IKULU YAWAZAWADIA WAFANYAKAZI WAKE BORA YAWAPA MAKOMBE
  | 
| Katibu
 Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akinyanyua juu mojawapo ya makombe 
matano ambayo Ikulu Sports Club ilinyakua kwenye michezo ya SHIMIWI ya 
mwaka huu mjini Dodoma katika  hafla ya kukabidhi makombe na kuwazawadia 
wafanyakazi bora iliyofanyika leo Desemba 17, 2012 Ikulu jijini Dar es 
salaam. Kwenye michezo hiyo iliyofanyika kuanzia Septemba 22 hadi Oktoba
 10 mwaka huu, ilishirikisha jumla ya wanamichezo 3500 kutoka wizara 
 56, mikoa 18 na idara za serikali 14 ambapo wanamichezo 91 wa Ikulu 
walioshiriki walifanikiwa kuibuka washindi wa kwanza katika michezo ya 
Baiskeli, Netbal,  Kuvuta kamba wanawake na wanaume  na kushika nafasi ya
 pili ya riadha kwa wanawake na wanaume. | 
  | 
| Katibu
 Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiwa katika picha na Bw. Miraji 
Ahmed Saleh ambaye ameibuka kuwa mfanyakazi Bora na Hodari kwa mpigo, 
akiwa kama Msaidizi wa Ofisi Mwandamizi katika Idara ya Huduma  za Ikulu
 na Zahanati katika  hafla ya kukabidhi makombe na kuwazawadia 
wafanyakazi bora iliyofanyika leo Desemba 17, 2012 Ikulu jijini Dar es 
salaam | 
  | 
| Katibu
 Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue  akiwa na  Mwadawa Twalibu, Sophie 
Komba na Pascalia Kibayasa wachezaji wa  netball wa Ikulu Sports Club 
ambao pia ni wachezaji wa timu ya Taifa (Taifa Queens) ya mchezo huo 
kwenye  hafla ya kuwazawadia iliyofanyika leo Desemba 17, 2012 Ikulu 
jijini Dar es salaam. | 
  | 
| Katibu
 Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa nane toka kulia ) pamoja na Naibu
 Katibu Mkuu Ikulu Mama Suzana Mlawi (kulia kwake)  na Mkurugenzi wa 
Huduma za Ikulu Bw Julius Mogore (kushoto kwake) wakiwa katika picha ya 
pamoja na wafanyakazi bora wa Ofisi ya Rais, Ikulu  katika hafla ya 
kukabidhi makombe na kuwazawadia wafanyakazi bora iliyofanyika leo 
Desemba 17, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam | 
  | 
| Naibu
 Katibu Mkuu Ikulu Mama Suzana Mlawi akiwa na  Mwadawa Twalibu, Sophie 
Komba na Pascalia Kibayasa  ambao  wachezaji wa timu ya netball ya Ikulu
 Sports Club ambao pia ni wachezaji wa timu ya taifa ya mchezo huo 
(Taifa Queens) kwenye  hafla ya kuwazawadia iliyofanyika leo Desemba 17,
 2012 Ikulu jijini Dar es salaam  | 
  | 
| Katibu
 Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akimpa zawadi Bw. Miraji Ahmed Saleh 
kwa kuibua mfanyakazi bora na pia mfanyakazi hodari wa  Ofisi ya Rais 
Ikulu. Bw Saleh ni  Msaidizi wa Ofisi Mwandamizi katika Idara ya Huduma 
 za Ikulu na Zahanati katika hafla ya kuwazawadia iliyofanyika leo 
Desemba 17, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam | 
 
No comments:
Post a Comment