TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Thursday, January 30, 2014

BANDARI DAR KUPAKUA MIZIGO TANI MILIONI 18 

BBBBBBB_d1c95.jpg 
BANDARI ya Dar es Salaam kwa kupitia mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), inatarajia kupakua mizigo tani milioni 18 ifikapo mwaka 2015 kutoka tani milioni 13.5 wanayopakua sasa.
Aidha,wanatarajia kuboresha bandari ndogo za kwenye maziwa kuongeza ufanisi wa kutoa mizigo ikiwemo kuongeza ufanisi wa Usafiri wa Reli ambao kwa sasa unatoa bandarini asilimia 1.2 ya mizigo tu.
Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Awadhi Massawe alimweleza hayo Waziri Mkuu wa Finland, Jyrki Katainen alipotembelea bandari hiyo, ikiwa sehemu ya ziara yake ya siku mbili nchini iliyomalizika jana.
Massawe alikuwa akielezea mafanikio na changamoto zinazoikabili bandari hiyo na kubainisha kuwa ifikapo mwaka 2028 wanatarajia kupakua tani milioni 41.5 za mizigo.
Akizungumza bandarini hapo, Katainen alisema amefurahishwa na uamuzi wa Serikali kuipa kipaumbele uboreshaji wa bandari kupitia mpango wa BRN kwani ikiwa na uwezo wa kutoa stahili pia biashara nchini itakuwa imara.
Wakati huo huo, Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyere aliwahakikishia watumiaji wa Bandari ya Dar es Salaam kuwa ni salama katika usafirishaji, uhifadhi na udhibiti wa kemikali mbalimbali hasa zile za salfa.
Alisema tangu mwaka 2003 kumekuwa na sheria ya kudhibiti usafirishaji na uhifadhi wa kemikali nchi nzima. Katika bandari hiyo alisema upo uangalizi maalumu.
CHANZO:HABARILEO

WAZIRI NYALANDU AAGIZA WAVAMIZI KUONDOKA

nyalandu_eb397.png
Na mwandishi wetu mwananchi
Tabora. Serikali imesema haitaogopa wala kumvumilia mtu atakayevamia maeneo ya hifadhi na mapori ya akiba kwa lengo la kuhujumu maliasili.
Hali kadhalika kuendesha shughuli za kilimo na ufugaji katika maeneo hayo.
Pia, imewataka watu wote waliovamia maeneo ya hifadhi kuondoka kwa hiyari yao badala ya kusubiri kuondolewa kwa nguvu.
Hayo yalisemwa juzi na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alipokuwa akizungumza na maofisa na watumishi wa Idara ya Wanyamapori katika Kanda ya Magharibi.
Agizo hilo limetokana na taarifa za kuvamiwa kwa baadhi ya maeneo ya Hifadhi za Pori la Akiba la Ugalla na Moyowosi, ambapo baadhi ya wafugaji wameingiza mifugo huku baadhi wakijihusisha na ujangili.
Maofisa wa wanyamapori walisema wafugaji hao wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuingia na silaha kwenye hifadhi na kuwinda wanyama wakiwemo tembo na mamba.
.
Nyalandu alisema wavamizi wote wa hifadhi za taifa na mapori ya akiba wataondolewa kwa mujibu wa sheria.
''Nataka wale wote waliovamia mapori ya akiba na hifadhi za taifa waondoke kabla sheria haijachukua mkondo wake. Hakuna ruhusa ya kuingiza mifugo wala kuendesha kilimo kwenye maeneo yaliyohifadhiwa, tutachukua hatua kwa hili,'' alisema.
Pia alisema Serikali imewataka watu wote wanaomiliki silaha zinazotumika katika ujangili kuzisalimisha ili wasichukuliwe hatua.
Waziri Nyalandu wakati umefika kwa kila Mtanzania kulinda rasilimali za nchi na kwamba wanaotaka kupora rasilimali hizo watachukuliwa hatua kali za kisheria.
"Tutatumia nguvu zetu zote kuhakikisha kuwa tunalinda rasilimali zetu kwa kushirikiana na vyombo vyote vya dola nchini ili kumaliza ujangili nchini."
Alisema si ujangili wa kuua wanyama pekee unaoathiri nchi bali hata wafugajji wanaoingiza mifugo katika hifadhi na kuharibu mazingira watachukuliwa hatua.

TANZANIA YAZIDI KUNG'ARA KIMATAIFA 

Mwakyembe_accb2.jpg
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe
TANZANIA imeendelea kupata miradi mikubwa ya maendeleo ya kimataifa, ambapo sasa imeibuka kuwa mshindi kimataifa na kukubaliwa kuanzisha mradi mkubwa wa Kanda ya Kati wa Uchukuzi. Mradi huo utakaohusisha miundombinu ya reli, barabara na bandari unatarajiwa kuanza kutekelezwa wakati wowote nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, alisema mradi huo ulishinda miradi 51 ya nchi zingine za Afrika katika mkutano wa Uchumi wa Dunia (WEF) uliofanyika Januari 22 jijini Davos, Uswisi.
Kabla ya ushindi huo, mradi huo uliingia kwenye miradi 16 bora kati ya 51 ya Afrika na kushindanishwa katika mkutano huo uliohudhuriwa na nchi kubwa kiuchumi, kampuni za kimataifa na mashirika makubwa ya fedha duniani.
“Kwa kweli ilikuwa neema na furaha kubwa kwa Tanzania kupewa heshima hii, kwani miradi mingine 16 iliyowasilishwa katika mkutano huo nayo ilikuwa na sifa nzuri, lakini mradi huu wa Kanda ya Kati ambao takribani asilimia 95 ya utekelezwaji wake itanufaisha Tanzania, ulionekana bora zaidi,” alisema Dk Mwakyembe.
Kutokana na ushindi huo, Dk Mwakyembe alimwomba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, aunde Tume maalumu ya kitaifa, itakayosimamia na kushughulikia kikamilifu utekelezaji wa mradi huo, ili uwe wa mfano Afrika na duniani kote.
Sifa zilizochangia mradi huo kutangazwa mshindi kati ya miradi bora 16 ya Afrika na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Gordon Brown, ni pamoja na mikakati iliyowekwa na Serikali ya Tanzania chini ya Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) ya kuendeleza Ukanda wa Kati wa Uchukuzi.
Nyingine ni dhamira ya dhati ya Serikali ya Tanzania iliyoonekana, pamoja na mfumo iliyojiwekea katika utekelezaji wa mradi huo unaolenga kupanua bandari za Tanzania na kufungua zaidi milango ya kiuchumi kwa nchi jirani.
Alipopewa nafasi ya kuzungumza baada ya mradi huo kutangazwa kushinda katika mkutano huo, Mwakyembe alishukuru washiriki wa kila pembe ya dunia, kwa kuiamini Tanzania na kuelezea mikakati ya utekelezaji wa mradi huo ambapo hata hivyo alibainisha upungufu wa fedha uliopo.
Alisema baada ya kuelezea changamoto zilizopo katika hotuba yake, Brown alimtaarifu kuwa mwaka huu viongozi wakuu wa nchi duniani, watakutana Abuja, Nigeria, kupokea tathmini ya utekelezaji wa mradi huo ambapo pia itafanyika warsha ya maandalizi ya utekelezaji wa mradi mwanzoni mwa Aprili nchini.
“Tuna mpango wa kumwomba Rais Jakaya Kikwete awe mgeni rasmi katika ufunguzi wa warsha hii, ili tuuthibitishie ulimwengu utayari wa Tanzania kuleta mapinduzi katika sekta ya uchukuzi,” alisisitiza Dk Mwakyembe.
Aidha, alisema kupitia warsha hiyo, Tanzania imejipanga kuionesha dunia kuwa na mipango mizuri na ndiyo maana akaombwa Waziri Mkuu aunde Tume itakayofanya kazi kwa saa 24 kusimamia utekelezaji wa mradi huo.
Alisema alipendekeza tume hiyo ya watu wanane ihusishe wataalamu kutoka wizara za Uchukuzi, Ujenzi, Fedha, Shirika la Reli Tanzania (TRL) na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Mradi huo kwa Tanzania utagusa Bandari ya Dar es Salaam, maeneo ya Mashariki, Magharibi na Kaskazini mwa nchi na utahusisha nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Rwanda na Burundi.
Miradi mingine Mradi huo mkubwa ni kielelezo kingine cha heshima ya Tanzania kimataifa, ambapo mwaka jana wakati wa ziara ya Rais wa Marekani nchini, Barrack Obama, nchi ilipata heshima nyingine ya kutekeleza mradi mkubwa wa umeme unaojulikana kama ‘Power Africa’, utakaoinufaisha nchi na kuwa kitovu cha uzalishaji wa nishati hiyo.
Katika mradi huo unaowezeshwa na Marekani kwa kushirikisha Serikali na sekta binafsi, una lengo la kuiwezesha nchi kuongeza kiwango cha uzalishaji sambamba na kupata umeme wa uhakika, utakoongeza ajira. Serikali ya Marekani ilitoa dola bilioni 7 kusaidia kupatikana megawati 10,000 za nishati hiyo, huku sekta binafsi ikitoa dola bilioni 9.
Moja ya kampuni kubwa zinazohusika na mpango huo ni General Electric (GE), ambayo imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha mradi unaendelea kwa kuahidi kutoa megawati 5,000 kwa gharama za kawaida kwa Tanzania na Ghana.
CHANZO:HABARILEO

MTOTO WA WAYNE ROONEY NDANI YA JEZI YA FC BARCELONA 

roo1 ec0b3
Kay Rooney akiwa na mama yake Coleen ndani ya 'uzi' wa Fc Barcelona (HM)

POLISI, WANANCHI WAPAMBANA KARATU

vurugu41 9561b
Mamia ya wananchi wenye hasira katika Kijiji cha Bashay kilichoko wilayani hapa wamepambana na polisi kwa kuwarushia mawe kwa kile walichodai kuishinikiza Serikali kuweka matuta katika Barabara ya Karatu hadi Ngorongoro. (HM)
Tukio hilo lililotokea saa 4 asubuhi baada ya watoto wawili Priska John(5) na Happiness Filbert (5) walipogongwa na gari wakati wakivuka barabara ambapo mmoja alifariki dunia papo hapo huku Priska akikimbizwa hospitali.
Wananchi hao walifikia uamuzi huo wa kufunga barabara na kuzuia magari yakiwamo ya watalii kwa nia ya washinikiza mkuu wa wilaya kwenda kuwasikiliza na ndipo polisi walipojaribu kuondoa mawe hayo bila mafanikio.
"Tumechoka kuwaona polisi wakiokota maiti za watoto wetu barabarani kama wanaokota mizoga ya mbwa na leo(jana) tunawapiga mawe mpaka wakitumwa tena kuja kuchukua maiti ya aliyegongwa na gari wakatae,"alisikika mama mmoja akipaza sauti kwa uchungu.
Vurugu kati ya wananchi na polisi zilianza huku wananchi wakiporomosha mawe pasipo kujali wanarushia polisi au magari yaliyokuwa
yakipita huku polisi walipambana kwa kurusha mabomu ya machozi kwa takribani saa mbili.
Hata hivyo katika vurugu hizo hakuna aliyeripotiwa kuumia huku wananchi wakiitupia lawama Serikali kwa kushindwa kuweka matuta katika barabara hiyo ambapo mara kwa mara ajali zimekuwa zikiripotiwa kutokea katika Barabara ya Karatu hadi Ngorongoro.
Akizungumzia tukio hilo Mtendaji wa Kijiji cha Bashay, Joseph Surumbu alikiri kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema, ajali katika eneo hilo zimekuwa zikitokea mara kwa mara huku akiitupia lawama Seriklai kwa kushindwa kuweka matuta katika eneo hilo.
Hili ni tukio la pili kutokea kwa kipindi cha miezi mitatu kwa wananchi kupambana na polisi baada ya watoto kugongwa wakishinikiza barababa hiyo kuwekwa matuta.
Daktari kiongozi wa Hospitali Teule ya Wilaya, Daniel Simpa alithibitisha kuupokea mwili wa mtoto Happiness Filbert huku mwenzie akiwa amejeruhiwa na anaendelea na matibabu. Chanzo: mwananchi

'Wapinzani' wabomolewa nyumba Syria

Wapinzani_a3d8a.jpg
Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limeishutumu serikali ya Syria kwa kubomoa maelfu ya nyumba za watu kama njia ya kuwapa adhabu wananchi wanaoshukiwa kuwaunga mkono waasi dhidi ya Rais Assad.
Shirika hilo limetoa picha za Satelite kama ushahidi wa kuthibitisha madai yao.
Ripoti hiyo ilisema kuwa ushahidi wa picha,video na picha za satelite, pamoja na ushahidi kutoka kwa waathiriwa,umeonyesha kuwa serikali ya Syria, iliharibu kwa maksudi nyumba za watu kinyume na sheria za vita.
Imesemekana hakuna sababu iliyotolewa na jeshi ya kubomolewa kwa nyumba hizo kwani washukiwa wangeadhibiwa tu ikiwa kuna makosa yoyote waliyafanya.
Picha za satellite zilionyesha uharibifu mkubwa wa nyumba na makazi ya watu viungani mwa mji wa Damascus na nyingine katika mji wa Hama ambako inaaminiwa kijiji kizima kiliharibiwa.
Shirika la Human Rights Watch limesema kuwa uharibifu ulifanyika bila onyo lolote wala malipo kwa wathiriwa na kuwa maelfu ya familia zimeachwa bila makao. chanzo BBC 
Kadhalika shirika hilo lilipuuzilia mbali taarifa kutoka kwa maafisa wa serikali kuwa nyumba zilibomolewa kwa sababu ya mipangilio mipya ya mji au kwa sababu zilijengwa kinyume na sheria.
Shirika hilo limetoa wito kwa baraza la usalama la umoja wa mataifa kuishitaki Syria kwa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita wito ambao umeungwa mkono na upinzani nchini Syria.
Hata hivyo hilo huenda lisifanyike kwani kutahitajika kuwepo makubaliano ya pamoja katika baraza hilo, jambao ambalo huenda lisiwezekane kwani Urusi na China zimekuwa zikiunga mkono Syria.

AU KUZUNGUMZIA MIGOGORO AFRIKA

AU_799a9.jpg
Viongozi wa Afrika wameanza mkutano wao katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa ambapo agenda yao kuu itakuwa swala la mizozo katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na Sudan Kusini.
Akifungua mkutano huo Mwenyekiti wa tume ya Umoja huo Nkosazana-Dlamini Zuma amewaambia viongozi 54 ambao ni wanachama wa Muungano wa Afrika, kwamba wanapaswa kushirikiana ili kuleta suluhu ya kudumu kwa migogoro Afrika.
Jamhuri ya Afrika ya kati imekumbwa na mgogoro wa kisisa kwa miezi kumi sasa tangu waasi kuipindua serikali.
Katika taifa jirani ya Sudan Kusini, makundi hasimu yalitia saini ya mapatano juma lililopita baada ya mapigano makali yaliyodumu mwezi mmoja, lakini mapigano yangali yanatokota kati ya serikali na waasi.
Maelfu ya watu wameuwawa katika mzozo huo.
Mkutano huo pia utaangazia,tatizo la uhaba wa chakula na kilimo katika bara hilo. Licha ya uchumi kukuwa katika sehemu nyingi za Afrika,eneo la Sahel na upembe wa Afrika ni maeneo ambayo hukumbwa na tatizo la uhaba wa chakula mara kwa mara.
Muungano wa Afrika umekosolewa kwa kujikokota katika kuchukua hatua kukabiliana na migogoro ya kisiasa Afrika ya Kati na Sudan Kusini.
Muungano huo umemteua Rais wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz kama mwenyekiti wake mpya.
Generali Abdel Aziz aliingia mamlakani nchini Mauritania mwaka 2009, baada ya kuongoza matukio mawili ya mapinduzi katika kipindi cha miaka minne. CHANZO BBC SWAHILI

Chadema kususia Bunge la Katiba ikiwa

 

Wakati Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akisema wabunge wa chama chake watasusia vikao vya Bunge Maalumu la Katiba ikiwa hoja ya kuundwa kwa Serikali tatu itapingwa na wabunge wa CCM, Mwakilishi wa Mji Mkongwe (CUF), Ismail Jussa Ladhu ametaka kuvunjwa kwa Muungano.
Akihutubia kwenye Uwanja wa Tubuyu nje kidogo ya Mji wa Morogoro juzi, Mbowe alisema wabunge wa chama chake wataandamana nchi nzima kufikisha ujumbe kwa wananchi kwamba maoni yao yamepingwa na wabunge wa CCM walio wengi.
"Tutawaeleza wananchi kwamba maoni ya CCM ndiyo yameonekana ya maana kuliko ya wananchi ambao ni wengi zaidi," alisema Mbowe kwenye mkutano huo ambao ni sehemu ya Operesheni ya Vuguvugu la Mabadiliko - M4C Pamoja Daima.
Alisema Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilikusanya maoni na kubaini kuwa asilimia 62 ya Watanzania wanataka Serikali tatu za Tanganyika, Zanzibar na ya Muungano.
"Serikali ya CCM haitaki kusikia maneno Serikali tatu wanasema sera yao ni ya Serikali mbili, wanafanya kila hila ili kuikataa hoja hiyo. Natangaza kwamba wakifanya hivyo tutasusia na kwenda kuwashtaki kwa wananchi," alisema Mbowe.
Aliongeza kwamba wataandamana kuanzia Kagera hadi Mtwara kuwaeleza wananchi kwamba hoja yao imepingwa na CCM.
Mbowe alisema baadhi ya viongozi wa CCM wamekuwa wakitoa kashfa dhidi ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kwamba amechukua maoni ya Chadema.
"Wanakosea hayo si maoni ya Chadema, bali ni maoni ya wananchi, Warioba amezingatia maoni ya wananchi," alisema.
Mwenyekiti huyo alisema Katiba inayotafutwa si ya chama, bali ni ya Watanzania na kwamba inashangaza CCM kuipinga hoja Serikali tatu.
"Tunafahamu wanaogopa kuikubali hoja ya Serikali tatu kwa sababu wanafahamu huo ndiyo utakuwa mwisho wao wa kuwa madarakani," alisema Mbowe huku akishangiliwa na wafuasi wa chama hicho.
Alisema CCM wanaelewa kwamba kukiwa na Serikali tatu, Chadema kitashinda Tanganyika na CUF Zanzibar katika uchaguzi wowote utakaoitishwa.
"Kwa hiyo hivi sasa wana wasiwasi kweli, wanatafuta kila njia ya kuichakachua hoja ya Serikali tatu lakini wafahamu kuwa Chadema wanaifuatilia hoja hiyo kwa ukaribu," alisema.
Aliwataka wananchi kufuatilia Bunge Maalumu la Katiba litakapoanza mwezi ujao ili kuangalia wabunge wao wanavyowawalisha katika suala hilo muhimu.
Hata hivyo, Mbowe alisema chama hicho kikishinda katika uchaguzi wa mwaka 2015 hakitahangaika kulipa kisasi kwa kuwachukulia hatua za kisheria viongozi, bali kitajikita kutafuta maendeleo.
"Wasituogope tutasamehe kama alivyosamehe aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela. Hatutalipa kisasi tukiingia Ikulu, kwa sababu hakuna binadamu asiye na makosa. Tutaelekeza nguvu zetu kuwaletea maendeleo Watanzania," alisema Mbowe.
Jussa na Muungano
Akihutubia mkutano wa kampeni katika Jimbo la Kiembesamaki jana, Jussa alisema hakutakuwa na maendeleo yatakayofikiwa Zanzibar ikiwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hautang'oka.
Jussa ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa la CUF, alisema Zanzibar yenye watu milioni 1.5 haiwezi kuwa na tatizo la watu kukosa ajira lakini sera na mipango ya kiuchumi imekuwa ikikwama katika utekelezaji wake kutokana na kukosa mamlaka kamili.
Alisema Zanzibar haiwezi kukopa katika taasisi za kimataifa bila ya kuwekewa dhamana na Waziri wa Fedha wa Muungano wakati Zanzibar ni nchi na kuwataka wananchi kutumia kura zao katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 kuleta mabadiliko ya kiutawala.
"Hakuna sababu ya vijana Zanzibar kukosa ajira, kuna watu wasiozidi milioni 1.5, Muungano umefika wakati ung'oke, ndiyo kikwazo cha maendeleo ya Zanzibar na watu wake kiuchumi na kisiasa," alisema Jussa.
Alisema mradi wowote unaobuniwa Zanzibar hauwezi kupata mfadhili bila kuwekewa dhamana na Serikali ya Muungano na kukwama kwa juhudi zote za kujiunga na jumuiya za kimataifa akitolea mfano Jumuiya ya Kimataifa ya Kiislamu (OIC).
Alisema Rais wa Zanzibar amepoteza mambo muhimu chini ya mfumo wa Muungano ikiwa ni pamoja na kutopigiwa mizinga 21 akiwa nje ya nchi, kupeperusha bendera ya Zanzibar, kutokagua gwaride na kupigiwa wimbo wa Taifa la Zanzibar.
"Haya ya sasa si mamlaka kamili, wapi Dk Shein alikokwenda akapigiwa mizinga 21 au alipeperushwa wapi bendera ya Zanzibar wakati wa safari zake za nje?" alihoji Jussa.

Muhongo: Hatudanganyiki tena na wawekezaji madini 

Madini1 d6791
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospiter Muhongo, amejigamba kuwa Tanzania haitadanganyika tena kwa wawekezaji wa sekta ya madini kutolipa kodi na kuifanya nchi kutofaidika na rasilimali zake. (HM)
Alisema hayo baada ya Serikali za Tanzania na Finland, kutiliana saini, makubaliano katika kutafiti na kukuza sekta ya madini.
"Kama ni kutuibia walifanya hivyo siku za nyuma, lakini kwa sasa hawawezi tena," alijigamba Profesa Muhongo akidai historia inaonyesha kuwa nchi zote zenye rasilimali za madini, mwanzoni zilidanganyika.
Alikiri kuwa awali wawekezaji katika migodi walikuwa wakijitetea kuwa walikuwa wanapata hasara lakini kwa sasa, sheria inawalazimisha kulipa asilimia 30.
Kauli ya Profesa Muhongo ilitokana na waandishi kumbana, kuhusu Watanzania kutonufaika na sekta ya madini wakati ina faida kubwa.
Profesa Muhongo alisema kwa sasa sekta ya madini inachangia asilimia 3.5 ya pato la Taifa.
Alisema malengo ni kuhakikisha kuwa sekta ya madini inachangia zaidi ya asilimia 10 ifikapo mwaka 2025.
Mapema, wakurugenzi wa sekta ya madini katika Serikali za Tanzania na Finland, walitiliana saini ya kukuza na kuendeleza sekta ya madini hapa nchini.
Akizungumzia makubaliano hayo, Profesa Muhongo alisema yanazingatia mambo matatu, ambayo ni pamoja na utafiti wa madini katika mikoa ya kusini.
Alisema kimsingi tayari wamegundua kuwa ukanda huo una makaa ya mawe, shaba, niko na platiniamu.
Alisema watakachokifanya ni kuainisha maeneo yenye madini na viwango halisi ili wakipatikana wawekezaji wa kuyachimba, waingie kwenye makubaliano ya uhakika. Chanzo: Mwananchi

Tuesday, January 28, 2014

ITF YAIBEBA TENISI YA TANZANIA

tenis1 e6a77
Shirikisho la Tenisi la Kimataifa (ITF) limetoa nafasi moja ya upendeleo kwa mchezaji wa Tanzania kushiriki kwenye mashindano ya Tenisi ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 18 yaliyopangwa kufanyika mapema Machi katika nchi mbili tofauti. (HM)
Awali Tanzania ilipitisha wachezaji wanne waliofuzu kushiriki kwenye mashindano hayo ambayo yatafanyika jijini Nairobi, Kenya kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 16 na Cassablanca, Morocco kwa wachezaji chini ya miaka 18.
Kwa mujibu wa kocha wa timu ya taifa ya vijana, Kiango Kipingu, chama cha Tenisi Tanzania (TTA) kimepewa nafasi nyingine moja kwenye michuano hiyo ambayo ITF imesema itachagua yenyewe mchezaji huyo ambaye itamghariamia kwa kila kitu.
"Kutokana na motisha hiyo ya ITF sasa Tanzania itawakilishwa na wachezaji watano ambao wanne kati yao walifikia viwango vya kushiriki mashindano ya Afrika baada ya kufanya vizuri kwenye yale ya Afrika Mashariki na kati hivi karibuni jijini Dar es Salaam," alisema Kipingu.
Alisema wachezaji waliofikia viwango, watatu wako Nairobi ambako huko wameweka kambi na watashiriki kwenye mashindano ya dunia ya vijana chini ya miaka 18 yanayoendelea kwa wiki tatu jijini humo ambayo yatakuwa sehemu ya maandalizi yao.
"Tumaini Mishuko, Emmanuel Malya na Omary Sule wako Nairobi ambapo baada ya mashindano ya dunia watakwenda Morocco kule watashiriki mashindano mengine ambayo yatakuwa sehemu ya maandalizi yao," alisema.
Kiango alisema, Georgina Kaindoa ambaye pia amefuzu anaendelea na mazoezi nchini Afrika Kusini kujiandaa na mashindano hayo ya Afrika na kuongeza kuwa wanategemea kuwagawa wachezaji hao baadhi kushiriki mashindano ya Cassablanca na wengine yale ya Nairobi. Chanzo: Mwananachi

KUELEKEA KOMBE LA DUNIA BRAZUCA 2014 

4281191 baaf8
Michuano ya kombe la dunia inataraji kuanza Juni hadi Julai, mwaka huu katika nchini ya Brazil. Michuano hiyo itakuwa ikichezwa kwa mara ya pili nchini humo huku mara ya mwisho ikichezwa miaka 64 wakati Uruguay ilipotwaa ubingwa wake wa pili na wa mwisho mbele ya Brazil kwa kuwafunga mabao 2-1 katika uwanja wa Maraccana mbele ya mashabiki wanaokadiliwa kufikia 200, 000. (HM)
Idadi kubwa zaidi ya watazamaji katika historia ya soka. Mabingwa mara tano Brazil ndiyo wenyeji wa michuano ya sasa. Miji 12 itaandaa michuano hiyo. Kuanzia wiki hii tutakuwa tukiwaletea orodha ya makundi, uchambuzi na matukio muhimu yaliyowahi kujitokeza katika michuano hiyo. Leo tutazame viwanja ambavyo vitazipokea timu 32 ambazo zitakuwa zikiwania taji hilo.
ARENA DE SAO PAULO
Mechi sita zitachezwa katika uwanja huu uliopo mjini, Sao Paulo.
Umepewa nafasi ya kuchezwa kwa mechi ya ufunguzi itakayo husisha
wenyeji wa michuano, Brazil dhidi ya Croatia, Juni 12. Ni uwanja mpya
kabisa na utafunguliwa rasmi mapema mwaka huu. Unauwezo wa kuchukua watazamaji wapatao 65, 867. Mechi nne za hatua ya makundi zitapigwa katika uwanja huu, na nyingine mbili katika hatua za mtoano.
ARENA DA BAIXADA
Ni uwanja unaoweza kuchukua watazamaji wapatao 41, 456. Upo katika mji wa Curitiba, na ulifunguliwa rasmi mwaka 1914. Mechi ya kwanza katika uwanja huu itakuwa ile kati ya Iran na Nigeria, Juni 16. Ni mechi nne
tu zitachezwa katika uwanja huu, na zote zikiwa za hatua ya makundi.
MARACANA- RIO DI JANEIRO
Wenyeji Brazil wanakumbukumbu mbaya na uwanja huu, walipoteza kwa mabao 2-1 mbele ya Uruguay katika fainali ya mwaka 1950. Fainali ambayo ilishuhudiwa na watu wapatao 200, 000, idadi kubwa zaidi ya watazamaji katika historia ya soka. Kwa sasa, Maracana umepunguzwa ukubwa na kufikia kuchukua idadi ya watazamaji 76, 804. Mechi ya kwanza katika uwanja huu itakuwa ni ile kati ya Argentina na Bosnia, na unatarajia kutumika katika michezo saba.
ESATADIO MINEIRAO- BELO HORIZONTE
Uwanja huu una uwezo wa kuchukua watazamaji wapatao, 62, 547. Ulijengwa mwaka 1965, mechi ya Colombia na Ugiriki, itakuwa ya kwanza kupigwa hapa. Mechi sita zitachezwa katika uwanja huu, nne za hatua ya makundi na mbili za hatua ya mtoano.
ESTADIO NACIONAL DE BRASILIA- BRASILIA
Uwanja huu ulifunguliwa rasmi mwaka 2012, una uwezo wa kukusanya watazamaji 66,000. Mechi ya kwanza kuchezwa katika uwanja huu ni ile ya Uswisi na Ecuador pia uwanja huu utatumika katika michezo saba sawa na ule wa Maracana.
ARENA FONTE NOVA- SALVADOR
Mechi kati ya Hispania na Uholanzi itachezwa katika uwanja huu, juni 13. Ni uwanja uliofungiliwa mwaka 1951 na una uwezo wa kuchukua watazamaji wapatao, 48, 747. Utatumika kwa michezo sita.
ARENA PERNAMBUCANO- RECIFE
Unatarajiwa kufunguliwa mapema mwaka huu, ukiwa na uwezo wa kuchukua watazamaji wapatao 44, 248, Ivory Coast na Japan zinataraji kuamana hapa, juni 14. Utachezewa kwa michezo mitano, minne ya hatua ya makundi na mmoja wa hatua ya mtoano.
ESTADIO BEIRA RIO- PORTO ALEGRE
Una uwezo wa kuchukua watazamaji wapatao 48, 849 na ulifunguliwa mwaka 1969. Mechi tano zitachezwa katika uwanja huu, nne za hatua ya makundi na moja ya mtoano.
Viwanja vingine ni Estadio Das Dunas, uliopo katika mji wa Natal. Uwanja huu unachukua watazamaji 42, 086, na mechi nne za hatua ya makundi zitachezwa katika uwanja huo. Pia upo Arena da Amazonia, uliopo katika mji wa Manaus. Chanzo: Baraka Mbolembole/shaffihdauda

DENI LA TAIFA LINAPAA,SERIKALINI NI MATANUZI

bot1 52cbf
Hivi karibuni The Citizen liliandika habari ya kushtua katika ukurasa wa mbele, likielezea wasiwasi wa wataalamu na mabingwa kadhaa wa masuala ya uchumi kuwa, Tanzania inakabiliwa na janga kubwa la mzigo wa madeni iwapo Serikali haitapunguza kasi ya mikopo isiyokuwa na tija katika kuinua uchumi. (HM)
Onyo la wataalamu hao linatukumbusha jinsi janga la Deni la Taifa lilivyoligharimu Taifa kiuchumi katika miaka ya 90, ambapo karibu rasilimali zote ambazo Serikali ingezitumia katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na pia kuziwekeza katika huduma muhimu za kijamii zilielekezwa katika kulipa madeni. Ni aibu na ukweli ulio mchungu kwamba ilipofika mwaka 2006, Deni la Taifa lilikuwa asilimia 70 ya Pato la Taifa, ingawa msamaha wa madeni ulipunguza kiwango hicho hadi asilimia 21 mwaka uliofuata.
Hata hivyo, kilichoendelea baada ya pale ni uthibitisho kwamba Serikali haikupata fundisho kutokana na janga hilo, kwani ilizidisha kasi ya kukopa kiasi kwamba
Deni la Taifa hivi sasa linakadiriwa kuwa kati ya asilimia 40 na 50 ya Pato la Taifa, ambalo linakadiriwa kuwa Sh50 trilioni. Ni vigumu kuamini kwamba Deni la Taifa limekua kwa kasi ya kutisha kutoka Sh10 trilioni mwaka 2005 hadi Sh27 trilioni mwishoni mwa mwaka uliopita.
Kama baadhi ya wataalamu wa masuala ya uchumi wanavyohadharisha, suala hapa siyo Serikali kukopa, bali ni kwamba mikopo hiyo inayokadiriwa kuwa Sh2 trilioni kila mwaka inachukuliwa kufanya kitu gani? Takwimu za Benki Kuu ya Tanzania (BoT), zinaonyesha kwamba Deni la Taifa lilipaa kwa Tsh5 trilioni kati ya Januari na Oktoba mwaka uliopita.
Mtaalamu mmoja wa uchumi ametukumbusha jinsi miaka ya 70 Serikali ilivyokopa Sh96 bilioni kuanzisha Kiwanda cha Viatu Morogoro, lengo likiwa kuuza viatu nchini Italia. Kutokana na kufilisika kilibinafsishwa miaka ya 90 na hivi sasa majengo yake yamegeuzwa kuwa ghala, huku deni la uanzishwaji wa kiwanda hicho likiwa limelipwa kupitia kodi za wananchi. Mfano mwingine ni bajeti ya Sh122.4 bilioni ya kusambaza pembejeo za ruzuku kwa wakulima kwa mwaka 2011/12, ambapo Tsh89 bilioni zilikuwa ni mkopo kutoka Benki ya Dunia.
Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imefichua uvundo na ufisadi mkubwa katika mfumo mzima wa pembejeo za ruzuku. Kwa hiyo, Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) inakutana leo kupokea na kujadili ripoti hiyo. Kwa mfano, katika Kijiji cha Lunyala
, wilayani Nkasi, mkoani Rukwa asilimia 70 ya wananchi walioorodheshwa kupata mbolea walikuwa bandia, huku Benki ya Dunia ikikaririwa ikisema asilimia 60 ya Bajeti ya pembejeo za ruzuku ililiwa na mafisadi.
Kinachosikitisha ni kwamba Deni la Taifa litalipwa na wananchi wote ingawa waliofaidika nalo ni mafisadi na viongozi wachache walio serikalini na mashirika ya umma. Lakini kinachosikitisha zaidi ni tabia ya Serikali kuendelea kukopa kwa lengo la kuendeleza matanuzi na matumizi makubwa yasiyo ya lazima.
Mfano mzuri ni ziara fupi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda mkoani Mtwara mwishoni mwa wiki, ambapo aliongozana na ujumbe mkubwa kupita kiasi na magari ya kifahari ya Serikali yasiyopungua 30. Sisi tunadhani unahitajika mjadala mpana wa kitaifa kuhusu Deni la Taifa.Chanzo: mwananachi

Thursday, January 23, 2014

RAISI CATHERINE SAMBA-PANZI AAPISHWA

RAISI_ed66a.jpg
Mashahidi wanaripoti uporaji mkubwa wa mali katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, huku kaimu rais mpya akianza rasmi kazi yake.
Mwandishi wa VOA Nick Long amabye yuko mjini Bangui, ameiambia Sauti ya Amerika kuwa maelfu ya watu walipora mali katika eneo linalojulikana kama PK13 lenye wakazi wengi Waislam.
Anasema majeshi ya Rwanda yaliwafukuza waporaji, lakini uporaji ukaanza tena baada ya walinda amani hao wa Rwanda kuondoka, kulinda sherehe za kuapishwa kwa kaimu rais mpya.
Rais huyo mpya wa muda Catherine Samba-Panza, ametoa mwito wa utulivu wiki hii kabla ya sherehe za kuapishwa kwake, ambako kumefanyika katika majengo ya bunge leo Alhamis
Chanzo, voaswahili.com (R.M).

UMOJA WA AFRIKA MASHARIKI KUIMARISHWA TENA

 eac_cbf2c.jpg

Bunge la Afrika Mashariki limeanza vikao vyake vya nne nchini Uganda na kuanza kwa kuzitolea mwito nchi zote wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki kutia bidii kwenye mchakato wa kuhakikisha kuwa wanaijenga na kuiboresha jumuiya. Bunge la Afrika mashariki linafanya vikao vyake vya wiki moja nchini Uganda.
Phillis Kandie Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri amesema kuwa mazungumzo ya kujadili upya muundo wa muungano wa kisiasa wa Afrika Mashariki na mpango wa utekelezaji utazingatiwa mwezi wa April mwaka huu.
Miongoni mwa mambo ambayo muungano wa jumuiya ya Afrika mashariki unaweza kujivunia ni pamoja na kuweko na forodha moja ambayo ilitekelezwa tarehe moja mwezi huu. Pia, jumuiya iliweza kutia saini itifaki ya kuanzisha sarafu moja ya jumuiya. (M.M).

Phillis Kandie Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri na ambaye pia ni waziri wa Mambo ya Afrika Mashariki nchini Kenya ametoa mwito kwa wabunge wazishinikize serikali zao zihakikishe kuhakikisha kuwa kutekelezwa kwa itifaki ya sarafu moja kunaanza tarehe moja mwezi wa Julai mwaka huu kama viongozi wa jumuiya walivyokubaliana walipokutana mara ya mwisho mwezi wa novemba mwaka uliopita.
Wakati huo huo Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Margaret Zziwa katika mkutano ya wanahabari alitangaza kwamba wataituma timu ya ukaguzi Sudan Kusini kukagua kama nchi hiyo iko tayari kujiungana jumuiya. Hii ni baada ya Sudan Kusini kuwasilisha rasmi ombi lao la kutaka kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Timu hii itakuwa ikiangalia kama Sudan Kusini inatimiza misingi bora ya utawala kama vile demokrasia, utawala wa sheria, utunzaji wa haki za binadamu na haki za kijamii.
Waziri wa Mambo ya Afrika Mashariki kutoka Kenya Bi Kandie amewatakia heri raia wa Sudan Kusini na akasema kama majirani hawatawetekeleza haswa wakati huu wanapohitaji usaidizi.
Chanzo, voaswahili.com

SERIKALI YA SUDANI KUSINI NA WAASI WATIA SAINI MAKUBALIANO

SUNA_fe485.jpg
Serikali ya Sudan Kusini na upinzani wametia saini mikataba miwili alhamisi katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa. Mkataba wa kwanza ni sitisho la haraka la hatua za kijeshi na wa pili unahusu kuachiliwa kwa wafungwa 11 wa kisiasa ambao wametiwa ndani tangu kuanza kwa mzozo katikati ya mwezi Disemba mwaka uliopita.
Mazungumzo ya amani yameongozwa na taasisi ya kieneo IGAD na yalianza mapema mwezi uliopita. Mpatanishi mkuu wa IGAD, Seyoum Mesfin anasema hatua kadhaa zinahitaji kuchukuliwa na pande zote kwa vile hivi sasa wametia saini mikataba miwili.(M.M).

Bwana Seyoum anasema moja ni kutekeleza mikataba ambayo wametia saini kwa nia nzuri na ya dhati. Pili, kuanza kufanya kazi za ukarabati na kuwasaidia maelfu ya watu waliokoseshwa makazi ndani ya nchi na wakimbizi. Tatu, lazima tuendelee haraka na majadiliano ya kisiasa na kufanya kazi kuelekea katika maridhiano ya kitaifa.
Mkataba wa sitisho la mapigano unayataka majeshi ya serikali na upinzani kubakia walipo. Wanajeshi wa Uganda ambao wanaisaidia serikali ya Sudan Kusini itawalazimu waache operesheni zote katika muda wa saa 24.
Mkataba unaozungumzia wafungwa 11 haujaelezea wataachiliwa lini.Hakuna maneno ya kirafiki yaliyozungumzwa kati ya serikali ya Sudan Kusini na upinzani wakati wa sherehe za utiaji saini.
Chanzo, voa.swahili.com

UPINZANI UKRAINE, WATOA ONYO KWA SERIKALI 

llllllll_51c99.jpg
Waandamanaji wakipambana na polisi mjini Kiev(MM)
Vifo hivyo ni vya kwanza tangu kuzuka kwa maandamano ya kuipinga serikali miezi miwili iliyopita. Waandamanaji na polisi nchini Ukraine wamepambana tena mapema leo (23.01.2014), baada ya ghasia kuzuka hapo jana Jumatano na kuigeuza sehemu ya katikati ya mji mkuu, Kiev kuwa uwanja wa vita, huku polisi wakitumia mabomu ya kutoa machozi na risasi za mpira dhidi ya waandamanaji waliokuwa wakirusha mawe.
Vifo hivyo vimezusha hofu mpya baada ya miezi miwili ya maandamano ya kuipinga serikali yaliyochochewa na hatua ya serikali kutosaini makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara na Umoja wa Ulaya, kutokana na shinikizo la Urusi.CHANZO DWSWAHILI

MKUTANO KUHUSU MZOZO WA SYRIA WAANZA USWIZI.

BAN_KI_MOON_4cc14.jpg
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ameziambia pande mbili zinazozozana nchini Syria kuwa wakati umefika kwao kufanya mashauriano ya kusitisha mzozo unaokumba taifa hilo.
Akizungumza siku moja baada ya siku ya kwanza ya mkutano wa amani unaofanyika nchini Uswisi, Bwana Ban amesema kuwa lazima raia wa Syria waungane ili kuokoa taifa lao na kuwalinda watoto. (R.M).

Awali, wajumbe wa Seriklai na wale wa Baraza la Upinzani walikutana ana kwa ana kwa mara ya kwanza, tangu mzozo huo uanze miaka mitatu iliyopita.
Wajumbe hao walishutumiana, kuashiria mgawanyiko mkali kuhusu ikiwa rais Bashar al Assad, anapaswa kuwa na juku katika serikali ya mpito.
Mabalozi wa mataifa ya magharibi wamesema kuwa uhasama huo unaweza kuhujumu, mazungumzo rasmi yatakayoanza siku ya Ijumaa.
Mjumbe wa wa Umoja wa Mataifa nchini Syria, Lakhdar Brahimi, amesema atashauriana na pande hizo mbili baadaye hii leo ili kujadili jinsi mazungumzo hayo yatakavyoendelea.
Balozi wa Syria, katika Umoja wa Mataifa Bashar Ja'afari amelalamika kuwa kumekuwa na mapungufu katika mazungumzo hayo kwa sababu ya kutokuwepo kwa Iran, nchi inayowaunga mkono kwa sababu wajumbe wengine wanaohdhuria mkutano huo ni wapinzani wa serikali.
Chanzo, bbc swahili.com

REAL MADRID YATAKA KUMSAJILI ROONEY 

ROONEY NA RONALDO1 d5d81
Taarifa kutoka jijini Madrid zinasema mshambuliaji Wayne Rooney ameingia kwenye orodha ya washambuliaji wanaowataka mwishoni mwa msimu. (HM)

Huku mkataba wa Rooney ukiwa umebaki miezi 18 na inavyoelekea hana nia ya kuongeza mkataba mpya pia klabu ya Manchester Utd haipo tayari kumuuza Rooney kwa vilabu vya England.

Kwenye orodha ya majina ya washambuliaji wanaotakiwa na Real Madrid ukiacha jina la Rooney ni Radamel Falcao na Kun Aguero.

Sababu inayompa nafasi kubwa Rooney kusajiliwa na Madrid ni uwezo wake kucheza nafasi mbali mbali ukiacha nafasi ya ushambuliaji pia kocha wa sasa wa Madrid Carlo Anceletti anamfahamu vizuri katika kipindi alichokuwa anaifundisha Chelsea.

Kama Rooney atafanikiwa kujiunga na Madridi msimu ujao basi atajiunga tena na mshambuliaji Cristiano Ronaldo waliyekuwa pamoja kwenye klabu ya Manchester Utd.Chanzo: shaffihdauda

OBAMA KUKUTANA NA VIONGOZI 50 WA AFRIKA

obama 84a02
White House inasema Rais wa Marekani Barack Obama atawaalika viongozi takribani 50 wa serikali za barani Afrika kushiriki mkutano wa mwezi Agosti mjini Washington. (HM)
Naibu msemaji wa White House, Jonathan Lalley anasema bwana Obama atawajumuisha wakuu wote wa nchi au serikali za bara la Afrika ukiwatoa wale ambao hawana uhusiano mzuri na Marekani au waliosimamishwa kwa muda uanachama na Umoja wa Afrika-AU.
Lalley anasema mwenyekiti wa AU, Nkosazana Dlamini-Zuma pia ataalikwa kwenye mkutano ambao unafanyika Agosti tano hadi sita. White House ilitangaza mkutano huo jumanne ikisema Marekani itautumia kuimarisha ushirikiano wa biashara na uwekezaji na bara la Afrika.
Maafisa wanasema bwana Obama pia anamatumaini ya kujenga mafanikio yaliyopatikana tangu ziara yake ya mwezi Juni mwaka 2013 barani afrika. White House inasema nchi ambazo zitapokea mialiko ya mkutano wa Agosti ni pamoja na Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC, Ethiopia, Sudan Kusini, Mali na Nigeria. Chanzo: voaswahili

TFF YAZUIA USAJILI WA OKWI YANGA 

okwiclip 1bef1 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesimamisha usajili wa mshambuliaji Emmanuel Okwi kutoka Uganda katika timu ya Yanga wakati likisubiri ufafanuzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA). (HM)
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF iliyokutana leo (Januari 22 mwaka huu) kupitia masuala mbalimbali, imesimamisha usajili huo baada ya kubaini kuwa Okwi aliruhusiwa kuichezea SC Villa ya Uganda kwa kibali maalumu kutoka FIFA.
Okwi ambaye aliingia mgogoro na klabu yake ya Etoile du Sahel ya Tunisia aliruhusiwa na FIFA kuchezea SC Villa kwa kibali maalumu (provisional permit) cha miezi sita ili kulinda kiwango chake wakati suala lake dhidi ya Etoile du Sahel likishughulikiwa na shirikisho hilo la kimataifa.
Katika FIFA kuna kesi tatu kuhusiana na suala la mchezaji huyo. Wakati Okwi ameishitaki klabu hiyo FIFA kwa kutomlipa mshahara, Etoile du Sahel imemshitaki mchezaji huyo kwa utoro. Nayo Simba imeishitaki Etoile du Sahel kwa kushindwa kuilipa ada ya mauzo ya mchezaji huyo ambayo ni dola za Marekani 300,000.
Hivyo, TFF imeiandikia FIFA kutaka kujua iwapo mchezaji huyo anaweza kucheza Ligi nchini Tanzania wakati Etoile du Sahel ikiwa imefungua kesi katika shirikisho hilo la kimataifa ikidai Okwi bado ni mchezaji wake.
MECHI ZA TANZANIA PRISONS YAZASOGEZWA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesogeza mbele mechi za raundi ya 14 na 15 zinazoihusu timu ya Tanzania Prisons zilizokuwa zichezwe Januari 25 na 29 mwaka huu.
Awali Tanzania Prisons ilitakiwa kutafuta uwanja mwingine wa kuchezea mechi hizo dhidi ya Ruvu Shooting na JKT Ruvu kutokana na Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine kutokuwa tayari kwa Ligi Kuu ya Vodacom wikiendi hii.
Mechi hizo sasa zitachezwa kati ya Februari 6 na 8 mwaka huu kwenye uwanja huo huo wa Kumbukumbu ya Sokoine. Chanzo: TFF

Tuesday, January 21, 2014

TUHUMA ZA MAUAJI YA WAFUNGWA SYRIA 

SYRIA_8c0cb.jpg
Ripoti iliyotolewa na viongozi watatu wa zamani wa mashitaka ya uhalifu wa kivita inasema kwamba kuna ushahidi wa kutosha wa kuthibitisha kuwa Syria imewatesa na kuwaua karibu wafungwa 10,000 tangu kuanza harakati za kumpinga Rais Bashar Al-Asaad.
Wachunguzi walipekua maelfu ya picha za wafungwa waliokufa zilizotolewa nchini Syria na mpiga picha mmoja wa jeshi aliyetoroka kazi.
Wanasema miili mingi ilikuwa imekonda na mingine mingi kupigwa na kunyongwa.
Mmoja wa waandaaji wa ripoti hiyo, Professa Geoffrey Nice, aliambia BBC kuwa wingi na uhakika wa ushahidi uliotolewa unaonyesha wazi kuwa Serikali ilihusika katika ukatili huo.
Uchunguzi huo ulifadhiliwa na Serikali ya Qatar inayowaunga mkono waasi wa Syria. BBC imejaribu mara kadhaa kupata majibu ya Serikali ya Syria kuhusu madai hayo lakini Serikali haijatamka lolote. (J.M)
Madai kuwa wafungwa wamekuwa wakiteswa na kuuawa katika magereza ya Syria yamekuwa yakitolewa mara kwa mara na wakereketwa wa haki za kibinadamu tangu maasi yaanze nchini humo miaka mitatu iliyopita.
Hata hivyo madai ya sasa yana upya fulani kwa njia ya kipekee.
Chanzo BBC Swahili
Habari hizi zina ushahidi kutoka kwa wandani wa Serikali wenyewe; mpiga picha wa kitengo cha jeshi cha polisi aliyetoroka kazi amewasilisha maelfu ya picha ambazo alipiga kabla ya kutoroka.
Na wachunguzi wa kimataifa, waliokuwa viongozi wa mashtaka sasa wanaamini kuwa picha walizoona za miili iliyoharibiwa vibaya, iliyopewa nambari na kupigwa picha mara kadhaa, ni ushahidi wa kuaminika.
Zaidi ya miili 11,000 ilipigwa picha ingawa bado kuna wasiwasi kuwa kuna maelfu ya watu ambao walizuiliwa magerezani lakini sasa hawajulikani waliko.

RIBERY AWAPONDA FIFA KUMPA RONALDO BALLON D'OR 

article-2542613-1AA2C37800000578-112 634x3161 889af
Cristiano Ronaldo (kushoto), Lionel Messi (katikati) na Frank Ribery wakisikilizia tuzo ya Ballon d'Or (HM)
riberrrrr 60260
NYOTA wa Bayern Munich, Franck Ribery ameuponda mfumo wa upigaji kura za kuchagua Mwanasoka Bora wa Dunia wa FIFA, Ballon d'Or na kusema alistahili zaidi kushinda tuzo hiyo kuliko Cristiano Ronaldo, kwa sababu alishinda mataji matano mwaka 2013, wakati mpinzani wake wa Real Madrid hakushinda chochote.

Mfaransa huyo alikubali kushika nafasi ya tatu nyuma ya mshindi, Ronaldo na Lionel Messi aliyekuwa wa pili katika sherehe za tuzo zilizofanyika mjini Zurich, Uswisi Jumatatu iliyopita na pia amesema tuzo binafsi si muhimu kwake.
Ribery alitwaa mataji ya Bundesliga, Kombe la Ujerumani, Ligi ya Mabingwa, Super Cup ya UEFA na Klabu Bingwa ya Dunia akiwa na Bayern mwaka 2013.
Nyota huyo wa Ufaransa pia alisema kwamba yalifanyika mabadiliko katika mfumo wa upigaji kura mwaka huu kumsaidia Ronaldo, kwa kuongeza muda wa kupiga kura wakati nyota huyo wa Ureno alikuwa kwenye mazingira ya kuiwezesha nchi yake kuitoa Sweden katika kinyang'anyiro cha tiketi ya Kombe la Dunia.
Tarehe ya mwisho ya kupiga kura ilisogezwa mbele kwa wiki mbili. Hii haikuwahi kutokea kabla. Haikuwa kwa ajili ya soka. Ulikuwa uamuzi wa kisiasa,"aliponda Ribbery.

Hasira zake hazikuishia kwenye tuzo hiyo tu, bali pia uteuzi wa kikosi bora cha wachezaji 11 wa FIFA wa mwaka- kuhusisha wachezaji watatu tu wa Bundesliga, licha ya Fainali ya Ligi ya Mabingwa mwaka 2013 kuzikutanisha Bayern na Borussia Dortmund. Chanzo: binzubeiry

Champagne ahaidi mabadiliko makubwa FIFA

140120142945 jerome champagne 304x171 bbc nocredit1 1632f
Mgombea wa kiti cha urais wa shirikisho la mchezo wa soka duniani FIFA, Jerome Champagne, amependekeza kuanzishwa kwa mfumo wa kutoa kadi ya chungwa wakati wa mechi za soka, ili kuruhusu marefa wa mechi kuwaruhusu wachezaji waliofanya madhambi kuondolewa uwanja kwa muda. (HM)
Champagne mwenye umri wa miaka hamsini na tano kutoka Ufaransa, aliyasema hayo siku ya Jumatatu wakati alipoanzisha kampeini yake ya kumrithi Sepp Blatter kama rais wa FIFA.
Amesema ikiwa atashinda atapendekeza vilabu vya soka kuadhibiwa ikiwa wachezaji wake watahoji maamuzi ya refa na vile vile kuchunguza uwezekan wa kutumia technolojia kutatua maamuzi muhimu.
Uchaguzi wa urais wa FIFA utafanyika mjini Zurich Juni mwaka wa 2015.
Miongoni mwa mapendekezo mengine aliyoyasema ni kuthibiti idadi ya wachezaji wa kigeni wanaosajiliwa na vilabu, kutangazwa kwa mshahara wa rais wa FIFA na maafisa wengine wakuu.
Aidha amehaidi kuwa atafutilia mbali sheria ya sasa inayotoa adhabu tatu kwa mchezaji ambaye atafadha madhambi katika eneo la hatari.
Kuambatana na sheria ya sasa mchezaji yeyote anayefanya kosa katika eneo la hatari, hupewa kadi nyekundi moja kwa mojha na pia kupigwa marufuku ya kutocheza mechi mbili zijazo. Chanzo: bbcswahili

KATIBA YA MFUNGULIA NJIA AL-SISI, LAKINI VIJANA WAJITENGA 

dw_ec4c6.jpg
Kuidhinishwa kwa katiba mpya nchini Misri kumemuimarisha zaidi mkuu wa jeshi la nchi hiyo , lakini vijana wengi waliosaidia kuwangusha marais wawili katika kipindi cha miaka mitatu walijitenga na kura kuhusu katiba hiyo.
Wapiga kura waliipitisha katiba hiyo wiki iliyopita kwa asilimia 98.1, na matokeo yake yanaonekana kama ishara ya ndiyo kwa Jenerali Abdel-Fattah al- isi kugombea urais. Sisi aliongoza njama za kumuangusha rais Mohammad Mursi mwezi Julai, kufuatia maandamano makubwa ya kupinga utawala wake wa mwaka mmoja, ambao ulikuja baada ya maandamano yaliyomuangusha mtangulizi wake Hosni Mubarak mwaka 2011.(R.M)
Hofu ya kurudi kwa udikteta
Makundi ya vijana yaliyokuwa msitari wa mbele katika maandamano yaliyohitimisha tawala za Mursi na Mubarak, hawakupinga wakati serikali iliyowekwa na jeshi ilipofanya ukandamizaji mkubwa dhidi ya wafuasi wa Mursi. Na wala hawakupinga pale kundi la Mursi la udugu wa Kiislamu lilipopigwa marufuku na kutajwa kuwa ni kundi la kigaidi.
Lakini walielezea kughadhabishwa baada ya serikali inayoungwa mkono na jeshi kupitisha sheria mwezi Novemba, ambayo inapiga marufuku maandamano yasiyoidhinishwa. Na hili lilionekana kuakisiwa wazi wakati wa zoezi la kupiga kura. Sisi aliwasihi vijana kushiriki katika kura ya maoni, akisema wanachangia zaidi ya asilimia 50 ya raia milioni 85 wa nchi hiyo.
Lakini waandishi wa habari wa shirika la AFP waliotembelea vituo vya kupigia kura walisema vijana hawakushiriki zoezi hilo kwa nguvu, na wachambuzi walithibitisha kuwa vijana wengi wanaopigania mabadiliko wajitenga na kura hiyo.
Mchambuzi wa kisiasa Hassan Nafea alisema mwitikio wa kura hiyo ulikuwa unakatisha tamaa. Nafea alisema vijana walikataa kushiriki kura ya maoni kwa sababu wanachukulia mambo yanayofanyika hivi sasa kama mapinduzi dhidi ya mapinduzi ya Januari.
Mkuu wa tume ya uchaguzi Nabil Salib alitangaza matokeo siku ya Jumamosi na kusema kuwa ushiriki ulifikia asilimia 38.6 ya wapiga kura milioni 53, ambapo ni asilimia 1.9 tu waliopiga kura ya Hapana. Salib alisema asilimia fulani ya vijana hawakushiriki kwa sababu kura hiyo ilifanyika wakati wa mitihani, vinginevyo mwitikio ungekuwa mkubwa zaidi.
Udugu wa Kiislamu wapinga.
Lakini kundi la Udugu wa Kiislamu lilisema katika taarifa kuwa wapiga kura vijana hawakuwa wanashughulishwa na mitihani, bali walikuwa wanashghulishwa na maandamano ya kupinga mapinduzi ya kijeshi na kura ya maoni isiyo halali.
Lakini Nafea alisema matokeo ya kura hiyo yalionyesha kuungwa mkono kwa Sisi kugombea urais, kwa sababu ya kile alichosema kuwa sehemu kubwa ya Wamisri wanauona Udugu wa Kiislamu kama kitisho kwa jamii.
Sisi amesema huenda akagombea urais ikiwa ataombwa kufanya hivyo. Jenerali huyo anapendwa na mamilioni waliyoingia mitaani dhidi ya Mursi, lakini wafuasi wa udugu wa Kiislamu wanamlaani kwa kile wanachosema ni mapinduzi dhidi ya rais wa kwanza aliechaguliwa kidemokrasia nchini Misri.
Udugu wa Kiislamu, ambao umekumbana na ukandamizaji mbaya kutoka kwa serikali na kuuawa kwa wafuasi wake zaidi ya 1,000, umeipuuza kura ya maoni kama kichekesho. Vijana wengi wanakubaliana, lakini kwa sababu tofauti.
Watenda kinyume na wasemavyo
Mohamed Ghorab kutoka kundi linalopinga raia kushtakiwa na makahama za kijeshi, alisema kwao ni jambo la kushangaza kuwa katiba hiyo inazungumzia uhuru wa kujieleza wakati wale walioipinga katiba hiyo wamefungwa jela.
Alisema kwa wengi huo ni ukumbusho wa enzi za utawala wa Mubarak. Viongozi maarufu wa vijana kutoka mapinduzi ya mwaka 2011 dhidi ya Mubarak wamefungwa katika wiki za hivi karibuni. Miongoni mwao ni Ahmed Maher, Ahmed Douma na Mohamed Adel, ambao walikutikana na hatia mwezi Desemba kwa kuandaa maandsmano yasiyoruhusiwa.
Kesi hizi zimelaaniwa na makundi ya haki za binaadamu na wataalamu wanaosema zinatishia mafanikio yaliyopatikana tangu kuondolewa kwa Mubarak, na ishara ya kurejea katika utawala wa kidikteta.
Siku ya Jumapili, katika jaribio la kuwapooza vijana, rais wa muda Adly Mansour alisema vijana ndiyo walikuwa Ingini ya mapinduzi yote, na kuongeza kuwa mchango wao bado haujaisha, na kuwataka washiriki mchakato wa kisiasa, kwa vile uhuru sasa umehakikishwa.
Chanzo, dw.de

Sunday, January 19, 2014

 

Watu wakiwa wanajiachia
Muda wa misosi
Wadau wa habari makini wakiwa bize na mazungumzo, wamependeza sana



DK. Mengi akiwa anaingia kwenye ukumbi wa Diamond
DK. Mengi akiwa anaongea na vijana walioko nje ya geti

Askali wakiwa kazini kuzibiti fujo

Mkutugenzi wa The Guardian Kiondo Mshana (kulia) akiwa na wafanyakazi wengine
Mkurugenzi wa ITV Joyce Mhavile akiwa bize na maandalizi


Wawezeshaji wa team nzima ya blog ya habari makini

Mabosi wakibadilisha mawazo
Mary akiwa bize ukumbini kwa maandalizi
Watoto wa IPP wakiwa wametulia ukumbini wamepeza sana
Pendeza sana , Hongera Dk. Mengi Mungu akubariki kwa kuwawezesha shughuli nzima.