JK KUFUNGUA MKUTANO WA GAVI 
Na Heka Paul na Shakila Galus- MAELEZO- Dar es salaam
 Rais
 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete 
anatarajiwa kufungua Mkutano wa Kimataifa wa wadau wa chanjo duniani 
(GAVI) utakaonza leo.
Mkutano huo unatarajiwa kuwa washiriki 600 kutoka nchi mbalimbali 
duniani wakiwemo wake wa Marais , Mawaziri wa Afya, fedha na watu 
mashuhuri kutoka nchi 73. 
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana mjini Dar 
es salaam na Kaimu Katibu Mkuu Regina Kikuli inasema kuwa lengo la 
mkutano huo ni pamoja na kujadili mafanikio na changamoto zinakabili 
huduma ya utoaji wa chanjo duniani. 
Taarifa hiyo inaongeza kuwa hii ni mara ya kwanza mkutano wa aina hiyo 
kufanyika Afrika mashariki na kuongeza kuwa sababu zilizopelekea mkutano
 kufanyika Tanzania ni pamoja na mafanikio makubwa katika utoaji wa 
huduma za chanjo za watoto na mama wajawazito.
 Hivyo basi washiriki watapata fursa ya kutembelea vituo vinavyotoa 
huduma za chanjo nchini ili kujionea mafanikio na changamoto zilizopo 
pamoja na kujifunza.
 
Vilevile washiriki watapata fursa ya kujadili masuala ya chanjo ikiwemo 
uingizwaji wa chanjo mpya na masuala ya afya ya mama na mtoto. 
Pia kutakuwepo na uzinduzi wa chanjo mbili mpya za magonjwa ya kuhara, 
homa ya uti wa mgongio kwa watoto chini ya mwaka mmoja ambazo zinatolewa
 nchini kwa hisani GAVI.

No comments:
Post a Comment