TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Friday, November 30, 2012

NGUO ALIZOVULIWA SHARO MILLIONEA ZAKAMATWA



Sharomilionea.
Siku kadhaa baada ya marehemu msanii sharomilionea kuzikwa, vile vitu ambavyo vilisemekana kupotea ama kuibiwa wakati wa ajali vimeanza kupatikana. 

Akithibitisha habari za kupatikana kwa vitu hiuvyo, swahiba wake wa karibu ambaye alikuwa akiishi na Sharomilionea Kitale amesema amepata taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa kijiji kule Muheza Tanga kwamba baadhi ya vitu vimepatikana.

Kwa mujibu wa maelezo yake, vitu ambavyo vilikuwa vimeibwa ni pamoja nasimu mbili aina ya Blackberry na Samsung, Viatu, Cheni, tairi la spea ya gari, Betri, Radio ya gari na shilingi milioni sita taslimu ambazo alikuwa akimpelekea mama yake.


Bwana kitale aliendelea kwa kusema, cha kusikitisha zaidi katika tukio hilo la wizi, ni unyama uliofanywa na wezi hao ambapo baada ya kushindwa kumvua pete kwenye kidole cha msanii huyo, waliamua kumkata kidole na kuondoka na pete hiyo.


Aidha alisema kuwa kwa mujibu wa taarifa alizonazo kutoka kwa mwenyekiti wa kijiji kuna wanakijiji wamerudisha baadhi ya vitu kama Simu ya Mkononi,Pete,Cheni, Jeans, T-shirt,Viatu, ambapo walisema wamerudisha baada ya kugunduliwa na wanakijiji wenzao ambao walitoa taarifa baada ya kugundua vitu walivyokuwa navyo ni mali ya marehemu msanii Sharomilionea.


Kitale alisema “kuna kijana mmoja anayeitwa David ambae ni ndugu na mwenyekiti na wenzake ambao walitajwa na wanakijiji wenzao kwa kuhusika yeye pamoja na wenzake kufanya kitendo hicho ya bila kujua wanao mfanyia alikuwa ni Sharro baada ya kutambua watu hao wakafanya ionekane vitu hivyo vimepatikana kutoka kwa wanakijiji."


Kitale alimalizia kwa kusema kwa sasa vitu ambavyo havijapatikana ni pamoja na Betri, Tairi la spea, Radio ya gari na pesa ambazo anasema suala hilo tayari lipo poilisi kwa uchunguzi zaidi.


Hata hivyo  habari zilizotufikia  zinadai kuwa Watu wanne wamekamatwa na Jeshi la Police kwa tuhuma hizo za za kumkata vidole na kumuibia marehemu Sharo Milionea baada ya kupata ajali ya gari 
LEO SIKU YA UKIMWI DUNIANI  WAKAZI WA DAR WAHIMIZWA KUPIMA AFYA ZAO NA  JK KUHUTUBIA TAIFA
Mratibu wa Ukimwi wa Mkoa wa Dar es salaa kutoka TACAIDS Bw. Omary Chambo akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu hali ya maabukizi ya ugonjwa huo katika jiji la Dar es salaam na kutoa wito kwa wakazi wa jiji hilo kushirikiana na serikali na wadau mbalimbali katika kupambana na Ugonjwa huo
Na: Aron Msigwa MAELEZO. Dar es salaam.
Wakazi wa mkoa wa Dar es salaam wameshauriwa kujitokeza kupima afya zao mara kwa mara na kujiepusha na vitendo vinavyochangia maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam leo jijini Dar es salaam Afisa habari wa mkoa huo Bi. Adrofina Ndyeikiza amesema kuwa kuna umuhimu wa jamii kujitambua na kushiriki kikamilifu katika kufanya tathmini ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi na namna bora ya kujikinga.
Amesema kila mwaka ifikapo tarehe 1 Desemba Tanzania huungana na mataifa mengine kuadhimisha siku ya Ukimwi Duniani kwa kuwahusisha wadau mbalimbali ambao wote kwa pamoja hupata nafasi ya kutathmini mikakati ya kudhibiti Ukimwi iliyofanyika kwa muda wa mwaka mzima na kutafuta mbinu za kuboresha harakati hizo.
Amesema maadhimisho hayo yatakayofanyika katika viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam umeichagua na kuipa heshima manispaa ya Kinondoni kuandaa maadhimisho hayo
“Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani mwaka huu yanabeba ujumbe ule ule uliotolewa mwaka jana ambapo kauli mbiu hii inaendelea mpaka mwaka 2015 na kwa mwaka huu jijini Dar es salaam yanafanyika katika uwanja wa Biafra yakiongozwa na kauli mbiu ya Tanzania Bila Maambukizi Mapya, Unyanyapaa na vifo vitokanavyo na Ukimwi Inawezekana”
Amesema lengo la kauli mbiu hiyo ni kuhamasisha na kuelimisha zaidi jamii kuhusu VVU na Ukimwi na kubadilisha tabia ili kujikinga na maambukizi ya mapya ya VVU, kuhamasisha jamii kuacha kabisa unyanyapaa, unyanyasaji na ubaguzi kwa watu wanaoishi na VVU na ubaguzi kwa watu wanaoishi na VVU na UKIMWI na kuboresha huduma za afya na tiba ya magonjwa nyemelezi na dawa za kufubaza makali ya VVU (ARVs).
Bi. Ndyeikiza amesema kuwa mbali na maadhimisho hayo katika mkoa wa Dar es salaam serikali kwa kushirikiana na Asasi zisizo za kiserikali zilizo katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo zinaendelea kuwapatia wananchi huduma za elimu, ushauri na upimaji wa hiari wa VVU katika maeneo mbalimbali.
Kwa upande wake mratibu wa Ukimwi wa mkoa wa Dar es salaam kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi nchini (TACAIDS) Bw. Omary Chambo amesema kuwa jamii bado inahitaji elimu juu ya namna na mikakati ya kukabiliana na virusi vya Ukimwi na hatimaye kupunguza maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi.
Amesema takwimu za mwaka 2012 kwa mkoa wa Dar es salaam zinaonyesha kuwa katika Manispaa ya Ilala hali ya maambukizi ni 8.3%, Temeke 6% na Manispaa ya Kinondoni ni 6.7 na kuongeza kuwa vitendo vya unyanyapaa miongoni mwa jamii kwa waathirika wa ugonjwa huo vinachangia watu wengi wasijitokeze kupima kwa hiari ili kujua kama wanaishi na VVU.
“Vitendo vya unyanyapaa vimekua sababu ya kuwafanya wengi wasijitokeze kupima kuhofia kutengwa na jamii pindi watakapogundulika kuwa wameathirika , hivyo tunaendelea na juhudi ya kuwaelimisha wananchi kuepuka vitendo hivyo na wajitokeze kupima afya zao kwa hiari” ameeleza Bw. Omary.
MKUTANO WA TABIA YA NCHI WAZIDI KUENDELEA DOHA
Evelyn Mkokoi Afisa Habari Ofisi ya Makamu wa Rais Doha 30/11/2012
 Utoaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa kupunguza hewa ukaa na uharibifu wa misitu (MKUHUMI) ulenge kunufaisha wananchi na nchi katika maeneo husika.

Tanzania imesema kuwa, mfumo wa utoaji fedha kwa ajili ya kupunguza utoaji wa gesijoto na uharibifu katika sekta ya misitu hususan kwa nchi zinazoendelea unatakiwa uwe wenye manufaa kwa nchi na wananchi katika maeneo husika. Hayo yameelezwa leo na Bwana Freddy K. Manyika, Afisa Misitu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, katika majadiliano kuhusu Mfumo wa Ufuatialia na Utaratibu wa utoaji wa fedha, yanayoendelea katika mkutano wa 18 wa nchi wananchama wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchia unaofanyika mjini Doha, Qatar.
 Akiwasilisha msimamo huo wa Tanzania, bw. Manyika ameleeza kuwa,Kuwepo kwa mfumo bora na wa ufuatialiaji na utoaji wa fedha utatoa motisha kwa uhifadhi na usimamizi endelevu katika sekta ya misitu kwa nchi maskini.. Akizungumza kwa niaba ya nchi zinazoendela (Least developed Countries -LDCs) Bw. Manyika alisema kuwa maisha ya wananchi katika nchi zinazoendelea husuan nchi maskini yanategemea sekta ya misitu kwa ajili ya kupata nishati, chakula, madawa, ujenzi wa makaazi na miundombinu, malisho ya mifugo, shughuli za kitamaduni, utalii, na huduma mbalimbali za kijamii kwa kiwango kikubwa, hivyo kwa kuzingatia umuhimu huo, mfumo wa ufuatilaiji na utaratibu wa malipo unaoandaliwa kwa ajili ya kusaidia sekta ya misitu hauna budi kutoa malipo yenye manufaa na motisha kwa wananchi wanaotunza misitu badala ya kutaka kutoa mwanya kwa makampuni ya kibiashara yenye mitaji mikubwa kunufaika na rasilimali hiyo. “Tanzania na nchi zinazoendelea hazikubaliani na mfumo unaolenga kuwafanya wananchi wanaozungukwa na kutunza misitu hiyo kwa miaka mingi kugeuzwa vibarua na wapakazi katika makampuni yenye lengo la kujinufaisha kwa kutumia rasilimali na nguvu za wananchi maskini, Alisisitiza.” Aidha Bw. Manyika aliongeza kuwa, kufikiwa kwa makubaliano kuhusu mfumo na utaratibu wa utoaji wa fedha kwa ajili ya shughuli za MKUHUMI katika mkutano wa Doha utasaidia kurejesha motisha kwa wananchi kuhifadhi misitu katika maeneo yao na hivyo kuendeleza shughuli za utunzaji mazingira na kuchochea maendeleo na uhifadhi endelevu kupitia sekta ya misitu. Katika majadiliano yanayoendelea hapa mjini Doha, nchi wanachama wanatakiwa kuandaa mfumo wa ufuatiliaji na utaratibu wa utoaji wa fedha kwa shughuli za upunguzaji wa gesijoto na utunzaji wa misitu ili kupunguza uharibifu. Mkutano wa 18 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi unafanyika Doha, Qatar, kuanzia tarehe 26 Novemba hadi 7
POLISI AFUKUZWA KAZI BAADA YA KUMBAKA MTUHUMIWA WA KIKE
JESHI la Polisi mkoani Mbeya limemfukuza kazi askari wake Enock Daffa (22) kwa tuhuma za kufanya  mapenzi na mtuhumiwa wa kike mwenye umri wa miaka 25 katika Kituo cha Polisi cha Mji mdogo wa Tunduma, Wilaya ya Momba, mkoani hapa. 

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Athuman Diwani, askari huyo alitenda kosa hilo Novemba 21,2012 na kwamba mtuhumiwa aliyefanya naye mapenzi alikuwa akikabiliwa na kosa la wizi.
 
Kamanda Athumani alisema kuwa mbali ya kufukuzwa kazi askari huyo tayari amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mbozi ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.

Aidha alisema kuwa hali kama hiyo haitaweza kuvumiliwa na Jeshi la Polisi na kwamba atakayebainika kufanya tukio kama hilo adhabu yake itakuwa ni kufukuzwa kazi.
 
Kamanda huyo alitoa wito kwa askari polisi kufanya kazi kwa kufuata sheria na kanuni za Jeshi la Polisi kama mwongozo unavyowaagiza ili kulinda maadili ya Jeshi la Polisi ambacho ndicho chombo kinachotumika na wananchi katika kuzisimamia sheria.
 
Akizungumzia tukio hilo, baba mzazi wa askari huyo alisema kuwa kitendo alichofaya mtoto wake si cha kiungwana ambacho pia kimetia fedheha familia yake pia kwa jeshi la Polisi ambalo limepewa dhamana ya kutunza usalama wa raia na mali zake.
WAHU KUPAMBA UZINDUZI WA DHANA YA 'WELLNESS' J/PILI UBUNGO PLAZZA
Umewahi kulisikia hili neno?
Kwa ufupi linasanifu dhana nzima ya AFYA.
Ila afya hii inaweza kuwa ya kimwili (physical), kiakili (mental), kipesa (financial), kinahusiano (relationship), kijamii (social), kikazi(occupational), kiroho (spiritual), kihisia (emotional), kimazingira (environmental) na hata ya kitabibu (medical).
Tunahitaji afya zote hizi kuwa kamili na wenye furaha (for optimal well-being).
Dhana hii ya WELLNESS itaelezewa kwa ufupi kwa nini ni muhimu kwako katika hotel wa Blue Pearl, Ubungo Plaza, jumapili tarehe 2 Desemba 2012 toka saa 8 mchana hadi 1 jioni. Wataalam wenye uzoefu katika fani hii watakuelimisha kwa muda mchache.
Uzinduzi huu utasindikizwa na mwanamuziki WAHU KAGWI toka Kenya akikuambia BETTER DAY. “Whatever you are going through today, there always gonna be a better day”.
Kiingilio: 20,000/= only per head

COME ONE, COME ALL.
Tickets zitapatikana 8020 fashions Sinza, maduka yote ya Mariedo ambayo ni IPS, Benjamini Mkapa Towers na Namanga , mlimani city Shear Illusions na Milepamba shop Mwenge Bus stop.

NB: HAKUNA TIKETI ZITAKAZOUZWA MLANGONI SIKU YA JUMAPILI. Deadline Jumamosi saa 4 asubuhi. Only limited seats

NB: Get ready to step on GREEN CARPET for pictures, the carpet of HEALTH
TUSKER LITE YAZINDULIWA RASMI JIJINI DAR ES SALAAM

























Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries imezindua rasmi kinywaji kipya cha tusker lite usiku wa kuamkia jana katika usiku wa Marketers Night Jijini Dar-es-Salaam.  
Hivyo wadau wa kinywaji hicho sasa full kujiachia kipo kinapatikana bila matatizo
JP MPIANA KUWASA MOTO NDANI YA LEADERS CLUB LEO




















MASHABIKI wa muziki wa dansi wametakiwa kujitokeza kwa wingi leo katika viwanja vya Leaders, Kinondoni, jijini Dar es Salaam, kushuudia onyesho la kukata na shoka litakalofanywa pamoja na nguli za muziki,  JB Mpiana, kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na  Bendi ya Mashujaa Musica (Watoto wa Mama Sakina).

 Kwa mujibu wa ofisa habari wa Mashujaa,  Asha Kigundula, alisema bendi yake ya Mashujaa imepania kuonyesha shoo ya nguvu na JB Mpiana.
JK AKUTANA NA MWENYEKITI WA KANU 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mwenyekiti wa chama cha KANU Mhe Gideon Moi aliyemtembelea leo (jana) Novemba 29, 2012 katika hoteli ya Nairobi Serena jijini Nairobi

Wednesday, November 28, 2012

JENGO LA AFRIKA MASHARIKI LAZINDULIA MJINI ARUSHA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiangalia mfano wa jengo jipya la makao makuu ya Jumuiya hiyo pamoja na maelezo yake baada ya kulifungua rasmi  Novemba 28, 2012 jijini Arusha
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifunua pazia  kufungua rasmi jengo jipya la makao makuu ya Jumuiya  Novemba 28, 2012 jijini Arusha

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na wakuu wenzie wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na wadau pamoja na wabunge wa Afrika Mashariki
PICHA NA IKULU

HII NDIO SAFARI YA MWISHO YA MPENDWA WETU SHARO MILIONEA
 

























Hivi ndivyo mamia ya watu walivyojitokeza kumsindikiza katika safari yake ya mwisho mpendwa wetu SharoMilionea Mkoani Tanga

Tuesday, November 27, 2012

TASWIRA ZA PICHA YA AJALI YA SHARO MILIONEA
 





























Gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 478 BVR alilokuwa akiendesha msanii wa filamu na muziki Hussein Ramadhani Mkieti ‘Sharo Millionea’ kutoka jijini Dar es salaam kuelekea Kijijini kwao Lusanga Wilaya ya Muheza  mkoa wa Tanga. Sharo Millionea alikufa papo hapo na mwili wake kuhifadhiwa Hospitali ya Teule Muheza Tanga.
Wakazi wa wilaya ya Muheza na maeneo mengine wakiwa wamefurika nje ya Chumba cha Maiti cha Hospitali Teule Muheza, kusubiri kushuhudia mwili wa Sharo Millionea, aliyefariki kwa ajali ya gari.

BALOZI WA CHINA AONGEA NA WANAHABARI























Balozi mdogo wa China Madam Chein Qiman kati kati akizungumza na Waandishi wa habari Ofisi kwake Mazizini Zanzibar kuhusu Mipango ya Serikali ya China kuisaidia Zanzibar na Afrika kwa ujumla
TANZANIA KATIKA KUNDI LA G77 NA CHINA






















Baadhi ya washiriki wa Tanzania wakifuatilia mkutano wa kundi la 77 na China (G77 and China) katika mkutano wa Dunia wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya Tabia Nchi unaoendelea mjini Doha, Kulia Bi Emelda Teikwa na Bw. Fred Manyika maafisa kutoka idara ya Mazingira ya Ofisi ya Makamu wa Rais. 
 
                      Picha na evelyn Mkokoi

HOSPTALI 37 NCHINI KUNUFAIKA NA BILION YA UHOLANZI
 Balozi wa Uholanzi nchini Dr. Ad Koekkoek (kulia) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam kuhusu msaada wa shilingi bilioni 33 uliotolewa na Uholanzi kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili kuimarisha huduma za uchunguzi wa magonjwa mbalimbali katika Hospitali 37 hapa nchini . Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah. Tanzania nayo inatakiwa kuchangia kiasi kama hicho katika huduma hiyo ili kuwa asilimia 50 kwa 50 kila pande yaani Tanzania na uholanzi.






















Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah (kushoto) na Balozi wa Uholanzi nchini Dr. Ad Koekkoek (kulia) wakibadilishana hati ya msaada wa shilingi bilioni 33 uliotolewa na Serikali ya Uholanzi kwa Serikali ya Tanzania 

TANZANIA imepokea msaada wa shilingi bilioni 33 kwa ajili kusaidia uboreshaji wa huduma za uchunguzi wa afya kwa kipindi cha miaka mitano ijayo hapa nchini.
 
Msaada huo huo utawezesha Serikali ya Tanzania kuboresha huduma ya uchunguzi katika hospitali 37 kwa ununuzi wa vifaa vya kisasa vya kufanyia uchunguzi ambavyo vitawasaidia wataalam kutoa matokeo ya matatizo yanayowakabili wagonjwa kwa haraka zaidi .
 
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dar es salaam mara baada ya kupokea msaada huo kutoka Ubalozi wa Uholanzi hapa nchini kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah alisema msaada huo utaiwezesha Serikali kunulia vifaa vya kufanyia uchunguzi wa kisasa kama vile kununulia vifaa vya X-ray na ultrasound ambazo vitasambazwa katika Hospitali hizo
 
Alisema kuwa msaada huo ni muhimu kwa Serikali ya Tanzania kwani utaisaidia Serikali kupunguza gharama ya kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa wale wanaohitaji kupatiwa huduma za uchunguzi wa kina wa afya zao badala yake kazi itafanyika hapa nchini mara baada ya ununuzi wa vifaa hivyo.
Khijah alisema katika makubaliano Serikali ya Tanzania nayo itachangia kiasi hicho fedha katika msaada huo ili kufanikisha ununuzi wa vifaa vya huduma ya uchunguzi .
 
Alisema kuwa msaada huo utadumu kwa kipindi cha miaka mitano ambapo mara baada ya miaka hiyo kumalizika Serikali ya Tanzania itasimamia yenyewe .
 
Alitaja mikoa itakayonufaika na msaada huo ni pamoja na Shinyanga, Kagera, Iringa, Mwanza, Pwani, Lindi, Mtwara, Dar es Salaam, Arusha, Dodoma, Kigoma, Manyara, Mbeya, Morogoro, Kilimanjaro, Mara, Rukwa, Singida, Ruvuma, Tanga na Tabora. Kufuatia hali hiyo Katibu Mkuu huyo aliwataka watendaji wa Hospitali zote zitakazonufaika na msaada huo kuwa makini katika utunzaji wa vifaa ili viweze kutumika kwa muda mrefu na uboreshaji wa afya za wananchi.
 
Naye Balozi wa Uholanzi nchini Dkt. Ad Koekkoek alisema kuwa msaada huo unalenga upatikanaji wa huduma za bora za ultra sound, CT scan ,na x-ray hapa nchini na hivyo kuboresha huduma za afya.
Aliongeza kuwa huduma hiyo inalenga kuufanya uchunguzi wa magonjwa uwe wa kisasa zaidi ambapo wataalam wataweza kufanya uchunguzi kwa haraka na kama kama utahijika sehemu nyingine kuweza kuutuma kwa njia mtandao(internet).
MATUKIO YA KUSIKITISHA HAYA KWA WASANII NI VILIO TUPU MWAKA HUU
Marehemu Steven Kanumba
Marehemu Mlopelo
Marehemu John Maganga
Na huyu ndiye Sharo Milionea, ambapo leo ametufanya tuwe na huzuni kubwa sana kufuatia kifo chake






















Poleni sana Wasanii wetu nchini kwa kuondokewa na wapenzi ambapo ni wachapakazi na vijana mahili katika Tasinia hiyo. Mungu awatie nguvu . Wote kwa ujumla tunamasikitiko makubwa sana kwa matukio hayo, lakini tunasema yote ni mapenzi ya aliyetuumba.

Monday, November 26, 2012

WAJUE MABILIONEA WATANO WA TANZANIA

WAFANYABIASHARA watano, Said Bakhressa Gulam Dewji, Rostam Aziz, Reginald Mengi na Ali Mufuruki, wametajwa na Jarida la Ventures Africa linalozungumzia masuala mbalimbali ya uchumi wa Afrika kuwa ndiyo matajiri zaidi nchini.
Anayeongoza katika orodha hiyo ni Bakhressa anayemiliki mali na fedha zenye thamani ya Dola za Marekani 620 milioni sawa na Sh992 bilioni (Dola moja Sh1,600) akifuatiwa na Dewji ambaye utajiri wake ni Dola 560 milioni (Sh896 bilioni). Wengine na kiasi cha mali na fedha wanazomiliki kwenye mabano ni Rostam (Sh672 bilioni- Dola 420 milioni) Mengi (Sh448bilioni- Dola 280 milioni) na Mufuruki (Sh176 bilioni - Dola 110 milioni).

Matajiri hao wamepatikana baada ya kuangalia nafasi zao kifedha, ufanisi wa kampuni zao katika soko la hisa, mfumo wa wanahisa katika soko la hisa na mtiririko mzima wa fedha katika akaunti zao kwenye benki mbalimbali. Jarida hilo linalotoka mara moja kwa mwezi kutoka Afrika Magharibi, limesema matajiri hao wa Tanzania ni kati ya Waafrika wenye utajiri ambao ni mabilionea 4,800 kutoka mataifa 17.Asilimia kubwa ya watu 1,523 ni mamilionea na wamo katika ripoti ya watu matajiri Afrika.Jarida hilo linataja jinsi matajiri hao walivyokuwa wajasiriamali wadogo kabla ya kuibuka na kuwa mabilionea.

MSANII WA MUZIKI NA MAIGIZO NCHINI SHARO MILIONEA AFARIKI DUNIA























Sharo Millione Enzi za Uhai wake
Msanii wa maigizo na muziki wa kizazi kipya Hussein Mkiety a.k.a Sharo milionea , amefariki dunia baada ya kupatwa na ajli mbaya eneo la kijiji cha Lusanga wilayani Muheza Mkoa wa Tanga ambapo ndipo nyumbani kwao
Siku zote tutamkumbuka sana hasa katika kipaji chake cha maigizo ya ushekeshaji na pia nyota huyo alitokea kuwa kivutio sana cha watoto katika maigizo yake.
Bwana ametoa na Bwana Ametwaa Amina
MWANAMUZIKI JB MPIANA AWASILI NCHINI USIKU HUU


























Mwanamuziki nguli wa dansi Barani Afrika JB Mpiana (mwenye kofia) akiongozona na baadhi ya wenyeji wake pamoja na wanamuziki wa bendi yake Wenge BCBG wakati wakiwa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jijini Dar es Salaam, Bendi hiyo inatarajia kufanya onyesho kubwa Nov 30, mwaka huu katika viwanja vya Leaders Kinondoni Jijini Dar es Salaa

Sunday, November 25, 2012

DKT BILAL AZINDUA MKOA WA KATAVI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungao ya Tanzania Dkt Mohamed Gharib Bilal na mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe wakizindua rasmi mkowa wa Katavi kwa kuweka jiwe la msingi katika kilima cha kijiji cha Kabungu kwa ajili ya kujenga kituo cha kumbukumbu ya historia ya mkoa wa Katavi, Kijiji Cha Kabungu ndipo palipozaliwa Wilaya ya Mpanda Mwaka 1947 na Boma la mtawala wa kwanza wa kikoloni Mpanda lilijengwa hapo, baada ya uwekaji wa jiwe la msingi kijijini Kabungu, Makamu wa Rais alirejea mjini mpanda katika viwanja vya Kashaulili ambapo kumefanyika shughuli mbalimbali za  uzinduzi rasmi wa mkoa huo na hotuba mbalimbali zikiendana na sherehe za  ngoma za makabila mbalimbali  ya asili ya mkoa wa Katavi
CHADEMA UONGOZI BALAA
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeitafutia dawa migogoro inayotokana na baadhi ya makada wake kuonyesha nia ya kuwania urais na ubunge mwaka 2015, baada ya kuanzisha utaratibu maalumu wa wanachama wake kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia gazeti  hili, mpango huo unakuja wakati Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe ametangaza nia ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao, kitendo ambacho kiliwashtua vigogo wa chama hicho akiwamo mwasisi wake, Edwin Mtei.

Mara kadhaa Mtei amekuwa akimwonya Zitto kuwa kitendo chake cha kutangaza nia yake ya kugombea urais kitasababisha mzozo na mpasuko ndani ya chama hicho.

Mtei amekuwa akisema kuwa Zitto anatakiwa kuwaunganisha wanaChadema na siyo kuwagawa, au kuwavuruga na kwamba siyo shida kuonyesha hisia za kuwania urais, lakini tatizo ni kuwa hali hiyo inatengeneza mzozo mkubwa.


Mtei ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki Kuu (BOT) enzi za utawala wa Mwalimu Julius Nyerere, alisema wakati mwafaka ukiwadia, Chadema kitaamua ni nani mwenye sifa za kugombea urais akisema kina utaratibu wake wa kuwapata wagombea mbalimbali wa uongozi.

Akizungumza wakati akijibu hoja mbalimbali katika mtandao wa Jamii Forum katikati ya wiki hii, Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, alisema viongozi wa chama hicho walikutana mjini Morogoro hivi karibuni na kutengeneza utaratibu wa watu kutangaza nia wanapotaka kugombea nafasi yoyote ya uongozi.

“Nadhani huu ni uamuzi mzuri wa chama maana watu wengine wana wasiwasi usio na msingi wowote kwamba kuwa na wagombea wengi kwenye chama ni kuvuruga chama,” alisema Zitto na kuongeza:

“Lakini watu haohao wanashangilia kweli wakiona demokrasia inavyotekelezwa kwenye nchi nyingine kama Marekani. Alisema kuwa tatizo la Watanzania wanapenda kuona demokrasia inatekelezwa, lakini wao wanaogopa kuitekeleza, hivyo mwongozo kwa wagombea ambao walipitisha Morogoro utasaidia sana.“Uamuzi wa Morogoro kuhusu mwongozo kwa wagombea utatusaidia sana kuondoa mashaka kama haya,” alisema Zitto.

Mwananchi Jumapili lilipomuuliza Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho, John Mnyika kuhusu jambo hilo  alionyesha kutofahamu lolote kuhusu utaratibu huo, wala ulipofanyika huo mkutano wa Morogoro.

“Mkutano upi wa Morogoro?” alihoji Mnyika. Alipoelezwa kuwa suala hilo lilizungumzwa na Zitto katika Mtandao wa Jamii Forum alisema: “Muulize kwanza Zitto akupe ufafanuzi ni kikao gani cha chama, pia juu ya huo utaratibu, akikueleza ndiyo urudi tena kwangu.”

Juhudi za kumpata Zitto kueleza kwa undani kuhusu utaratibu huo hazikuzaa matunda, kwani simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita bila majibu, baadaye kuzimwa kabisa. Akizungumzia azma yake ya kuachana na ubunge kama alivyoahidi mwaka 2005 kuwa, atagombea vipindi viwili pekee Zitto, alisema kuwa aliwaambia wapigakura wake kwamba nia yake ni kuwa rais wa nchi.

“Nia yangu ni kupisha wengine nao wakimbize kijiti cha maendeleo ya jimbo letu na mkoa wetu,” alisema Zitto na kufafanua, “ Nimeshasema mara kwa mara kwamba ukiachana na siasa kazi ninayoipenda zaidi ni ualimu.”

Alisema kuwa akiachana na ubunge atakwenda kufundisha kwa kuwa anapenda kufanya tafiti, kusoma, kuandika na kufundisha.

“Hivi sasa tunaandaa mpango wa kuanzisha Chuo Kikuu cha Ziwa Tanganyika (Lake Tanganyika) mkoani Kigoma, nitafurahi kama nitakuwa mmoja wa wahadhiri wa mwanzo wa chuo hiki,” alisema Zitto.

Katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe alisimama kugombea nafasi ya urais akishindana na Rais Jakaya Kikwete ambaye alikuwa akisimama kwa mara ya kwanza.

Mwaka 2010, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willbrod Slaa aligombea nafasi hiyo na kuibuka mshindi wa pili kwa kupata asilimia 26.34 nyuma ya Rais Kikwete ambaye alipata asilimia 61.17.

Hivi sasa tayari kumetokea maneno ya chinichini miongoni mwa wabunge waliopo madarakani wakiwatuhumu baadhi ya wanachama wa chama hicho ambao wameaanza kuingia katika majimbo yao kutaka kugombea viti hivyo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Wabunge hao wanahoji kama wanachama hao wanaofanya hivyo wanataka kugombea ubunge katika uchaguzi ujao ili kukifanya chama kiongeze idadi ya wabunge bungeni, kwa nini wasiende kugombea katika majimbo ambayo hayana  wabunge wa chama hicho?Vilevile, chama hicho kilipata msukosuko katika mchakato wa kupata wabunge wa Viti Maalumu katika uchaguzi uliopita na kulazimika kuweka vigezo ambavyo viliondoa manung’uniko hayo.

Baadhi ya vigezo hivyo ni elimu, mchango wa mgombea katika chama, wanawake waliogombea katika majimbo na uzoefu katika ubunge.

Saturday, November 24, 2012

KAZI ILIKUWA HIVI WAKATI WANACHANA WA CCM WAKIMPOKEA JK VIWANJA VYA MNAZI MMOJA
Baadhi ya viongozi wa CCM wakiingia uwanjani


Hao ni viongozi wa CCM wakielekea jukaani

Kama unavyoona usalama wa kutosha ulikuwepo

Ukiona dalidali hizi ujue Mwenyekiti yupo uwanjani hapo


Segere lilikuwepo uwanjani hapo
Msanii Marow nae alikuwepo ndani ya nyumba


TMK nao ndani ya nyumba


T.OT nao walitoa burudani ya kufa mtu

Haya sasa hapo



Wanachama hao
 


Palikuwa hapatoshi