TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Thursday, October 31, 2013

SERIKALI YATANGAZA VIWANGO VIPYA VYA ALAMA ZA UFAULU ELIMU YA SEKONDARI

a_97eff.jpg
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akifafanua kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya upangaji wa viwango vya alama, matumizi ya alama endelevu ya mwanafunzi na ufaulu leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Kamishna wa Elimu Profesa Eustella Bhalasesa.
b_3754b.jpg
_ Baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Sifuni Mchome (hayupo pichani).
c_5b2ab.jpg
Waandishi wa habari na maafisa wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome(hayupo pichani).(P.T)
Picha zote na Eliphace Marwa (MAELEZO)
UPANGAJI WA VIWANGO VYA ALAMA, MATUMIZI YA ALAMA ENDELEVU YA MWANAFUNZI NA UFAULU
UTANGULIZI
Wizara imekusanya maoni ya Wadau wa Elimu kuhusu Upangaji wa Viwango vya Alama (Grade Ranges) katika Mitihani ya Kuhitimu Kidato cha Nne na cha Sita pamoja na Matumizi ya Alama za Tathmini Endelevu ya Mwanafunzi (Continuous Assessment ama CA) kwa ajili ya kuamua kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi. Maoni ya wadau yamekusanywa kwa sababu kwa muda mrefu sasa upangaji wa viwango vya alama vinavyotumika na utaratibu wake katika mitihani ya kuhitimu Kidato cha Nne na Kidato cha Sita umekuwa haufanani pamoja na kwamba mitihani hiyo yote ni ya elimu ya sekondari. Pia mfumo masuala mbalimbali ya mitihani katika elimu ya sekondari umekuwa na miundo tofauti ikiwemo ule unaotumika shuleni na ule wa Baraza la Mitihani la Taifa. Kwa sasa kuna miundo mikuu miwili katika mfumo huo.
Muundo wa Kwanza ni upangaji wa viwango katika ngazi ya Shule ambapo Alama Mgando (Fixed Grade Ranges) zifuatazo hutumika kupanga madaraja: A = 81 – 100; B = 61 – 80; C = 41 – 60; D = 21 – 40 na F = 0 – 20. Muundo huu umetumika kwa muda mrefu na umezoeleka kwa walimu na wanafunzi wa elimu ya sekondari kwa ujumla.
Muundo wa Pili ni wa viwango vinavyotumiwa na Baraza la Mitihani la Taifa ambapo ambapo kabla ya mwaka 2012 muundo wa viwango nyumbufu (flexible grade ranges) ulitumika. Katika muundo huu uwigo wa alama ulibadilika badilika kulingana na hali ya matokeo ilivyokuwa kwa mwaka husika. Lakini kuanzia mwaka 2012, Serikali iliamua kutumia mfumo wa Upangaji wa Alama Mgando (Fixed Grade Range) kwa Kidato cha Nne na Kidato cha Sita. Katika mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012 Baraza lilitumia mfumo huu wa alama mgando ambapo: A = 80 – 100, B = 65 – 79, C = 50 – 64, D = 35 – 49, F = 0 – 34. Kwa upande wa Kidato cha Sita Baraza lilitumia mfumo wa A = 80 – 100; B = 75 - 79; C = 65 – 74; D = 55 – 64; E = 45 – 54; S = 40 – 44 na F = 0 – 39. Mifumo hii ya Baraza haikuwa inafahamika kwa wadau na hivyo kuwa sehemu ya malalamiko katika sekta ya elimu na mafunzo.
Vilevile, Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995 imeelekeza kwamba katika kuamua kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi wa elimu ya sekondari, Alama za CA zitachangia asilimia hamsini (50%) na Mtihani wa mwisho utachangia asilimia hamsini (50%). Kwa upande wa Zanzibar, CA zimekuwa zikiandaliwa kwa mfumo wa asilimia arobaini (40%) na mtihani wa mwisho asilimia sitini (60%). Pamoja na kwamba Baraza halijawahi kuutumia mifumo hii tangu ilipowekwa, kumekuwa na mitazamo, maoni na mapendekezo tofauti katika muundo na matumizi ya alama za CA. Kuna mawazo pia kwamba mfumo wa CA kuchangia matokeo ya mwisho ya mwanafunzi pia utumike kwa watahiniwa wa kujitegemea (private candidates). Kwa sasa matokeo ya mitihani ya watahiniwa hawa yamekuwa yakitumia alama za mtihani wa mwisho tu na hivyo kutafsiriwa kama utaratibu ambao unamwonea mwanafunzi ambaye anahamu ya kujiendeleza kielimu lakini anakwama kwa sababu mfumo unaotumika siyo rafiki kwa mtahiniwa.
Kwa mantiki hii, Wizara imedhamiria kufanya harmonization ya masuala ya alama katika mitihani ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita ili kupata muundo mmoja na ulio wazi kwa wadau wote wa elimu ya sekondari. Lakini pia serikali imedhamiria kuhakikisha tathmini za wanafunzi katika ngazi mbalimbali zinakwenda sambamba na matarajio ya mitaala inayotumika na ambayo inahuishwa mara kwa mara ili iendane na wakati na mahitaji ya elimu katika ngazi mbalimbali.
VIWANGO NA UTARATIBU KUANZIA MWAKA 2013 KWA KIDATO CHA NNE NA
MWAKA 2014 KIDATO CHA SITA
Baada ya kufanya tathmini ya maoni mbalimbali ya wadau, misingi ifuatayo ilizingatiwa katika maamuzi kuhusu makundi ya alama na muachano wake:
a) Alama zitakazotumika zitakuwa A, B, C, D, E na F. Muachano wa alama kati ya kundi moja hadi jingine utafanana, isipokuwa tu pale ambapo itaonekana kuna sababu na hakuna athari za kuwa na muachano tofauti na ule ambao umetumika katika makundi mengine.
b) Makundi ya alama hayatakuwa na clusters isipokuwa pale ambapo itaonekana kufanya hivyo kunaleta tija katika kupata picha ya wahitimu kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Kwa mantiki hii
(i) makundi ya alama A, C, D, E na F yabaki na cluster moja moja bali kundi la alama B litakuwa na clusters mbili. Kundi la kwanza litakuwa la wale ambao wamepata alama kati ya 50 mpaka 59 na litaitwa B na lingine litakuwa la wale ambao wamevuka uwigo wa 50 hadi 59 na kuelekea uwigo wa 60 hadi 74 na hili litaitwa B+ (angalia jedwali hapo chini).
(ii) Pamoja na kuwa na muachano wa alama 26 kama jedwali linavyoonesha hapo chini, alama A kwa miaka mingi imekuwa ikianzia alama 75 hadi 100 na kwamba pamoja na uwigo huo bado wanaofaulu kwa kiwango hicho ni wachache sana. Kwa mantiki hii, hakuna haja ya kubadilisha uwigo ila juhudi ziendelee katika ufundishaji na ujifunzaji ili kiwango cha ufaulu kiongezeke na kupata wanafunzi wengi zaidi wanaofaulu katika kundi hili.
(iii) Pia, pamoja na kuwa na muachano wa alama 20 kama jedwali linavyoonesha hapo chini kwa miaka mingi, huko shuleni mwanafunzi aliyepata alama 21 na hadi 30 alihesabiwa kuwa na ufaulu wa chini kabisa au hafifu kwa kiwango cha alama D na ingawa ilikubalika ufaulu wa aina hiyo kwa mazingira ya nchi yetu unaridhisha. Alama F ilikuwa ni kwa wale waliopata chini ya hapo. Hivyo, alama F itaendelea kuwepo na itaanzia alama 0 hadi 19 na E itaanzia alama 20 hadi 29 na D – 30 -39. Lengo la muundo huu ni kuwa alama mbalimbali, isipokuwa kwa makundi machache, zianzie kwenye 0 yaani 0, 10, 20, 30, 40 na kuendelea badala ya kuanzia kwenye moja yaani 1, 11, 21, 31, 41 na kuendelea. Hii ni kwa ajili ya kuleta mtizamo unaofanana katika ngazi mbalimbali za elimu ambapo kwa sasa ngazi ambazo siyo za elimu msingi na sekondari zinatumia muundo wa kuanzia kwenye 0 badala ya 1.
c) Uwigo wa jumla wa alama kwa Kidato cha Nne na Kidato cha Sita utaendelea kuwa wa alama 0 hadi 100 na kila kundi katika uwigo huu limepewa tafsiri kwa ajili ya kuamua mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya mwanafunzi kulingana na malengo ya mtihani husika. Kimsingi, tafsiri zifuatazo zitakatumika
(i) Alama A itakuwa na maana ya ufaulu uliojipambanua (distincion or outstanding performance),
(ii) Alama B+ itakuwa na maana ya ufaulu bora sana (excellent performance),
(iii) Alama B itakuwa na maana ya ufaulu mzuri sana ( very good perfomance),
(iv) Alama C itakuwa na maana ya ufaulu mzuri (good performance);
(v) Alama D itakuwa na maana ya ufaulu wa wastani (low performance),
(vi) Alama E itakuwa na maana ya ufaulu hafifu (very low performance), na
(vii) Alama F itakuwa na maana ya ufaulu usioridhisha (unsatisfactory performance).
Wataalamu katika maeneo mbalimbali ya elimu na ulimwengu wa kazi, kwa kushirikiana na Wizara, watatoa maana ya tafsiri hizi kiutendaji katika maeneo yao kulingana pia na mahitaji yao.
d) Alama C iwe ndiyo alama ya ufaulu mzuri ambao hauhitaji urekebu wa lazima, wakati alama D na E ni alama za ufaulu unaohitaji urekebu kadri mwanafunzi atakavyokuwa anaendelea na masomo ili kuthibitisha kama mlengwa anaweza na kulingana na mahitaji ya eneo husika (targeted remediation). Alama F iwe alama ya eneo linalohitaji urekebu wa hali ya juu (intesive remediation) ili mwanafunzi huyo aweze kumudu masomo kadri anavyoendelea kukua kielimu ama atakapoingia katika ulimwengu wa kazi.
e) Makundi ya alama yatajumuisha CA kwa kiwango cha asilimia isiyozidi 40 na mtihani wa mwisho kwa asilimia isiyozidi 60 kwa makundi yote ya watahiniwa ikiwemo wale wa kujitegemea (private candidates). Hii ni kwa kuzingatia kwamba CA siyo vizuri izidi uwigo wa alama ya ufaulu mzuri unapoanzia ambayo ni C au 40.
f) CA kwa upande wa Kidato cha Nne zitokane na mtihani wa Kidato cha Pili (alama 15), matokeo ya Kidato cha Tatu (alama 5 kwa kila muhula, na hivyo jumla ya alama 10), mtihani wa Mock (alama 10) na kazi mradi au Projects (alama 5). Kwa upande wa Kidato cha Sita, CA iendelee kutokana na muundo unaotumika sasa.
g) CA zitumike pia kwa watahiniwa wa kujitegemea. Kwa upande wa watahiniwa wa kujitegmea ambao wanarudia Mitihani, CA zao zitumike zile zilizotumika kutoa matokeo yake ya mitihani ya awali. Kwa watahiniwa wa kujitegemea waliopitia mfumo wa Qualifying Test (QT), matokeo ya QT yatumike kama CA na mtihani wa mwisho uchangie alama 60.
h) Kwa vile alama endelevu kwa mwaka 2013 kwa wanafunzi wa Kidato cha Nne tayari zimeshawasilishwa Baraza la Mitihani Tanzania, alama hizo zichangie asilimia 40 katika mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2013.
i) Muundo wa wastani wa alama katika ufaulu (Grade Points Average ama GPA) utaandaliwa na kuanza kutumika pale utakapokuwa tayari na wadau wataelimishwa kuhusu muundo huo ili wapate kuufahamu na manufaa yake katika elimu ya sekondari.
j) Muundo huu mpya wa alama utatumika kwa mzunguko wa miaka minne kabla haujahuishwa tena ili kuupa muda wa kutosha kuona aina ya changamoto zinazojitokeza na jinsi ya kuzishughulikia. Aina hii ya muda itaruhusu vidato vinne vya elimu ya sekondari ya kawaida na nane ya elimu ya sekondari ya juu kupimwa. Hata hivyo, uhusihaji wa masuala ya mitihani unaweza ukafanyika iwapo matokeo ya uhuishaji wa mitaala kwa ujumla utahitaji pia eneo la mitihani liguswe na kuhuishwa pia.
Kwa mantiki hii, viwango vya alama na ufaulu ni kama inavyooneshwa kwenye jedwali la 1 hapa chini

SALAMU ZA PONGEZI ZAMIMINIKA KWA MALINZI 

sepp-blatter_4e5fb.jpg
Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Jamal Malinzi ameendelea kupokea salamu za pongezi baada ya kushinda wadhifa huo katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 27 mwaka huu.
Salamu nyingine za zimetoka kwa Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Sepp Blatter ambapo amempongeza Malinzi kwa kuchaguliwa na kumtakia kila la kheri katika majukumu yake ya kuongoza mchezo huo nchini.
Blatter amesema ana uhakika ufahamu wake na uwezo wake katika uongozi ni muhimu katika kuimarisha maendeleo ya mpira wa miguu nchini, na kuongeza kuwa milango ya FIFA iko wazi wakati wowote anapotaka kujadili masuala yanayohusu mchezo huo.
"Nakutakia wewe na kamati mpya ya Utendaji iliyochaguliwa kila la kheri, nguvu, na kila aina ya mafanikio kwa changamoto zilizo mbele yenu," amesema Rais Blatter katika salamu zake.(P.T)
Wengine waliomtumia Rais Malinzi salamu za pongezi ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kenya (FKF), Sam Nyamweya, Rais wa Heshima wa Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Uganda (FUFA), Lawrence Mulindwa, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA) na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Arumeru (ADFA), Peter Temu.
YANGA, JKT RUVU UWANJANI KESHO
Raundi ya 12 ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea kesho (Novemba 1 mwaka huu) kwa mechi kati ya JKT Ruvu na Yanga itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Viingilio katika mechi hiyo ni sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A. Tiketi zitauzwa siku ya mechi uwanjani katika magari maalumu kuanzia saa 4 asubuhi.
Novemba 2 mwaka huu kutakuwa na mechi nne; Mgambo Shooting na Coastal Union (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Tanzania Prisons na Oljoro JKT (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).
Raundi hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7 mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashani United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, Rhino Rangers vs Tanzania Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar.
Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City wakati Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

‘Marubani waliotorosha twiga walitumia hati za kidiplomasia’ 

twigapx_051a7.jpg
Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Moshi, imeelezwa kuwa marubani wa ndege ya kijeshi ya Qatar, walitumika katika kutorosha twiga wanne kwenda Uarabuni na kwamba washtakiwa walikuwa na hati za kusafiria zenye hadhi ya kidiplomasia.
Shahidi wa 13, Prisca Sabugo ambaye ni Ofisa Uhamiaji, aliiambia mahakama juzi kuwa hati hizo hazikugongwa mihuri wala kupewa viza.
Akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Kobelo, shahidi huyo alidai kuwa ndege hiyo ilitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) Novemba 24 mwaka 2011.(P.T)
"Baada ya hiyo ndege ya jeshi kutua, alikuja wakala wao kutoka Kampuni ya Equity Aviation akaniletea Diplomatic Passport zao na akaniambia wamekuja kwa shughuli za utalii kwa siku tatu," alisema.
Huku akiongozwa na mawakili wa Serikali, Evetha Mushi na Joseph Maugo, shahidi huyo alidai kuwa marubani na wafanyakazi wa ndege huwa hawapitii utaratibu wa kawaida wa kujaza fomu na kupewa viza. Alisema, tangu wageni hao waingie nchini kama watalii, hawakuwahi kuhojiwa na chombo chochote kuhusu kutogongwa mihuri kwenye hati zao.
Shahidi wa 12, Oscar Jullius ambaye ni Ofisa Wanyamapori, alidai kuwa vibali vilivyotumika kukamata wanyama hao vilikuwa vya kampuni mbili ambazo ni Ham Market na Luega Birds Traders.
Kwa mujibu wa shahidi huyo, vibali hivyo vilikuwa vya kumiliki nyara na si vya kukamata wanyamapori hai na kwamba yeye ndiye aliyeandika ripoti ya thamani ya wanyama hao.
Alisema thamani ya wanyama wote waliotoroshwa ilikuwa ni Sh170.5 milioni na kwamba twiga hao wanne kila mmoja alikuwa na thamani ya Dola 10,000 za Marekani sawa Sh60 milioni za Tanzania.
Alipoulizwa na mmoja wa mawakili wanaowatetea washtakiwa, Edmund Ngemela, kama vibali walivyokuwa navyo vilikuwa halali, alikiri kuwa vilikuwa halali na vilikuwa ni vya kumiliki nyara.
Kesi hiyo imepangwa kuendelea Novemba 29 mwaka huu.
Washtakiwa katika kesi hiyo ni pamoja na raia wa Pakistan, Kamran Ahmed, Hawa Mang'unyuka, Martin Kimath na Michael Mrutu ambao wote wako nje kwa dhamana.
Katika hatua nyingine, madiwani watatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro akiwamo mwenyekiti wa halmashauri hiyo, wanashikiliwa na maofisa wa Kikosi cha Maalumu cha Kupambana na ujangili.
Huko Dodoma, watu sita wamekamatwa na polisi wilayani Kondoa baada ya kupatikana na vipande vinane vya meno ya ndovu yenye thamani ya Sh 25milioni.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma Suzan Kaganda, aliwambia waandishi wa habari jana kuwa, watuhumiwa hao walikamatwa katika operesheni maalum ya kupambana na ujangili.
Chanzo:Mwananchi

Wednesday, October 30, 2013

Ripori ya ajali ya Treni Nairobi October 30 2013

kenya bus 4
Hii ajali imegharimu maisha ya watu kumi na mbili pamoja na wengine kujeruhiwa baada basi lililokua likiwaisha watu katikati ya jiji la Nairobi kugongwa na treni kwenye eneo ambalo vibanda vinadaiwa kusogelea reli hivyo ni ngumu kuona kama treni inakuja.
Hata hivyo Citizen TV wameripoti kwamba tayari dereva Edward Githae (43) wa basi amekamatwa na atafikishwa Mahakamani wakati wowote kutoka sasa ambapo abiria mmoja aliejeruhiwa anasema dereva huyu alisimamishwa na polisi kwa kupewa onyo kwamba asivuke kwa sababu kuna Treni inapita ila alikaidi agizo na kupitiliza matokeo yake yakawa hii ajali.
Kenya bus 3
kenya bus 2
Kenya bus 1

Alichosema David Beckham kuhusu kumkosoa Sir Alex Ferguson juu ya ile kauli

David Beckham on fergieTunafahamu kwamba siku Sir Alex Ferguson anazindua kitabu chake ambacho ameandika mambo mbalimbali kuhusu kazi yake kwa miaka yote akiifundisha club ya Manchester United, aliweka wazi kwamba alimuuza Beckham kwenda Real Madrid 2003 kwa sababu staa huyu wa soka alijiona yeye ni mkubwa kuliko Manager, alijiona mkubwa kuliko club na kwamba alipoanza mapenzi na Victoria ndio kama alianza kulegeza uzi kwenye kazi.
Pamoja na hayo maneno ambayo ndio yalipewa headlines za kutosha huku wengi wakiamini kwamba yatamkasirisha Beckham, staa huyu ameileta hii ishu kwenye upande mwingine baada ya kusema hawezi kumponda Sir Ferguson wala kusema chochote kibaya kuhusu Mwanaume huyu aliesababisha ndoto zake za kuwa staa wa soka kutimia.
Alex-Ferguson-and-David-Beckham
Beckham ambae amepongezwa na wengi kwa hekima hii, anakwambia ‘Sir Ferguson ndio aliniamini na kunipa nafasi, siwezi kukaa hapa kuongea mabaya au kumkosoa mtu alienifanya niishi kwenye ndoto yangu niliyoitaka toka kitambo’

WAPINZANI KUSIMAMISHA MGOMBEA MMOJA 2015

mbatia-k1 596f0
UPEPO wa mabadiliko ya kisiasa unaovuma kuelekea kambi ya upinzani, sasa unaonekana kuwaamsha viongozi wa vyama hivyo baada ya kutolewa kwa taarifa kuwa wanafikiria kusimamisha mgombea mmoja wa urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. (HM)

Taarifa zilizolifikia gazeti hili kabla ya kuthibitishwa na mmoja wa viongozi hao, zilieleza kuwa hatua ya vyama hivyo imekuja baada ya ushirika wao waliouunda kupinga upungufu uliokuwemo kwenye Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kuzaa matunda.
Pamoja na hilo, inaelezwa kuwa maamuzi hayo magumu ya wapinzani yametiwa chachu na kauli aliyoitoa Rais Jakaya Kikwete ya hivi karibuni ya kukitabiria anguko Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika uchaguzi wa mwaka 2015 au ule wa 2020, kutokana na kile alichodai kuwa viongozi wa chama hicho kuendekeza rushwa.
Mmoja wa viongozi wanaounda ushirika huo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia alithibitisha taarifa hizo huku akisisitiza kuwa nia ya kufanya hivyo ni kuhakikisha wanaiondoa madarakani CCM mwaka 2015.
Kwa mujibu wa Mbatia, walichokifanya kwenye Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba si nguvu ya soda na badala yake wataendeleza hadi kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Mbatia alisema kuwa uongozi wa vyama vya upinzani unatarajia kuungana na kumsimamisha mgombea mmoja, ili kuhakikisha wanaiondoa madarakani CCM.
Mbatia ambaye alikuwa akizungumza katika mahojiano maalumu na RAI Jumatano, alisema hatua hiyo pamoja na ushirika wao unalenga kudumisha amani na uzalendo kwa kuweka utaifa mbele.
Alisema umoja wanaoendelea kuuonyesha kwenye mchakato wa Katiba Mpya, ambao unalenga kuweka mbele maslahi ya Taifa ili kuhakikisha inapatikana Katiba bora yenye kushirikisha Watanzania wote, wataufanya pia kwenye chaguzi mbalimbali.
"Ili jambo lolote litokee lazima kuwepo na chanzo, mwanzo wetu wa ushirikiano ulioanza Septemba mwaka huu ndani ya ukumbi wa Bunge, tutauendeleza.
"Tupo kwenye maridhiano zaidi, hata muungano wetu wa Tanzania bara na Zanzibar si wa kisheria, viongozi wetu Nyerere na Mzee Karume walikaa na kuzungumza, hata sisi tunafanya hivyo, tunatakiwa kuzungumza kwa maslahi ya nchi," alisisitiza Mbatia.
Alisema vyama vyao viliamua kuwa na ushirikiano wa pamoja kutokana na kubaini kwamba, bila umoja hakuna kitakachofanikiwa.
"Tumeshaanza kuzungumza kwa mapana juu ya ushirikiano wetu, ukweli ni kwamba kuna mwelekeo mzuri," alisema.
Alisema hatua ya vyama kujadili kwa pamoja mchakato wa Katiba ni dalili njema za kuelekea kwenye mafanikio na ndio maana wanaona ipo haja ya kuuendeleza ushirika huo hadi kwenye chaguzi mbalimbali nchini.
"Tunapaswa kuvifanya vyama vyetu viwe vya maslahi mapana kwa taifa, ili visionekane vipo kwa ajili ya maslahi ya viongozi.
"Kwa kuwa tumeweka maslahi ya taifa mbele kwenye suala la Katiba, tumeona tuwe na mfumo ambao utalisaidia taifa, ndio maana hata tulipotoka Ikulu tumekubaliana kuwa Tanzania kwanza vyama baadaye, naamini kwa nia njema hata ule ushirikiano wetu utaendelea mbele zaidi kwa maslahi mapana ya taifa letu, tunategemea hivyo... tuna mategemeo mazuri, lazima tufikirie chanya," alisema Mbatia.
Kauli ya Mbatia imeungwa mkono na Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara, Julius Mtatiro ambaye ameeleza kuwa chama chao hakina tatizo kwenye suala la kumsimamisha mgombea mmoja na wako tayari kwa sababu ushirikiano ni suala la msingi na lenye maana.
"Kulingana na upepo wa kisiasa ulivyo sasa, ni dhahiri tunahitaji kushirikiana ili kukiondoa chama tawala madarakani, kwa sababu mahali tulipo sasa ni pagumu.
"Tunachosubiri sasa ili kukamilisha muungano wetu ni tamko la pamoja kutoka kwa viongozi wa juu wa vyama vyote, lakini naamini nia ya kusimamisha mgombea mmoja itakubalika bila kupingwa," alisema Mtatiro.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Habari kutoka Chadema, John Mnyika, alisema ushirikiano kwa sasa umejikita kwenye suala la kunusuru mchakato wa Katiba na kuwezesha nchi kupata Katiba bora.
Alisema ushirikiano katika masuala mengine ikiwamo pendekezo la kushirikiana katika uchaguzi, litatafakariwa kwa kuzingatia mafanikio katika ushirikiano kwenye suala la mchakato wa Katiba Mpya ambao tunaendelea nao kwa sasa.
"Huu ndio msimamo ambao naamini pia viongozi wote wanao.
"Kwa kuzingatia kauli zilizotolewa na wenyeviti wote watatu Septemba 15 mwaka huu kwenye mkutano na waandishi wa habari, wakati wa kutoa tamko la pamoja la ushirikiano," alisema.
Hata hivyo, mchambuzi wa masuala ya siasa nchini, Dk. Benson Bana ameukosoa uamuzi huo kwa kudai kuwa hawawezi kuungana kwa sababu hawana kiwango cha kuing'oa CCM madarakani.
Dk. Bana aliweka wazi kwamba, hadhani kama vyama hivyo vitafaulu kuitoa CCM madarakani, kwa sababu havina mtaji wa kutosha wa wanachama.
Alieleza kuwa vyama vyote vitatu vinavyojiona vinaisumbua CCM, ambavyo ni CUF, Chadema na NCCR-Mageuzi, havijafanya utafiti wa kutosha kubaini mtaji wa wapiga kura walio nao.
Alisema Chadema ina nguvu ndogo Bara hasa kwenye maeneo ya mijini, CUF ina nguvu Zanzibar na NCCR-Mageuzi haina nguvu ya aina yoyote jambo linaloashiria udhaifu wa vyama hivyo, ambapo alivitaka kujipa muda wa kujipanga kabla ya kufikiria kuing'oa CCM.
Wenye mtazamo tofauti na huo wanasema kuwa endapo hatua hiyo ya vyama vya upinzani itafanikiwa, ni wazi itathibitisha kauli ya Mwenyekiti wa CCM kwamba chama hicho kijiandae kung'oka mwaka 2015 au 2020.
Hata hivyo bado kuna shaka juu ya maamuzi hayo ya vyama vya upinzani, kutokana na yale ambayo yamepata kushuhudiwa katika chaguzi nyingine zilizotangulia hususani zile za viti vya ubunge.
Imeshuhudiwa katika chaguzi kadhaa vyama hivyo vikisigana kufikia maamuzi ya kuachiana maeneo ya kusimamisha wagombea wenye nguvu.
Mwaka 2010 kwenye uchaguzi Mkuu, CUF kilikitaka Chadema kutosimamisha mgombea kwenye Jimbo la Tunduru kutokana chama chao kuwa na nguvu, hata hivyo wenzao walikataa.
Hali hiyo pia ilijitokeza kwenye Jimbo la Kiteto, Chadema iliitaka CUF kutosimamisha mgombea jambo ambalo halikutekelezwa. Chanzo: mtanzania

MAN U YAIBAMIZA NORWCH 4-0 

man u2 e7dc7
Chicharito (HM)
man u 309a1
MSHAMBULIAJI Javier Hernandez 'Chicharito' ameendeleza takwimu zake nzuri ndani ya Manchester United, licha ya kupewa nafasi chache za kucheza kwenye timu hiyo.

Nyota huyo wa Mexico usiku wa jana amefunga mabao mawili katika ushindi wa 4-0 wa Manchester United dhidi ya Norwich katika Kombe la Ligi.

Nyota huyo mwenye kipaji cha kufunga, alitikisa nyavu katika dakikaa 20 na 54 kwa penalti jana, wakati mabao mengine yalifungwa na Jones dakika ya 87 na Fabio dakika ya 90 na ushei.

Kikosi cha Man Utd jana kilikuwa: Lindegaard; Rafael, Ferdinand, Vidic, Büttner; Zaha/Rooney dk78, Cleverley/Anderson dk90, Jones, Young, Januzaj/Fabio dk90+3 na Hernandez.

Norwich: Bunn; Whittaker, R. Bennett, Bassong, Garrido; Snodgrass/Pilkington dk65, Fer, Johnson, Redmond/Murphy dk76, Hoolahan/Hooper dk89 na Elmander.

MAGUFULI BADO ALIA NA WENYE MALORI

magufuli21 16f82
WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli amesema tatizo la uzidishaji wa mizigo unaofanywa na magari makubwa iwapo litaendelea, barabara zote zitaharibika. Dk. Magufuli alitoa kauli hiyo bungeni jana, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF). (HM)
Katika swali lake, Hamad alitaka kujua sababu ya barabara zinazojengwa kuharibika ndani ya kipindi kifupi.
Dk. Magufuli alisema tatizo la kuharibika kwa barabara linasababishwa na ujenzi duni wa wakandarasi, lakini kwa kiasi kikubwa huharibiwa na magari yanayozidisha mizigo.
"Kwa mfano katika Barabara ya Dar es Salaam hadi Dodoma tayari upande wa kushoto wa barabara umeshabonyea.
"Kwa Tanzania uzito unaotakiwa kupita barabarani hautakiwi kuzidi tani 56, lakini magari yanazidisha hadi kati ya tani 90 na 98, tukiendelea hivyo si tu barabara zitavimba bali zitapasuka kabisa," alisema.
Alitoa viwango vya uzito unaotakiwa katika nchi kama Marekani kuwa ni tani 36.2, Uingereza Tani 44, Ufaransa Tani 40 na Ujerumani ni Tani 40.
Awali akijibu swali la msingi la Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige, Dk. Magufuli alisema Mkoa wa Geita umeingia mkataba na Mhandisi Mshauri kwa ajili ya kuifanyia marekebisho barabara ya Geita, Bukoli hadi Kahama.
Alisema mkataba huo ni kwa ajili ya kuifanyia upembuzi yakinifu pamoja na usanifu wa kina barabara hiyo kwa gharama ya Sh milioni 403.9 katika kipindi cha miezi 13.
Katika swali lake, Maige alitaka kujua lini utekelezaji wa kuiwekea lami barabara hiyo utaanza. Chanzo: mtanzania

MAJESHI YA SERIKALI YA CONGO YAKOMBOA MJI WA BUNAGANA 

congo fface
Jeshi la jamhuri ya kidemokrasi ya Congo limefanikiwa kuuteka mji wa mpakani na Uganda wa Bunagana ngome ya mwisho iliyobaki ya kundi la waasi wa M23. Maafisa wa serikali na mashahidi wanasema majeshi ya serikali yaliingia katika mji huo baada ya wapiganaji wa M23 kuondoka huko. (HM)

Kundi hilo la waasi liliuteka mji wa Bunagana na miji mingine ya jimbo la Kivu Kaskazini la Mashariki ya Congo lilipoanza uasi wake mwaka jana. Kumekuwa na mapigano makali kuanzia siku ya Ijumaa wakati majeshi ya serikali ya Congo yakisaidiwa na majeshi ya Umoja wa Mataifa kuanzisha mashambuklizi ya kukomboa miji hiyo inayoshikiliwa na waasi.
Idara ya Umoja wa Mataifa inayowahudumia wakimbizi – UNHCR, inaeleza kwamba mapigano yamesababisha maelfu ya wakongo kukimbilia Uganda. Chanzo: voaswahili

SIR ALEX FERGUSON AVUNJA YA MAUZO YA KITABU CHAKE 

Alex-ferguson-24901951 8a6f6
Kitabu cha Sir Alex Ferguson kimeweka rekodi ya kuwa kitabu kilichooza kwa haraka zaidi ndani ya Uingereza kikiuza nakala 115,547 katika siku chache za mauzo. (HM)

Kwa mujibu wa taarifa kutoka The Bookseller, kitabu hicho cha mocha wa zamani wa Manchester United kimevunja rekodi ya Delia Smith, ambaye kitabu chake cha mwaka 1999 cha mapishi kiliuza kopi 112,000 katika wiki take ya kwanza.
Pia kitabu cha Fergie kimevunja rekodi ya mauzo ya kitabu cha rafiki yake waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair, ambacho kiliuza kopi 92,000 katika wiki ya kwanza.
VITABU VILIVYOUZA ZAIDI UK:
Sir Alex Ferguson - My Autobiography - 115,547
Delia Smith - How to Cook - book two - 112,000
Tony Blair - A Journey - 92,000
David Beckham - My Side - 86,000
Paul Burrell - A Royal Duty - 77,000

BARCELONA YAENDELEzA MPANGO WA KUMSAJILI KIPA WA LIVERPOOL 

 reina 0b33b

KLABU ya Barcelona imeendelea na nia yake ya kumsajili kipa wa Liverpool, Pepe Reina. (HM)

Kipa huyo wa Hispania mwenye umri wa miaka 31 amepelekwa kwa mkopo wa muda mrefu Napoli, laki Rafa Benitez bado hajaamua kumnunua jumla wakati Liverpool inataka kuachana naye moja kwa moja.
Barca imefanya mazungumzo na kipa mwenye thamani ya Pauni Milioni 8 wa Borussia Monchengladbach, Marc-Andre Ter Stegen, mwenye umri wa miaka 21, lakini bado inamsaka mbadala wa Victor Valdes.
Katibu wa Ufundi, Albert Valentin alikwedna kumuona Reina akiiongoza timu yake kushinda 2-1 dhidi ya Marseille katika mechi ya Ligi ya Mabingwa wiki iliyopita kabla hajaenda kumuona Ter Stegen akimenyana na Eintracht Frankfurt.
Lakini mabingwa hao wa La Liga pia wanamfuatilia Fraser Forster baada ya Xavi kusema kipa huyo wa Celtic ni wa kiwango cha dunia.
Valdes atakamilisha miaka yake 11 ya kuishi Nou Camp mwishoni mwa msimu huku Forster akipewa nafasi kubwa ya kurithi mikoba yake.

M23 YACHAKAZWA ,VIONGOZI WATIMKA

mejakomba_edffb.jpg
Kuna ripoti kwamba Kundi la Waasi la M23 ambalo limekuwa likisababisha mapigano katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), limesambaratishwa katika operesheni kali iliyoendeshwa kwa ushirikiano baina ya vikosi vya nchi hiyo na vile vya Umoja wa Mataifa.
Taarifa za kusambaratishwa kwa kundi hilo zimekuja siku chache baada ya kuzuka mapigano makali yaliyosababisha kuuawa kwa askari mmoja wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Rajab Ahmed Mlima aliyeuawa kwa kupigwa risasi akiwa katika operesheni ya kuwaokoa raia, waliokuwa wamenasa kwenye eneo la mapigano.
Wanajeshi wa Tanzania ni sehemu ya vikosi vya Umoja wa Mataifa vya Kulinda Amani huko Congo (Monusco) vyenye askari pia kutoka Afrika Kusini na Malawi, vikiwa na kazi ya kupambana na kupokonya silaha za vikundi vya waasi wanaopigana kwenye nchi hiyo.(P.T)
Mkuu wa Vikosi vya Monusco, Martin Kobler alithibitisha taarifa za kusambaratika kwa kundi hilo la M23 na kuongeza kuwa vikosi vya Serikali na vile vya UN vilikuwa vikiendesha doria katika maeneo yaliyokuwa yakidhibitiwa.
Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) liliripoti jana kuwa Kiongozi wa M23, Bertrand Bisimwa amekimbia mashambulizi kwa kuvuka mpaka na kuingia Uganda wakati majeshi ya Congo yalipokuwa yanakaribia ngome yao.
Katika taarifa yake aliyoitoa mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juzi, Kobler alisema Kundi la M23 limepoteza mwelekeo.
"Ninachoweza kusema sasa tumefanikiwa kuwasambaratisha waasi na sasa vikosi vyetu kwa kushirikiana na vile vya DRC Congo vinadhibiti maeneo yote," alisema Kobler.
Hata hivyo, Msemaji wa JWTZ, Meja Eric Komba alisema asingeweza kutoa maelezo ya kina kuhusiana na taarifa za kusambaratishwa kwa kundi hilo la waasi, kwa vile wazungumzaji wakuu wa suala hilo ni Umoja wa Mataifa.
"Kama mnavyojua sisi tumekwenda DRC Congo kwa ridhaa ya Umoja wa Mataifa, hivyo kufanikiwa ama kushindwa kwa operesheni yoyote iko chini ya Umoja wa Mataifa wenyewe. Tanzania haiwezi kusema kwamba vikosi vyetu vimewasambaratisha waasi wakati mwenye jukumu la mwisho kutoa tamko hilo ni UN wenyewe," alisema Meja Komba.
Wakati hali ikiripotiwa kuwa hivyo, taarifa zinasema kuwa kundi hilo la M23 limemeguka mara mbili na kuzaliwa kundi jingine linalojiita M18. Maofisa wa Serikali ya Uganda wamesema kuwa kujitokeza kwa kundi hilo jipya kunaashiria kifo cha Kundi la M23 ambalo kwa miaka mingi limekuwa likidhibiti maeneo yanayotajwa kuwa na utajiri wa madini.
Kundi hilo la waasi ambalo limekuwa likidaiwa kupata msaada wa kijeshi kutoka kwa mataifa ya Rwanda na Uganda, limeelezwa kuelemewa nguvu na limesalimu amri katika maeneo liliyokuwa likishikilia.
Vikosi hivyo vya M23 vilianzisha upya mapigano hayo na kufanikiwa kuteka baadhi ya miji muhimu baada ya kuvunjika kwa mazungumzo ya amani yaliyokuwa yakiendelea Kampala, Uganda.
Waasi wakimbilia porini
Baada ya kutorokwa na viongozi wao, kuna taarifa askari wa kawaida wa Kundi la M23 wamejificha kwenye misitu ya mpaka wa DRC Congo na nchi za Rwanda na Uganda.
Msemaji la Jeshi la DRC, Olivier Hamuli aliliambia Shirika la Habari la Uingereza (Reuters) katika eneo la mapigano karibu na Goma kuwa Kundi la M23 limedhoofika baada ya kukimbiwa na askari wapatao 40, ambao wamejificha kwenye milima ya karibu na mpaka wa Rwanda.
"Kuna kundi dogo la M23 linapigana karibu na milima ya Rwanda," alisema. "Nadhani Rwanda watapaswa kufanya uungwana na kuwakamata."
Kundi la M23 lilianzisha vita mwaka 2012 baada ya baadhi ya askari wa Jeshi la DRC Congo kuasi baada ya kutoridhishwa na utekelezaji wa mkataba wa amani wa mwaka 2009, uliosainiwa na waasi hao wanaoaminika kusaidiwa na Rwanda.
DRC waandaa dua
Habari zaidi kutoka DRC Congo zinasema kuwa wafuasi wa dini ya Kiislamu katika mji wa Goma walifanya swala maalumu kwa ajili ya kuwaombea askari wa nchi hiyo na wale wa Umoja wa Mataifa waliofariki dunia kwenye operesheni hiyo.
Pia waliahidi kuandaa maandamano makubwa kwa ajili ya kushinikiza kuondoka kwa raia kutoka India na wale kutoka nchi za Ulaya kwani wanaamini ndio wamekuwa wakiwasaidia waasi kifedha.
Chanzo:Mwananchi

SAINI ZAKUSANYWA KUMNG'OA MAKINDA

makindapx_3a480.jpg
Spika wa Bunge, Anne Makinda (kulia) akizungumza na Mbunge wa Viti Maalumu, Clara Mwatuka na Mbunge wa Kilolo, Profesa Peter Msola katika Viwanja vya Bunge, mjini Dodoma jana.PICHA NA EDWIN MJWAHUZI
Mbunge wa Nzega, Dk Khamis Kigwangalla, (CCM), leo anatarajiwa kuanza kukusanya saini za wabunge akitafuta kuungwa mkono katika hoja ya kutokuwa na imani na Spika wa Bunge, Anne Makinda kwa madai kwamba amekuwa akikiuka kanuni za Bunge.
Dk Kigwangalla aliibua hoja ya kutokuwa na imani na Spika katika kikao cha wabunge wote cha kuelezea shughuli zitakazofanywa na Bunge katika mkutano wa 13, kilichofanyika juzi jioni kwenye ukumbi wa Pius Msekwa.
Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, jana alithibitisha kuwapo kwa mjadala huo katika kikao cha wabunge, lakini hakuwa tayari kueleza kwa undani na badala yake alisema kwamba leo ataanza kukusanya saini za wabunge kwa ajili ya kukamilisha hoja ya kutokuwa na imani na Spika Makinda.
Chanzo chetu kutoka katika kikao hicho cha wabunge kilibainisha kuwa Kigwangalla alihoji kuhusiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge (CCM-Bariadi Magharibi) kuteuliwa na Spika wakati katika kamati nyingine wenyeviti na makamu huchaguliwa na wajumbe wa kamati husika.(P.T)
Pia Dk Kigwangala alisema Spika Makinda alivunja kanuni kwa kuwapa posho ya Sh430,000 kwa siku wajumbe wa kamati inayoongozwa na Chenge wakati wajumbe wa kamati nyingine wamekuwa wakipewa Sh130,000.
"Anachokifanya Spika ni matumizi mabaya ya fedha za umma, inakuwaje wengine wafanye kazi hata bila posho lakini wao (Kamati ya Bajeti), walipwe posho ya Sh430,000 kwa siku?" chanzo hicho kilimkariri Dk Kigwangalla akihoji. Hata hivyo, Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah akizungumza na gazeti hili jana alisema mazingira ya kamati fulani kupata malipo ya ziada tofauti na viwango vya kawaida hutokea pale uongozi wa kamati husika unapoomba kwa Spika.
"Si kweli kwamba Kamati ya Bajeti inalipwa fedha za ziada kila wakati, hapana, ni pale tu wanapoomba malipo hayo kutokana na sababu ambazo lazima Spika aridhike nazo. Ieleweke kuwa siyo kamati hiyo tu, kwa sasa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ambayo inachambua miswada mingi nayo imekuwa ikiomba na baada ya Spika kuridhia basi nao wanapewa," alisema Dk Kashililah.
Katibu huyo wa Bunge alieleza kuwa zaidi ya kamati nane zimewahi kuomba malipo ya ziada kwa maana ya kutaka posho zaidi, ulinzi, usafiri na hata chakula, ikiwa zinakabiliwa na majukumu ya ziada pia katika mazingira tofauti nje ya utaratibu wa kawaida.
"Kimsingi, kamati nyingi zinapewa malipo tofauti, watu wanaweza kuwa na kazi mpaka saa saba au nane usiku, au wanakwenda kufanya kazi katika mazingira yasiyokuwa ya kawaida, taratibu zinamruhusu Spika kama akiridhika na maelezo ya kazi husika, basi anaruhusu kutekelezwa kwa maombi hayo," alisema Dk Kashililah.
Kuhusu Serukamba
Aidha, Dk Kigwangalla alinukuliwa akisema Spika amekiuka kanuni kwa kumchagua Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu, Peter Serukamba (Kigoma Mjini-CCM), kuwa mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti.
"Hakuna mbunge yeyote aliyepo katika kamati mbili lakini hata kungekuwa na sababu maalumu basi wa kuteuliwa angekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara, Mahmoud Mgimwa (Mufindi Kaskazini-CCM) ambaye TRA (Mamlaka ya Mapato Nchini) ipo chini ya kamati yake," kilisema chanzo hicho.
Chanzo hicho kilisema Dk Kigwangalla alisema badala ya kumweka karibu katika ushiriki, Mgimwa alipokwenda katika kamati hiyo aliambulia kufukuzwa.
Akizungumzia suala hilo, Dk Kashililah alisema Serukamba pamoja na wabunge wengine kadhaa waliteuliwa na Spika kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kamati hiyo wakati wa kipindi cha Bajeti Kuu ya Serikali.
Aliwataja wabunge wengine walioteuliwa kushiriki katika Kamati ya Bunge ya Bajeti kuwa ni John Cheyo (Bariadi Mashariki-UDP), Salahe Pamba (Pangani - CCM) na Hamadi Rashid Mohamed (Wawi - CUF).
Kanuni za Bunge
Kwa mujibu wa kanuni za Bunge katika toleo la mwaka 2007, kifungu cha 137(1), ili kumwondoa Spika madarakani, mbunge anayetaka kuwasilisha hoja hiyo atatakiwa kuwasilisha taarifa ya maandishi ya kusudio hilo kwa Katibu, akieleza sababu kamili ya kutaka kuleta hoja hiyo.
Kifungu kidogo cha pili kinasema baada ya kupokea taarifa ya maandishi ya kusudio la kumwondoa Spika kwenye madaraka, Katibu atapeleka taarifa hiyo kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa ajili ya kujadiliwa.
Kifungu cha tatu kinabainisha kuwa endapo kamati hiyo itaridhika kuwa zipo tuhuma mahususi dhidi ya Spika zinazohusu uvunjaji wa masharti ya ibara husika za Katiba, sheria au kanuni zinazoongoza shughuli za Bunge, basi kamati hiyo itaidhinisha hoja hiyo ipelekwe bungeni ili iamuliwe.
Kanuni zinasema Naibu Spika, atakalia Kiti cha Spika wakati wa kujadili hoja ya kutaka kumwondoa Spika madarakani na Spika atakuwa na haki ya kujitetea wakati wa mjadala na kwamba ili kumwondoa zinahitajika kura zisizopungua theluthi mbili ya idadi ya wabunge wote

MIILI 87 YA WAHAMIAJI YAPATIKANA JANGWANI

 miili_71e3a.jpg

Waokozi nchini Niger wanasema kuwa wamepata miili 87 ya watu waliofariki baada ya magari yao kuharibika walipokuwa wanajaribu kuvuka jangwa la Sahara.
Mmoja wa waliokuwa wanaendesha shughuli ya ukozi Almoustapha Alhacen, alisema kuwa miili yao ilikuwa katika hali mbaya ya kuharibika na kuwa ilikuwa imeliwa sehemu moja na wanyama pori.
Miili hiyo inaaminika kuwa ya wafanyakazi wahamiaji na familia zao. Wengi walikuwa wanawake na watoto.
Niger ni kivukio kikubwa cha wahamiaji wanaokuwa safarini kufika Kusini mwa Jangwa la Sahara kuelekea Ulaya.
Lakini wengi wa wanaofanikiwa kukamilisha safari hiyo huishia kufanya kazi katika mataifa ya Afrika Kaskazini.(P.T)
Kulingana na Bwana Alhacen, moja ya magari ambayo wahamiaji hao walikuwa wanatumia kwa usafiri, liliharibika walipotoka mji wa Arlit mwishoni mwa mwezi Septemba, au mwanzoni mwa Oktoba.
Maafisa wa usalama pia wamesema kuwa gari la pili liliharibika lilipokuwa njiani kurejea Arlit ili kutengenezwa.
Inaonekana kuwa miongomi mwa wasafiri hao takriban watu 10 walisafari kurejea Arlit na kutoa taarifa ya wenzao kukwama jangwani.
Iliarifiwa kuwa miili mitano ilipatikana.
Mnamo siku ya Jumatano, wafanyakazi wa kujitolea pamoja na wanajeshi, walipokuwa wanawatafuta wahamiaji hao, wakafanikiwa kupata maiti zaidi umbali wa kilomita 10 kutoka katika mpaka wa Algeria.
Kati ya maiti 48 waliopatikana, kulikuwa na miiili ya watoto na vijana na Alhacen alisema kuwa walikuwa wanaelekea nchini Algeria kutafuta vibarua vya mishahara midogo sana.
Akizungumza kutoka katika kiwanda cha kuchimba madini ya Uranium, Kaskazini mwa Agadez, aliambia BBC kuwa hiyo ndiyo iliuwa siku mbaya kwake baada maishani mwake baada ya kupata miili hiyo.

TANZANIA:TUNAWEZA KUJITOA A. MASHARIKI

130920062743_kikwete_kikwete_304x171_bbc_nocredit_340d9.jpg
Serikali ya Tanzania imesema inatafakari ushiriki wake ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na inaweza kujitoa ndani ya Jumuiya hiyo iwapo itaendelea kutengwa katika baadhi ya vikao.
Aidha imesema Tanzania haitambui vikao vinavyofanywa na nchi tatu zilizopo ndani ya Jumuiya hiyo ambazo zimekuwa zikizitenga Tanzania na Burundi.
Waziri anayehusika na masuala ya Afrika Mashariki wa Tanzania Samwel Sitta ameliambia Bunge la Tanzania kuwa makubaliano ya vikao hivyo vinavyofanywa na nchi za Kenya, Rwanda na Uganda yatatekelezwa na nchi hizo zinazofanya vikao hivyo kwa sababu vinafanyika nje ya utaratibu wa mkataba wa jumuiya hiyo.(P.T)
Katika mikutano iliyofanyika hivi karibuni Tanzania na Burundi hazikualikwa kwenye vikao hivyo.
Kwa mujibu wa Waziri Sitta mikutano ya wakuu wa nchi za Rwanda, Kenya na Uganda ambayo ilianza kwa kuitenga Tanzania ilifanyika Entebbe nchini Uganda mwezi Juni mwaka huu na kufuatiwa na mkutano wa pili uliofanyika Agosti mwaka huu huko Mombasa nchini Kenya ambapo nchi hizo tatu bila kuishirikisha Tanzania walizungumzia uanzishaji wa himaya moja ya forodha.
Mambo mengine waliyozungumza wakuu hao ilikuwa uanzishaji wa visa moja ya utalii kwa nchi zao na matumizi ya vitambulisho vya uraia ambavyo vitatumika kama hati za kusafiria miongoni mwa nchi hizo.
Aidha Waziri Sitta amesema ndani ya mikutano hiyo pia walizungumzia kuanzisha mchakato wa kuanzisha shirikisho la nchi hizo.
Tayari Tanzania imeanza mazungumzo na nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kuangalia ni kwa namna gani zitaanzisha ushirikiano nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kama zinavyofanya nchi za Rwanda, Uganda na Kenya.

RUFAA YA BABU SEYA, PAPII KOCHA KILICHOBAKI HUKUMU 

babuseyarufaa3_93851.jpg
Nguza Viking 'Babu Seya' (kulia) na mwanaye Johnson Nguza 'Papii Kocha' wakitoka mahakamani kwa furaha.
babuseyarufaa1_c9aa8.jpg
Nguza Viking 'Babu Seya' (wa pili kulia) na mwanaye Johnson Nguza 'Papii Kocha' (wa pili kushoto) wakiwa mahakamani.
babuseyarufaa3_1_3a090.jpg
Babu Seya na Papii Kocha wakiwa na furaha nje ya mahakama.
Baada ya majaji wa Mahakama ya Rufaa jijini Dar es Salaam kupitia hoja za mawakili wa serikali na utetezi kwenye Rufaa ya hukumu ya kifungo cha maisha jela katika kesi iliyokuwa ikimkabili mwanamuziki Nguza Viking 'Babu Seya' na mwanaye Johnson Nguza 'Papii Kocha', wameamua kuhairisha rufaa hiyo mpaka tarehe husika ya kutoa hukumu ya kesi hiyo itakapopangwa hapo baadaye.
(Picha na Richard Bukos / GPL) (P.T)

TANZANIA KUTOA MSIMSMI WIKI HII KUTWENGWA NA EAC

sitasamweli_26ea3.jpg
Tanzania imesema itatoa msimamo wake wiki hii kuhusu mkutano wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ngazi ya marais, uliotarajiwa kufanyika jana kujadili masuala yanayohusu maslahi ya nchi zilizoko katika ukanda huo bila kushirikishwa.
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, aliliambia NIPASHE mjini hapa jana kuwa mkutano huo ulitarajiwa kufanyika nchini Rwanda jana na kwamba ungehusisha marais wa nchi za Rwanda, Paul Kagame; Rais wa Uganda, Yoweri Museveni; Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza.
Alisema hayo alipokuwa akijibu swali la NIPASHE lililotaka kauli ya serikali kuhusu uamuzi wa nchi hizo kuendeleza tabia yao ya kuitenga Tanzania katika mikutano yao.(P.T)
"Mkutano wa Rwanda unafanyika leo ngazi ya marais. Tunasubiri kupata maazimio. Tanzania itatoa msimamo wiki hii," alisema Waziri Sitta bila kutaka kuingia kwa undani kuhusiana na suala hilo.
Mkutano huo ni wa tatu kufanyika bila kuishirikisha Tanzania. Mara mbili mfululizo, marais wa nchi hizo walikutana na kujadili mchakato wa kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo, huku wakiitenga Tanzania.
Marais Kenyata, Museveni na Kagame alikutana mara zote hizo bila kumualika Rais Jakaya Kikwete.Kwenye vikao viwili vilivyofanyika nchini Uganda na Kenya, viongozi hao walikubaliana kutekeleza kwa haraka miradi ya ujenzi wa reli itakayounganisha nchi hizo na bomba la mafuta litakalojengwa kuanzia Sudan Kusini hadi Mombasa na lingine kutoka Kenya hadi Rwanda.
Pia nchi hizo zilitangaza kuanzia Januari Mosi, raia wao watembeleane bila kuwa na hati za kusafiria, pia kuwa na viza moja kwa watalii.
Mkutano wa Kenya ulioambatana na ufunguzi wa gati katika bandari ya Mombasa, nchi za Burundi na Sudani Kusini zilialikwa na kuwakilishwa na mawaziri wao waandamizi, lakini Tanzania haikualikwa.
Vile vile, vyombo vya habari viliwakariri baadhi ya mawaziri wa nchi hizo waliopewa jukumu la kusimamia makubaliano hayo, wakiyaeleza kuwa ni ya jumuiya nzima na endapo Tanzania ikipenda kuingia itakaribishwa. Kutokana na hali hiyo, Serikali ya Tanzania ilionyesha wasiwasi wake juu ya mwenendo wa nchi hizo.
Ilipinga dalili zinazoonekana kwa nchi za Kenya, Uganda na Rwanda kutumia jina la EAC kuomba fedha au kugharimia miradi inayopaswa kuwa ya jumuiya.
Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Abdullah Juma Saadalla.
Alisema malalamiko hayo yalishawasilishwa pia katika kikao cha Baraza la Mawaziri wa EAC, kilichofanyika jijini Arusha.
Dk. Saadalla alisema serikali imemtaka Katibu Mkuu wa EAC, Dk. Richard Sezibera, kutoa maelezo juu ya gharama ya miradi kadhaa inayoaminika kuwa sehemu ya jumuiya hiyo. Pia alisema hatua zilizochukuliwa na nchi hizo kwa kukubali kuanzisha utaratibu wa matumizi ya viza moja na vitambulisho vya pamoja, ni mfano wa ubabe usiokidhi matakwa ya kidemokrasia.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, alisema hivi karibuni kuwa Tanzania ikibaini kuwapo haja ya kujitoa EAC itafuata utaratibu kwa kulifikisha suala hilo bungeni ili wabunge waliamue.
CHANZO: NIPASHE

OMARI KIMWERI KUGOMBANIA UBINGWA WA DUNIA WA WBC 

 1236109_514193065317691_1031784424_n_8afe6.jpg

BONDIA MTANZANIA Omari Kimweri 'Lion Boy' anaefanya shughuli zake Deer Park, Victoria, nchini Australia anatarajia kuwa mtanzania wa kwanza kupanda ulingoni November 30 kugombea ubingwa wa Dunia unaotambuliwa na WBC uzito wa kg47.5 minimum weight
Mpambano huo utakaopigwa nchi ya China November 30 na bingwa wa dunia wa uzito huo nchini china
xiong zhao zhong ni bingwa wa dunia WBC minimum weight ambaye anashikilia taji hilo kwa sasa katika uzito huo.(P.T)
Kimweri anakuwa mtanzania wa kwanza kuwania taji kubwa kabisa Duniani akitokea nchini Austalia uku sapoti kubwa akitegemea kutoka Tanzani ambapo alipo zaliwa
na kigezo cha kufanya apate pambano hilo kubwa ni kutokana na rekodi yake pamoja na kutakiwa mtu ambaye anatokea bara la Afrika ambapo kula imemdondokea bondia Omari Kimweri kwa mara ya kwanza mtanzania huyo ataonekana Dunia nzima akijaribu kuwania ubingwa wa WBC
Ambapo ni kiu ya mabondia wengi duniani kumiliki mikanda mikubwa ya kimataifa Kimweri mwenye rekodi ya kucheza michezo 16 ambapo ameshinda michezo 13 na kuchezea kichapo michezo 3 na mpinzani wake
Xiong Zhao Zhong amecheza michezo 26 akishinda 21 kupigwa 4 na kutoka droo moja
Mabondia hawo wote vijana wenye umri mdogo wa miaka 31 wate wawili wakitofautiana mwezi mmoja tu katika kuzalia mpambano huo umekuwa gumzo katika nchi tatu kwa sasa kwani kila mmoja anajiandaa kivyake
Kimweri kwa sasa anaefanya mazoezi makari uku akipewa sparng na bondia Randy petalcoria wa Philippines ambaye ni bingwa wa light fly weight
Omari Kimweri kwa sasa yupo katika mazoezi mazito ya kujiandaa na mpambano huo huku akitegemea zaidi duwa za watanzania kwa kuwa ushindi wake ni ushindi wa watanzania wote Mungu Ibariki Tanzania Mungu Mbariki Bondia Omari Kimweri

Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi NSSF Watembelea Miradi Dar 

IMG_0777_ac441.jpg
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) pamoja na maofisa wa NSSF wakitembelea mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam.
IMG_0449_ee346.jpg
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) pamoja na maofisa wa NSSF wakitembelea mradi wa nyumba za bei nafuu eneo la Mtoni Kijichi.
IMG_0868_281bc.jpg
Meneja Mradi wa NSSF, Mhandisi Karim Mattaka (wa kwanza kulia waliokaa mezani) akitoa taarifa fupi kwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii na maofisa waandamizi wa taasisi hiyo juu ya maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni.
IMG_0585_25268.jpg
Meneja Mradi wa NSSF, Mhandisi Karim Mattaka (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii na maofisa waandamizi wa taasisi hiyo juu ya maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni.(P.T)
IMG_0315_37968.jpg
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) pamoja na maofisa wa NSSF wakiteremka kwenye gari katika moja ya miradi ya taasisi hiyo walipotembelea jana.
IMG_0372_e383f.jpg
Mmoja wa maofisa wa juu na mhandisi kutoka NSSF akifafanua jambo kwa wajumbe wa bodi.
IMG_0326_ff2ff.jpg
Afisa Mradi msimamizi na Msanifu wa NSSF, Deogratias Mponeja (wa kwanza kushoto) akitoa maelezo juu ya mradi wa awamu ya tatu ya ujenzi wa nyumba nafuu kwa wajumbe.
IMG_0472_93d1c.jpg
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau (wa pili kulia) akiwa na Eunice Chiume wakizungumza jambo katika ziara ya wajumbea wa Bodi ya NSSF kutembelea miradi jijini Dar es Salaam.
IMG_0450_f87b0.jpg
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi NSSF Watembelea Miradi Dar
IMG_0330_9bfec.jpg
Mkurugenzi wa Mradi na Msanifu Majengo wa NSSF, Mkurugenzi wa Mipango, Miradi na Uwekezaji wa NSSF, Yacoub (aliyesimama) akitoa taarifa fupi juu ya maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu kwa wajumbw wa bodi.
Na Joachim Mushi, Dar es Salaam
WAJUMBE wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wamefanya ziara ya kutembelea baadhi ya miradi kadhaa inayotekelezwa na shirika hilo iliyopo jijini Dar es Salaam. Miradi iliyotembelewa katika ziara hiyo ni pamoja na ule wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu uliopo eneo la Mtoni Kijichi na ujenzi wa Daraja la Kisasa eneo la Kigamboni.
Akitoa taarifa fupi kwa wajumbe wa bodi ya NSSF wakiwa eneo la ujenzi wa nyumba za bei nafuu na za kisasa eneo la Mtoni Kijichi, Mkurugenzi wa Mipango, Miradi na Uwekezaji wa NSSF, Yacoub Kidula alisema eneo hilo linatekelezwa kwa awamu mbili za ujenzi wa nyumba aina mbalimbali.
Alisema awamu ya pili ambayo iliendelea baada ya kukamilika ya kwanza ya ujenzi wa nyumba 85, imetekelezwa kwa ujenzi wa nyumba 215 eneo la Mtoni Kijichi mradi ambao tayari umekamilika na nyumba zimeanza kuuzwa kwa wanachama wa NSSF. Alisema nyumba 200 tayari zimekamilika huku 15 zilizosalia zikiwa katika hatua za mwisho kukamilika.
Alisema tayari Shirika hilo limeanza kutekeleza ujenzi mwingine wa awamu ya tatu utakaowezesha ujenzi wa nyumba za kisasa na bora zaidi zenye uwezo wa kuchukua familia 820 zikiwa na ghorofa moja huku zikiwa zimeboreshwa zaidi kihuduma ukilinganisha na zilizojengwa awali.
Aidha akifafanua juu ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu zinazoendelea kujengwa na NSSF, alisema mbali na kuwa za bei ya chini zinahuduma muhimu za kijamii kama umeme, maji, mfumo mzuri wa kuifadhi maji taka, eneo la nje la ziada pamoja na vifaa vingine zikiwemo feni vyumba vyote, mfumo wa maji ya moto kwenye mabafu na sakafu ya kisasa 'tiles'.
Alisema nyumba zinazojengwa zinaukubwa na idadi ya vyumba tofauti kulingana na maitaji ya mteja, yaani kuanzia vyumba viwili hadi vitatu vya kulala huku vyote vikiwa na sebule, jiko, choo pamoja na stoo. Aliongeza kuwa milango na madirisha yamejengwa kwa vioo na chuma (nondo) ili kuimarisha zaidi kiusalama huku jiko likiwa na kabati maalumu na za kisasa kwa ajili ya kuifadhia vitu.
Kidula alisema nyumba ya chini itauzwa takribani sh milioni 66 za kitanzania bei hiyo ikiwa ni pamoja na VAT. Wajumbe wa bodi pia walitembelea mradi mkubwa wa NSSF wa ujenzi wa daraja la Kigamboni ambao unafanywa na taasisi hiyo kwa kushirikiana na Serikali.
Akitoa taarifa za maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo, Meneja Mradi huo, Mhandisi Karim Mattaka alisema licha ya ujenzi huo kuendelea vizuri kwa sasa zipo changamoto kadhaa za ujenzi ambazo zilijitokeza hivyo kushughulikiwa mara moja.
Alisema daraja hilo la kisasa litakalokuwa na njia (barabara sita) yaani tatu za kwenda Kigamboni na tatu za kurudi linatarajiwa kuunganishwa kisasa na barabara ya Mandela huku likiwa na njia za kutosha kuzuia msongamano wa magari.
Akizungumzia ziara hiyo ya Wajumbe wa Bodi, Meneja Uhusiano Kiongozi, Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume alisema ni ziara ya kawaida ya wajumbe hao kukagua miradi ya taasisi hiyo na huenda ziara hiyo ikawa na manufaa ya punguzo la riba kwa wanachama wanunuzi wa nyumba hizo.
Imeandaliwa na www.thehabari.com

KIONGOZI WA NGAZI YA JUU WA AL-SHABAAB AUAWA SOMALIA 

017116949_35400_d76ec.jpg
Kiongozi wa ngazi ya juu anayeongoza mashambulizi ya kujitoa mhanga ya kundi la al-Shabaab lenye mafungamano na al-Qaeda ameuawa katika shambulizi la ndege isiyoruka na rubani Kusini mwa Somalia
Waziri wa Mambo ya Ndani, Abdikarin Hussein Guled, ameiambia redio ya serikali kuwa idara ya ujasusi ilikuwa ikimfuatilia Ibrahim Ali Abdi, maarufu kama Anta-Anta, kwa muda sasa kabla ya shambulizi hilo kufanywa jana Jumatatu 28.10.2013
Waziri huyo hajasema ni nani aliyefanya shambulizi hilo, lakini afisa mmoja mjini Washington amesema jeshi la Marekani lilifanya shambulizi la ndege isiyoruka na rubani likililenga kundi la al-Shabaab nchini Somalia jana Jumatatu.(P.T)
"Operesheni hiyo ambayo mtu huyu aliuawa ilikuwa muhimu kwa serikali. Mtu huyu alikuwa na jukumu kubwa kwa raia wengi wasio na hatia na kifo chake kitasaidia kurejesha amani," alisema waziri huyo kupitia Radio Mogadishu.
Maafisa kutoka serikali ya Somalia inayoungwa mkono na jamii ya kimataifa wamemtaja mwanamgambo aliyeuawa kuwa anayefahamika vyema kwa kutengeneza mabomu ya kuvaa mwilini pamoja na ya kutengwa ndani ya gari ambayo hutumiwa mara kwa mara na waasi kuyashambulia maeneo ya serikali. Hapajakuwa na kauli yoyote kutoka kwa wapiganaji hao.
Shambulizi hilo linakuja wiki chache baada ya shambulizi kali kufanywa katika jumba la maduka ya Westgate jijini Nairobi, Kenya, lililodaiwa kufanywa na al-Shabaab ambapo watu 67 waliuawa.
Kisha kikosi maalumu cha jeshi la wanamaji la Marekani kikafanya shambulizi katika bandari ya kusini ya Barawe mapema mwezi huu (Oktoba) na kushindwa kufikia lengo lake: ambalo lilikuwa ni kiongozi mmoja wa ngazi ya juu wa al-Shabaab na Mkenya mwenye asili ya kisomali kwa jina Abdulkadir Mohammed Abdulkadir, pia anayefahamika kama Ikrima.
Afisa mmoja wa Marekani ambaye hakutaka kutajwa jina lake, hajasema sehemu ambayo ndege hiyo isiyoruka na rubani ilianzia safari yake, lakini jeshi la Marekani huendesha shughuli zake za ndege hizo kutoka kambi za nchini Djibouti na Arba Minch kusini mwa Ethiopia.
Wapiganaji wa al-Shabaab wametimuliwa kutoka miji mikuu ya Somalia, ikiwa ni pamoja na Mogadishu na bandari ya kusini mwa nchi hiyo Kismayo, kufuatia operesheni ya jeshi la Umoja wa Afrika linalosimamiwa na Umoja wa Mataifa na ambalo sasa lina wanajeshi 17,700.
Kundi hilo hata hivyo linayadhibiti maeneo makubwa ya kusini mwa Somalia na katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita, limekiongeza kiwango cha mashambulizi yake ya kujitoa mhanga.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP

Tuesday, October 29, 2013

Kuhusu Daktari wa Michael Jackson kutoka jela

2Taarifa ikufikie kwamba aliekua daktari wa mwimbaji staa wa Pop duniani Michael Jackson, Conrad Murray ameachiwa huru kutoka jela baada ya kutumikia kifungo kwa miaka miwili kati ya minne aliyokua amehukumiwa kutokana na kifo cha MJ mwaka 2009.
CNN wameripoti kwamba Daktari huyu ilibidi atumie mlango mwingine kutoka jela ili kukwepa waandishi wa habari pamoja na baadhi ya mashabiki wa Michael Jackson wenye hasira waliokuwemo nje ya jela baada ya kupata taarifa kwamba anatolewa kwenye jela hiyo ya Los Angeles.
Mwanasheria wake amekaririwa akisema kwamba Doctor Conrad anaweza kurudi kuendelea na kazi yake ya udaktari lakini moja kati ya kauli za familia ya Michael Jackson ni ‘ni wazi kwamba Conrad ndio alimuua Michael Jackson, tunamatumaini kwamba hatofanya udaktari tena na kumuumiza wengine’

Picha za ajali ya pili aliyoipata David Beckham na mwanae

7
Staa wa soka David Beckham (38) pamoja na mtoto wake wa kwanza aitwae Brooklyn walipata ajali ndogo nje ya nyumba yao huko Beverly Hills Marekani baada ya gari lao kugongana na gari jingine wakati wakitoka nyumbani.
Hakuna alieumia kwenye hii ajali ambayo iliihusisha Range Rover ya Beckham yenye thamani ya dola za Kimarekani elfu 75 ambapo iliumia sehemu ya mbele na mashuhuda wanasema baada tu ya ajali David Beckham hakuondoka kwenye eneo la tukio, alichofanya ni kusubiri Polisi.
Hii inakua ajali ya pili ya gari kwa Beckham kuipata akiwa na mtoto wake huyu wa kwanza mwenye umri wa miaka 14, kama unakumbuka ajali ya kwanza waliipata mwaka 2011 huko Los Angeles ambapo hakuna aliejeruhiwa.
1
4
6
2
5

Monday, October 28, 2013

YANGA, MGAMBO JKT KUVAANA TAIFA LEO

Yanga-Mgambo_d3a44.jpg
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Bara leo itashuka katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kupambana na Mgambo JKT katika mchezo wa raundi ya kumi na moja ya ligi hiyo.
Yanga inaingia uwanjani leo ikiwa na pointi 19 ilizopata katika mechi 10 ilizocheza huku ikiwa nafasi ya nne. Azam inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 23 ikifuatiwa na Simba yenye pointi 20 huku zote zikiwa zimecheza mechi 10. Mbeya City ni ya tatu ikiwa na pointi 20 katika mechi 10.
Kwa upande wao, Mgambo wanaingai uwanjani wakiwa na pointi tano walizopata katika mechi 10. Timu hiyo inaburuza mkia katika ligi hiyo.
Kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya leo kutakuwa mchezo utakaozikutanisha timu mwenyeji za mkoa huo ambazo ni Mbeya City na Tanzania Prisons. Rhino Rangers na JKT Ruvu zitacheza katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.(P.T)
Raundi ya 12 ya ligi hiyo itaanza Oktoba 31 mwaka huu kwa mechi kati ya Simba na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Novemba Mosi mwaka huu kutakuwa na mechi kati ya Yanga na JKT Ruvu kwenye uwanja huo huo.
Novemba 2 mwaka huu kutakuwa na mechi nne; Mgambo Shooting na Coastal Union (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Tanzania Prisons na Oljoro JKT (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).
Raundi hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7 mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashani United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, Rhino Rangers vs Tanzania Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar.
Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City wakati Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

ABSENCE OF PRES.KIKWETE,NKURUNZIZA LOOMS LARGE IN 3rd INFRASTRUCTURE SUMMIT ROOMzzzzzeast_africa_8cd01.jpg

From left: Presidents Salva Kiir (South Sudan) Yoweri Museveni (Uganda) Paul Kagame (Rwanda) and Uhuru Kenyatta (Kenya). President Jakaya Kikwete of Tanzania and Pierre Nkurunziza of Burundi stayed out of the loop of the third infrastructure summit in Kigali, Rwanda.
Cross-posting this article by DANIEL K. KALINAKI from the AFRICA REVIEW — President Jakaya Kikwete of Tanzania and Pierre Nkurunziza of Burundi stayed out of the loop of the third infrastructure summit in Kigali, Rwanda but their absence loomed large in the conference room.
President Museveni told journalists in a brief press conference on Monday that talk of a "coalition of the willing" involving Uganda, Rwanda and Kenya was inaccurate since the three countries were only discussing infrastructure projects along the
northern corridor and would involve Tanzania once discussions moved to the southern corridor.
However, the final communiqué read out after the meeting of the three heads of state did not include an update on efforts to fast-track the East African political federation, a matter whose discussion outside the East African Community Tanzanian officials have expressed concern over.(P.T)
At the last infrastructure summit in Mombasa Uganda was tasked to spearhead efforts to fast-track the political federation and a committee headed by the country's Internal Affairs Minister Gen. Aronda Nyakairima met in Kampala this month to kick-start the writing of a draft constitution. They had been expected to provide an update to the summit on Monday.
Gen. Nyakairima on Monday declined to comment on the exercise while Kenya's East African Affairs, Commerce and Tourism minister Phyllis Kandie said talk of a political federation was a "side-show" which had not been discussed by the ministers or the heads of state in Kigali.
Tanzania's ministry of East African Cooperation recently issued a statement warning that the tri-lateral talks among Kenya, Rwanda and Uganda are against the EAC protocol.
The statement argued that all EAC member states had to endorse the regional infrastructure deals signed by Presidents Kenyatta, Museveni and Kagame otherwise they contravene Article 7(1) (e) of the EAC protocol.
"Even though this Article allows member countries to enter bi-lateral or Tri-lateral agreements, it is a must that issues under consideration for implementation under this arrangement are fully discussed and agreed upon by all member countries," the statement from the ministry said.
However President Museveni said yesterday he was unaware of complaints from Tanzania about the trilateral agreements.
"Unless I get an official letter from the state, I consider what I see in the press as lies," he said in response to a journalist's question.
Tanzanian diplomats are understood to have expressed their concerns about being left out of the regional plans through the Council of Ministers. Officials in Dar es Salaam say they have not been invited to participate in the Coalition of the Willing and are expected to raise the matter more directly at the next EAC Heads of State Summit in Kampala in late November.
Burundi sent a ministerial delegation to the last summit in Mombasa and President Nkurunziza visited with President Kenyatta a few days later on what was said to be a private visit. We were unable to confirm whether Bujumbura or Dar es Salaam had been invited to Monday's summit.
---
DANIEL K. KALINAKI
Twitter: @kalinaki
Email: dkalinaki@ke.nationmedia.com
Source: http://www.wavuti.com

UN: WAASI WA M23 SIO TISHO TENA

131028190903_drc_rumangabo_304x171_reuters_nocredit_088c6.jpg
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, ameambia baraza la usalama la Umoja huo kuwa makali ya kundi la waasi la M23 kama tisho la kijeshi yamekwisha
Martin Kobler alisema kuwa kundi hilo limeondoka katika maeneo yao ya kivita mashariki kwa DRC, na kwamba sasa wako katika eneo dogo karibu na mpaka wa Rwanda.
Eneo lengine la tano lililokuwa ngome ya waasi hao liliweza kudhibitiwa na jeshi la serikali siku ya Jumatatu.
Waasi hao wanasema kuwa wameondoka katika maeneo yao ya vita kwa muda.
Aidha bwana Kobler aliambia baraza al usalama kupitia kwa njia ya Skype kuwa kwa sasa ni kama kundi ilo limefika mwisho wake.(P.T)
Aliongeza kwamba waasi wameondoka katika ngome yao moja kuu ya mlima Hehu karibu na mpaka wa Rwanda.
Baada ya mkutano huo, balozi wa Ufaransa Gerard Araud alisema anatumai kutakuwa na mazungumzo sasa kati ya waasi hao na serikali.
Alisema: ''Bwana Kobler ametuarifu kuwa wanashuhudia mwisho wa kundi la M23 kama tisho la kijeshi. Kwa hivyo naona kama ni hatua nzuri na kwamba hata kulikuwa na makubaliano kuwa sasa tushinikize mazungumzo kuanza tena mjini Kampala.''
Mazungumzo ya amani kati ya serikali na waasi wa M23, mjini Kampala, yalisitishwa wiki jana.
Hali hata hivyo hali ilikuwa imetulia Mashariki mwa DRC kwa muda wa wiki moja.
Watu walionekana wakishangilia wakati wanajeshi walipoingia mji wa Rumangabo ambao ulikuwa umetekwa na waasi hao
Na sasa serikali inadhibiti hali mjini humo, kwa mujibu wa gavana wa jimbo la Kivu Kaskazini, Julien Paluku.
''Tumekuwa na mikutano miwili ili kujadili tutakavyoimarisha hali ya wananchi...na tutatangaza kuanza tena kutolewa kwa huduma za serikali katika muda wa masaa 24,'' alisema Paluku.
Mji wa Rumangabo – ulio umbali wa kilomita 50 Kaskazini mwa Goma, mji rasmi wa Mashariki mwa DRC, ulikuwa na kambi tatu kubwa za kijeshi nchini humo kabla ya kutekwa na waasi wa M23 mwaka jana.
Hapana shaka kuwa majeshi ya serikali yamefikia hatua kubwa na kupata ushindi mkubwa dhidi ya waasi,

TRL KUCHUNGUZA AJALI ZA TRENI TABORA 

mwakyemba_f50eb.jpg
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania, (TRL) umeunda tume kuchunguza chanzo cha ajali zilizotokea Urambo na Usoke mkoani Tabora.
Tume hiyo inajumuisha wafanyakazi wa Idara za Usafirishaji, Fundi mitambo, Ujenzi na Usalama wa Reli.
Akizungumza na gazeti hili jana ofisini kwake, Msemaji wa kampuni hiyo, Midladjy Maez, alisema treni hiyo ya mizigo ilikuwa ikitoka Dar es Salaam kwenda Kigoma.
Kwa mujibu wa Maez, ilianguka ikiwa na mabehewa 10 ya mafuta na manne kati ya hayo yalianza kuvuja.
Alisema hasara iliyotokana na kumwagika kwa mafuta hayo yaliyokuwa mali ya Kampuni ya GBP, TRL itafahamika baada ya tume hiyo kumaliza kazi yake.
Maez alisema hakuna abiria aliyeathiriwa na ajali hiyo na kwamba jana jioni treni ilitarajiwa kuendelea na safari yake.(P.T)
Wakati hayo yakitokea, Serikali imetangaza mkakati wa Matokeo Makubwa Sasa katika sekta ya Uchukuzi na Ujenzi kwa kununua mabehewa 123 na vichwa 21 vya treni ili kukabiliana na changamoto zilizopo katika sekta hizo.
Serikali pia ipo katika hatua ya kupunguza vituo vya ukaguzi wa mizigo kutoka vituo 15 hadi kufikia vituo vitatu na kufunga mitambo ya kisasa ya kupima mizigo wakati gari inapotembea barabarani ili kurahisisha upekuzi wa mizigo.
Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, alipokuwa akifungua mkutano wa saba wa mwaka wa wadau wa sekta ya usafiri, uchukuzi na ujenzi.
Dk Mwakyembe alisema "Serikali kwa sasa imeanza kufufua miundombinu ya reli ili kurahisisha usafirishaji wa mizigo."

SUDAN MBILI KUSHAURIANA KUHUSU ABYEI 

130902030247_bashir_kiir_304x171_ap_nocredit_23d16.jpg
Rais wa Sudan, Omar al-Bashir, anasema kuwa atashirikiana na mwenzake wa Sudan Kusini kutatua mgogoro kuhusu eneo wanalozozania la Abyei.
Bwana al-Bashir alisema kuwa anataka mwafaka utakaokubalika kwa watu wa Abyei kupatikana.
Hali ya Abyei haijajulikana tangu Sudan Kusini kujipatia uhuru mwaka 2011.
Watu wa kabila la Ngok Dinka -- walio na uhusiano na Sudan Kusini wanajiandaa kwa kura ya maoni kuhusu ikiwa watakuwa upande wa Sudan au Sudan Kusini.
Watu wa kabila la kiarabu wa Misseriya -- ambao pia wanaishi katika eneo hilo -- hawatashiriki kwenye kura hiyo ya maoni.(P.T)
Muungano wa Afrika mnamo siku ya Jumapili waliituhumu serikali ya Sudan kwa kuzuia wajumbe wa muungano huo kuzuru eneo la Abyei.
Wanasema kuwa hawatakubali matokeo ya kura hiyo ya maoni.
Hatua hii ikiwa itafanyika, bila shaka itasababisha taharuki zaidi katika jimbo la Abyei , moja ya chanzo cha mgogoro kati ya Sudan na Sudan Kusini.
Hakuna mmoja kati ya nchi hizo anataka kukosa udhibiti wa jimbo hilo, hasa kwa sababu ya visima vya mafuta vilivyoko katika jimbo lenyewe ingawa visima vyenyewe vinadidimia.
Pia kuna ardhi yenye dhoruba.
Bashir kweli amesema kuwa atashirikiana na mwenzake Salva Kiir. Lakini je anaweza kukubali kupoteza Abyei, hususan anapokabiliwa na maandamano dhidi ya utawala wake ?