AJALI HIZI ZINAMALIZA WATU : WATU 5 WA FAMILIA MOJA WAFA KWA AJALI IRINGA
Baadhi ya akina mama wasamaria wema wa Tanangozi Iringa wakijaribu kumpepelea mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo |
Ajali mbaya imetokea mkoani Iringa mchana wa leo na kusababisha vifo vya watu wanne wa familia moja pamoja na mfanyakazi wa ndani mmoja.
Ajali hiyo imetokea katika eneo la Tanangozi wilaya ya Iringa kwenye kizuizi cha barabara cha mafundi wa kutengeneza barabara kuu ya Iringa -Mafinga mkoani Iringa mida ya saa nane mchana
Kwa mujibu wa mashuda wa tukio hilo wameueleza mtandao wa www.francisgodwin.blogspot.com kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari dogo aina ya Rav 4 lenye namba za usajili T 770 BMP kulipalamia lori lenye tela kwa nyuma.
Huku
chanzo kikitajwa kuwa ni kuendesha kwa mwendo kasi wa dereva wa
gari ndogo marehemu Ezekiel Mwaiteleke na kushindwa
kulimudu na kulipalamia lori kwa nyuma.
Kwa mujibu
wa mashuda wa tukio hilo wameueleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva
wa gari dogo aina ya Rav 4 kuendesha kwa mwendo kasi na kushindwa
kulimudu na kulipalamia lori kwa nyuma na kuwa gari hiyo ilikuwa ikitokea jijini Dar es Salaam kwenda Kyela mkoani Mbeya.
Hivyo katika ajali hiyo abiria wote wanne akiwemo baba na mama wa watoto wawili waliokuwemo katika gari hiyo pamoja na watoto hao kufa papo hapo na maiti zote kupelekwa katika Hospitali ya mkoa wa Iringa.
Majina ya waliokufa ni pamoja na Ezekiel Mwaiteleke ambaye ni dereva wa gari hilo na baba wa familia hiyo ,mkewe Grace Mwaiteleke ,mtoto Kelvin Mwaiteleke (2),Happy Mwandike na mfanyakazi wao wa ndani aliyefahamika kwa jina la Linda Ezekiel huku majeruhi katika ajali hiyo ni mmoja na amekimbizwa Hospital ya mkoa wa Iringa.
No comments:
Post a Comment