MAJESHI YA SERIKALI YA CONGO YAKOMBOA MJI WA BUNAGANA
Jeshi la jamhuri ya kidemokrasi ya
Congo limefanikiwa kuuteka mji wa mpakani na Uganda wa Bunagana ngome ya
mwisho iliyobaki ya kundi la waasi wa M23. Maafisa wa serikali na
mashahidi wanasema majeshi ya serikali yaliingia katika mji huo baada ya
wapiganaji wa M23 kuondoka huko. (HM)
Kundi hilo la waasi liliuteka mji wa Bunagana na miji mingine ya jimbo la Kivu Kaskazini la Mashariki ya Congo lilipoanza uasi wake mwaka jana. Kumekuwa na mapigano makali kuanzia siku ya Ijumaa wakati majeshi ya serikali ya Congo yakisaidiwa na majeshi ya Umoja wa Mataifa kuanzisha mashambuklizi ya kukomboa miji hiyo inayoshikiliwa na waasi.
Idara ya Umoja wa Mataifa inayowahudumia wakimbizi – UNHCR, inaeleza kwamba mapigano yamesababisha maelfu ya wakongo kukimbilia Uganda. Chanzo: voaswahili
No comments:
Post a Comment