CHEKA NA CHIMWENE KUUMANA ETHOPIA
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
DECEMBER 18,
2012
Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) tayari
imemtafutia bondia Francis Cheka mpambano wa marudiano kati yake na bondia
Chiotra Chimwemwe wa Malawi katika jiji la Addis Ababa, Ehtiopia.
Mpambano huo utafayika January 26, siku ya ufunguzi
wa mkutano wa wakuu wa nchi za Africa (AU Summit) katika jiji hilo la Wafalme
la Abesinia!
Cheka na Chimwemwe watakutana jijini Arusha Desemba 26 (Boxing Day) katika mpambano wa
kutafuta nani mbabe wa uzito wa Super Middle katika bara la Afrika, Mashariki
ya Kati na Ghuba ya Uajemi (IBF AMEPG). Katika mpambano huo mafahali hawa wawili wataumana kiume kwa raundi 12 za
dakika tatu kila mmoja!
Mpambano
wa Cheka na Chimwemwe jijini Arusha umeandaliwa na kampuni ya Screen
Hills (T) Investment ya jijini Dar-Es-Salaam inayomilikiwa na promota
maarufu aliyewahi kuwa bingwa wa taifa katika ngumi za ridhaa na kulipwa
Andrew George aka Chagga Boy!
Umaarufu wa
wawili hawa umewafanya mapromota wanaoandaa tamasha la kuchangisha pesa kwa
ajili ya kulisha watu wenye njaa katika bara la Africa kuwaingiza Cheka 26(15)-6(3)-1
na Chiotra 26(15)-4(2)-1 katika mpambano hwa marudiano utakaofanyika jijini Addis
Ababa, Ethiopia tarehe 26 Januaru 2012!
Katika tamasha hilo, pambano kuu litakuwa kati ya bondia Oliver McCall 56(37)-12(1)-0
kutoka Marekani ambaye aliwahi kuwa bingwa wa uzito wa juu duniani akipambana
na bondia Sammy Retta - 18(17)-3(2)-0 kutoka Ethiopia kugombea ubingwa wa IBF
Africa, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi (IBF AMEPG) katika uzito wa juu
(Heavyweight)
Mapambano mengine yatawakutanisha mabondia Daniel
Wanyonyi 14(12)-5(2)-2 wa Kenya atakayechuana na bondia Issac Hlatswayo 30(10)-5(3)-1
kutoka Afrika ya Kusini katika kugombea ubingwa wa IBF Afrika, Mashariki ya Kati
na Ghuba ya Uajemi (IBF AMEPG) katika uzito wa Welterweight
Naye Manzur Ali 7(4)-8(3)-0 bingwa wa uzito wa juu
kutoka nchi ya Misri atachuana vikali na bondia Harry Simon 27(20)-0-0 kutoka Namibia
ubingwa wa IBF Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi (IBF AMEPG) katika
uzito wa Light heavyweight.
Mpambano huu umeidhinishwa na Shirikisho la Ngumi la
Kimataifa (IBF) na Cheka kupewa kibali na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC).
Imetolewa na:
Onesmo A,M,
Ngowi
Rais, TPBC
Rais, IBF /Africa
No comments:
Post a Comment