Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Mh. Dkt Terezya
Huvisa akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa Taarifa ya Hali ya Mazingira
ya Jiji la Dar es Salaam ambapo amesema katika Mkutano wa Tisa wa
Mawaziri wa Mazingira wa Afrika (AMCEN) uliofanyika mjini Kampala Julai
2002, ulibaini kuwa ukosefu wa taarifa za hali ya mazingira katika bara
la Afrika ni moja ya sababu zinazochangia mipango duni ya usimamizi wa
shughuli za maendeleo na utekelezaji Mikataba ya Kimataifa ya utunzaji
mazingira.
Amesema kutokana na hali hiyo AMCEN
iliiomba UNEP wafadhili program ya Afrika ya Mtandao wa Hali ya
Mazingira (Africa Environmental Information Network) ili kuongeza uwezo
wa nchi za Afrika wa kuwa na Taarifa za Hali ya Mazingira na Mtandao wa
Habari baina ya nchi za
Afrika.
Mh. Huvisa ameweka wazi kuwa
taarifa hiyo imekamilika na iko tayari kwa ajili ya utekelezaji, na kuwa
taarifa hiyo imeezea Historia ya jiji la Dar es Salaam, Jiografia na
Fiziolojia yake, suala la uchumi Jamii, Sera, Sheria na Mfumo wa Utawala
Kimazingira, Usimamizi wa Rasilimali ya Ardhi, Rasilimali Maji, Madini
na Nishati, Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira, Uchafuzi wa
Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi. (Picha zote na Mo Blog)
No comments:
Post a Comment