ZAIDI YA DOLA MILLION MOJA KUPATIKANA KUPITIA TUKIO LA 'WINGS OF KILLIMANJARO
ZAIDI ya dola milioni moja za Marekani zinatarajiwa kukusanywa
kwa ajili ya kusaidia kazi mbalimbali katika taasisi za kijamii
kupitia tukio la ‘Wings of Kilimanjaro’ linalotarajiwa kufanyika
mwanzoni mwa Mwaka ujao.
Katika taarifa iliyotolewa kwa
vyombo mbalimbali vya habari, imeeleza kuwa tukio hilo hutokea mara
moja sana litafanyika mwezi Januari, mwakani na linategemea kupata kiasi
hicho cha fedha kutoka kwa watu zaidi ya 200 watakaohudhuria tukio
hilo.
Aidha kutakuwa na michezo
mbalimbali ikiwemo ya kupaa na parachuti na mingine mingi, na kupata
fursa ya kutembea kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro. Fedha
zitakazopatikana zitasaidia taasisi za Plant With Purpose, One
Foundation na World Service International ambazo zinasaidia jamii za
kitanzania.
Meneja wa Wings of Kilimanjaro
Paula Mc Rae alisema hata Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk
Jakaya Kikwete amefurahishwa juhudi zao za kutafuta fedha kwa ajili ya
kusaidia watu wenye matatizo lakini pia kuutangaza mlima Kilimanjaro
ulimwenguni kote.
“Katika uzinduzi wa Wings of
Kilimanjaro, wataalamu wa ‘paragliding’ ikiwemo wale ambao ni maarufu
duniani na abiria wao ambapo siku hiyo watakwenda mpaka eneo la Moshi
ambapo watatua kwa kutumia muda wa dakika 40 tu” alisema.
Aidha aliongeza kuwa kati ya
watu hao baadhi yao watatoka nje ya nchi kwa ajili ya tukio hilo lakini
pia kushuhudia mlima mrefu kuliko yote barani Afrika mlima Kilimanjaro.
No comments:
Post a Comment