SWAHILI FASHION WEEK YAHITIMISHWA
SWAHILI FASHION WEEK 2012 YAHITIMISHWA MWISHONI MWA WIKI
HII
GABRIEL MOLLEL ANYAKUA TUZO MBILI
GABRIEL KUIWAKILI SWAHILI FASHION WEEK KATIKA MAONYESHO
YA MITINDO MSUMBIJI 2012
Baada ya miezi mingi ya maandalizi,
waandaji wa Swahili Fashion Week wamefanikia kuhitimisha onyesho kubwa la
mitindo na mavazi katika nchi za Afrika mashariki na kati, tukio lilinaloendelea
kuiweka tasnia ya mitindo katika ramani ya mitindo Afrika na Duniani
kiujumla.
Ikiwa na viwango vipya na vyenye
ubora, waandaji wamefanikiwa kuwa na tukio bora la mwaka na kuwaacha
wahudhuriaji wakihitaji maelezo zaidi kuhusu onyesho la 2013. Kama ilivyo ada
vitu vizuri lazima viwe na mwisho, Swahili Fashion Week 2012 ilimalizika kwa
kutolewa tuzo siku ya Jumamosi ya tarehe 8, Desemba 2012.
Tuzo za Swahili Fashion Week 2012 zimelenga kutambua
mchango wa wabunifu mbalimbali ambao wametoa mchango mkubwa katika maendeleo ya
tasnia ya mitindo Afrika Mashariki. Tuzo hizo zinaongeza chachu ya uvumbuzi na
ubunifu katika tasnia ya mitindo. Hii inaendana na kuifanya mitindo ya Kiswahili
kujulikana duniani. Alisema Mustafa Hassanali, Mmiliki na Muandaaji wa Swahili
Fashion Week.
Swahili
Fashion Week 2012, imefanyika katika Hoteli ya Golden Tulip iliyopo jijini Dar
es salaam, kuanzia tarehe 6-8 Desemba, ikiwa tukio kubwa la Mitindo ukanda wa
Afrika Mashariki na Kati lililokutanisha wabunifu zaidi ya 50 kutoka ndani na
nje ya Tanzania.
Mshindi
wa Tuzo mbili mwaka huu, Mbunifu Mvumbuzi wa mwaka na Mbunifu Bora wa Mwaka,
Gabriel Mollel ataiwakilisha Swahili Fashion Week katika week ya mitindo
Msumbiji inayoanza Desemba 7-15. Kwa mwaka wa tano sasa Swahili Fashion Week
imefanikiwa kuendeleza uhusiano na Mozambique Fashion Week.
“Ni
faraja kuiwakilisha Tanzana na Swahili Fashion Week katika maonyesho ya
Msumbiji, kushinda tuzo mbili mwaka huu, kwangu ni matokeo ya kujituma na
ubunifu mzuri, ninatumia muda mwingi kutengeneza kazi zangu. Hii tuzo inanipa
nguvu kubwa lakini ni changamoto kwani kazi ngumu katika maisha ni kubaki katika
hadhi ile ile ambayo watu walikuamini na kukupa katika shughuli unayoifanya”
Alisema Gabriel
“Kama
Swahili Fashion Week ni jambo la fahari na kujivunia kuwa sehemu ya Mozambique
Fashion Week, Gabriel Mollel hataiwakilisha tu Swahili Fashion Week nchini
Msumbiji, ila pia anaiwakilisha nchi yetu kwa kuonyesha ubunifu na mitindo
iliyotengenezwa Tanzania” Alisema Mustafa Hassanali.
Huu ni mwaka wa Tano sasa tangu Swahili Fashion Week
ianze kushirikiana na Mozambique Fashion Week ambapo Mustafa Hassanali
alishiriki mwaka 2007 na 2008 huku Jamila Vera Swai akiwakilisha 2009, Manju
Msita 2010, Robbi Morro na Ailinda Sawe wote walienda 2011.
“Swahili Fashion Week inalengo la kutangaza, kuinua na
kutafuta masoko ya bidhaa za wabunifu wa Afrika Mashariki katika soko la Afrika
na duniani kote. Tasnia ya Mitindo afrika inaitaji kutambiliwa na kuwekwa katika
ramani ya dunia” Aliongeza Mustafa Hassanali.
Licha
ya kutambua mchango wa wadau mbalimbali wa tasnia ya mitindo Afrika Mashariki,
SFW pia ilitoa nafasi kwa wabunifu vijana wanaochipukia kuonyesha kazi zao na
mitindo yao kwa mashabiki wa mitindo waliohudhuria katika Swahili Fashion Week
mwaka huu ambapo wabunifu mbalimbali walionyesha ubunifu wao.
Wabunifu wa Swahili Fashion Week
pia walipata nafasi ya kushiriki katika semina iliyoandaliwa na USAID COMPETE
kwa kushirikiana na ORIGIN AFRIKA juu ya kutafuta masoko kwa bidhaa
wanazozitengeza.
Swahili Fashion Week 2012
imedhaminiwa na Vodacom, USAID Compete, Origin Africa, EATV, East Africa Radio,
Golden Tulip Hotel. Amarula, Precision Air, 2M Media, Global Outdoor Ltd, Vayle
Springs Ltd, Eventlites, Ultimate Security, BASATA (Baraza La Sanaa Taifa),Strut
It Afrika, Ndibstyles, PKF Tanzania, DARLING, PUSH Mobile, DarLife, Century
Cinemax, Natol na 361 Degrees.
Kwa Picha zaidi za Swahili Fashion
Week 2012: http://ramp.sdr.co.za/1212SFW/
KUHUSU SWAHILI FASHION WEEK
Swahili Fashion Week ni jukwaa kubwa la mitindo ya mavazi la kila mwaka katika ukanda wa
Afrika mashariki na kati kwa sasa. Huu ni mwaka wa Tano sasa, ambapo Swahili Fashion Week
imekuwa ni Jukwaa la wanamitindo na watengeneza vito vya urembo kutoka katika
nchi zinazoongea Kiswahili na bara zima la Afrika kwa ujumla kuweza kuonesha
vipaji, kutangaza ubunifu wao na kukuza mtandao wa mawasiliano ya kibiashara
ndani na nje ya nchi kwa wadau wa mitindo. Hili limelenga kuhamasisha ukanda huu
wa Afrika Mashariki na Kati kwamba ubunifu wa mavazi ni njia moja wapo ya
kujipatia kipato na wakati huo huo kukuza bidhaa zinazotengenezwa Afrika ( Made in Africa
concept)
Ikiwa imeanzisha uhai na jukwaa la matumaini kwa
kilinge cha mitindo katika ukanda huu, Swahili Fashion Week Swahili Fashion week
imelenga kuwa maonyesho ya ubunifu wa mavazi linaloonekana sana Afrika na hasa
kwa ajili ya soko la kimataifa, lililoundwa, kutengenezwa na kujengwa mwaka 2008
na Mustafa Hassanali.
Ifikapo mwaka 2013, Swahili Fashion Week ina lengo
la kuwa ni tukio litakalotokea mara mbili kwa mwaka, ambapo kwa kuanza tukio la
kwanza litafanyika nchini Kenya kama sehemu ya kwanza kisha tukio lenyewe kabisa
kufanyika baadae nchini Tanzania kama sehemu ya pili.
KUHUSU GABRIEL MOLLEL
Gabriel Mollel ni muasisi wa Sairiamu Community Action Foundation,
ambayo ndio nembo yake ya ubunifu, Sairiamu inamaana “Mtu anaetoa kwa mikono
miwili” katika lugha ya kimasai. Gabriel amekua akifanya kazi zake kwa mikono
yake mwenyewe kwa ajili ya jamii yake kwa da mrefu kabla hajawa na jina kubwa
katika uwanda wa sanaa ya ubunifu hapa Tanzania, ameweza kushiriki katika
maonyesho mbalimbali ikiwemo Harusi Trade Fair, Swahili Fashion Week na mengine
mengi ambapo pia amekua mshindi wa Swahili Fashion Week katika kipengele cha
Mbunifu Bora 2011.
No comments:
Post a Comment