IJUE HISTORIA YA MWANAMZIKI NICK MINAJI
Kila mtu ambae
amefanikiwa kwa kupanda mwenyewe kutoka chini kwenda juu lazima
anasimulizi la maisha yake ambalo lina mabonde na milima ya kushangaza
kidogo, lakini inavuta usikivu na hisia sana pale msichana mrembo
aliyefanikiwa kuwa kati ya list ya juu duniani kimuziki akiwa na
simulizi la maisha yake linalotisha ama kuogofya tena akitishwa na yule
aliyemzaa.
Jina lake la kuzaliwa ni Onika Tanya Maraj a.k.a Nicki Minaj, first lady wa Young Money mwenye umri wa miaka 30.
Nicki
Minaj ali-experience maisha ya kusikitisha hasa katika familia yake
mwenyewe iliyomlea, lakini pia mikiki mikiki toka kwa dingi mkorofi
ilikuwa balaaa.
Baba yake mzazi alikuwa mtumiaji wa madawa ya kulevya
kupitiliza, kiasi cha kuwa Teja ajabu, lakini pia alikuwa mkorofi na
mkatili sana kitu kilichopelekea wanafamilia hao kuishi kwa uoga na
mashaka.
Ilifikia
hatua baba Nicki Minaj aliwasha moto kwenye nyumba ya familia hiyo
akijaribu kumuua mama yake Nicki Minaj, jaribio ambalo halikufanikiwa.
Lakini
Nicki Minaj mwenyewe anasema alijaribu sana kumsaidia mama yake kadri
anavyoweza na alitaka awe shupavu sana lakini mama yake hakuweza, Nicki
alijiwekea malengo ya kuwa mwenye mafanikio baada ya kufanya kazi ili
amsaidie mama yake.
“Siku
zote nilikuwa na hiki kitu cha kuwawezeshesha wanawake kwenye akili
yangu”, aliliambia jarida la Details, “kwa sababu nilitaka mama yangu
awe shupavu, na hakuweza. Niliwaza, kama ntakuwa mwenye mafanikio,
Naweza kubadili maisha yake.” Huyo ni Nicki Minaj.
Nicki
Minaj alianza kuandika mashairi akiwa na umri wa miaka 12 tu, na baada
ya kumaliza La Guardia High School, ambayo inatoa elimu ya sanaa na
Muziki aliwaza moja kwa moja kuingia kwenye biashara ya muziki. Alianzia
chini na alianza kwa kufanya back up kwa rapperz wa jiji la New York.
Muda
mfupi baadae alianza kuandika mashairi yake mwenyewe, na baadae
akakutana na Lil Wayne aliyegundua kipaji chake ni silaha ya biashara ya
muziki na kumsaini Young Money, ambapo alimsaidia kuifanya mixtape ya
“Playtime is Over”, baada ya hapo akaishika dunia na michano yake na
kuchukua tuzo kibao zenye heshima duniani, na kupata heshima pia hivi
karibuni kuwa jaji wa shindano la kuimba la American Idol wakati album
yake ya Pink Friday Roman Reloaded; Re-Up iko sokoni.
NB:" USITAKE MAFANIKIO PASIPO KUWEKEZA KATIKA JUHUDI"
No comments:
Post a Comment