TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Monday, December 31, 2012

ORODHA YA MASTAA 10 WALIOFANYA VIZURI

JACOB STEVEN ‘JB’
Huyu  ni mwigizaji mkongwe kunako gemu la filamu Bongo. Kupitia kampuni yake ya Jerusalem, JB anakiri kuwa ndani ya mwaka huu amefanya kazi nyingi. Amecheza filamu 23 na zote zipo sokoni na zinafanya vizuri katika mauzo tofauti na mwaka uliopita. Unaikumbuka DJ Ben?

STEVEN KANUMBA
Marehemu Steven Kanumba alitisha sana mwanzoni mwa mwaka 2012, kila mwezi alitupia kitu sokoni. Alipofariki dunia Aprili 7, filamu zake zote ziligombewa kama njugu sokoni. Filamu zaidi ya 10 ziliuzwa kwa kipindi hicho, mpaka sasa ile ya Ndoa Yangu ambayo ndiyo ya mwisho kuigiza, bado inatamba sokoni.

MZEE MAJUTO
Mwanzoni King Majuto alitisha kwenye filamu na maigizo ya kuchekesha. Ijumaa Wikienda linamzawadia nafasi kwa kuwa kila kona zilipouzwa filamu kulikuwa na muvi aliyocheza na biashara ilifanyika. Unakumbuka ripoti ya kutisha ya utajiri wake iliyotokana na kazi yake ya uigizaji? Mzee yupo vizuri.

VINCENT KIGOSI ‘RAY’
Nafasi hii tunaitoa zawadi kwa Ray kwani kupitia kampuni yake na mwigizaji Blandina Chagula ‘Johari’, RJ Production, aliweza kutengeneza filamu takribani 10 ambazo zipo sokoni na nyingine hazijatoka hadi sasa. Mzigo wa mwisho ni Waves of Sorrow, uliotanguliwa na Sister Mary.

DOKTA CHENI
Jamaa alifanya poa sana sokoni. Alikimbiza na anakimbiza na muvi kibao ambazo bado zinagombewa, mzigo wake wa mwisho ni Majanga.

WEMA SEPETU
Kwa upande wa wanawake, mwanadada Wema ameonekana kuuza katika filamu kibao ndani ya mwaka huu kwani wengi wanavutiwa na muonekano wake, hali iliyosababisha kufanya kazi zaidi. Ndani ya mwaka 2012 alicheza filamu zaidi ya 13 za watu. Mwisho akacheza moja ya kwake ya The Super Star aliyoizindua kwa kishindo kwa kumdondosha Bongo staa wa Nollywood, Omotola Jalade.

IRENE UWOYA
Hakuwa nyuma katika kufanya kazi japokuwa kuna kipindi alionekana kushuka kidogo. Baadaye filamu za watu alizocheza na za kwake zilikamata soko ghafla na kuwa gumzo kila sehemu zilipouzwa.

JACQUELINE WOLPER
Ijumaa Wikienda linamzawadia nafasi hii mwanadada huyu kwani kupitia kampuni yake alifanikiwa kutengeneza filamu saba ambazo zipo sokoni na nyingine kibao alizoshirikishwa na watu ambazo hakumbuki idadi yake.

MONALISA
Mwaka 2012 ulikuwa wa mafanikio kwa mwigizaji huyu kwani alipata tuzo ya msanii bora wa kike ambapo alicheza filamu kibao za kwake na nyingine zipatazo tano alishirikishwa na watu.

ELIZABETH MICHAEL ‘LULU’
Kabla ya kukumbwa na mkasa wa kuhusishwa kwenye kifo cha Kanumba, Lulu alifanya poa sana mwanzoni mwa mwaka huu. Akiwa mahabusu, hivi karibuni ilitoka filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Dangerous Girl inayofanya vizuri sokoni.

Sunday, December 30, 2012

SUAREZ AIONGEZEA QPR HOFU YA KUSHUKA DARAJA
Luis Suarez (kulia) akiifungia Liverpool goli dhidi ya QPR wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Loftus Road mjini London jana Desemba 30, 2012. Liverpool ilishinda 3-0.


















KIWANGO kibovu cha QPR kiliiongeza hofu yao ya kushuka daraja wakati walipozamishwa na 3-0 na Liverpool yenye ushawishi mkubwa wa Luis Suarez.

Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers hakuwapo kwenye mechi hiyo kutokana na kuwa mgonjwa lakini Suarez mara mbili alitumia makosa ya ulinzi na kuwaweka wageni 2-0 ndani ya dakika 16 tu za kwanza.

QPR walinyimwa penalti wakati 'fri-kiki' ya Adel Taarabt ilipougonga mkono wa Jordan Henderson, kabla ya Daniel Agger kuifungia Liverpool goli la tatu kwa kichwa.

Shuti la Steven Gerrard liliokolewa juu ya mstari wa goli la QPR katika mechi ambayo Liverpool walishinda kirahisi.

QPR wanaoshikilia mkia baada ya vipigo 12 katika mechi 20 msimu huu wako hatarini kushuka daraja huku tofauti ya pointi nane ikiwatenganisha na walio katika nafasi ya kunusurika.

Waliwashuhudia wenzao walio pamoja katika nafasi tatu za chini Reading wakishinda na Southampton wakitoka sare Jumamosi na, wakati QPR walitarajiwa kuonyesha nia ya kutaka kubaki katika ligi kuu, jambo hilo halikuwapo.

Liverpool walikuwa na haraka, wenye njaa na ngangari zaidi, na ingawa waliachiwa nafasi ya kutawala mchezo, waliutawala kwa soka la kuvutia ambalo bila ya shaka litamsaidia Rodgers kupona haraka.

Katika mechi iliyochezwa mapema jana Frank Lampard alikumbushia uwezo wake wa kufunga magoli wakati mabao yake mawili yalipoirejesha Chelsea katika nafasi ya tatu ya msimamo kwa ushindi mgumu wa 2-1 dhidi ya Everton.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 34, ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu, alifunga kwa kichwa krosi ya Ramires na akafunga kutokea jirani ya lango baada ya timu yake kuruhusu goli la kutanguliwa katika sekunde ya 62.

Steven Pienaar aliwafungia Everton goli la kuongoza la mapema, baada ya mpira wa kichwa wa Victor Anichebe kugonga nguzo na kumkuta mfungaji.

Nikica Jelavic naye kisha aligongesha nguzo ambayo ingeweza kuwafanya Everton waongoze 2-0 na akaja akakosa nafasi ya wazi ya kuisawazishia timu yake katika dakika za lala-salama.

Ushindi wa nne mfululizo wa Chelsea katika ligi chini ya kocha wa muda Rafael Benitez, baada ya kushindwa kupata ushindi katika mechi zake tatu za kwanza, unamaanisha kwamba Blues wamemaliza mwaka 2012 wakiwa pointi nne nyuma ya Manchester City na 11 nyuma ya Manchester United, lakini wana mechi moja mkononi.

Swali kama Lampard ataongezwa mkataba Stamford Bridge bado ni gumu, huku Muingereza huyo akiwa huru kuzungumza na klabu aitakayo Januari.

Licha ya vipaji vya nyota wapya kama Oscar na Eden Hazard na uwezo usio na shaka wa Juan Mata, mashabiki waliosafiri na timu wa Chelsea waliweka wazi kwamba bado ni mapema sana kumfanya Lampard, ambaye alijiunga na klabu hiyo miaka 11 na nusu iliyopita, awe historia ya timu.

Magoli yake yalihitimisha mwendo mzuri wa Everton bila kufungwa katika mechi 14 kwenye Uwanja wa Goodison Park, tangu walipofungwa kwa mara ya mwisho 1-0 na Arsenal mwezi Machi. 



MSIMAMO WA MWISHO WA LIGI KUU YA ENGLAND MWAKA 2012


Nafasi Timu Mechi Goal Difference Pointi
1. Man Utd 20 22 49
2. Man City 20 19 42
3. Chelsea 19 21 38
4. Tottenham 20 10 36
5. Arsenal 19 18 33
6. Everton 20 8 33
7. West Brom 20 3 33
8. Stoke 20 4 29
9. Liverpool 20 5 28
10. Swansea 20 5 28
11. Norwich 20 -9 25
12. West Ham 19 -1 23
13. Sunderland 20 -5 22
14. Fulham 20 -6 21
15. Newcastle 20 -11 20
16. Wigan 20 -13 18
17. Aston Villa 20 -24 18
18. Southampton 19 -11 17
19. Reading 20 -15 13
20.QPR 20-20 10

SCENES ZA MAPENZI NI HATARI KWA WASANII

MSANII wa filamu anayejichukulia umaarufu bongo Irene Uwoya, amedai kuwa kuna baadhi ya wasanii wenye majina makubwa wanapenda kucheza filamu za mapenzi na uchezeana huku wakishindwa kuelewa kuwa wananuka midono na mara nyingine huwa wanavumulia pasipo kutoa ukweli huo.

Kauli kama ya msanii huyu iliwahi kutolewa na Janet Jackson kwenye filamu ya ‘Poetic Justice’ iliyozinduliwa mwaka 1993 akimtaka Tupac Shakur kupima vizuri vya ukimwi kwani kuna kipande walitakiwa kuonekana wakipeana midomo kwani walicheza kama wapenzi ndani ya filamu hiyo, ndiyo kitu ambacho hata kwa wasanii wa kitanzania wanatakiwa kujifunza na si kukurupuka kupeana midomo..


Uwoya alisema kuwa kuna sehemu huwa wanakosea na kupeana midomo bila kupima afya kwani wapo wasanii wengine si wasafi na wananuka midomo huku wengine wakiwa wanatumia sana dawa za kulevya hivyo kuna hatari kubwa ya kuambukizwa magonjwa endapo wasipo chukua hatua.

Alisema kuwa wengine wanajijua walivyo lakini wanashindwa kujisafisha na kuwa katika hali nzuri badala yake ndani ya filamu wanaanza kupeanda kiss na kuchezeana bila kujua afya ziko vipi.


“Sasaivi naanza kuwa mkali kwa sababu endapo tukiendelea kuwa kimya tunaweza kujikuta magonjwa yanatukuta hivi hivi” aliongeza.

Hata hivyo msanii huyo aliwashauri baadhi ya wasanii wenye tabia za kupenda kupeana midomo ndani ya filamu wawe makini kwani huwezi jua ni ugonjwa gani anaoweza kupata, na kikubwa zaidi ni kupima kabla ya kazi kuanza ili kama kuna mtu mwenye tatizo apewe tiba mapema.

LEO SAA SITA KAMILI USIKU MITAMBO YOTE YA ANALOJIA ITAZIMWA RASIMI JIJINI DAR ES SALAAM

MKOA wa Dar es Salaam leo saa 6 usiku unakuwa wa kwanza kuzimiwa mitambo ya analojia ya utangazaji wa televisheni kwa ajili ya kupokea mfumo mpya wa digitali.

Hatua hiyo ya kuhama kutoka analojia kwenda digitali ni utekelezaji wa makubaliano ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa katika hotuba yake ya jana kuashiria uzimaji wa mitambo ya analojia, alisema uzimaji kwa zamu unalenga kuepusha usumbufu kwa wananchi.

Mbarawa alisema kuwa mchakato huo wa uzimaji wa mitambo utafanyika tena Januari 31, 2013 na mikoa itakayohusika ni Dodoma na Tanga. Mkoani Mwanza mitambo itazimwa Februari 28, 2013 na Kilimanjaro (Moshi) na Arusha mitambo itazimwa Machi 31, 2013.

Kwa mujibu wa Waziri, mkoa wa saba kuingia kwenye mfumo wa digitali utakuwa Mbeya ambao mitambo itazimwa Aprili 30, 2013. Utaratibu wa kuzima mitambo ya analojia utakuwa kwa maeneo yenye matangazo ya digitali na kwa yasiyo na miundombinu ya digitali hayatazimwa.

Taarifa ya Waziri inaonesha kwamba miundombinu ya mitambo ya digitali imeenea katika mikoa minane pekee. Mabadiliko hayo yanahusu matangazo kwa njia ya utangazaji wa satelaiti, waya (cable) na redio.

“Tunawataka wananchi wasitupe televisheni zao za analojia bali wanunue ving’amuzi ili kupata matangazo ya digitali,” alisema na kuongeza kwamba Serikali inatarajia kupata ushirikiano kutoka kwa wadau wa sekta ya utangazaji na wananchi katika kipindi cha uzimaji wa mitambo ili kufanikisha kazi hiyo.

Aidha imeelezwa kwamba watoa huduma za miundombinu ya digitali wamejipanga kusimika mitambo hiyo katika mikoa mingine minane ndani ya miezi minane ijayo.

Kampuni zenye leseni za kusambaza ving’amuzi zimetajwa kuwa zimejipanga kuhakikisha vinakuwepo vya kutosha. “Na vingine vimeagizwa ili kukidhi mahitaji ya baadaye,” alisema Waziri Mbarawa kupitia hotuba yake.
IJUE HISTORIA YA MWANAMZIKI NICK MINAJI 

Kila mtu ambae amefanikiwa kwa kupanda mwenyewe kutoka chini kwenda juu lazima anasimulizi la maisha yake ambalo lina mabonde na milima ya kushangaza kidogo, lakini inavuta usikivu na hisia sana pale msichana mrembo aliyefanikiwa kuwa kati ya list ya juu duniani kimuziki akiwa na simulizi la maisha yake linalotisha ama kuogofya tena akitishwa na yule aliyemzaa.

Jina lake la kuzaliwa ni Onika Tanya Maraj a.k.a Nicki Minaj, first lady wa Young Money mwenye umri wa miaka 30.

Nicki Minaj ali-experience maisha ya kusikitisha hasa katika familia yake mwenyewe iliyomlea, lakini pia mikiki mikiki toka kwa dingi mkorofi ilikuwa balaaa.
 
 Baba yake mzazi alikuwa mtumiaji wa madawa ya kulevya kupitiliza, kiasi cha kuwa Teja ajabu, lakini pia alikuwa mkorofi na mkatili sana kitu kilichopelekea wanafamilia hao kuishi kwa uoga na mashaka.

Ilifikia hatua baba Nicki Minaj aliwasha moto kwenye nyumba ya familia hiyo akijaribu kumuua mama yake Nicki Minaj, jaribio ambalo halikufanikiwa.

Lakini Nicki Minaj mwenyewe anasema alijaribu sana kumsaidia mama yake kadri anavyoweza na alitaka awe shupavu sana lakini mama yake hakuweza, Nicki alijiwekea malengo ya kuwa mwenye mafanikio baada ya kufanya kazi ili amsaidie mama yake.

“Siku zote nilikuwa na hiki kitu cha kuwawezeshesha wanawake kwenye akili yangu”, aliliambia jarida la Details, “kwa sababu nilitaka mama yangu awe shupavu, na hakuweza. Niliwaza, kama ntakuwa mwenye mafanikio, Naweza kubadili maisha yake.” Huyo ni Nicki Minaj.

Nicki Minaj alianza kuandika mashairi akiwa na umri wa miaka 12 tu, na baada ya kumaliza La Guardia High School, ambayo inatoa elimu ya sanaa na Muziki aliwaza moja kwa moja kuingia kwenye biashara ya muziki. Alianzia chini na alianza kwa kufanya back up kwa rapperz wa jiji la New York.

Muda mfupi baadae alianza kuandika mashairi yake mwenyewe, na baadae akakutana na Lil Wayne aliyegundua kipaji chake ni silaha ya biashara ya muziki na kumsaini Young Money, ambapo alimsaidia kuifanya mixtape ya “Playtime is Over”, baada ya hapo akaishika dunia na michano yake na kuchukua tuzo kibao zenye heshima duniani, na kupata heshima pia hivi karibuni kuwa jaji wa shindano la kuimba la American Idol wakati album yake ya Pink Friday Roman Reloaded; Re-Up iko sokoni. 
 
NB:" USITAKE MAFANIKIO PASIPO KUWEKEZA KATIKA JUHUDI"

Friday, December 28, 2012

ROMA MKATOLIKI KUTOA NGOMA MPYA IITWAYO 2030

























Baada ya kukaa kimya kwa zaidi ya mwaka bila kutoa ngoma mpya, hatimaye rapper Roma anatarajia kutoa ngoma yake mpya kesho Ijumaa.

Ngoma hiyo inaitwa 2030 na kama kawaida yake amezungumza masuala mengi pamoja na kutaja majina ya watu wengi maarufu kwa kuoanisha na matukio. 

Hit ya mwisho aliyoitoa Roma ni Mathematics.
KINYANG'ANYIRO CHA UNIQ MODEL NI LEO






















Ile siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na watanzania wengi kutaka kujua nani ataibuka mshindi wa shindano la kumsaka mwanamitindo wa mwaka mwenye sifa za pekee nchini Tanzania (Unique Model 2012) sasa imewadia.

Homa ya shindano imezidi kupanda ikiwa usiku wa leo atajulikana nani atavishwa taji la unique model of the year 2012 taji lenye heshima katika tasnia ya mitindo nchini Tanzania.

Jumla ya washiriki kumi na mbili wanapanda jukwaani kuwania taji hilo kwenye fainali zake zitakazofanyika katika ukumbi wa maraha wa New Maisha club uliopo Oysterbay jijini Dar usiku wa leo.

Washiriki wanaowania taji hilo ni Vestina Jax,Judith sangu,Amina Ayoub,Catherine Masumbigana,Elizabeth Pertty,Elizabeth Boniface,Vivian Gilbert ,Darline Mmari , Zeenath Habibb,Sandra Suleiman,Cecilia Emmanuel,Magreth Msafiri.

Mratibu wa shindano hili Bwana Methusela Magese amewaomba watanzania wajitokeze kwa wingi siku ya leo kwani kuna mambo mazuri ya kufurahisha ikiwemo burudani ya muziki wa bendi toka kwa mashujaa,ngoma za asili na bongo flava kwa kiingilio cha Tshs 15,000/= tu.


Shindano hili limedhaminiwa na Giraffe ocean view hotel,Kitwe general Traders,sophanaa investment ltd,dtv,88.4 clouds fm,Gazeti la Tanzania Daima,Gazeti la Kiu,mashujaa investment ltd,Michuzi blog,jiachie blog,Lmada Apartments & Hotel,mtaa kwa mtaa blog,Fabak fashins,Genessis health center na Yung don Records,Paka wear,Mtoko Design,Dina ismail blog na Unique Entertainment Blog.

Thursday, December 27, 2012

LUDACRIC NA MPENZI WAKE KWENYE VOCATION HAWAI
Maisha ni furaha jamani Ludacric akiwa na mpenzi wake hapo ufukweni

Raha ni kupeana au ???


SHOW YA DIAMOND NA DIMPOZ ILIKUWA HIVI NDANI YA DAR LIVE
 

 

Mheshimiwa ndani ya jukwaa


Nataka kulewa hiyo


Wageni waalikwa wakifuatilia show

Diamond akifanya vitu vyake huku mashabiki wakimshangilia

Wednesday, December 26, 2012

CHRISS BROWN NA RIHANNA WATOKA PAMOJA X-MASS KWENDA KUSHUHUDIA LIGI YA KIKAPU
Rihanna na Chriss Brown wakiwa beneti huku Rihanna akilaza kichwa chake kwa Brown wakati wakifuatilia mechi kali ya Ligi Kuu ya Mpira wa Kikapu Marekani (NBA) kati ya New York Knicks na Los Angeles Lakers mjini Los Angeles, jana Desemba 25, 2012. Lakers ilishinda kwa pointi 100-94 (Picha: REUTERS).

Mapenzi ni furaha kama unavyowaona wawili hao wakiwa na nyuso za furaha

Pozi muhimu  kuna la kusema hapo jamani!


Wanacheeeeeeeka...! Wasanii Chris Brown (kushoto) na Rihanna wakifurahi wakati wakiwa wameketi pamoja kushuhudia mechi kali ya Ligi Kuu ya Mpira wa Kikapu katia ya New York Knicks na Los Angeles Lakers mjini Los Angeles, jana  Desemba 25, 2012. Lakers ilishinda kwa pointi 100-94 (Picha: REUTERS)
 

MESSI AMPELEKA MWANAE KWAO ARGENTINA 



















LIONEL Messi hivi sasa yuko mapumziko nyumbani kwao Rosario, Argentina. Aliwasili asubuhi ya Jumatatu na atakaa huko hadi Januari 2 wakati atakaporejea mazoezini Barcelona.

Mshambuliaji huyo ameambatana na mchumba wake Antonella na mwanae mwenye umri wa wiki nane, Thiago, ambaye ametembelea nchi ya baba yake kwa mara ya kwanza.

"Niko Rosario sasa na familia yangu nzima. Wazazi wangu walikuja kunipokea uwanja wa ndege. Kuna joto sana katika mji wa nyumbani kwetu, lakini nina furaha nimerejea nyumbani", alisema nyota huyo wa Barca kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa ‘Weibo’.

"Nimemaliza vyema kwa magoli na rekodi, lakini mwaka ungekuwa mzuri zaidi kama tungebeba mataji. Daima nimekuwa nikisema kwamba kilicho muhimu zaidi ni tuzo ya pamoja. Magoli yangu bila ya makombe, haina maana.

"Kuzaliwa kwa Thiago kulikuwa ni jambo kubwa sana kati ya yote yaliyowahi kutokea maishani mwangu. Ilikuwa ni kipindi 'spesho' sana maishani mwangu," supastaa huyo wa Barca alisema katika gazeti la Catalunya la 'El Mundo Deportivo'.


Monday, December 24, 2012

WAPENDWA WOTE WA BLOG HII !!!

NAPENDA SANA KUWATAKIA MAANDALIZI MEMA YA X-MASS  MUNGU AWE PAMOJA NANYI....! AWALINDE NA KUWAONGOZA KATIKA MAMBO YOTE.

AMEN

Saturday, December 22, 2012

MTANZANIA AIBUKA MSHINDI MISS EAST AFRICA
Joyceline akiwapungia mkono mashabiki baada ya kutangazwa mshindi.
Joyceline akijieleza kabla ya kutangazwa kuwa mshindi
Zawadi ya gari alilozawadiwa baada ya kushinda
Waliofanikiwa kuingia tano bora

MSHIRIKI wa Tanzania katika Shindano la Miss East Africa 2012, Jocelyne Diana Maro, jana ameibuka kidedea katika fainali zilizofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar.

Ushindi huo umemfanya Jocelyne azawadiwe Dola 30,000 ambazo ni pamoja na gari aina ya Mazda lenye thamani ya Dola 15,000 na mkataba wa kufanya kazi na Miss East Africa Organization wenye thamani ya Dola 15,000.


WASANII WAENDA IKULU KUMSHUKURU RAIS KWA KUWAJALI
 
 






















Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo Desemba 21, 2012 amepokea ujumbe wa wasanii wakongwe wa muziki wa dansi pamoja na filamu
uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaaam kwa kuwajali wasanii wa aina zote na hata kuamua kutoa tuzo kwa wasanii
ambapo mwaka huu amewatunuku Muhidin Maalim Gurumo na Hayati Marijani Rajabu.

PICHA NA IKULU

JERRY SLAA NDANI YA HEKALU KUOMBEA AMANI
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wahindu Tanzania Bw. Ramesha Patel akimpokea na kumtambulisha mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa wakati alipowasili kwenye msikiti mkuu wa Dhehebu hilo ulioko jijini Dar es Salaam kwa shughuli maalum ya kuliombea taifa Amani.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akilakiwa na kuvishwa shada la maua.
Ibada ikendelea kwa namna ya kipekee.
 Pichani Juu na Chini watoto kwa wakubwa wakicheza ngoma za asili ya Hindu kwenye Ibada hiyo.
 

Mstahiki Meya Jerry Silaa akioneka kufurahishwa na ngoma hizo.
 Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wahindu ya Shreen Sanatan Dharma Sabha Bw. Rajesh Mistry akimkaribisha mwenyekiti wa jumuiya hiyo kuzungumza maneno machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi.
 Bw. Ramesh Patel akimkaribisha mgeni rasmi kuzungumza na wanajumuiya hiyo wakati wa Ibada maalum ya kuliombea Taifa Amani.


























Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akizungumza na wanajumuiya ya Hindu ambapo amewashukuru kwa kumkaribisha kuungana nao katika Ibada hiyo maalum na kuwataka kuendelea kuwa na mshikamano na jamii nyingine pamoja na Serikali.
Mstahiki Meya ametumia fursa hiyo kuwataka wanajamii hiyo pale wanapokwama au kukwazwa kibiashara katika manispaa ya Ilala kwa jambo wanaloona linaweza kutatuliwa wasisite kuwaona viongozi wao na kuwaambia viongozi wao wasisite kumuona yeye moja kwa moja ili watafute ufumbuzi kwa manufaa ya Manispaa na jiji kwa ujumla. Kulia ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bw. Ramesh Patel

Friday, December 21, 2012

DK. SLAA TUNASUBIRI TAARIFA YA ARF






















KATIBU mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa amesema chama hicho kinasubiri kupokea taarifa ya mgogoro unaofukuta ndani ya chama hicho mkoani Katavi na kusababisha Makamu Mwenyekiti wake Taifa , Said Arfi, kutupa kadi yake ya uanachama.

Ameeleza kuwa Katiba ya chama hicho inaeleza wazi kwamba unapoibuka mgogoro, unatakiwa kuripotiwa katika ofisi ya Katibu Mkuu Taifa ndani ya siku 14. Tukio la Arfi kutupa kadi ya Chadema lilikuwa la pili ndani ya wiki moja, kwani juma lililopita uliibuka mgogoro mwingine wilayani Karatu ambako pamoja na mambo mengine uliishia kwa Kamati Kuu kuusimamisha uongozi wote wa chama hicho wilaya.

Arfi ambaye ni Mbunge wa Mpanda Mjini, alitishia kujitoa Chadema juzi, katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya chama hicho Mikoa ya Katavi na Rukwa kilichoketi Namanyere, Nkasi na kufikia uamuzi wa kumsimamisha Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Mkoa wa Rukwa, Laurent Mangweshi.

Katika kikao hicho, Arfi anadaiwa kuichukua kadi yake ya Chadema na kumtupia Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Rukwa, John Mallack akitangaza kuachia nyadhifa zote alizonazo, kisha kuondoka ukumbini, kabla ya kufuatwa na wazee wa chama hicho na kumsihi aichukue kadi yake hiyo.

Hata hivyo, Mangweshi jana aliliambia Mwananchi kwamba hajapewa barua hiyo mpaka sasa na kwamba yeye bado ni Mwenyekiti wa Bavicha mkoa wa Rukwa, kauli ambayo ilipingwa na Katibu wa chama hicho mkoani Rukwa na Katavi, Ozem Chapita aliyesema kuwa ipo tayari na wameisafirisha kwa basi jana mchana ili imfikie.

Akizungumzia tukio hilo jana Dk Slaa alisema  taarifa hizo amezisikia ila hawezi kutoa maamuzi kwa kuwa Chadema kinafuata taratibu za vikao pamoja na Katiba yake.

“Utaratibu wa chama ni kwamba malalamiko yeyote ni lazima yawasilishwe katika ofisi ya Katibu Mkuu ndani ya siku 14” alisema Dk Slaa na kuongeza; “Mimi kama Katibu Mkuu ni lazima nifuate taratibu za chama na sio kufanya vinginevyo.” Alisema kuwa taarifa hizo amezisikia kupitia vyombo vya habari na kwamba anachokisubiri ni taarifa rasmi ya maandishi ili kama chama kiweze kukaa vikao na kujadili mgogoro huo.

Alipoulizwa kuna taarifa kwamba baadhi ya makada wa chama hicho wanatumiwa kukivuruga, Dk Slaa alisema kuwa inawezekana hilo likawa na ukweli lakini kama kawaida ya chama hicho, hakitoi maamuzi bila ya kukaa vikao.

“Hizo ni taarifa ambazo zipo na zinaandikwa kila siku katika vyombo vya habari, zikija rasmi katika ofisi ya chama zitajadiliwa” alisema Dk Slaa.

Arfi alifikia hatua hiyo baada ya kutokea sintofahamu kati ya wajumbe wa kikao hicho katika uamuzi huo uliofikiwa kwa kupiga kura za ndiyo na hapana.


Vyanzo vya habari kutoka ndani ya kikao hicho vilifafanua kuwa Arfi alikerwa na kauli iliyotolewa na Mangweshi kuwa katika Uchaguzi Mkuu uliopita, alipokea rushwa kutoka kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Vyanzo hivyo vya habari vimeeleza kuwa kutokana na hali hiyo, Arfi alipandwa na hasira na kuamua kumrushia kadi Mallack kisha kutoka nje ya ukumbi. “Hatua hiyo ilifanya wajumbe wa kikao hicho nao kutoka nje ya ukumbi na kuanza kumbembeleza ili asichukue uamuzi huo na kisha wakamwekea kadi yake ya uanachama katika mfuko wake wa shati,” alisema mmoja wa makada hao.Arfi mwenyewe hakupatikana juzi kuzungumzia tukio hilo na hata jana alipotafutwa simu zake zote zilikuwa zimezimwa.


Imeandaliwa Fidelis Butahe, Dar na Juddy Ngonyani, Katavi, Burhani Yakub, Tanga na Mussa Juma, Arusha

Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz/habari
LEMA ARUDISHIWA UBUNGE NA MAHAKAMA YA RUFAA
Lema,Mbowe na nassari mahakamani

Lema akianza kutoa hotuba fupi baada ya kutoka mahakamani kulia ni Joshua Nassar

 Vitalisi kimomogoro,wakili wa lema huyu ndiye amekuwa na kesi hii tangu kuanza


 Askari wakisindikiza msafara wa wafuasi wa CHADEMA