DRC YASITISHA MAZUNGUMZO NA M23
Mazungumzo ya amani kati ya Serikali
ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na waasi wa M23 yamesitishwa tena
licha ya Umoja wa Mataifa kuweka msukumo wa kuendelea kwa majadiliano ya
pande hizo mbili.
Mazungumzo hayo yamekuwa yakiendelea
mjini Kampala Uganda tangu Septemba mwaka huu ambapo kila upande umetoa
tamko lake kuhusiana na kusitishwa kwa mazungumzo hayo.
Msemaji wa Serikali ya Kongo Lambert
Mende amesema kuwa mazungumzo yamesitishwa kutokana na kutofikiwa
makubaliano kuhusu msamaha kwa M23 na jinsi watakavyo jumuishwa katika
jeshi la Taifa la nchi hiyo FARDC.(P.T)
Mjumbe wa M23 katika mazungumzo hayo
Roger Lumbala alisema kumekuwa na vikwazo lakini wao wako tayari kurejea
kwenye meza ya majadiliano wakati wowote.
Awali serikali ilionya kuwa majadiliano yaliyoanza upya mwezi Septemba chini ya shinikizo la Viongozi wa nchi za Maziwa Makuu yalikuwa yanakwenda taratibu mno hali iliyoashiria mwisho wa maafikiano.
Awali serikali ilionya kuwa majadiliano yaliyoanza upya mwezi Septemba chini ya shinikizo la Viongozi wa nchi za Maziwa Makuu yalikuwa yanakwenda taratibu mno hali iliyoashiria mwisho wa maafikiano.
No comments:
Post a Comment