DAKTARI NA NESI WAFIKISHWA KORTINI KWA KUDAI RUSHWA YA SH. MILLION 1.5
Daktari na Muuguzi wa wa taasisi ya Tiba ya mifupa Muhimbili (Moi) wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,Jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka mawili kuomba Sh.million 1.5 na kupokea rushwa ya Sh. Million moja.
Washtakiwa hao ni Dkt. Deodata Matiku (30) na Erick Kimomwe (28) wakidaiwa kuomba fedha hizo kwa ajili ya kumsaidia Sandford Mhina kumfanyia upasuaji ndugu yake Fanuel Gideon aliyekuwa amelazwa hospitalini hapo.
Mashtaka hayo yalisomwa mbela ya hakimu Hellen Riwa na mwendesha mashtaka wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Allen Kasamala akisaidiana na Sophia Gulla.
Washtakiwa hao walidaiwa kutenda kutenda kosa hilo Novemba 27, mwaka huu katika Taasisi ya Mio Upanga Wilata ya Ilala,ambapo ilidaiwa waliomba pesa hizo kwa ajili ya kumfanyia upasuaji wa haraka mgonjwa wa huyo mlalamikaji ambaye alikuwa amelazwa wodi namba 8 katika jengo la sewahaji.
Hata hivyo kesi hiyo ilihairishwa hadi Desemba 24 mwaka huu itakapotajwa tena.
No comments:
Post a Comment