ASKOFU SOLLO AMPONGEZA RAIS KIKWETE KWA KUENDESHA NCHI KWA AMANI
HUKU
nchini kenya hofu ya vitendo vya ugaidi vilivyofanywa na watu
wanaosadikika kuwa kundi la wanamgambo wa al-Shabaab katika eneo la
maduka ya bidhaa la Westgate mjini Nairobi ikiendelea kutawala nchini
Kenya, askofu wa kanisa la maombezi na uponyaji cha Overcomers (OPC)
mkoani Iringa Dr Boaz Sollo amempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa
kuendelea kuliongoza Taifa katika hali ya amani na utulivu na kuwataka
viongozi wa madhehebu ya dini kote nchini kujikita katika maombi ya
kuliombea Taifa la Tanzania amani ili yaliyotokea Kenya yasiikumbe
Tanzania (hd)
Askofu Dr
Sollo alitoa kauli hiyo jana katika ibada yake ya kwanza baada ya
kupokelewa na waumini wake akitokea nchini Marekani kwa huduma ya
maombezi kwa Taifa la Marekani .
Alisema
kuwa Tanzania ni moja kati ya nchi za mfano barani Afrika kwa kuwa na
amani kutokana na uwajibikaji na utendaji mzuri wa Rais Kikwete na
watendaji wake wote na kuwa ili yale yaliyotokea nchini Kenya kwa watu
kuvamiwa na kudi hilo la kigaidi la Al-shabaab ni vema sasa viongozi
wote wa madhehemu ya dini kuelekeza nguvu zao zote za kimaombi katika
ibada maalum za kuliombea Taifa amani .
Kwani
alisema kuwa silaha kubwa katika kupambana na adui awaye yoyote ni
maombi na kuwa siku zote Mungu husimama katikati ya wanamaombi na kamwe
shetani hafungamani na Taifa lolote ambalo watu wake watakuwa ni wacha
Mungu .
" Awali
ya yote naungana na watanzania wote pamoja na viongozi wa serikali yetu
tukufu katika kuwafariji ndugu zetu na jirani zetu wa Kenya ambao ndugu
zao wamepoteza maisha katika shambulio baya lililotokea hivi karibuni
katika eneo la maduka la Westgate mjini Nairobi....Mungu aendelee kuwapa
roho za uvumilivu ....ila pia kwetu viongozi wa dini nchini Tanzania
tunawajibu wa kutenga muda wa kuliombea Taifa letu amani "alisema askofu
Dr Sollo
Kuwa
kanisa lake la OPC limejipanga kuendeleza maombi ya kuliombea Taifa na
kuwa hadi sasa jamii ya wana Iringa kwa ujumla kutokana na kazi kubwa
inayofanywa na kanisa hilo hata matukio ya ajabu ajabu ambayo yalikuwa
yakitokea kutokana na watu kuanguka katika dhambi yameanza kutoweka.
Wakati
huo huo askofu Dr Sollo alitaka viongozi wa dini kuendelea kuuombea
mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya ya jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ili umalizike salama na kuwa Taifa moja kama ambavyo
lilivyosasa pia kuiombea katiba kuendelea kutoa uhuru wa kuabudu pamoja
na kutowanyima uhuru watu wake hasa viongozi wa dini kukemea vitendo vya
ushoga kama ilivyo nchini Marekani ambapo wahubiri wamezuiwa kabisa
kugusia wala kuzungumzia kwa maana ya kupinga suala la ushoga katika
nyumba za ibada.
" kabla
ya kuanza kufanya shughuli zangu za mahubiri nchini Marekani wenyeji
wangu waliniweka sawa na kunieleza kuwa sipaswi kuzungumzia suala la
ushoga katika mahubiri yangu na nikifanya hivyo nitafukuzwa nchini
humo.....ila sisi huku Tanzania serikali haitupangii mambo ya kuzungumza
bora mradi hatuzungumzii kauli za kichochezi"
No comments:
Post a Comment