KUTOKA IKULU : MARC REVALOMANANA AMEKUBALI KURUDI NCHINI KWAKE
Na: Veronica Kazimoto –
MAELEZO
Dar es
Salaam
Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete amefanikiwa kufanya mazungumzo na Rais
wa zamani wa Madagaska Marc Ravalomanana ambaye amekubari kurudi nchini kwake
baada ya kuwa uhamishoni nchini Afrika Kusini tangu
mwaka 2009.
Akizungumza na wahariri wa
vyombo vya habari Ikulu jijini Dar es Salaam leo, Raisi Kikwete
amesema Ravalomanana amekubali pia kutokugombea katika uchanguzi utakaofanyika
nchini humo mwezi Mei 2013 ili kuleta amani na
utulivu.
“Nimezungumza na Rais
Ravalomanana na amekubali kurudi nchini kwake madagaska na
kukubali kutokukugombea uchaguzi ujao kama maamuzi ya
Jumuiya
ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika
(SADC)
yalivyofikiwa katika vikao vyake vya hivi karibuni”, amesisitiza Rais
Kikwete.
Raisi
kikwete amefafanua kuwa Ravalomanana anarudi nchini
Madagaska bila masharti yoyote na atapewa ulizi na Serikali ya nchi hiyo
ikisaidiana na Jumuiya ya SADC.
Kwa upande
wake Rais Ravalomanana amemshukuru Rais kikwete kwa kufanikisha mazungumzo hayo
na amesema anaheshimu maamuzi yaliyotolewa na SADC
kwa lengo la kuisaidia Madagaska kuwa katika hali ya
amani.
“Ninamshukuru Rais Kikwete kwa kufanikisha mazungumzo
haya na niko tayari kurudi nchini kwangu kujenga, kuimarisha na kushirikiana na
wananachi ili kuleta amani na utulivu,” amesema
Ravalomanana.
Rais
kikwete alipewa jukumu na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi
za Kusini mwa Afrika
la kufanya mazungumzo na Marais wote wa wawili, Rais
wa sasa wa Madagaska Andry Rajoelina
na Rais wa zamani Marc Ravalomanana ambapo mazungumzo bado yanaendelea kwa
upande wa Rais Rajoelina.
No comments:
Post a Comment