HOTUBA YA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM
Ndugu wananchi wa Mkoa wa 
Dar es Salaam,
 
Tarehe
 11/12/2012 siku ya Jumanne kutakuwa na Sherehe za makabidhiano ya 
majengo ya huduma za mama na mtoto katika Hospitali za Mnazi Mmoja, 
Sinza na Rangi tatu.Makabidhiano hayo yatafanywa na Balozi wa Korea 
kusini kwa niaba ya watu wa Korea Kusini kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano
 wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Ndugu wananchi wa Mkoa wa 
Dar es Salaam,
Makabidhiano
 hayo yataanzia katika hospitali ya Mnazi Mmoja iliyopo katika Wilaya ya
 Ilala kuanzia saa 2:30 asubuhi mpaka saa 5:00 asubuhi.Baada ya hapo 
makabidhiano hayo yataelekea katika hospitali ya Sinza iliyopo katika 
Wilaya ya Kinondoni kuanzia saa 5:00 asubuhi mpaka saa 7:00 mchana na 
kuishia katika hospitali ya Rangi Tatu iliyopo katika Wilaya ya Temeke 
kuanzia saa 7:00 mchana mpaka saa 9:00 alasili.
Ndugu wananchi wa Mkoa 
wa Dar es Salaam,
Wakati
 huo huo,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho 
Kikwete atazindua na kukabidhi nyumba 36 za waathirika wa mabomu ya 
Gongo la Mboto zilizojengwa katika eneo la Msongola lililopo katika 
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.Makabidhiano hayo yatafanyika kuanzia 
saa 8:00 mchana mpaka saa 10:00 jioni.
Ndugu wananchi wa Mkoa 
wa Dar es Salaam,
Nawaomba
 mfike kwa wingi kushuhudia makabidhiano ya majengo ya huduma za mama na
 mtoto katika Hospitali za Mnazi Mmoja, Sinza na Rangi tatu pamoja na 
uzinduzi na kukabidhi nyumba 36 za waathirika wa mabomu ya Gongo la 
Mboto.
Asanteni kwa kunisikiliza.
Said Meck Sadiki
MKUU WA MKOA WA 
DAR ES SALAAM

No comments:
Post a Comment