KINYANG'ANYIRO CHA UNIQ MODEL NI LEO
Ile siku 
iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na watanzania wengi kutaka kujua nani 
ataibuka mshindi wa shindano la kumsaka mwanamitindo wa mwaka mwenye 
sifa za pekee nchini Tanzania (Unique Model 2012) sasa imewadia.
Homa ya 
shindano imezidi kupanda ikiwa usiku wa leo atajulikana nani atavishwa 
taji la unique model of the year 2012 taji lenye heshima katika tasnia ya
 mitindo nchini Tanzania.
Jumla ya 
washiriki kumi na mbili wanapanda jukwaani kuwania taji hilo kwenye 
fainali zake zitakazofanyika katika ukumbi wa maraha wa New Maisha club 
uliopo Oysterbay jijini Dar usiku wa leo.
Washiriki
 wanaowania taji hilo ni Vestina Jax,Judith sangu,Amina Ayoub,Catherine 
Masumbigana,Elizabeth Pertty,Elizabeth Boniface,Vivian Gilbert ,Darline 
Mmari , Zeenath Habibb,Sandra Suleiman,Cecilia Emmanuel,Magreth Msafiri.
Mratibu 
wa shindano hili Bwana Methusela Magese amewaomba watanzania wajitokeze 
kwa wingi siku ya leo kwani kuna mambo mazuri ya kufurahisha ikiwemo 
burudani ya muziki wa bendi toka kwa mashujaa,ngoma za asili na bongo 
flava kwa kiingilio cha Tshs 15,000/= tu.
Shindano
 hili limedhaminiwa na Giraffe ocean view hotel,Kitwe general 
Traders,sophanaa investment ltd,dtv,88.4 clouds fm,Gazeti la Tanzania 
Daima,Gazeti la Kiu,mashujaa investment ltd,Michuzi blog,jiachie 
blog,Lmada Apartments & Hotel,mtaa kwa mtaa blog,Fabak 
fashins,Genessis health center na Yung don Records,Paka wear,Mtoko 
Design,Dina ismail blog na Unique Entertainment Blog. 
No comments:
Post a Comment