WATANZANIA WATAKIWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUSOMA VITABU
Na: Heka Wanna na Shakila Galus,MAELEZO
MWENYEKITI wa WAMA Mama Salma 
Kikwete wito kwa wananchi tabia ya kujisomea vitambu na machapisho 
mbalimbali ili kujiongezea maarifa yatakayowawezesha kujiletea 
maendeleo.
 Mama Kikwete alitoa kauli hiyo 
kwenye Makumbusho ya Taifa  leo  jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi
 wa makatba kwa ajili ya watoto na watu wazima.
 Alisema kuwa elimu ndio silaha 
pekee ya kukabiliana na maadui watu ambao ni ujinga,maradhi na umaskini 
na hivyo kujiletea maendeleo.
 Mama Kikwete aliongezea mbinu za 
kujiendeleza kimaisha zinapatikana pia kwa njia elimu kupitia  vitabu na
 machapisho mbalimbali yanayopatikana kwenye maktaba mbalimbali ndani na
 nje ya Tanzania.
 Alisema kuwa hiyo itasaidia 
katika kuongeza maarifa kwani kutakuwa na vitabu,kompyuta na mitambo ya 
mawasiliano ambayo itawawezesha watumiaji kupata elimu ya taaluma 
mbalimbali.
 Aidha Mama Kikwete aliwasihi 
watumishi wa Makumbusho hiyo kuwa ni jukumu lao kutunza maktaba hiyo ili
 isaidie kukidhi malengo ya kuanzishwa kwake kwa kuandaa taratibu bora 
za kudhibiti matumizi yasiyo na tija ya maktaba ikiwemo upotevu 
machapisho na vitabu mbalimbali  na uhalibifu wa vitabu unaofanywa na 
watu wasiotaka  maendeleo.
 Mwenyekiti huyo WAMA alimshukru 
Balozi wa Korea Kusini Young Shimo Dho kwa niaba ya nchi yake  kwa 
msaada wa vitabu na vifaa mbalimbali kwa ajili ya maktaba hizo mbili .

No comments:
Post a Comment