Mchungaji Shadrack Langu (katikati), wa kanisa la KKKT Amani akiwa na baadhi ya watoto na kikundi cha VICOBA baada ya kukabidhi
KANISA
la KKKT-Dayosisi ya kati Usharika Amani Singida mjini, umetoa wito
kwa madhehebu ya dini kusaidia makundi maalumu yasiyojiweza ikiwemo
watoto wanaoishi mazingira hatarishi.
Wito
huo umetolewa na Mchungaji wa usharika huo, Shadrack Langu, wakati wa
makabidhiano ya msaada wa chakula na vitu mbalimbali kwa kituo cha
Malezi, Kititimo mjini Singida.
A u, ili kujemesema utoaji wa misaada hiyo kwa makundi yasiyojiweza, itasaidia kuijenga moyo wa upendo baina yao.
Msaada
huo wa kibinadamu uneotolewa na kikundi cha VICOBA, chini ya kanisa
hilo, kwa ajili ya kituo hicho, chenye jumla ya watoto 40.
Mchungaji
Langu amesema moja ya majukumu ya kanisa ni kuia
jamii, hususani makundi yasiyojiweza ili kuwajenga kimwili na kiroho
baadaye wamudu maisha yao.
“Kazi
ya kanisa ni kuhakikisha mwanadamu anakombolewa katika maisha
yake…ndiyo maana hata wamisionari walipokuja kwetu, walipojenga shule,
walijenga pia zahanati na hospitali ili kusaidia jamii kimwili,”alisema
mchungaji Langu.
Mapema
akimkaribisha mgeni rasmi, katibu wa VICOBA –KKKT Amani, Mwalimu Anna
Abdalah aliwaasa watoto hao kuondokana na huzuni badala yake wajione
wapo sawa na watoto wanaokula, kulala na kuishi na sehemu nzuri wakiwa
na wazazi wao.
Kwa
upande wake mwangalizi wa kituo hicho anayetumia maisha yake kuishi na
kuwahudumia watoto hao, Ali Makala alishukuru msaada huo na kuiomba
jamii kuiga mfano wa akina mama wa VICOBA kutoka usharika wa Amani
katika kusaidia kituo hicho.
Msaada
huo unaojumuisha unga wa sembe kilo 150, mchele kilo 100, mafuta ya
kula, sabuni, maharage, mafuta ya kupaka, dawa ya meno, kalamu,
daftari, juisi, biskuti, miswaki na dawa ya kuulia kunguni, una thamani
ya zaidi ya Sh. Milioni 1.1. |
No comments:
Post a Comment