MARKEL :OBAMA HAKUJULISHWA KUHUSU UDAKUZI
Mkuu wa shirika la ujasusi nchini
Marekani NSA hakuzungumzia madai ya udukuzi wa simu ya Chansela wa
Ujerumani Angela Markel na rais Barack Obama .
Kwa mujibu wa msemaji wa shirika hilo,
Gen Keith Alexander hakuwahi kumtajia Obama kitendo cha kudukua simu ya
Markel, kinachodaiwa kufanywa na shirika hilo.
Vyombo vya habari nchini Ujerumani
vinasema kuwa Marekani imekuwa ikinasa mawasiliano ya kwenye simu ya
Markel tangu mwaka 2002, na kuwa Rais Obama alifahamishwa kuhusu habari
hiyo mwaka 2010.
Kashfa hii imesababisha mgogoro mkubwa wa kidiplomasia kati ya nchi hizo kuwahi kushuhudiwa katika historia ya mataifa hayo.(P.T)
Ripoti kwenye gazeti moja la udaku
nchini Ujerumani zinasema kuwa Genrali Alexander mwenyewe aliwahi
kumhabarisha Obama kuhusu kitendo cha kudukua simu ya Markel.
Hata hivyo jarida hilo limesea kuwa
kulingana na taarifa kutoka ndani ya NSA Obama hakuwahi kusitisha
kitendo hicho, kwani alitaka kujua kila kitu kuhusu Marke kwani
hakumuani sana.
Hata hivyo taarifa hizo zimekanushwa
vikali na shirika hilo zikisema kuwa Obama hakuwahi kujulishwa kuhusu
kitendho hicho na kuwa taarifa zinazosema vinginevyo ni za kupotosha.
Obama hata hivyo ameripotiwa kumwambia Bi Markel kuwa hakujua chochote kuhusu udukuzi huo wakati walipokutana.
Ujerumani inatuma maafisa wake wakuu
wa ujasusi nchini Marekani wiki ijayo ili kushinikiza kufanywa uchunguzi
katika madai ya udukuzi wa simu ya Bi Markel ambayo yamesababisha
ghadhabu nchini humo
No comments:
Post a Comment