tanzania, aliiambia Sabahi kuwa serikali ilipokea barua mbili kutoka kikundi cha M23, ambacho kinapigana ili kuiangusha serikali ya Kongo.

Barua ya kwanza ilielekezwa kwa Mwenyekiti Mkutano wa Kimataifa wa Maziwa Makuu, Raisi wa Uganda Yoweri Museveni, na nyakala kupelekwa kwa wakuu wote wa serikali wa kanda hiyo, akiwemo Raisi wa Tanzania Jakaya Kikwete.

Barua ya pili ilitumwa kwa spika wa Bunge la Taifa Anne Makinda na kutiwa saini na Bertrand Bisimwa, mkuu mpya wa tawi la kisiasa la M23, iliyofika bunge la Tanzania siku ya Jumamosi (tarehe 20 Aprili), vyanzo viliiambia Sabahi.

Mkuu wa kijeshi wa M23 Jenerali Sultani Makenga (katikati) akiwaashiria baadhi ya maafisa wake karibu na mji wa Sake, mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, tarehe 30 Novemba, 2012. [Na Phil Moore/AFP]

Katika barua hiyo, M23 iliwataka wabunge wa Dar es Salaam kuishauri serikali dhidi ya kupeleka majeshi huko DRC, na hata kutishia "mauaji" ya majeshi ya Tanzania na wapiganaji wa M23 ikiwa Tanzania itaendelea mbele na upelekaji wa majeshi yake huko.

Kurejesha amani

"Lengo la majeshi ya Tanzania sio kuwaua Wakongo bali kurejesha amani," naibu Spika wa Bunge la Taifa la Tanzania Job Ndugai aliiambia Sabahi. "M23 wataona hili kuwa ni tatizo ikiwa hawataki amani. Hatupeleki askari wetu kwenda kuua au kuuliwa na M23."

Hapo tarehe 28 Machi, Baraza la Usalama la UN kwa kauli moja lilipitisha Azimio 2098, ambalo lilisafisha njia kwa chombo cha kwanza cha kimataifa cha kikosi cha "mashambulizi". Mamlaka ya kikosi hicho cha kuingilia kati, itakayoundwa na vikosi vya askari wa miguu kutoka Tanzania, Afrika Kusini, Msumbiji na Malawi, ni "kuwamalizia nguvu na kuwanyang'anya silaha" wa M23, waasi wa Kongo na vikundi vyenye silaha vya kigeni huko mashariki ya DRC, kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Umoja wa Mataifa.

Katika barua ya tarehe 11 Aprili, Bisimwa alionya kwamba M23 itaishinda kikundi cha UN itakachoongozwa na jenerali wa Tanzania.

Mnamo tarehe 7 Aprili, Bisimwa alitoa vikosi kama hivyo kwa majeshi ya Afrika Kusini katika akaunti yake ya Twitter, lakini Afrika Kusini ilisema kuwa itaendelea na mipango yake ya kujiunga na kikosi cha uingiliaji kati cha UN huko DRC.

Kwa majibu ya barua ya Bisimwa kwa Spika Makinda, Azimio 2098 "linabadilisha Misheni ya UN ya Kulinda Amani huko DRC na kuifanya kuwa kikosi cha vita chenye amri ya kufanya operesheni za mashambulizi dhidi ya wananchi wa Kongo".

Bisimwa, ambaye anaushutumu Umoja wa Mataifa kwa kuingilia kati DRC kwa ajili ya kuiokoa serikali ilioko madarakani, kiliapa kuwa vikosi vya M23 vitaishinda kikosi cha uingiliaji kati.

Alisema kuwa anamheshimu sana raisi wa kwanza wa Tanzania, marehemu Mwalimu Julius Nyerere, lakini bado M23 itakuwa haina chaguo jengine bali "kuyaua majeshi ya ndugu zao kutoka Tanzania".

Kanali Kapambala Mgawe, msemaji mkuu wa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi la Tanzania, alirudia kusema kuwa vikosi vya Tanzania vinakwenda Mashariki mwa DRC kuleta amani katika eneo hilo.

"Ambapo maisha ya wananchi wa DRC au walinda amani itakuwa katika hali ya hatari, vikosi vyetu vitaokoa maisha na kuwanyang'anya silaha wale wanaosababisha hatari hiyo," aliiambia Sabahi. "Huu ni msimamo na maelekezo kutoka UN."

Vitisho huko nyuma
Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa Bernard Membe aliiambia Sabahi kuwa Tanzania imezowea kupokea vitisho kama hivyo visivyo na msingi kutoka vikundi vya waasi kila mara majeshi yake yanapoingilia kati kuwaokoa watu wasio na hatia.

Kama mfano, alitaja uingiliaji kati kijeshi wa Umoja wa Afrika huko Anjuan, katika visiwa vya Komoro, ambao ulimuondoa madarakani raisi wa zamani Kanali Mohamed Bacar. Licha ya vitisho kama hivyo dhidi ya mchango wa majeshi kutoka Dar es Salaam, vikosi vya Tanzania havikurudi nyuma, Membe alisema.

"Nadhani wao [M23] wangemuenzi Mwalimu Nyerere kwa kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vinasababisha ubakaji uliotapakaa, vifo vya watoto na wanawake, na watu wanaokimbia makazi yao," alisema.

Membe alisema M23 kinapaswa kumaliza uasi wake na kuacha kuua watu wasio na hatia, kwa hivyo kutoipa Tanzania sababu yoyote ya kupeleka kikosi chake DRC.
WALIOFUKIWA MGODINI WAOKOLEWA WAKIWA HAI
mg ce981
 Watu wanne wamenusurika kufariki dunia baada ya udongo wenye mawe kuwafukia chini katika shimo zaidi ya saa 12 walipokuwa wakichimba dhahabu katika Kijiji cha Patamela wilayani Chunya.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Deodatus Kinawiro alithibitisha k wa njia ya simu jana juu ya tukio hilo na kwamba lilitokea Ijumaa iliyopita, ambapo uokoaji ulifanywa na Kampuni ya Shanta Gold Mining inayochimba dhahabu kilometa 10 kutoka eneo la tukio.
Kinawiro aliwataja walionusurika kuwa ni Antony Rwegasira(28), Pascal Claud(33) , John Gideon(47) na Noni Kwandu (40) wote wakazi wa wilayani humo.CHANZO MWANANCHI.
BAYERN YAIBUKA KIDEDEA BARCELONA YALALA KWA 4-0
9 54585
Mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich wamejiweka katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya baada ya kuitandika Barcelona 4-0 katika mchezo wa kwanzawa nusu fainali nchini Ujerumani.
Mabao mawili ya Thomas Müller, na yale ya Mario Gomez na Arjen Robben yaliizamisha Barcelona ambayo ilikuwa na nyota wake wote wakutegemewa,akiwemo Messi ambaye alikosa michezo kadhaa kabla ya kuanzishwa usiku huu.
Hii imekuwa mara ya kwanza kwa Barcelona kufungwa mabao 4-0 tangu mwaka 1997 walipofungwa na Dynamo Kiev ya Urusi mwaka 1997 kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani ulaya: chanzo bbc.
DKT. MGIMWA AKUTANA NA WAZIRI WA USHIRIKANO WA KIMATAIFA WA CANADA
IMG 3851 27839
Waziri wa ushirikiano wa Kimataifa nchini Canada, Julian Fantino aliyesimama, akisoma hotuba yake mbele ya ujumbe wa Tanzania. Aliyekaa kushoto kwake ni Margaret Biggs ambaye ni Rais wa shirika la maendeleo la kimataifa (CIDA).


IMG 3847 269b9

Waziri wa Fedha, Dkt. Wiliam Mgimwa akisisitiza jambo kwa Waziri wa ushirikiano wa Kimataifa, Julian Fantino mara baada ya kikao kumalizika

IMG 3862 91dac
Waziri wa Fedha, Dkt Wiliam Mgimwa pamoja na ujumbe wa Tanzania katika majadiliano ya pamoja na  Mhe. Julian Fantino ambaye ni Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa katikati mbele.  Aliyekaa kushoto kwake ni  Margaret Biggs ambaye ni Rais wa Taasisi ya maendeleo ya  kimaifa(CIDA).


IMG 3849 86b17
Kamishna wa Fedha za Nje Zanzibar, Bihindi Nassor akisalimiana na Waziri wa ushirikiano wa Kimataifa nchini Canada, Julian Fantino.

IMG 3846 82beb
Waziri wa Fedha, Dkt. Wiliam Mgimwa akisalimiana na Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa nchini Canada, Julian kabla ya kikao kuanza Fantino. Chanzo: Ingiahedi Mduma