TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, September 30, 2015

Hizi ni safari ndefu zaidi za Ndege Duniani, unakaa mpaka saa 17 angani mtu wangu.. (+Pichaz)

Unaweza ukaona safari ya kutoka Mwanza mpaka Dar es Salaam ni ndefu kwa sababu unatumia kati ya saa 12 mpaka 16 ndani ya basi, lakini kwa Usafiri wa Ndege ni kama saa moja tu hivi unakuwa umemaliza safari !!
Sasa hizo saa za kukaa kwenye basi safari ya Mwanza-Dar kuna watu wanazitumia wakiwa angani kwenye Ndege… Nimezipata Rekodi Mitandaoni, zinaonesha safari kumi za Ndege ambazo wasafiri wanatumia muda mwingi zaidi hewani kwenye safari moja.
1.Dubai Mpaka Panama– Hii ni Safari ambayo inachukua saa 17 na dakika 35 angani… yani Ndege ikiruka Dubai hakuna sehemu inatua mpaka ifike Panama. Hii ndio safari ndefu zaidi kwa sasa ambayo inafanywa na Ndege za Emirates… umbali toka Dubai mpaka Panama ni Kilometa 13, 820.
emirates (1)2. Dallas mpaka Sydney- Unaambiwa umbali toka Dallas Marekani mpaka Sydney Australia ni Kilometa 13,804. Hiyo ni safari ambayo inachukua saa 17 kwa Ndege za Qantas.
3. Atlanta mpaka Johannesburg– Hapo kuna umbali wa Kilometa 13,580.. safari hii inakamilika kwa Ndege za Shirika la Delta kukaa angani kwa saa 16 na Dakika 55 ambazo ni kama saa 17 hivi mwanzo mpaka mwisho wa safari.
60966325
4. Los Angeles mpaka Dubai– Kama kuna wakati unawaza kufanya safari kati ya hayo Majiji mawili, basi utambue kabisa kwamba umbali wake ni Kilometa 13,420.. na Ndege inatumia saa 16 na Dakika 30. Hii sio safari fupi hata kidogo mtu wangu !!
5. Los Angeles mpaka Jeddah– Shirika la Ndege la Saudi Arabia ndio ambao wamekamata hii njia, unaambiwa umbali toka Los Angeles Marekani mpaka Jeddah Saudi Arabia inakuchukua saa 17 pia kuimaliza hiyo safari yenye umbali wa Kilometa 13,409.
Picha ya muonekano wa juu wa Jeddah Airport mpya, Saudi Arabia.
Picha ya muonekano wa juu wa Jeddah Airport mpya, Saudi Arabia.
6. Los Angeles mpaka Abu Dhabi– Umbali kati ya hiyo Miji miwili ni Kilometa 13,500.. sio safari ndogo aisee, Ndege za Etihad zinakamilisha hiyo safari kwa saa 16 na Dakika 50 mwanzo mwisho.
7. Houston mpaka Dubai– Kilometa 13,145 zimetajwa kwamba ndio umbali kati ya Miji hiyo miwili, safari yake mwanzo mpaka mwisho kwa Ndege inachukua muda wa saa 16 na Dakika 10… Ndege za Emirates zinahusika pia kusafirisha watu kati ya Miji hii miwili.
8. San Francisco mpaka Abu Dhabi– Umbali kati ya hiyo Miji ni Kilometa 13,130.. na safari yake inachukua saa 16 kukamilika.
9. Dallas mpaka Hong Kong– Hapo unazungumzia Marekani na China, umbali wake ni Kilometa 13,700 na umbali huo kwa safari ya Ndege inachukua saa 16 na Dakika 15… Ndege za American Airlines zimeunganisha hii Miji miwili kwa Ndege za moja kwa moja.
American_Airlines_Boeing_777-200ER_N775AN_PVG_2013-5-21
10. San Francisco mpaka Dubai– Hii nayo imo kwenye list ya safari ndefu za Ndege, umbali wake ni Kilometa 13,040… Ndege za Emirates zimeunganisha hii Miji pia kwa safari ya Ndege ya moja kwa moja. Safari yote inakamilika ndani ya saa 16 na Dakika 40.

Selfie nyingine iliyosababisha kifo cha mwanafunzi huyu.

Bado matukio ya watu kupoteza maisha kutokana na upigaji wa picha za Selfie yameendelea kuripotiwa kila siku.
Hii nyingine ni mwendelezo wa matukio hayo ambapo huko Russia kuna mwanafunzi mmoja kawachukua marafiki zake na kutaka wamsindikize kwenda kupiga selfie ya kipekee kwenye moja ya majengo marefu nchini humo.
Walipofika mwanafunzi huyo akapanda juu ya jengo hilo lenye gorofa tisa na akaanza kupiga picha ili atimize lengo lake la kupiga selfie ya kipekee.
selfie
Sekunde chache baadaye aliteleza na kudondoka chini ambapo alikimbizwa hospitali akiwa na majeraha makubwa na baada ya masaa mawili kupita alifariki dunia.
selfie3

Chris Brown anajutia makosa yake baada ya kuzuiwa kuingia Australia? Kayaandika haya.

Kesi ya Chris Brown kumpiga mpenzi wake wa zamani itabakia kuwa moja ya makosa ambayo Chris Brown anajutia sana kuyafanya… story ambayo iligusa Vichwa vya Habari kwenye Entertainment ikiwa na jina la staa Chris Brown siku chache zilizopita ilikuwa ishu ya Chris kuzuiwa kuingia Australia December 2015 kwa ajili ya kupiga show.
Maombi ya Viza yalikataliwa huku wanaharakati wakionekana kuchochea zaidi Chris azuiwe, hiyo yote ilitokana na hatia aliyokutwa nayo Chris baada ya kumpiga Rihanna miaka zaidi ya mitano iliyopita ..!!
231020130803484502293
Chris kaandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba yeye sio yule mtu mkorofi tena, kingine amesema anakubali makosa yake na anaamini makosa yake ingekuwa ni kitu ambacho wengine wangejifunza kupitia kwake…
Chris II Chris
Chris III

Hii ndio adhabu aliyoipata Juma Nyoso baada ya kumfanyia kitendo cha kidhalilishaji John Bocco

Jioni ya September 27 ilikuwa ni siku ambayo wadau wengi wa soka walikuwa wakijadili kuhusiana na tukio la kidhalilishaji, lilitokea katika mechi ya Azam FC dhidi ya Mbeya City, mechi ambayo ilipigwa katika uwanja wa nyumbani wa Azam FC Azam Complex Mbande Chamazi.
Tukio lililotokea katika mechi hiyo ambalo kila mpenda soka Tanzania hakulipenda ni beki wa kati na nahodha wa klabu ya Mbeya City Juma Nyoso kumfanyia kitendo cha kidhalilishaji nahodha wa Azam FC John Bocco, baada ya tukio kufanyika kila mtu aliongea lake ila Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi alithibitisha kupitia account yake rasmi ya twitter kuwa sheria kali zitachukuliwa dhidi ya Juma Nyoso.
DSC_0104
Juma Nyoso wa Mbeya City akimdhibiti John Bocco katika mechi ambayo ilimalizika kwa Azam FC kuibuka na ushindi wa goli 2-1
Taarifa mpya kutoka katika kamati ya uendeshaji wa Ligi, zinaeleza kukaa chini na kupitia kosa la Juma Nyoso na kuamua kumpa adhabu ya kumfungia kucheza soka katika kipindi cha miaka miwili pamoja na faini ya milioni 2. Kamati hiyo imefikia maamuzi hayo kutokana na Juma Nyoso kuwa mkosefu sugu wa kitendo hicho cha kidhalilishaji katika mchezo wa soka.
DSC_0107
Hii sio mara ya kwanza kwa Juma Nyoso kufanya tukio kama hilo, kwani alishawahi kufungiwa mechi nane kwa tukio kama hilo, baada ya kumfanyia mshambuliaji wa zamani wa Simba Elias Maguli, hayo ndio matukio ambayo Nyoso amewahi kukamatwa na kuadhibiwa nayo ila September 28 beki wa zamani wa Yanga Amir Maftah amekiri kuwahi kufanyiwa kitendo hicho na Juma Nyoso na yeye kupatwa na hasira na kumpiga kichwa katika mechi dhidi ya Simba, tukio ambalo lilisababisha Amir Maftah kuonyeshwa kadi nyekundu.

Kama wewe ni mtumiaji wa Twitter basi mpango huu ukufikie!

Kumekuwa na tetesi nyingi kuhusu mtandao wa Twitter kuongeza idadi ya maneno ya kutweet kwa Tweet moja… kwa sasa Twitter inamruhusu mtumiaji kutumia uwingi wa maneno 140 tu kutweet message moja lakini kwa wale ambao wanapenda kuchat kwa marefu, Twitter iliamua kongeza idadi ya maneno kufikia 10,000 kwa private messages… je tutegemee mabadiliko yoyote hivi karibuni?
TWEET2
Nimekutana na habari muda huu ambayo ningependa kushare na wewe mtu wangu… inasemekana kuwa Twitter ipo kwenye mpango wa kuongeza idadi ya maneno ambayo mtu anaweza kuandika kwa Tweet moja na kwa mujibu wa mtandao wa http://www.complex.com Twitter ina mpango wakuleta huduma itakayowaruhusu watumiaji wake kutweet ama kuandika Tweets/post zenye maneno zaidi ya 140!
TWWET6
Baadhi ya mitandao kama Re/Code  wa Marekani wanaamini kuwa maamuzi haya yamesukumwa na mabadiliko ya idadi ya maneno ya kutumia kwenye private messages za Twitter>>> “watu wamepokea vizuri ongezeko la maneno ya Twitter kwenye message za private, hii inaonyesha jinsi gani ambavyo bado kampuni ina nafasi ya kukua zaidi ya hapa…” <<< mmoja ya wafanyakazi wa Twitter aliuambia mtandao wa Re/Code.
Je Twitter itaweza kukuza biashara yake katika ushindani wa Teknolojia na mitandao ya kijamii safari hii? Kama ilikuwa haijakufikia basi ichukue hiyo mtu wangu na pengine tutegemee kufaidika very soon na mpango huu!

Monday, September 28, 2015

Mwaka mmoja tangu kupotea wanafunzi Mexico, msimamo wa wazazi ni huu..Serikali je?

Tarehe kama ya leo Mexico iliingia kwenye headlines baada ya kuwepo na taarifa ya kupotea kwa wanafunzi 43 katika mji wa Iguala Kusini mwa nchi hiyo.
Demonstrators take part in a march to mark the first anniversary of the disappearance of the 43 students from Mexico's Ayotzinapa College Raul Isidro Burgos, in Mexico City, September 26, 2015. REUTERS/Ginnette Riquelme
Pamoja na kuwepo utata wa kupotea kwa wanafunzi hao huku ndugu wa wanafunzi hao wakigoma kupokea taarifa ya Serikali iliyotolewa baada ya uchunguzi uliodai wanafunzi hao walitekwa na kuuawa na kundi la kigaidi.
MEXICO2
Maelfu ya ndugu na jamaa wa wanafunzi hao wakiandamaa nchini humo
Ripoti hiyo haijakataliwa tu na ndugu wa wanafunzi hao, bali pia ripoti kutoka kwa kundi la wataalamu wa uchunguzi hivi karibuni ilihoji uhalali wa ripoti hiyo ya uchunguzi wa serikali.
Ndugu wa wanafunzi hao wamesisitiza kuwa hawataacha kuandamana hadi pale watakapojua ukweli juu ya ndugu zao hao.
MEXICO3
Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto, ameahidi uchunguzi upya ufanywe.

Hawakujali kuzungumziwa..uhusiano wa mastaa hawa umeendelea kudumu!!

Watu wengi huamini watu wengi maarufu hawawezi kukaa muda mrefu katika uhusiano wao wa kimapenzi kutokana na umaarufu walionao na kuchangia mahusiano yao kuvunjika.
Pamoja na wengi kushindwa kuvumiliana na kujikuta wakiachana lakini wapo hawa mastaa ambao mpaka sasa bado wameendelea kubaki ndani ya ndoa zao kitu ambacho wengi hawakukitarajia.
Hawa ni miongoni mwa mastaa ambao licha ya kuzungumziwa sana na vyombo vya habari lakini mahusiano yao yameendelea kuimarika.
juuu
Kim na Kanye West

pink
Will na Jada Pinkett Smith

bil
Bill na Hillary Clinton

love
Jay-Z na Beyonce

pt
Brad Pitt na Angelina Jolie

vic
David And Victoria Beckham

douglas
Michael Douglas And Catherine Zeta

Friday, September 25, 2015

Umewahi kuona kisiwa kinahama? Hiki hapa, unaweza kuhisi ni Boti au Meli ..!! (+Pichaz)

Ubunifu wa binadamu na maendeleo ya Teknolojia ni vitu ambavyo huwa vinatuletea mambo mapya kila siku, hakuna mtu asiyependa kusifiwa baada ya kufanya kazi nzuri.. ubunifu wa hiki kisiwa ni kazi nzuri ambayo tayari pongezi zimeanza kuwafikiwa wabunifu walioona kuna umuhimu kuwa na kitu kama hiki cha kuvutia.
Tunajivunia uzuri wa Zanzibar yetu, huo ni uzuri kwenye kisiwa cha asili kabisa.. taarifa ikufikie kwamba wapo waliowaza kutengeneza kisiwa kinachohama kwa kutembea juu ya maji kama ilivyo meli au Boti.
Najua kwamba Dunia inavitambua pia visiwa vilivyotengenezwa na binadamu ikiwepo Palm Island, ambacho kiko Dubai… lakini Dunia inatambulishwa pia kwenye Kisiwa ambacho kimebuniwa na wataalam wa Kampuni ya Migaloo ambao wanadili sana na kutengeneza Boti za kifahari.
150918124529-migaloo-floating-island-overview--super-169
Muonekano wa juu wa Kokomo Ailand, kisiwa cha aina yake ambacho kinatembea juu ya maji.
Ubunifu huu utasogezwa kwenye Maonesho maalum ya Monaco Yatch Show na tayari watu wenye pesa zao wameonekana kuvutiwa sana na hii kitu, kwa hiyo tayari ni biashara ambayo inatarajia wateja wa nguvu kabisa any time kuanzia sasahivi !!
150918125750-migaloo-floating-island-city-super-169
Ukiangalia nje mpaka ndani Kisiwa hiki kinavutia, na kina mahitaji yote muhimu kwa mtu anayehitaji kuishi ndani yake, kwenye vilivyomo unaambiwa mpaka Beach za nguvu kabisa zipo ndani !!
tumblr_inline_nv6lgtcn8I1tvnn6i_500
2CA24B1D00000578-3244528-Luxury_Around_the_complex_residents_will_find_all_the_amenities_-a-6_1442962302661
Hii ni Beach ambayo iko kwenye kisiwa hicho cha kisasa kabisa, na ardhi ambayo iko kwenye kisiwa ni kama ambayp iko kwenye maeneo yenye hali ya kitropiki.
2CA24B4300000578-3244528-On_the_move_Designers_at_Migaloo_Private_Submersible_Yachts_put_-a-5_1442962292608
2CA2584B00000578-3244528-Picturesque_With_a_80_metre_high_penthouse_suite_and_its_own_wat-a-3_1442962270223
Juu kwa juu mtu wangu, hapo kuna Beach ya nguvu kisiwani, Bustani na miti.. vyote vinaongeza uzuri wa Kisiwa hiki.
150918125046-migaloo-floating-island-interior-super-169
Ndani kunavutia mtu wangu, yani huku ndani unaambiwa kuna Beach nyingine na mazingira poa kabisa ya kujienjoy !! Ukiingia mpaka unajisahau kwamba uko kwenye kisiwa kinachoelea.
  150924122848-kokomo-ailand-top-view-super-169
Ubunifu huo wa nguvu huu hapa pia kwenye video mtu wa nguvu, teknolojia ina mazuri yake ya kuvutia kila siku yani !!

Wajue Marais wa Afrika waliovunja rekodi kwa kukaa muda mrefu madarakani..

Nchi nyingi katiba huruhusu kiongozi wa nchi kukaa madarakani kwa mihula miwili lakini nyingine zimekuwa zikibadilisha katiba zao ili tu waendelee kubaki madarakani.
Wapo marais wengine wa Afrika ambao wamevunja rekodi kwa kukaa madarakani kwa kipindi kirefu na wengine kusababisha hata migogoro ya kisiasa ndani ya nchi zao.
Wajue Marais waliovunja rekodi kwa kukaa muda mrefu madarakani.

guinea
1. Teodoro Obiang Nguema Mbasogo -Rais wa Equatorial Guinea, amekaa madarakani kwa miaka 36

2. Jose Eduardo dos Santos-Rais wa Angola, amekaa madarakani miaka 36

mug
3. Robert Mugabe-Rais wa Zimbabwe amekaa madarakani kwa miaka 35

biya
4. Paul Biya- Rais wa Cameroon, amekaa madarakani kwa miaka 32

ngoo
5. Denis Sassou Nguesso – Rais wa Congo, amekaa madarakani kwa miaka 30

museven
6. Yoweri Museven- Rais wa Uganda, amekaa madarakani kwa miaka 29

Monday, September 21, 2015

Picha 11 nje ya Mahakama baada ya Mwimbaji wa Gospel Emmanuel Mbasha kushinda kesi ya kubaka

September 21 2015 moja ya stori kubwa iliyogusa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania ni ishu ya Hukumu ya kesi ya Mwimbaji wa Gospel Tanzania, Emmanuel Mbasha ambapo alikuwa anakabiliwa na Kesi ya kumbaka shemeji yake na kesi imekuwa Mahakamani tangu mwaka 2014.
IMG_20150921_112732
Stori kwenye Ukurasa wa 5 Gazeti MWANANCHI, September 21 2015.
Tayari hukumu ya Kesi hiyo imetolewa Mahakama ya Wilaya ya Ilala Dar es Salaam leo, Mwimbaji huyo ameachiwa huru baada ya Mahakama kumkuta hana hatia kwenye Kesi hiyo.
Screen Shot 2015-09-21 at 11.58.58 AM
Emmanuel Mbasha akiwa amepiga magoti huku akitokwa machozi nje ya Mahakama ya Ilala, Dar es Salaam baada ya Hukumu kutolewa.
Hizi hapa Picha nje ya Mahakama ya Ilala baada ya Hukumu kutolewa Mahakamani na Emmanuel Mbasha kutoka nje ya Mahakama.

Screen Shot 2015-09-21 at 11.59.05 AM
Screen Shot 2015-09-21 at 11.59.12 AM
Screen Shot 2015-09-21 at 11.59.36 AM
Screen Shot 2015-09-21 at 11.59.21 AM
Screen Shot 2015-09-21 at 11.59.28 AM
Screen Shot 2015-09-21 at 11.59.42 AM
Screen Shot 2015-09-21 at 11.59.49 AM


Screen Shot 2015-09-21 at 11.59.57 AM
Screen Shot 2015-09-21 at 12.00.02 PM