POLISI WATUHUMIWA KUBAMBIKIZA WATU KESI ARUSHA
Mahmoud Ahmad Arusha
Jeshi la polisi mkoani hapa
linatuhumiwa kwa kuwabambikia kesi wanafamilia moja jijini hapa licha ya kesi
ya msingi kuwepo kwenye mahakama kuu ikiendelea.
Wakizungumza na mwandishi wa
habari hizi mmoja wanafamilia hiyoMgeni Ally Hatibu alisema kuwa wamekuwa
wakifanyashughuli zao za kujipatia riziki kwa kufuatwa na askari wa jeshi hilo
huku wakiwa teyari wamefunguliwa kesi moja mara nne ya kuvamia eneo ambalo ni
nyumba ya marehemu baba yao.
Mgeni alikwenda mbali kwa
kusema kuwa wao wanaendelea kufanyabiashara kwenye eneeo hilo ambalo ni nyumbani kwao licha ya
kuvunjiwa nyumba hiyo na mfanyabiashara wa kampuni ya Napako Enterprises
akishirikiana na jeshi la polisi mkoani hapa saa nane usiku kwa madai kuwa
aliuziwa nyumba hiyo.
Alisema kuwa teyari kumekuwa
na mlolongo mrefu wa wenye fedha kupewa kipaumbele kwenye haki yao huku wao wakiendelea
kutaabika bila msaada wa serekali na mfanyabiashara huyo kununua askari
kuwazuia kufanyashughuli za kujipaitia kipato chao cha kila siku.
Bi Mgeni alisema kuwa uonevu
wanaofanyiwa na mfanyabiashara huyo mkoani hapa bila ya serekali kuchuwa hatua
inaonekana kuwa wamenunuliwa kwa bei poa na mfanyabiashara huyo anayeshinda
kila siku kwenye kituo kikuu cha polisi jijini hapa.
Akawataka jeshi la polisi kufanyakazi
za kulinda raia na mali
zao na kuacha kutumiwa na wenye fedha kuwanyima haki zao raia wenye hali za
chini aidha alipotafutwa kamanda wa polisi mkoani hapa Liberatus Sabas
hakupatikana kwa njia ya simu kwani ilikuwa inatumika muda mrefu.
No comments:
Post a Comment