DK. MWINYI ATAKA WAGANGA WA TIBA ASILI KUSHIRIKIANA NA WATAFITI
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.
Hussein Mwinyi amewataka waganga wa tiba asili washirikiane na
wataalamu wa utafiti ili kuwezesha upatikanaji wa dawa bora na salama.
Kauli hiyo ilitolewa leo na Waziri
huyo wakati akitoa tamko kuhusu maadhimisho ya siku ya tiba ya asili ya
mwafrika ambayo huadhimishwa kila mwaka Agosti 31, lakini mwaka huu
hayakufanyika kutokana na uhaba wa fedha. Maadhimisho hayo yanatarajiwa
kufanyika mwakani kipindi katika hicho.
" Tanzania tunayo mitidawa mingi na
mingi haijafanyiwa kazi katika utafit na kuweza kubaini uwezo wa kutibu
magonjwa mbailmbali tatizo lililopo ni jinsi gani mitidawa hiyo inweza
kufanyiwa utafiti na kuwa dawa bora na salama kwa watumiaji kwa
kuziwekea mifumo ya huduma za afya ili kila mwenye kuhitaji aweze
kuzipata," alisema Dk. Mwinyi .(P.T)
Dk. Mwinyi aliwataka waganga hao
kushirikiana na watafiti kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa
ya Binadamu (NIMR) na Taasisi ya Utafiti wa Dawa za Asili iliyokpo
katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shiriki- (MUHAS).
Aliongeza kuwa waganga wote wa tiba asili na tiba ya kisasa wanatakiwa kufanya kazi kwa kuelewana ili kuwezesha kupata taarifa za awali kabla ya utafiti kamili kufanyika.
Aliitaja kauli mbiu ya maadhimisho hayo kuwa ni ' Tiba Asili : Utafiti na Maendeleo' kuwa inalenga kutoa majukumu kwa waganaga wa tiba asili na tiba mbadala katika sula zima la utafiti. Pili inatoa changamoto juu ya uendelezaji wa taarifa za utafiti wa mitidawa katika kutafuta dawa ya kutibu magonjwa mbalimbali.
Aidha aliwahimiza waganga wa tiba asili kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao na huduma za afya.
Mwisho.

No comments:
Post a Comment