Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi NSSF Watembelea Miradi Dar
Baadhi ya
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
(NSSF) pamoja na maofisa wa NSSF wakitembelea mradi wa Ujenzi wa Daraja
la Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
(NSSF) pamoja na maofisa wa NSSF wakitembelea mradi wa nyumba za bei
nafuu eneo la Mtoni Kijichi.
Meneja
Mradi wa NSSF, Mhandisi Karim Mattaka (wa kwanza kulia waliokaa mezani)
akitoa taarifa fupi kwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la
Taifa la Hifadhi ya Jamii na maofisa waandamizi wa taasisi hiyo juu ya
maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni.
Meneja
Mradi wa NSSF, Mhandisi Karim Mattaka (wa kwanza kushoto) akifafanua
jambo kwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi
ya Jamii na maofisa waandamizi wa taasisi hiyo juu ya maendeleo ya
ujenzi wa daraja la Kigamboni.(P.T)
Baadhi ya
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
(NSSF) pamoja na maofisa wa NSSF wakiteremka kwenye gari katika moja ya
miradi ya taasisi hiyo walipotembelea jana.
Mmoja wa maofisa wa juu na mhandisi kutoka NSSF akifafanua jambo kwa wajumbe wa bodi.
Afisa
Mradi msimamizi na Msanifu wa NSSF, Deogratias Mponeja (wa kwanza
kushoto) akitoa maelezo juu ya mradi wa awamu ya tatu ya ujenzi wa
nyumba nafuu kwa wajumbe.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau (wa pili
kulia) akiwa na Eunice Chiume wakizungumza jambo katika ziara ya
wajumbea wa Bodi ya NSSF kutembelea miradi jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi NSSF Watembelea Miradi Dar
Mkurugenzi
wa Mradi na Msanifu Majengo wa NSSF, Mkurugenzi wa Mipango, Miradi na
Uwekezaji wa NSSF, Yacoub (aliyesimama) akitoa taarifa fupi juu ya
maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu kwa wajumbw wa bodi.
Na Joachim Mushi, Dar es Salaam
WAJUMBE wa Bodi ya Wakurugenzi ya
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wamefanya ziara ya
kutembelea baadhi ya miradi kadhaa inayotekelezwa na shirika hilo
iliyopo jijini Dar es Salaam. Miradi iliyotembelewa katika ziara hiyo ni
pamoja na ule wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu uliopo eneo la Mtoni
Kijichi na ujenzi wa Daraja la Kisasa eneo la Kigamboni.
Akitoa taarifa fupi kwa wajumbe wa
bodi ya NSSF wakiwa eneo la ujenzi wa nyumba za bei nafuu na za kisasa
eneo la Mtoni Kijichi, Mkurugenzi wa Mipango, Miradi na Uwekezaji wa
NSSF, Yacoub Kidula alisema eneo hilo linatekelezwa kwa awamu mbili za
ujenzi wa nyumba aina mbalimbali.
Alisema awamu ya pili ambayo
iliendelea baada ya kukamilika ya kwanza ya ujenzi wa nyumba 85,
imetekelezwa kwa ujenzi wa nyumba 215 eneo la Mtoni Kijichi mradi ambao
tayari umekamilika na nyumba zimeanza kuuzwa kwa wanachama wa NSSF.
Alisema nyumba 200 tayari zimekamilika huku 15 zilizosalia zikiwa katika
hatua za mwisho kukamilika.
Alisema tayari Shirika hilo limeanza
kutekeleza ujenzi mwingine wa awamu ya tatu utakaowezesha ujenzi wa
nyumba za kisasa na bora zaidi zenye uwezo wa kuchukua familia 820
zikiwa na ghorofa moja huku zikiwa zimeboreshwa zaidi kihuduma
ukilinganisha na zilizojengwa awali.
Aidha akifafanua juu ya ujenzi wa
nyumba za bei nafuu zinazoendelea kujengwa na NSSF, alisema mbali na
kuwa za bei ya chini zinahuduma muhimu za kijamii kama umeme, maji,
mfumo mzuri wa kuifadhi maji taka, eneo la nje la ziada pamoja na vifaa
vingine zikiwemo feni vyumba vyote, mfumo wa maji ya moto kwenye mabafu
na sakafu ya kisasa 'tiles'.
Alisema nyumba zinazojengwa zinaukubwa
na idadi ya vyumba tofauti kulingana na maitaji ya mteja, yaani kuanzia
vyumba viwili hadi vitatu vya kulala huku vyote vikiwa na sebule, jiko,
choo pamoja na stoo. Aliongeza kuwa milango na madirisha yamejengwa kwa
vioo na chuma (nondo) ili kuimarisha zaidi kiusalama huku jiko likiwa
na kabati maalumu na za kisasa kwa ajili ya kuifadhia vitu.
Kidula alisema nyumba ya chini itauzwa
takribani sh milioni 66 za kitanzania bei hiyo ikiwa ni pamoja na VAT.
Wajumbe wa bodi pia walitembelea mradi mkubwa wa NSSF wa ujenzi wa
daraja la Kigamboni ambao unafanywa na taasisi hiyo kwa kushirikiana na
Serikali.
Akitoa taarifa za maendeleo ya ujenzi
wa daraja hilo, Meneja Mradi huo, Mhandisi Karim Mattaka alisema licha
ya ujenzi huo kuendelea vizuri kwa sasa zipo changamoto kadhaa za ujenzi
ambazo zilijitokeza hivyo kushughulikiwa mara moja.
Alisema daraja hilo la kisasa
litakalokuwa na njia (barabara sita) yaani tatu za kwenda Kigamboni na
tatu za kurudi linatarajiwa kuunganishwa kisasa na barabara ya Mandela
huku likiwa na njia za kutosha kuzuia msongamano wa magari.
Akizungumzia ziara hiyo ya Wajumbe wa
Bodi, Meneja Uhusiano Kiongozi, Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la
Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume alisema ni ziara ya kawaida ya
wajumbe hao kukagua miradi ya taasisi hiyo na huenda ziara hiyo ikawa na
manufaa ya punguzo la riba kwa wanachama wanunuzi wa nyumba hizo.
Imeandaliwa na www.thehabari.com
No comments:
Post a Comment