TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Saturday, October 26, 2013

ANCELOTTI HAJAAAMUA KUHUSU BALE KAMA ATAANZA AU

bale2 10233
KOCHA Carlo Ancelotti hajaamua kama atamuanzisha Gareth Bale katika mechi ya El Clasico kesho, lakini amesema nyota huyo wa Wales yupo tayari. (HM)

Mtaliano huyo, akizungumza katika Mkutano wa Real Madrid na Waandishi wa Habari leo mchana amesema kwamba maamuzi yoyote kuhusu Bale atayafanya baada ya mazoezi ya mwisho kuelekea mechi hiyo jioni ya leo kabla ya mechi na Barcelona Uwanja wa Camp Nou Jumamosi jioni.
Ancelotti alisema; "Ikiwa kutakuwa na Mkutano na Waandishi wa Habari baada ya mazoezi ya jioni, nitawaambia vizuri kuhusu Bale kama ataanza,".
Baada ya kubanwa sana kwa maswali juu ya suala hilo, Ancelotti alisema kwamba Bale yuko tayari na hayuko katika wakati mgumu tena, lakini amejtuma sana na ametumia mapumziko ya mechi za kimataifa kujiweka fiti.'
"Kwa maoni yangu, na maoni yake pia, yuko tayari kucheza tangu mwanzo,"alisema.
Bale hajawa na mwanzo mzuri Real kutokana na kuandamwa na majeruhi tangu ajiunge na klabu hiyo ya Hispania. Kwa ujumla, mwanasoka huyo wa kimataifa wa Wales amecheza dakika 178 tu katika mechi tano na kufunga bao moja. Chanzo: binzubeiry

No comments:

Post a Comment