KIONGOZI WA NGAZI YA JUU WA AL-SHABAAB AUAWA SOMALIA
Kiongozi wa ngazi ya juu anayeongoza
mashambulizi ya kujitoa mhanga ya kundi la al-Shabaab lenye mafungamano
na al-Qaeda ameuawa katika shambulizi la ndege isiyoruka na rubani
Kusini mwa Somalia
Waziri wa Mambo ya Ndani, Abdikarin
Hussein Guled, ameiambia redio ya serikali kuwa idara ya ujasusi ilikuwa
ikimfuatilia Ibrahim Ali Abdi, maarufu kama Anta-Anta, kwa muda sasa
kabla ya shambulizi hilo kufanywa jana Jumatatu 28.10.2013
Waziri huyo hajasema ni nani
aliyefanya shambulizi hilo, lakini afisa mmoja mjini Washington amesema
jeshi la Marekani lilifanya shambulizi la ndege isiyoruka na rubani
likililenga kundi la al-Shabaab nchini Somalia jana Jumatatu.(P.T)
"Operesheni hiyo ambayo mtu huyu
aliuawa ilikuwa muhimu kwa serikali. Mtu huyu alikuwa na jukumu kubwa
kwa raia wengi wasio na hatia na kifo chake kitasaidia kurejesha amani,"
alisema waziri huyo kupitia Radio Mogadishu.
Maafisa kutoka serikali ya Somalia inayoungwa mkono na jamii ya kimataifa wamemtaja mwanamgambo aliyeuawa kuwa anayefahamika vyema kwa kutengeneza mabomu ya kuvaa mwilini pamoja na ya kutengwa ndani ya gari ambayo hutumiwa mara kwa mara na waasi kuyashambulia maeneo ya serikali. Hapajakuwa na kauli yoyote kutoka kwa wapiganaji hao.
Shambulizi hilo linakuja wiki chache baada ya shambulizi kali kufanywa katika jumba la maduka ya Westgate jijini Nairobi, Kenya, lililodaiwa kufanywa na al-Shabaab ambapo watu 67 waliuawa.
Kisha kikosi maalumu cha jeshi la wanamaji la Marekani kikafanya shambulizi katika bandari ya kusini ya Barawe mapema mwezi huu (Oktoba) na kushindwa kufikia lengo lake: ambalo lilikuwa ni kiongozi mmoja wa ngazi ya juu wa al-Shabaab na Mkenya mwenye asili ya kisomali kwa jina Abdulkadir Mohammed Abdulkadir, pia anayefahamika kama Ikrima.
Afisa mmoja wa Marekani ambaye hakutaka kutajwa jina lake, hajasema sehemu ambayo ndege hiyo isiyoruka na rubani ilianzia safari yake, lakini jeshi la Marekani huendesha shughuli zake za ndege hizo kutoka kambi za nchini Djibouti na Arba Minch kusini mwa Ethiopia.
Wapiganaji wa al-Shabaab wametimuliwa kutoka miji mikuu ya Somalia, ikiwa ni pamoja na Mogadishu na bandari ya kusini mwa nchi hiyo Kismayo, kufuatia operesheni ya jeshi la Umoja wa Afrika linalosimamiwa na Umoja wa Mataifa na ambalo sasa lina wanajeshi 17,700.
Kundi hilo hata hivyo linayadhibiti maeneo makubwa ya kusini mwa Somalia na katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita, limekiongeza kiwango cha mashambulizi yake ya kujitoa mhanga.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP

No comments:
Post a Comment