MASHINDANO YA WABUNGE AFRIKA MASHARIKI
Maandamano ya uzinduzI |
Kikosi cha Tanzania wakati wa uzinduzi. |
Kikosi chaTanzania kilichoidhibu vikali
Kenya.
Kikosi cha Afrika Mashariki Kikosi cha Tanzania kikiusoma mchezo kati ya Uganda
na Afrika Mashariki Muamuzi wa mchezo huo Bi Damaris Kimani
kutoka Kenya.
Tanzania yaiangamiza Kenya kwa
5-1
Tanzania Bunge Sports Club Football imefanya maajabu katika uwanja wa Nyayo
jijini Nairobi jana kwa kuwabamizwa wenyeji wao timu ya Kenya Bunge Sports Club
Football mabao 5 kwa nunge katika michezo ya mabunge ya nchi za Jumuiya ya
Afrika Mashariki yanayoendelea jijini Nairobi. Mashindano hayo yaliyofunguliwa
rasmi juzi tarehe 7 Disemba na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mh. Margreth
Natongo Zziwa akisisitiza "let the best team win" tayari
yamezikutanisha timu ya Bunge la Uganda na timu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
ambapo timu hizo zimetoka sare ya 1-1.
Wakati wa kuhitimisha karamu ya
mabao kwa timu ya Kenya, Watanzania walijikuta uwanjani peke yao wakishangilia
huku mashabiki-wenyeji wakiwa wameondoka uwanjani hapo. Leo Tanzania itapambana
na Rwanda kwenye mpira wa miguu katika uwanja wa City Stadium, na Wabunge wanawake watakutana na Kenya kwenye
mpira wa kikapu Nyayo Stadium. Mashindano haya yanalenga kuimarisha ushirikiano
na kuitangaza zaidi Jum uiya ya Afrika Mashariki.
Katika mashindano haya ambayo
hufanyika kila mwaka huyakutanisha mabunge ya nchi za Tanzania, Kenya, Uganda,
Burundi na Rwanda. Waratibu wa michezo hii ni Jumuiya pamoja na Bunge la Afrika
Mashariki. Kwa mwaka huu Burundi haikushiriki.
Chini ya ukufunzi wa Naibu Waziri
(TAMISEMI) Mhe. Kasim Majaliwa (Mb) .na uongozi wa Mhe. Idd Azzan (Mb) mabao
hayo yalifungwa na Mhe Amos Makala (Mb), Yusuf Soka (2), Mark Tanda na Mhe.
Joshua Nassari.
Na Mahmoud Ahmad aliyekuwa Nairobi
No comments:
Post a Comment