WAZIRI AKUTANA NA BODI ZA USHAURI WA MAGAZETI ZANZIBAR
Na Mwanaisha Muhammed Maelezo Zanzibar 20/12/2012.
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk amesema kuwepo kwa magazeti mengi katika nchi kunasaidia sana kuharakisha harakati za Maendeleo .
Aliyasema hayo huko ofisini kwake Kikwajuni wakati alipokuwa akibadilishana mawazo na wajumbe wa Bodi ya ushauri wa Magazeti na Vijarida Zanzibar .
Waziri alisema kwa sasa Zanzibar magazeti yaliyopo ni machache mno kilinganisha na nchi nyengine kama Tanzania Bara, hivyo kutokuwepo kwa Magazeti mengi kunadumaza maendeleo
Aliitaka
bodi hiyo kutokuwa wakali wakati wa kusajili magazeti hayo na daima
wawe wanawafahamisha wenye magazeti pale wanapokosea na wasichoke ila tu wakiona muhusika hafahamishiki ndipo hatua za kisheria zichukuliwe.
Amesema
kuwa jukumu kubwa kwa hivi sasa kwa bodo hiyo kihakikisha inasajili
magazeti ya kutosha pamoja na vijarida kwa mujibu wa sheria na taratibu
ziliopo ili Zanzibar iweze kupiga hatua za maendeleo kwa kuwa na
magazeti mengi kama ilivyokuwa siku za nyuma..
Hata
hivyo Waziri alisema bodi inakazi muhimu katika nchi kwa kuhakikisha
kwamba magazeti yatakayo ruhusiwa yawe ni yenye uhakika na sio ya
kubahatisha na kuleta mfarakano katika jamii.
Nae
kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo ambae pia ni Mshauri wa Rais wa
masuala ya Utalii Issa Ahmed Othman alisema kuwa madhumuni makubwa ya
kuanzishwa kwa Bodi hiyo ni uangalizi wa magazeti na vijarida ili
yasikiuke taratibu na sheria zilizowekwa .
Alisema kuwa kwa upande wa Bodi hiyo huwa hawapitishi gazeti wala majarida kama vigezo husika vya kisheria havijakidhi haja kama sheria ilivyoelekeza ili kuepusha migogoro kutotokea katika jami
Mwenyekiti
huyo alisema kuwa bodi inaona choyo kwa wazanzibari kutokuwa na
magazeti mengi hivyo inakaribisha kwa watanzania kwa ujumla kuanzisha
magazeti ili maendeleo yaweze kupatikana Zanzibar.
Alisema kuwa Serikali imeweka chombo cha kushughulikia vyombo vya Habari sio kuwabana bali ni kuweka utaratibu ambao utasaidia utendaji mzuri wa kazi za waandishi wa habari .
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR .20/12/2012.
No comments:
Post a Comment