UNIQE MODEL KUANZA MAZOEZI LAMADA HOTEL
Washiriki wanaowania taji la 
mwanamitindo mwenye sifa za kipekee Unique model 2012 wanatarajiwa 
kuanza mazoezi ya miondoko ya kimaonyesho alhamisi hii katika hoteli ya 
Lamada iliyopo jijini Dar. 
Jumla ya washiriki kumi na mbili wataanza mazoezi hayo kwa nia ya 
kujifua kimazoezi ya kutembea miondoko ya kimaonyesho na dansi ili 
kuukabili mchuano mkali uliopo baina ya washiriki hao.
Akiongea na mwandishi wa habari hizi mratibu wa shindano hilo Bw. 
Methuselah Magese amesema kuwa washiriki wapo katika hali ya ushindani 
sana na mwaka huu namshukuru mungu wamejitokeza wanamitindo wengi wenye 
sifa ukilinganisha na mwaka 2010 hii inaonesha kiwango cha ubora wa 
shindano kinapanda juu. 
Magese aliyataja majina ya washiriki hao ni Janecy Maluli,Judith 
Sangu,Vestina Charles,Catherine Masumbigana,Darling Godfrey,Amina 
Ayoub,Elizabeth Pertty,Lulu Mramba ,Sadory Kendra,Elizabeth Borniface na
 Zeenarth Habib,
Mwalimu wa dansi ya washiriki Denis Lucas amejiandaa vyakutosha 
kuhakikisha kuwa washiriki hao wanatoa burudani ya dansi amabayo 
haijawahi kutokea ambapo watu watapata mengi ya kukonga nyoyo zao kwa 
kiingilio cha elfu kumi na tano tu.
Mwalimu wa miondoko atakuwa mwanamitindo mwenye uzoefu na majukwaa ya 
mitindo nchini Tanzania ambae ametajwa kwa jina la Wancy Nells ambae 
amejipanga kuwanoa vema wanamitindo hao tayari kwa fainali.
Fainali za Unique model 2012 katika kumtafuta unique model of the year 
2012 zifanyika tarehe 28 mwezi huu katika ukumbi wa maraha New Maisha 
club uliopo oysterbay jijini Dar.
No comments:
Post a Comment