MSANII SAJUKI AANGUKA JUKWAANI ARUSHA
![]()  | 
| Msanii huyo akitafakari kwa kina mara baada ya kuanguka chini ya jukwaa huku wenzake wakimpa pole | 
![]()  | 
| Msanii wa filamu nchini,Juma Kilowoko akiwa ameshikiliwa na wenzake wakimshusha chini ya jukwaa mara baada ya kuanguka alipopewa nafasi ya kuwasalimia mashabiki wake | 
Na: Mahmoud Ahmad,Arusha
HALI ya msanii  wa filamu 
nchini,Juma Said Kilowoko maarufu kama Sajuki imeelezwa si ya kuridhisha
  mara baada ya msanii huyo juzi kuanguka jukwaani mara baada ya 
kuishiwa na nguvu wakati alipopewa kipaza sauti kuwasalimia mashabiki 
waliofurika kumtizama.
Tukio hilo lilitokea juzi 
jumapili katika tamasha la wasanii wa filamu na wale wa muziki wa kizazi
 kipya lililofanyika  ndani ya uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid  
wakati msanii huyo alipopandishwa jukwaani kuwasalimia mashabiki wake.
Mara baada ya msanii huyo 
kupandishwa jukwaani alipewa kipaza sauti ili aweze kuwasalimia 
mashabiki wake lakini katika hali ya kawaida alifanikiwa kutamka neno 
moja tu”ahhh” na kisha kudondoka chini ya jukwaa lakini kabla ya kutua 
chini alidakwa na wasanii waliokuwa pembeni yake.
Hatahivyo,wasanii hao 
walimkalisha chini ya jukwaa hilo ili aweze kupumzika na kisha baada ya 
muda mfupi walimshusha chini ya jukwaaa hilo ili aweze kupata muda wa 
kupumzika zaidi.
Akihojiwa na gazeti hili muda 
mfupi mara baada ya kushuka jukwaani Sajuki kwa sauti ya upole alisema 
kwamba hali yake kiafya si nzuri kwa kuwa hana nguvu na anahitaji 
matibabu zaidi.
”Kaka hali yangu si nzuri kabisa naumwa sana sijisikii vizuri”alisema Sajuki huku akionekana mnyonge zaidi
 Hatahivyo,baadhi ya mashabiki 
waliokuwa wamefurika uwanjani hapo walionyeshwa kustushwa na hali ya 
msanii huyo huku wengine wakiwatupia lawama nzito baadhi ya wasanii wa 
filamu nchini walioambatana na msanii huyo kwa madai kwamba wanamtumia 
ili wapate pesa ilhali mwenzao ni mgonjwa.
Wakihojiwa kwa nyakati tofauti 
mashabiki hao kwa jazba walisema kwamba msanii huyo alipaswa kupewa muda
 mwingi wa kupumzika kuliko kuambatana na wenzake mikoani kwani hali 
hiyo inamchosha zaidi.
“Hawa watu wa Bongo movie ni 
watu wa ajabu sana huyu mtu anaumwa sana sisi tunashangaa wanaambatana 
na mtu mgonjwa mikoani wampe muda apumzike na si kumtumia kwa kupata 
pesa”alisikika shabiki mmoja akiongea kwa jazba.



No comments:
Post a Comment