TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, October 30, 2013

MAGUFULI BADO ALIA NA WENYE MALORI

magufuli21 16f82
WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli amesema tatizo la uzidishaji wa mizigo unaofanywa na magari makubwa iwapo litaendelea, barabara zote zitaharibika. Dk. Magufuli alitoa kauli hiyo bungeni jana, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF). (HM)
Katika swali lake, Hamad alitaka kujua sababu ya barabara zinazojengwa kuharibika ndani ya kipindi kifupi.
Dk. Magufuli alisema tatizo la kuharibika kwa barabara linasababishwa na ujenzi duni wa wakandarasi, lakini kwa kiasi kikubwa huharibiwa na magari yanayozidisha mizigo.
"Kwa mfano katika Barabara ya Dar es Salaam hadi Dodoma tayari upande wa kushoto wa barabara umeshabonyea.
"Kwa Tanzania uzito unaotakiwa kupita barabarani hautakiwi kuzidi tani 56, lakini magari yanazidisha hadi kati ya tani 90 na 98, tukiendelea hivyo si tu barabara zitavimba bali zitapasuka kabisa," alisema.
Alitoa viwango vya uzito unaotakiwa katika nchi kama Marekani kuwa ni tani 36.2, Uingereza Tani 44, Ufaransa Tani 40 na Ujerumani ni Tani 40.
Awali akijibu swali la msingi la Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige, Dk. Magufuli alisema Mkoa wa Geita umeingia mkataba na Mhandisi Mshauri kwa ajili ya kuifanyia marekebisho barabara ya Geita, Bukoli hadi Kahama.
Alisema mkataba huo ni kwa ajili ya kuifanyia upembuzi yakinifu pamoja na usanifu wa kina barabara hiyo kwa gharama ya Sh milioni 403.9 katika kipindi cha miezi 13.
Katika swali lake, Maige alitaka kujua lini utekelezaji wa kuiwekea lami barabara hiyo utaanza. Chanzo: mtanzania

No comments:

Post a Comment