Kuhusu Daktari wa Michael Jackson kutoka jela
Taarifa
 ikufikie kwamba aliekua daktari wa mwimbaji staa wa Pop duniani Michael
 Jackson, Conrad Murray ameachiwa huru kutoka jela baada ya kutumikia 
kifungo kwa miaka miwili kati ya minne aliyokua amehukumiwa kutokana na 
kifo cha MJ mwaka 2009.
CNN wameripoti kwamba Daktari huyu ilibidi atumie mlango mwingine 
kutoka jela ili kukwepa waandishi wa habari pamoja na baadhi ya 
mashabiki wa Michael Jackson wenye hasira waliokuwemo nje ya jela baada 
ya kupata taarifa kwamba anatolewa kwenye jela hiyo ya Los Angeles.
Mwanasheria wake amekaririwa akisema kwamba Doctor Conrad anaweza 
kurudi kuendelea na kazi yake ya udaktari lakini moja kati ya kauli za 
familia ya Michael Jackson ni ‘ni wazi kwamba Conrad ndio alimuua 
Michael Jackson, tunamatumaini kwamba hatofanya udaktari tena na 
kumuumiza wengine’
No comments:
Post a Comment