TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Saturday, December 15, 2012

WAZIRI MKUU AAHIDI MATREKTA KWA VIJANA WA ILUNDE

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameahidi kutoa trekta moja kwa ajili yakikundi cha vijana katika kata ya Ilunde ili waweze kuondokana na kilimo cha jembe la mkono na waboreshe uchumi wa eneo hilo.mAmetoa ahadi hiyo leo (Ijumaa, Desemba 14, 2012), wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Ilunde kwenye uwanja wa shule ya msingi Ilunde katika siku ya pili ya ziara yake jimboni kwake Katavi wilayani Mlele,
mkoani Katavi.
Waziri Mkuu ambaye ni mbunge wa jimbo la Katavi alisema atawapatia trekta hilo kama mkopo ili nao wakirudisha trekta jingine, liweze kukopeshwa kwa kikundi kingine. “Hapa naanzisha ‘Kopa trekta lipa trekta’. Litakuja likiwa na jembe lake pamoja na harrow,” alisema Waziri Mkuu huku akishangiliwa.
“Ni lazima tuondokane na kilimo cha jembe la mkono kwa sababu hakina tija… na zaidi nasisistiza kuondokana na kilimo cha matuta kwa sababu kinatumia nguvu nyingi na kupoteza eneo kubwa ambalo lingetumika kupanda mazao,” alisisitiza.
Waziri Mkuu alielezwa matatizo yanayowakabili wakazi hao yakiwemo ubovu wa barabara ya kutoka Inyonga (km. 60) na ukosefu wa wauguzi wa kike kwa ajili ya akinamama wajawazito. Pia waliomba kupatiwa minara wa mawasiliano ya simu kwa sababu wanapotaka kupiga simu, wanalazimika kupanda mti mmoja tu ambao uko km.12 kutoka kijijini hapo
Akijibu maombi yao, Waziri Mkuu aliwaita Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mpanda na Mhandisi wa Wilaya hiyo ili watoe maelezo kwa wananchi hao.Kuhusu wauguzi, mganga mkuu wa wilaya hiyo, Dk. Emmanuel Kamgobe alisema wanashugulikia suala hilo.

No comments:

Post a Comment